Msuva? Ah Wapi, yanga yakataa,
Mkude ajazwa manoti na Simba
SIMBA imemjaza noti na kumwongezea
mkataba wa miaka miwili kiungo wake,
Jonas Mkude na sasa
Jonas Mkude (Katikati) akisaini mkataba wa
kuendelea kuichezea timu ya Simba, chini ya
viongozi wakuu waandamizi wa timu hiyo.
SIMBA imemjaza noti na kumwongezea
mkataba wa miaka miwili kiungo wake,
Jonas Mkude na sasa imetangaza rasmi
kwamba itakwenda Yanga kumnunua
winga Simon Msuva kwa gharama yoyote.
Lakini Mwenyekiti wa Kamati ya
Mashindano ya Yanga, Isack Chanji,
amesema: “Msuva? Ndio kwanza ana
mkataba wa miaka miwili na hatuna
mpango wa kumuuza wala Simba
wasihangaike kupoteza muda.”
Mkude alikuwa kwenye rada ya Yanga
ambayo ilipanga kumsainisha Jumanne
usiku, lakini saa chache kabla Simba
wakashtukia mchezo wakamalizana naye.
Mkude alifanya mazungumzo awali na
Simba mbele ya Mwanasheria wake lakini
akagoma kusaini mpaka apewe dau lake
na masharti yake yatimizwe, saa chache
baada ya kuondoka kwenye kikao hicho
Yanga wakaanza kumsaka ndipo Simba
iliposhtua na kumsaka haraka
ikamalizana naye.
Ingawa jana Jumatano Simba iliitisha
mkutano na waandishi na kumsainisha
Mkude mkataba mpya, Mwanaspoti
linaweza kuthibitisha kwamba mkataba
huo ulikuwa wa kupigia picha kwani
tayari mchezaji huyo alishasaini mbele ya
watu wake wa karibu na Mwanasheria
wake Jumanne jioni maeneo ya Bamaga,
Jijini Dar es Salaam.
Mwanaspoti linafahamu kwamba Yanga
walipanga kumpa Mkude Sh80 milioni
kama alivyotaka, lakini Simba ikampa
Sh70 milioni na akasaini mkataba wa
miaka miwili. Mchezaji huyo atakuwa
akilipwa mshahara wa Sh2 milioni kwa
mwezi, atapatiwa nyumba ya kisasa yenye
samani ndani huku akikatiwa bima ya
afya mambo ambayo awali alikuwa
hayapati.
Timu hiyo pia imempa gari aina ya
Toyota Mark II Grand GX115 kumalizia
deni la dau lake la usajili wa msimu
uliopita. Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili, Zacharia Hans Poppe, alisema:
“Wakati tunamsajili Emmanuel Okwi,
Mwenyekiti wa Yanga alisema ana uwezo
wa kuinunua Simba nzima na kuipeleka
kucheza soka la ufukweni, lakini
amekwama kumsajili Mkude kwa sababu
hana uwezo huo, hivyo basi tunatangaza
rasmi kumalizana na Mkude na pia
tunatangaza kuandika barua kwenda
Yanga kumwomba Msuva kwa gharama
yoyote.
“Tunaamini hakuna lisilowezekana kwani
kinachotakiwa ni kufuata taratibu
ambazo hazitakuwa na madhara, usajili
ni makubaliano ya pande zote tatu, hivyo
tupo tayari kwa masharti watakayotupa.”
Lakini Mwanaspoti limeambiwa kwamba
Simba hawana uhakika wa kumpata
Msuva ila wameelekeza nguvu zao zaidi
kwa kipa Juma Kaseja na Mbuyu Twite.
Kaseja ana mkataba na Yanga ila Simba
wamefanya mazungumzo na Meneja wake
ambaye yuko katika mchakato wa
kusitisha mkataba wa Yanga kwa madai
kwamba kuna vipengele vimekiukwa,
lakini kwa upande wa Twite ambaye ni
kiraka, Simba inafikiria kumchukua ili
kuimarisha kiungo na beki yao. Mchezaji
huyo raia wa Rwanda amegoma kuongeza
mkataba na Yanga.
“Ndani ya siku mbili hizi (jana na leo
Alhamisi) tutapata ripoti ya kocha
ambayo itatupa mwongozo wa nini
anataka kifanyike katika kuboresha kikosi
chetu nasi tutaanza kazi mara moja,”
alisema Hans Poppe.
Hans Poppe alifafanua pia juu ya
wachezaji wao wanaodaiwa mikataba yao
kumalizika kuwa watawaongeza mikataba
mipya wakati wowote.
Wachezaji ambao
inaelezwa mikataba yao inamalizika hivi
karibuni baadhi yao ni Ramadhan
Singano ‘Messi’, Said Ndemla anayetajwa
kutakwa na Azam FC wanaosemekana
wapo tayari kumpa Sh40 milioni na
William Lucian ‘Gallas’.
Kwa upande wake Mkude alisema: “Ni
kweli nilikuwa nafuatwa na timu hizo,
lakini nimeamua kubaki Simba kwa
sababu ndiyo timu iliyonilea tangu
mwanzo, najua huu si mwisho wangu
kwenye soka ila muda wa kuondoka
Simba bado haujafika.
“Nimeridhika na kiwango walichonipa na
ninafurahia maisha Simba kwa sababu
napewa chochote ninachokihitaji, hivyo
hakuna haja ya mimi kuondoka kwa sasa
na nipo tayari kwa lolote.
0 comments:
Post a Comment