Leo tarehe 5/6/2015, baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo vikuu tumeweza kuonana na m/kit wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Damian Lubuva.Ambayo ilikuwa ni makubaliano tuliyoyafanya juzi tarehe 3/06/2015 kuhusu kuonana nae.
Madhumuni ya kuonana na m/kiti wa NEC ,ni kama ifuatavyo
Moja ni kujua namna gani wanafunzi tunaweza kujiandikisha na kupata fursa ya kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.
Pili ni namna gani tutaweza kupiga kura ikiwa maeneo tuliyojiandikishia yatakuwa tofauti na ambapo tutakuwa wakati wa uchaguzi.
Mengine zaidi ya hayo tumeyaeleza kwenye WARAKA WETU KWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI(NEC).
Makubaliano yetu na Jaji Damiani Lubuva ni kama ifuatavyo
Moja wanafunzi wote wa vyuo vikuu atahakikisha tunajiandikisha na kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu maeno mbalimbali ambayo tutakuwa wakati wa uchaguzi......Pia swala hili limejieleza wazi katika ibara ya 5(3)(c) kwenye katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
Pili WARAKA WETU KWA TUME YA UCHAGUZI(NEC), utajibiwa pia kwa maandishi tarehe 10/06/2015, baada ya kikao cha wajumbe wa Tume kukaa na kujadili namna gani wataweza kutuandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu.
Changamoto tulizokutana nazo ni
Viongozi wa shilikisho la vyuo vikuu Tanzania(TAHILISO) waliofika ofisi za tume ya uchaguzi(NEC), Kutaka kujaribu kukwamisha mazungumzo yetu na m/kiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva kwa malengo yao binafsi.
Lakini tunashukuru watendaji wa Tume ya uchaguzi(NEC) kwa pamoja na m/kiti wa NEC waliweza kuheshimu makubaliano yetu ya kufanya nao mazungumzo.
Hata hivyo viongozi hao wa TAHILISO walishindwa kujumuika nasi katika mazungumzo hayo na kutokomea kusikojulikana.
Wito wetu kwa Wanavyuo vikuu Tanzania tunahitaji ushirikiano kwa pamoja ili kuweza kufanikisha na sisi tunapata haki yetu ya msingi ya kikatiba kushiriki kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi wakitaifa tunao wataka na hatuwezi kuchagua viongozi hao kama tutakuwa hatujajiandikisha.
Wanafunzi walioshiri kwenye mazungumzo hayo ni wafuatao
1.)LUSEKELO AMIMU-Chuo kikuu Ardhi
2.)BARAKA NYEUA-T.I.C.D Arusha
3.)NTILE JOEL-UDSM
4.)PATRICK JOHN-UDSM
5.)MWIDADI MSANGI-Ardhi
6.)FRANK JOASH-CPS &CPA
7.)SHIRIMA JUVENAL-Ardhi
8.)SHITINDI VENANCE-UDSM
Baada ya Tume ya uchaguzi NEC kutoa majibu kwa maandishi tutawaletea tena mrejesho kwenu.
Kwa mawasiliano zaidi:
0684-615128