Mchezaji wa klabu ya Ac
Bongoville,Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke la kichwani
wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon.
Kipa huyo alifariki alipokuwa akipelekwa
hospitalini baada ya tokeo hilo wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya
Centre Mberi Sportif.Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa amelisimamisha kombora lililopigwa langoni mwake, lakini mshambulizi alipoteza mwelekeo na kumkanyaga Azougoui kichwani.
Mechi hiyo ya siku ya Jumapili ilichezwa Bongoville ambako ni umbali wa kilomita 800 kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon.
"Ni vigumu sana kushuhudia hali hii ya uchungu ,'' ilisema taarifa katika mtandao wa klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment