Kituo cha sheria na haki za binadamu
kimesema kimesikitishwa na kauli aliyoitoa
waziri mkuu Mh Mizengo Pinda bungeni
wakati akiahirisha bunge kuwa hakuna
uhakika kwamba fedha zilizokuwa katika
akaunt ya Escrow.
Kituo cha sheria na haki za binadamu
kimesema kimesikitishwa na kauli aliyoitoa
waziri mkuu Mh Mizengo Pinda bungeni
wakati akiahirisha bunge kuwa hakuna
uhakika kwamba fedha zilizokuwa katika
akaunt ya Escrow kama ni za serikali ama
la jambo ambalo amesema kwa kufanya
hivyo ni kutaka kuwalinda waliohuska
katika wizi huo.
Akizungumza katika makao makuu ya kituo
hicho mkurugenzi wa utetezi na maboresho
mwanasheria Harold Sungusia amesema
kwa kauli aliyoitoa waziri mkuu bungeni
kushangaza umma vile kamati ya bunge ya
hesabu za serikali PAC imesema wazi kuwa
fedha ni za umma.
Kwa upande wake afisa programu dawati la
uangalizi wa serikali katika sakata la wizi
wa fedha za umma Bw. Hussein Sengwa
amesema miongoni mwa watu ambao
wametajwa ndio walikuwa waandishi wa
katiba mpya na ndiyo maana hata vipengele
muhimu vya kuwabana viongozi
wasiokuwa wadilifu walivifuta.
Aidha afisa programu dawati la bunge na
uchaguzi Bw Hamis Mkindi amesema
kutokana na sakata la IPTL watu wengi
wameamka na kutaka kushiriki katika
uchaguzi unaoendelea sasa wa viongozi wa
serikali za mitaa ambao wameonekana
kutaka kuwaweka viongozi wanaona ni
waadilifu.
0 comments:
Post a Comment