Facebook

Sunday, 16 November 2014

Waziri nchini akiri kopekea fedha za ufisadi za ESCROW.

Kumekuwepo na taarifa nyingi juu ya ufisadi wa
fedha za akaunti ya Tegeta ESCROW..
Baadhi ya
wanasiasa wametuhumiwa kupewa mgao ili
kuzima suala hilo.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa kuna Waziri
mmoja alipewa zaidi ya Billion 1 na akazigawa
jimboni mwake. Lakini vyombo vya habari havikutaja jina la
waziri husika..

Sasa Waziri huyo ameamua
kujitokeza hadharani na kukiri kupokea fedha hizo.
Prof.Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba na Makazi
amekiri kupokea mgao wa Dollar Mil.1 sawa na
Sh.Bilioni 1 na Milioni mia Saba, ikiwa ni sehemu
ya fedha za ESCROW.

Katika akaunti yake ya
Twitter amesema alipokea hela hizo kwa nia njema
(good faith) na hakujua kama zilikua ni fedha za
ufisadi.

Pesa hizo anadai alizigawa kwa shule za
sekondari za wasichana jimboni kwake. Je nini
maoni yako??

0 comments:

Post a Comment