Facebook

Wednesday, 18 February 2015

UCHAMBUZI MECHI YA LEO LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA :SCHALKE 04 vs R.MADRID


          Baada ya kushuhudia Psg,Chelsea,Bayern na S.Donesk wakitoa sare katika michezo yao ya hapo jana hii leo pale nchini Ujerumani katika dimba la  Veltins-Arena,Mjini Gelsenkirchen tutashuhudia patashika nyingine katika hatua hii ya 16 bora ambapo Schalke -04 watawakaribisha mabingwa mara 10 wa Uefa ambapo pia ni mabingwa watetezi  Real Madrid.

    Kama unakumbuka Msimu uliopita kwenye hatua kama hii ya Mashindano haya ya Uefa Real ilifanikiwa kuifunga  Schalke iliyokuwa chini ya Jens Keller magoli  6-1 pale pale Ujerumani huku matokeo ya jumla yakiwa 9-2.

     Vijana hawa walio chini ya Roberto Di Matteo aliyejiunga na timu hiyo 07/10/2014 na mkataba wake kuisha 30/06/2017 ,kocha pekee aliye ipatia Chelsea ubingwa wa Uefa-2012 ataingia katika mchezo huu kwa dhamira ya kufuta ubabe wa Real mbele ya timu yake, ingawa pia anakabiliwa na majeruhi ya baadhi ya wachezaji wake kama Draxler, Goretzka na J Farfan.

    Kwa upande wa muitaliano mwenzake kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti yeye katika mchezo huu atawakosa  James Rodriguez, Luca Modric na Sergio Ramos.
  Licha ya safu yake ya ushambuliaji (BBC ) kutokufanya vyema tangu mwaka 2015 uanze lakini bado safu ya ulinzi ya Schalke-04 wanakazi nzito ya kuwadhibiti.

   Kama ilivyo kawaida Ancelotti mara nyingi mbinu zake ni kushambulia zaidi kutokana na aina ya wachezaji alio kuwa nao huku mpinzani wake Di Matteo mara nyingi amekuwa akitumia mbinu ya kuzuia zaidi na kushambulia kwa kushtukiza.

   Ngoja tusubiri kama yatajiri ya msimu uliopita au vinginevyo.
      NB::: Roberto Di Matteo ndiye kocha pekee muitaliano kuifundisha Schalke-04.

Imeandaliwa na....................
                                             Hero Sangatiti
                                 Choikangta.ckt@gmail.com
                                          0765 691418

0 comments:

Post a Comment