Wanawake mjini Nairobi, Kenya leo
wameandamana kupinga kitendo cha
mwanamke mmoja kuvuliwa nguo wiki jana
kwa madai kuwa alikuwa amevalia sketi
fupi sana.
Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho
wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya
kuvalia mavazi yanayomfurahisha.
Hiyo wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa
mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke
huyo ambaye hakutajwa jina hadi sasa
akivuliwa nguo zake na wanaume katika kituo
cha magari ya abiria kati kati mwa Nairobi.
Wanawake mashuhuri wakiwemo wasanii,
wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo
hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke
yanamhusu nini mwanamume ambaye sio
mumewe wala jamaa yake.
Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha
kinyama na kinachokiuka haki za wanawake.
Msanii mmoja mashuhuri Nyota Ndogo
alinukuliwa akisema ikiwa wanaume
wanawavua nguo wanawake kwa kile
wanachosema ni mavazi yasiyo ya kiheshima,
basi na wanaume wanaolegeza long'i zao na
wao basi pia wavuliwe nguzo zao.
Chanzo:BBC
0 comments:
Post a Comment