Wakati Ligi Kuu England ikizidi kutajirika kwa
kuongeza Mapato yake kwa Asilimia 29 na
kufikia Pauni Bilioni 3.3, Manchester United
ndiyo inayoongoza kwa kuwa na Mapato ya
juu kabisa.
Mahesabu hayo yametolewa na Magwiji wa
ushauri wa Kifedha Duniani, Deloitte, ambao
wamesema Man United ipo juu kwa kuvuna
Pauni Milioni 433.2 kwa Mwaka wa Fedha wa
2013/14.
Deloitte imesema Klabu zilizopiga hatua
kubwa katika kipindi hicho ni Everton, Aston
Villa na Chelsea lakini Man United imeendelea
kuwa juu.
Deloitte imesema kukua kwa Mapato hayo
kumetokana hasa na kuongezeka kwa Mapato
yatokanayo na Matangazo ya TV.
LIGI KUU ENGLAND
LISTI YA MAPATO 2013/14:
Man United £433.2m
Man City £348.3m
Chelsea £324.4m
Arsenal £300.5m
Liverpool £255.8m
Tottenham £180.5m
Newcastle £129.7m
Everton £120.5m
West Ham £116.5m
Aston Villa £111.2m
Southampton £106.1m
Sunderland £104.4m
Swansea £98.7m
Stoke £98.3m
Norwich £94.4m
Fulham £92.1m
Crystal Palace £90.4m
West Brom £86.8m
Hull £84.5m
Cardiff £83.1m
0 comments:
Post a Comment