Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli leo
amepokea kivuko kipya cha MV Dar es Salaam
chenye uwezo wa kubeba abiria 300!.
Kivuko hiki kipya kitatoa huduma ya usafiri
kati ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao wa
Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo.
Kivuko cha
MV Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko
kivuko chochote Afrika ya Mashariki na hasa
mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika
ya Kusini.
Leo Waziri wa Ujenzi Dk.Magufuli
amekipokea rasmi kivuko cha MV DAR ES
SALAAM kama utakavyokiona katika picha
mbalimbali. Mbali na Dk.Magufuli wengine
waliohudhuria mapokezi hayo ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki
Saidi, RAS wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Balozi H.Mlango
(Katibu Mkuu Mstaafu - Ujenzi) ambaye ni
Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA, Mkurugenzi
Mtendaji wa TEMESA, Kaimu Mkurugenzi wa
Bandari Mhandisi Matei, Meneja wa Bandari
ya Dar es Salaam
Itakumbukwa waziri Magufuli amekuwa
akiahidi kufanya jitihada za kupunguza
msongamano katika Jiji la Dar es Salaam
ikiwa ni pamoja na kununua kivuko
kitakachofanya safari zake katika mwambao
wa bahari ya Hindi mpaka Bagamoyo.
Kivuko hiki mkombozi wa wakazi wa Jiji la
Dar es Salaam kimejengwa na kampuni
kutoka Denmark kwa gharama ya shilingi
(Tanzania) bilioni 7.9.
Sifa kubwa ya kivuko cha MV DAR ES
SALAAM:
1. Kina uwezo wa kubeba abiria kati ya 306
waliokaa hadi 400,
2. Kina spidi (speed) kubwa kuliko vivuko
vyote Tanzania na hata Afrika ya Mashariki
3. Kina ghorofa mbili (Two Floors)
4. Kwa ndani kina makochi mazuri kabisa ya
kisasa ikiwa pmoja na life jacket
5.Kina tekinorojia ya kisasa kabisa ya
Nivigation.
Picha za matukio mbalimbali pindi
Dk.Magufuli akikipokea kivuko:
0 comments:
Post a Comment