
Tamasha hilo amabalo litafanyika tarehe 13 juni kwenye uwanja wa Taifa na Makamu wa raisi DR Mohamed Gharib Bilal amealikwa kuwa mgeni rasmi.katiaka mahojiano mzee Jangala alisema”nimepanga kutangaza nia ya kugombea uraisi siku hiyo kwenye uwanja wa taifa mbele ya makamu wa raisi, najua watu watafikiri natania katika jambo hili lakini siko hivyo.
Msanii huyo mkongwe ambaye hakutaka kutaja atawania kupitia chama gani alisema kilicho mpeleka kuwania ni mapenzi yake kwa nchi na pia kuondoa tatizo la mmongonyoko wa maadili kwa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana na wananchi.
“Rushwa imekua changamoto mojawapo,sasa basi mimi nina uwezo,najiamini kuongoza na kupambana na tatizo hili.kinacho hitajika ni watanzani a kuniunga mkono pindi nitakapo tanzangaza nia.uraisi hauna kijana wala mzee kinachohitajika ni je? Una sifa na uzalendo kutoka moyoni.sitaki ubunge nia yangu ni kuwasaidia Watanzania endapo nikipata ridhaa ya kuongoza nchi kupitia nafasi ya uraisi” alisema mzee Jangala ambaye ni mshindi wa Tuzo ya mafanikio ya muda mrefu kukaa kaika fani.
Sorce: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment