Facebook

Wednesday, 3 June 2015

Mtanzania ajishindia tuzo baada ya kubuni teknolojia ya hali ya juu.

 
Mbunifu kutoka Tanzania atapatiwa dola 38,000 kwa ajili ya kufanikisha mradi wake ulioshinda tuzo ya ubunifu kutoka taasisi ya Uingereza ya uhandisi - Royal Academy of Engineering.
Mtanzania huyo Dr Askwar Hilonga, ametengeneza chujio maalum ya maji ambayo inatumia mchanganyiko wa mchanga na teknolojia ya nano na kufanya maji kuweza kutumika.
Hilonga amesema kuwa amefurahi kushinda tuzo hiyo, ambayo itampa fursa ya kutengeneza mitambo zaidi nchini Tanzania ambapo anasema zaidi ya asilimia 70 ya watu hawana maji safi na salama ya kunywa.Katika picha Dr Askwar Hilonga (kulia) akipokea tuzo.


0 comments:

Post a Comment