Facebook

Thursday, 13 November 2014

Wawili wanusurika kifo katika lile jengo jipya la World Trade Centre-Marekani.

Wasafisha madirisha wawili mjini New York
wanabahati ya kipekee kuepuka kifo baada
ya jukwaa walilolitumia kusimama
kuvunjika,na kuwaacha wakining'nia
ghorofa ya sitini na tisa juu ya mji wa
Manhattan ya chini.

Wanaume hao wawili wote ni wasafisha
madirisha ya majengo marefu nchini humo,na
jukwaa hilo lilipokuwa likikatika walikuwa
wamejihami na vifaa vya usalama.

Baada ya taarifa za jukwaa lao kukatika na wao
kubaki wakining'inia kusambaa, walikuja
okolewa na kitengo cha zimamoto baada ya
kukata tundu kwenye mojawapo ya madirisha
ya ghorofa ya sitini na tisa.

Maafisa wa Jengo hilo la One World Trade
Centre wameeleza kuwa wanahisi jukwaa hilo
lilikuwa na matatizo ya kiufundi.
Jengo hilo lina urefu wa mita zaidi ya miatano
na arobaini na ndilo jengo refu zaidi nchini
Marekani.

0 comments:

Post a Comment