Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa
wanasiasa wa kiislamu nchini Morocco za kumtaka waziri wa mawasiliano
nchini humo kujiuzulu kufuatia Tamasha la muziki lililomuhusisha msanii
Jenifer Lopez mjini Rabat ambalo wamelitaja kama kuukosea adabu uma
kulingana na vyombo vya habari vya taifa hilo.
J-lo kama
anavyojulikana alipanda jukwaani ili kushiriki katika tamasha la muziki
la Mawazine huku vyombo vya habari vya serikali vikitaja utendaji wake
kama wa hali ya juu.Lakini malalamishi yalianza baada ya J-lo kuonyeshwa katika runinga huku wito wa kujiuzulu kwa waziri huyo ukitolewa.
Hatahivyo waziri huyo amekataa kujiuzulu.
0 comments:
Post a Comment