Polisi nchini Kenya wamefanya msako
mkali dhidi ya misikiti inayotoa mafunzo ya
itikadi kali za kidini mjini Mombasa pwani
ya Kenya.
Mtu mmoja ameuawa kwenye msako huo
ulioanzishwa Jumapili dhidi ya misikiti
inayosemekana kutoa mafunzo ya kuunga
mkono harakati za kundi la wapiganaji wa
kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia.
Misikiti ya kwanza kulengwa katika msako huo
ni ile ya Masjid Musa na Sakina.
Mkuu wa polisi mjini Mombasa alinukuliwa na
shirika la habari la AFP akisema kuwa walipata
taarifa kwamba kundi hilo limekuwa likipanga
kufanya mashambulizi na hiyo ndiyo sababu ya
msako huo kuanzishwa.
Watu 200 wamekamatwa ikiwemo washukiwa
wakuu sita.
Polisi wanasema kuwa mtu mmoja aliuawa
ingawa hawajatoa taarifa zaidi kuhusu kifo cha
mtu huyo na kwamba uchunguzi utafanywa.
Viongozi kadhaa wa kidini wameuawa mjini
Mombasa katika kinachodaiwa kuwa mauaji ya
kiholela huku kukiwa na ushindani pamoja na
uhasama kati ya makundi kinzani ya kiisilamu.
Makanisa pia yamekuwa yakilengwa kwa
mashambulizi.
0 comments:
Post a Comment