
Lakini kwa mujibu wa Magazeti ya Spain, Cuatro na El Mundo, Real Madrid
imeikataa Ofa hiyo ya Man United ya kuwanunua Bale na Varane ingawa wao
wenyewe wanataka kufanya dili kumchukua Kipa wa Man United David De
Gea.
Huko Brazil Chombo cha Habari Sambafoot kimedai Man United
wako mstari wa mbele kumnasa Staa mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil
Roberto Firmino anaechezea Klabu ya Bundesliga huko Germany, Hoffenheim,
kwa Dau la Pauni Milioni 18.

0 comments:
Post a Comment