Facebook

Thursday, 19 February 2015

Huyu ndiye 'dikteta' Luis Van Gaal.


1. Javier Hernandez
2. David De Gea
3. Wayne Rooney
4. Shinji Kagawa
5.Juan Mata
Katika orodha hii ya tano bora, wawili hawapo Manchester United hivi sasa  mmoja kauzwa jumla na mwengine kapelekwa kwa mkopo. Mahaba niue kwa jina la kisasa ndivyo mashabiki wa United walivyokuwa wakiwapenda wachezaji hawa duniani kote huku Chicharito akiongoza kwa kupendwa zaidi na mashabiki.

Baada ya hapo Man Utd ikampata kocha mpya ambaye ni Louis Van Gaal. Huyu bwana mkubwa
yeye yupo tofauti kidogo, hatizami mashabiki wanampenda mchezaji gani isipokuwa mchezaji
anaonesha kiwango gani.Aina ya ushangiliaji ya Javier Hernandez pindi anapoweka alama C hakuna shabiki wa United asingependa kuiona tena kwa mwaka huu. Umaarufu wa Shinji Kagawa Japan na bara zima la Asia ilikua ni moja ya mauzo makubwa ya jezi lakini kwa Van Gaal ni tofauti kidogo.

Inawezekana Luis Nani akawa kwenye 10 bora ya mashabiki wanaopendwa zaidi lakini si ajabu kwa
Van Gaal akimlaumu David Moyes kwa nini alimpa mkataba wa miaka mitano. Upo kwenye nchi inayotawaliwa na soka la kiingereza,vyombo vya habari, magazeti na namna wanavyowanadi wachezaji wao kwa bei za gharama lakini bado sikio la Van Gaal alikusikia dawa.

Akawatoa Dany Welbeck na Tom Cleverley na baadae akasema kama Darren Fletcher imeshindikana West Ham basi mpelekeni ata West Brom lakini hapa simtaki.
Hakuangalia uchekeshaji wa Anderson kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wala ingizo jipya kama akina Keane na Lawrence bali ubongo wake ulisimama kwenye siwataki na kuwauza.
"[[Manutd]] KOCHA WA MANUTD VANGAAL ANASEMAJE PALE ANAPOULIZWA KUHUSU VALDES KUANZA MECHI YA KESHO <3 

 [[ManUtd]] VANGAAL"" nimekiona hicho kitu inashangaza jinsi gani vyombo vya habari vinasema kwamba valdes ataanza.sitaki kusemaa chochote kuhusu kikosi changu kiatakachoanza mpaka robo tatu ya lisaa(yaani dakika 45) kabla ya mchezo kuanza <3"
Analetwa Valdez kumpisha Lindegard huku akiwatoa kwa mkopo Jakho na Jesse Lingard.
Huyu ndio kocha mwenye sura ya kidikteta kutoka katika taifa la kiuholanzi. Juan Mata ana
nyota ya kupendwa tangu akiwa Valencia, Chelsea na sasa Man Utd lakin Van Gaal hajali
sana thamani aliyonunuliwa au jinsi anavyowafundisha wachezaji wenzake lugha ya kiingereza kwa wachezaji wa taifa lake na la Argentina.

"I have to wait and see:" msemo anaopenda sana kuutumia kocha wetu mara kwa mara.Ndani ya miezi 8 tu tayari kashatimua wachezaji 10. Anakupa nafasi uoneshe kipaji chako akiona
wa njegere njegere anakuweka kapuni. Usiwe muoga na pengine huwe mbishi kufundisha
klabu yenye mashabiki zaidi ya mil 600. Christiano Ronaldo hupenda kusema Sir Alex Ferguson ni Baba wake wa pili baada ya Baba yake mzazi.
"[[ManUtd]] HATIMAYE MCNAIR ASAINI MKATABA AKIWA NA VANGAAL ATAENDELEA  KUWEPO MPAKA JUNE 2017 <3 <3"
 Si ajabu baada ya miaka mitano tukasikia maneno haya kutoka kwa James Wilson au Pady McNair wakimzungumzia Van Gaal. Luis Nani alikua hana maelewano mazuri na Sir Alex baada ya kutaka mkataba kama ilivyo kwa Wayne Rooney kuchezeshwa kiungo na atimaye kutishia kuondoka. Lakini kwa dikteta LVG hali ni tofauti, wachezaji wapo kimya na hakuna anayethubutu kutoa kauli.

TURUDI KWA FALCAO
Radamel Falcao Mshambuliajo bora aliyetikisa nyavu akiwa na vilabu vya Porto, Atletico na baadae Monaco kwa mabao yake safi na jinsi anavyojituma mpaka kupachikwa jina la El tigre.
Leo hii yupo kwenye mikono ya dikteta LVG ambaye kwa miaka ya nyuma aliwahi kuvua bukta yake mbele ya wachezaji wake na kuonesha kwamba nini maana ya mwanaume kamili.
Kwa matarajio ya wengi mpaka kufika muda huu nafikiri hajafanya kile tulichokuwa tukikusudia.
Amepewa nafasi lakini kwa kiwango chake anashindwa kumaliza dakika 90 na kufanyiwa mabadiliko.
"[[ManUtd]] VANGAAL akizungumza na BLIND wakati wa mazoezi <3"
Tunaweza tukasema tumpe muda lakini tukumbuke mwisho wa msimu tunatakiwa tutoe Pound mil 43 kumchukua jumla. Kwa wachezaji wapya wa United anaweza akawa kwenye 3 bora ya kupendwa zaidi mbele ya Di Maria na Marcos Rojo na inawezekana pia mauzo yake ya jezi yakawa makubwa zaidi kufikia ya Robin Van Persie lakini tukae tukijua hapa tunacheza kamari ya kutembea na boti
kwenye mto wenye mamba.Kitu pekee kinachonipa matumaini ni kuwa nimesimama na Baba asiyetetereka. Angalia uoga wa David Moyes kutomtoa mchezaji yoyote kuhofia kukosolewa na mashabiki na ata kumpa  mkataba mpya Luis Nani lakini kwa Van Gaal alimtoa kwa mkopo na kisha kuanza kumuuza muholanzi mwenzake Alexander Büttner na baadae kutowapa mkataba Rio Ferdinand na Patric Evra.

Moyes alitimuliwa pamoja na ukarimu wake lakini kwa LVG itabaki stori.Ameweza ata kumuonesha Sir Alex kuwa alikosea kumnunua Wilfried Zaha kwa Pound mil 15. Kwa soka analocheza Falcao kwa sasa la kucheza nje ya nafasi aliyoizoea sina shaka na yeye akafata treni la
Mwakyembe.

Kocha muoga ndie anayeweza kumshikilia Falcao ata kama tumefungwa bao 3 na timu inahitaji kushinda lakini kwa Van Gaal sahau kuhusu ulichokionesha tangu ukiwa Porto. Mashabiki tuliomtusi Sir Alex Ferguson kwa kumnyima mkataba wa kudumu Carlos Tevez
basi tusubiri na hii kamari nyingine. Akiwekwa benchi mechi 3 tupige yale mayoe yetu yasiyo
na tija ya Van Gaal Out.

Kujiamini/Ubishi na Ubabe ndio viongozi waUnited wanaupenda.Mata alimsusia Mourinho kwenye mechi na Sunderland lakini kwa Van Gaal anabaki kutizama movie na si ajabu bado anamsifia kupitia blog yake  kila wiki.

SUALA LA FALCAO IPO MIKONINI MWA DIKTETA LVG!!
Unaweza kuwa miongoni mwa 5 Bora kwa
kupendwa na Mashabiki lakini Mfumo wake
Usikupende.

0 comments:

Post a Comment