BEKI
wa Atletico Madrid, raia wa Brazil, Miranda amesema kuwa wanamheshimu
sana kocha maarufu Jose Mourinho, lakini haoni sababu ya Atletico Madrid
kuiogopa Chelsea.
Atletico
Madrid imekuwa tishio baada ya kuwatupa nje ya mashindano FC Barcelona
hatua ya robo fainali na sasa inaongoza ligi kuu nchini Hispania, La
Liga kwa pointi nne mbele ya wakatalunya.
Mafanikio
ya Atletico msimu huu yamewashangaza watu wengi, lakini Miranda amesema
hajui kwanini watu wanajadiliana kama Diego Simeone anaweza kumfunga
Mourinho usiku wa leo katika uwanja wa Vicente Calderon.
“Baadhi
ya watu wanaonekana kushangazwa na sisi kuwatoa Barcelona, nawashangaa
kwasababu Atletico msimu huu imekuwa na ubora mkubwa”. Beki huyo
ameliambia gazeti za The Guardian.
“Kwa
heshima kubwa aliyonayo kocha mkubwa Mourinho tunatakiwa kujipanga.
Tunahitaji kumfanya akose furaha muda wote wa mchezo kadri tuwezavyo”.
“Sioni sababu ya kuiogopa Chelsea. Mbona hatukumuogopa Mreno huyo alipokuwa na Real Madrid kati ya 2010 na 2013”.
“Chelsea ni timu kubwa lakini ilikuwa Barcelona. Wanahitaji kufika fainali yawezekana zaidi yetu” . Alisema Miranda.
Wakati
huo huo, Miranda ameeleza kuwa mechi ya leo ni muhimu sana na watu
wengi wanaelewa kuwa kuna uwezekano wa kikosi cha Simeone kupungua
makali majira ya kiangazi kwasababu wachezaji wao wakubwa wanasemekana
kuondoka hususani Diego Coasta kwenda Chelsea.
“Tunafahamu
kuwa tunaweza kupoteza wachezaji msimu ujao, kwahiyo tunaona hii ni
nafasi yetu ya kufanya vizuri kwa faida ya maisha yetu ya soka. Nafasi
kama hii haiji mara mbili”.
“Kwasababu
ya kutambua hili, tumekuwa tukicheza kila mechi kwa nguvu. Tunadaiwa
sana na mashabiki wetu na kocha wetu Simeone”. Alisea Miranda.
0 comments:
Post a Comment