Ghana imetangaza siku tatu za
maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu mia na hamsini
vilivyotokana na mafuriko na mlipuko kwenye kituo kimoja cha mafuta.
Mlipuko
huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi
katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Rais wa Ghana,John Mahama amesema janga halitajirudia tena.
Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu ,Accra alipotembelea eneo la tukio.
Amesema
watu wanapaswa kuachana na tabia ya kujenga kwenye mikondo ya maji na
inabidi utekelezaji ufanyike ili kuzuia janga lingine kama hilo kutokea.
"Tutachukua hatua fulani kuzuia hili lisitokee katika wakati ujao na
mara kwa mara. Hatua hizi zinapokuwa kali, mnakuwa na huruma na kutaka
zisitekelezwe. Lakini nafikiri wakati umefika, mnafahamu, kwa kuziondoa
nyumba katika maeneo ya maji na umma lazima uelewe kuwa ni lazima kila
mtu kuhudumiwa. Nina maana kupotea kwa maisha kwa namna hii ni janga
kubwa ambalo halijawahi kutokea hapo kabla."Anasema Rais Mahama.
Miili
ya watu imeendelea kutolewa kutoka eneo la tukio na kuwekwa katika
malori. Serikali ya Ghana bado inajaribu kupata idadi kamili ya watu
waliokufa au kuathirika kutokana na ajali hiyo. Wengi wa waliokufa
walijihifadhi katika kituo cha petroli kukwepa mvua kubwa iliyokuwa
ikinyesha ambayo imesababisha mafuriko katika sehemu kubwa ya mji wa
Accra.
0 comments:
Post a Comment