Baada ya kumsajili Mkenya Victor
Wanyama, Southampton FC ya Ligi Kuu ya England (EPL), imesajili
mchezaji wa pili kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kumpa
mkataba wa miaka miwili na nusu Mganda Bevis Kristofer Kizito Mugabi.
Hata hivyo, beki huyo ambaye wazazi wake wote wawili ni
Uganda, ana uraia wa nchi mbili unaomruhusu kuichezea timu ya taifa ya
Uganda (Cranes) kwakuwa bado hajacheza katika kikosi cha wakubwa cha
timu ya taifa ya England.
Mchezaji huyo amekaririwa katika mtandao rasmi wa klabu Southampton
FC akisema amefurahi kupewa nafasi ya kukipiga katika klabu hiyo baada
ya kuachwa huru na Fulham U18 Julai 2011. Amesema ana matumaini ya
kufanya vizuri kwa kujituma kazini.
“Nimefurahi kupata nafasi hii, nimesaini na kila kitu
kimekamilika. Lengo langu ni kucheza katika kikosi cha kwanza. Nitafanya
kazi kwa bidii mazoezini na wakati wa mechi,” amesema beki huyo mwenye
umri wa miaka 19.
“Klabu imenipa nafasi baada ya Fulham
kuniacha niende zangu. Hii ni sehemu nzuri kwa mchezaji mchanga.
Southampton imetoa wachezaji wakubwa na ninaamini nitakuwa mmoja wao,”
amesema zaidi.
England U17
Beki huyo wa kati aliitwa kwa mara
ya kwanza katika vikosi viwili vya England U17 lakini hakufanya vyema
kutokana na majerha ya goti, amekichezea kikosi cha Fulham mechi nane
akifunga mabao matatu yakiwamo mawili katika mechi mbili dhidi ya two
Chelsea na Everton.
Anaungana na Jordan Turnbull na Jason McCarthy
ambao wote wiki hii wametia saini ya kukipiga katika kikosi cha Martin
Hunter cha U21 kabla ya kupelekwa Kikosi A cha Ronald Koeman.
0 comments:
Post a Comment