Akizungumza na Clouds FM, alisema kuwa viongozi wa sasa wameshindwa kutekeleza sera zao kutokana na sababu mbalimbali hasa za binafsi, kitaifa na kimataifa na sera hizo hubadilika kila wakati.
Akimzungumzia rais ajaye kama anaweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Tanzania hivi sasa alisema kuwa anaweza kama akija na sera nzuri na pia mabadiliko ya kimaendelea duniani kote huja taratibu.
‘’Naamini rais ajaye atafanya mabadiliko ya kimaendeleo kama akija na sera nzuri lakini naamini maendeleo duniani kote huja taratibu,’alisema Niki.
Pia akizungumzia uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao utafanyika mwezi Oktoba alisema kuwa utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na wagombea wengi kujitokeza kuwania kugombea uraisi kupitia chama cha CCM,na pia upande wa upinzani kuna ushindani mkubwa wa kumteua mgombea wa uraisi.
Niki Wa Pili ametaja vipaumbele vyake pindi atakapokuwa raisi wa Tanzania
1. Serikali lazima irudi kuwekeza kwenye uchumi
Wawekezaji nawapa sector zilizodumaa hamna uwekezaji wa kuvuna bali wa kuzalisha lectures za vyuo zitarekodiwa na kutakuwa na YouTube chanells za accounting, marketing, sociology na kadhalika…….so kwa waliokosa vyuo na mikopo, unaweza ukawa unazitazama….then chuo unakuja kufanya mitihani….vitabu navyo online.
Shule za vipaji maalumu narudisha, division one ya kwanza haulipi ada, masomo ya sayansi 60% kwa vitendo.
2. Mbunge lazima uwe na masters
3. Kipimo cha maendeleo ni watu
4. Kipimo cha miradi, sera, wizara ni matokeo yake kwa watu
5. Ukipatikana na rushwa unafutiwa kazi na vyeti vyako
0 comments:
Post a Comment