Papa Francis ametaka viongozi
duniani wanaoshiriki mkutano wa G20
mjini Brisbane kuwafikiria watu masikini
ulimwenguni.
Amewataka Viongozi hao kupata ufumbuzi wa
kuimarisha hali ya maisha ya watu walio
masikini.
Viongozi wa nchi 20 zilizo na uchumi mkubwa
wanakutana Brisbane nchini Australia mwishoni
mwa juma hili kujadili maswala mbalimbali
yahusuyo uchumi.
Kiongozi huyo wa juu wa kanisa katoliki
amesema pia mkutano huo unatarajiwa kujadili
hali ya mambo mashariki ya kati.
Amewataka viongozi kutotupia kisogo maisha
ya watu yaliyo hatarini na kuonesha matumaini
kuwa mkutano huo utatathimini kuinua maisha
ya watu walio masikini na kupiga vita hali ya
ukandamizaji ambao haukubaliki.
Mkutano wa G20 utaanza siku ya jumamosi.
0 comments:
Post a Comment