Facebook

Friday, 22 August 2014

Kuku aishi bila kichwa;wengi wapigwa bumbuwazi !

 
Wakazi wa Kware wakimwangalia jogoo asiye na kichwa ila anatembea! 

Wakazi wa eneo la Kware huko Ongata Rongai nchini Kenya wako kwenye mshangao mkubwa kwa kioja ambacho wengi mnaweza msiamini kusikia.
Maajabu haya ni ya kuku anayeishi bila kichwa! Wengi wanaamini
jogoo huyo alitumika kwa mambo ya kishirikina na haonyeshi kusikia maumivu. 


Rachel Danson, mkazi wa Kware alisema, “Niliona kitu kama
karatasi jeupe karibu na kibanda changu lakini sikujishughulisha nacho kwa sababu nilidhani ni uchafu tu umetupwa!”


Jirani yake Rachel aliupekua mfuko huo wa karatasi ndipo alipobaini kulikuwa na kiumbe kinachopumua! Ikabidi amwambie jirani yakekibiashara yaani Rachel.


 “Manzo tuliogopa kabla ya kupata ujasiri wa kuufungua mfuko huo na ndipo jogoo asiye na kichwa alipotoka na kuanza kutembea!” Aliongeza Rachel.

Hata hivyo, ndani ya mfuko huo kulikutwa jogoo mwingine aliyekuwa amekufa na kuoza na kilichowashangaza wengi ni huyo jogoo aliyekuwa mzima lakini hana kichwa! Mmoja wa wakazi hao alisema inawezekana kabisa yule jogoo alitumika kwa mambo ya kishirikina kwani eneo hilo ni maarufu sana kwa uchawi!

0 comments:

Post a Comment