Facebook

Saturday, 6 June 2015

Simba yakaribia kumnasa mshambuliaji hatari kutoka Burundi.


SIMBA SC imekaribia kabisa kukamilisha usajili wa mchezaji mpya wa sita kuelekea msimu ujao, na huyo si mwingine bali mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba SC, Collins Frisch yuko mjini Bujumbura kukamilisha usajili wa mchezaji huyo na habari zisizo rasmi zinasema, amefanikiwa.
Chanzo cha habari kutoka Simba SC kimedai kwamba Mavugo tayari ni mchezaji wa Wekundu wa Msimbazi kwa miaka miwili ijayo.
Kijana huyo aliyezaliwa Oktoba 10, mwaka 1989 kwa sasa anachezea Vital’O ya kwao Burundi, lakini awali alichezea Kiyovu na Polisi za Rwanda na aliyekuwa kocha wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic ndiye aliyempendekeza mkali huyo wa mabao asajiliwe.
Kopunovic amewahi kufanya kazi na Mavugo katika timu ya Polisi ya Rwanda, kabla ya wawili hao kuihama timu hiyo kwa wakati tofauti.
Iwapo Simba SC itamtangaza rasmi Mavugo kuwa mchezaji wao mpya- atakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa ndani ya kipindi cha wiki tatu, baada ya awali Wekundu hao wa Msimbazi kuwasaini kipa Abraham Mohammedwa JKU, mabeki Samih Hajji Nuhu wa Azam FC, Mohammed Fakhi wa JKT, kiungo Peter Mwalyanzi wa Mbeya City na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi kutoka Mtibwa Sugar.

0 comments:

Post a Comment