Facebook

Tuesday, 2 June 2015

Rais wa FIFA Sepp Blatter atangaza kujiuzulu

Taarifa zilizotufikia BantuTz hivi punde ni kwamba Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema kuwa atajiuzulu kama rais wa shirikisho hilo.Ikumbukwe Sepp Blatter ameiongoza FIFA kwa muda wa miaka 17 hadi hivi sasa na wiki iliyopita alichaguliwa tena kwa kipindi cha muhula wa 5.
Sepp Blatter aliitisha mkutano wa ghafla na kusema uchaguzi wa kiongozi mpya wa FIFA utafanyika hivi karibuni.Akizungumza katika mkutano huo wa ghafla kufuatia tuhuma mbalimbali za ufisadi na rushwa zinazolikumba shirikisho hilo Sepp Blatter amesema atashughulikia na kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi wa kiongozi mpya huku yeye hatosimama kugombea nafasi hiyo.Blatter alichaguliwa tena wiki iliyopita licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi .

Vilevile Blatter amesema ataendelea kuliongoza Shirikisho hilo mpaka pale ambapo uchaguzi mpya utafanyika.Lakini Rais Sepp Blatter hakuelezea na hakutoa sababu kwa nini ameamua kujiuzulu huku ikiwa ni siku kadhaa akiwa anasherehekea ushindi wake na Mamlaka zinazosimamia masuala yote ya rushwa kutoka Uswisi yamesema walisisitiza Blatter hachunguzwi na hatochunguzwa kwa lolote lile.
Lakini alisema kuwa mamlaka yake hayaungwi mkono na kila mtu..Blatter amesema FIFA inahitaji mabadiliko makubwa ya uongozi ili kuongeza uwajibikaji.













0 comments:

Post a Comment