Habari kutoka zilizotufikia BantuTz.com kutoka katika mji mkuu wa Libya,
Tripoli, zinasema kuwa mabomu mawili ya
kutegwa ndani magari yamelipuliwa , moja
karibu na ubalozi wa Misri na jingine karibu
na ubalozi wa milki za kiarabu .
Balozi zote hizo mbili zimefungwa kwa miezi
kadhaa .
Hakuna taarifa kuhusu majeruhi kufuatia
mashambulizi hayo.
Makundi ya kiislam yanayodhibiti mji mkuu
awali yaliishutumu Misri kwa kuanzisha
mashambulizi ya anga dhidi ya vikosi vya
kiislam nchini Libya , shutuma ambazo
zimekabushwa na serikali ya Misri.
Wakati huo huo Misri imeyashutumu makundi
ya wapiganaji ya Libya kuwasaidia wapigganaji
wa kiislam wa Misrui katika rasi ya Sinai
0 comments:
Post a Comment