Kama unamini kwenye bahati basi
kasome maisha ya Vince Lombard.Hakuna mtu
aliyetegemea kuwa Lombard atakuwa mtu wa
kukumbukwa kwenye ardhi ya Marekani.Lakini
Lombardi aliamini ipo siku juhudi zake
zitamfikisha kwenye ndoto zake.Ndivyo
ilivyokua,Mpaka sasa Lombardi anahesabiwa
kama kocha bora kuwai kutokea kwenye ardhi
ya marekani.
Lombardi ni kocha mwenye
mafanikio zaidi kwenye ligi ya marekani. Japo
watu wengi walikua wanamuhesabu kama mtu
mwenye bahati,Lakini Lombardi mpaka anafika
alipofika alikua anaamini kwenye
kujituma.”Football is like life,It requires
Preseverance,Self-
denial,Hardwork,Sacrifice,Dedication and
Respect for Authority”.(“Mpira ni kama
maisha,Unahitaji
uvumilivu,kujinyima,Kujitma,kujitoa na
kuheshimu mamlaka”).Hiyo ni kauli kuu ya
bwana Lombardi katika
mchezo pendwa wa mpira wa miguu.
Kauli
hiyo ilikuwa ikiwalenga haswa wachezaji
wavivu.Bila shaka kauli hiyo ina ukweli mtupu
ndani yake. Ukiangalia wachezaji wote
waliofanikiwa Duniani lazima wawe na vitu
alivyovisema Kocha Lombardi.
Nashukuru Mungu kwa kuniwezesha
kuangalia timu zote zinazoshiriki ligi kuu
Tanzania bara msimu huu.Wakati naendelea
kuangalia ligi hiyo nilikua naendelea kutafuta
wachezaji walioelewa maneno ya hekima ya
Lombardi.Mara nyingi nikawa mbaguzi kwa
kufuatilia zaidi wachezaji wetu(Watanzania)
kuliko wachezaji wa kigeni.
Wachezaji wetu
wengi wamepitwa kabisa na busara za bwana
Lombardi.Wachezaji wengi,waaliyadanganya
macho yangu kwa viwango
vyao.Msuva ,Mkude na Ame Ally angalau
waliupoza moyo wangu.
Nikaamua kulitupa jicho langu pia
kwa hawa wanaojiita ‘Maprofeshino’.Nikafikiri
kuwa wao watanionesha tofauti kidogo.Lakini
nikagundua kuwa maprofeshino hao nao
wengi ni waongo.Katika mechi chache hizi
nilizoangalia sikuona haja ya kuwa na
wachezaji wa kigeni watano katika timu.Eti Jaja
na kwizera nao ni wachezaji wa kulipwa?,Hii ni
hatari.Wachezaji hao hawana msaada kwenye
timu zao kuwazidi wachezaji wetu wa
ndani.
Siwezi kumchezesha jaja wakati kuna
Tegete na Javu kwenye benchi.Siwezi kumpa
nafasi ya hata kukaa kwenye benchi la
wachezaji wa akiba mtu kama kwizera.Azam
nae wanae ‘Profeshino’ Ismail Diarra ambaye
anakula pesa za mzee bakhresa bila kugusa
uwanjani.
Labda kama sielewi maana halisi ya
kuwa na wachezaji wa kigeni hapa
nchini.Lengo kuu la watu hawa ni kuleta
changamoto kwenye ligi yetu na kuwapa
changamoto wachezaji wetu.Lakini wengi wao
hawana tofauti na wachezaji wetu wa
ndani.Matatizo ya wachezaji wengi ni yale yale
aliyoyasema bwana
Lombardi,Kutokujituma,Kutojitoa,Kutokua na
bidii,Kutokuwa wavumilivu na wengine kufikia
hatua hata ya kukosa heshima kwa watawala
wao.Hakuna mengine zaidi ya hayo.
Waswahili wanasema kwenye msafara
wa mamba hawakosi kenge.Licha ya wachezaji
wengi wa timu zetu kukosa mambo muhimu
yanayowafanya wasifikie ubora wao,Lakini
kuna wachezaji ambao wamekua vioo vya
wachezaji wavivu ligi Tanzania bara.Mpaka ligi
ilipofika nimemuona mchezaji mmoja tu
ambaye ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji
wetu na hata hawa ‘maprofeshino’.Si
mwingine ni Emmanuel Okwi.Mguu wa Okwi
hausemi uwongo na wala akili yake
haidanganyi hasilani.
Pamoja na Simba kutofanya vizuri
mpaka sasa lakini Okwi ameonyesha tofauti
kubwa kati yake na wachezaji wengine.Okwi ni
mchezaji
anayejituma ,anayejitoa,mvumilivu,mwenye
bidii,anayejinyima na pia mwenye heshima
kwa mamlaka iliyo juu yake.
Kuhusu kujituma
na kujitoa kwake bila shaka kila mmoja
atakuwa shahidi,Anachofanya Okwi huwa
nakifananisha zaidi na anachokifanya Sanchez
wa Arsenal.Popota mpira ulipo utamkuta okwi
karibu yake.Pale simba wanaposhambulia ujue
mpira upo kwenye mguu wa Okwi.Pale Simba
wanapofunga goli ujue limefungwa au
kutengenezwa na okwi.Hakuna goli la simba
lilofungwa bila mchango wa okwi,Kati ya
magoli 7 simba ambayo wamefunga,Matatu
yamefungwa na okwi,matatu yametengenezwa
na okwi pia moja limefungwa kwa mpira wa
adhabu baada ya okwi kuangushwa karibu na
eneo la hatari la timu pinzani.Kila unapotaja
simba lazima utaje jina la Okwi,Kila
unapozungumzia ligi kuu Tanzania utakua
mchoyo kama hutomzungumzia mwanaume
huyu.
Pia Okwi amekuwa mvumilivu
sana,pamoja na chokochoko zinazoendea
klabuni,tena nyingine zikimhusu yeye dhidi ya
wachezaji wenzake.Lakini aliziba masikio na
kufanya yale yaliyomleta Tanzania ndani ya
uwanja.
Tatizo linakuja kwa wachezaji wetu
wengi kuamini sana kwenye bahati kuliko
juhudi.Tena wengi wataacha kuiga mazuri na
juhudi ya Emmanuel Okwi badala yake
watakaa chini kutafuta mbinu za kummaliza
Okwi.Wachezaji wengi wa Afrika wamejawa na
mioyo ya husuda kwa watu haina ya
Okwi.
Lakini hiyo haitawasaidia kitu.Wachezaji
wetu pamoja na hawa maprofeshino upepo
hawana budi kuwa na roho ya kujituma kama
aliyo nayo Okwi,Inabidi wabadilike na kuona
mpira kama sehemu ya maisha yao,Kujituma
na kuongeza bidii kwao Uwanjani ndio
kutawaletea manufaa kwenye maisha
yao.Wasipofanya hivo wakubali kuendelea
kubuluzwa na profeshino wa ukweli Emmanuel
Okwi,Kwani mpaka sasa ni yeye pekee ndie
amesikiliza na kuzifanyia kazi nasaaa za Vince
Lombardi.
Imeandaliwa Na
Allen Kaijage
0655106767
0 comments:
Post a Comment