Kampuni ya mtandao wa Google imeomba
radhi baada ya picha za waziri mkuu wa India Narendra Modi kuonekana
katika picha za watu kumi wahalifu.
''Tunaomba radhi kwa
kuchanganyikiwa na kutoelewana ambako kumesababishwa na picha
hizo'',taarifa iliotoka kwa kampuni hiyo ilisema.Viongozi wengine duniani waliomo katika orodha hiyo ni aliyekuwa rais wa Marekani George Bush na Libya Muammar Gaddafi.
Viongozi wengine wakuu wanaopatikana ni waziri mkuu wa Delhi Arvind Kejriwal,wakili Ram Jethmalani na mtoro Dawood Ibrahim pamoja na mwigizaji wa Bollywood Sanjay Dutt ambaye kwa sasa anahudumia kifungo kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea mjini Mumbai mwaka 1993.
''Haya matokeo yanatushangaza na hayawakilishi maoni ya Google'',kampuni hiyo ilisema katika taarifa yake iliotolewa jumatano usiku.
Picha za Modi zinaonekana unapowatafuta watu 10 wahalifu pamoja na magaidi,wauaji na madikteta.
Kampuni hiyo imesema kuwa matokeo hayo yanatokana na gazeti moja la Uingereza ambalo lilichapisha picha ya Modi kimakosa.
Msamaha huo unajiri baada ya wanasiasa wengi wa India kuonyesha wasiwasi wao katika mitandao ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment