Sasa Amber
Rose ameamua kuingia vitani na kina dada wa familia ya Kardashian
/Jenner, baada ya kumchana Kim Kardashian kwa kumuita "Malaya" alipokuwa
akijibizana na Khloe Kardashian jana kupitia mitandao ya kijamii,
Twitter na Instagram.
ishu nzima
imeanza baada ya Amber Rose ambae ni rafiki wa karibu na alikuwa
girlfriend na mama mtoto wa Tyga kumpa makavu Tyga kupitia interview ya
radio aliyofanya, kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mdogo wa kina
Kim "Kylie" ambae ana miaka 17.
Khloe aliamua
kusimama na kumpigania mdogo wake Kylie kwa kuandika tweet kuwakumbusha
watu kuwa Amber Rose alishawahi kukubali kuwa "stripper (mcheza uchi)
tangu alipokuwa na miaka 15".
Baada ya tweet
hiyo sasa, Amber ndio akapamba moto na kuanza kutuma picha zenye
maandishi (Meme|) moja ikiwa ni picha ya Kanye West yenye maandishi
yanayosomeka
"wakati shemeji yako anapomchana X wako kwa kuwa stripper....wakati mkeo ana sex tape".
na hiyo ilikuwa ni tweeet ya pili akimchana Kim, ya kwanza aliandika
Khloe " nitakuwa malaya kusaidia familia yangu kama dada ako mkubwa alivyo malaya kusapoti familia yake."
Drama ziliendelea kati ya Khloe na Amber Rose, ila kama ilihamia kwa
waliokuwa watu wao wa karibu pale ambapo Tyga ambae aliamua kuwa upande
wa dada wa girlfriend wake kwa kum- follow Khloe , huku Rage Bush (X wa
Kim) sasa hivi anam-follow Amber.
0 comments:
Post a Comment