Evgenia Svidirenko
Mwanamke mmoja huko Urusi amefariki
dunia baada ya kutumia simu aina ya Iphone akiwa bafuni kwake wakati
akiwa anaoga huku akiwa anapekua ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Kwa mujibu wa jirani wa mwanamke huyo, Evgenia Svidirenko mwenye umri wa miaka 24 alikuwa akitazama ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kama Facebook lakini kwa taifa la urusi unaoitwa VKontante kabla ya kifo chake kutokea.
Jirani huyo ambaye walikuwa wkaiishi na marehemu Evgenia kwenye jengo moja anayeitwa Yaroslav Dubinina
mwenye umri wa miaka 23, aliona mwanadada huyo amechelewa kutoka bafuni
baada ya kukaa huko kwa muda mrefu na baada ya kwenda kumtazama
alimkuta akiwa anaelea kwenye kibeseni cha kuogea huku akiwa tayari
amefariki dunia.
Mwanadada huyo aliyeshuhudia tukio hilo
anasema kuwa kitu cha kwanza alichoona ni simu yake aina ya Iphone
ambayo ilikuwa kwenye chaja ya simu ambayo ilikuwa chini ya beseni la
kuogea ambapo marehemu alikuwemo ndani yake.
Jirani huyo alisema kuwa wakati
alipoukuta mwili wa Evgenia ulikuwa bado unatetemeka kutokana na shoti
ya umeme ambayo ilianzia kwenye chaja ya simu.
Polisi nchini Urusi bado wanafanya
uchunguzi kutambua kwanini chaja hiyo haikukata umeme wakati ilipopata
shoti na pia wanaifuatilia simu ya marehemu kuweza kutambua kama ni
bidhaa iliyosajiliwa toka kampuni ya Apple.
Kifo cha Evgenia
kinakuja siku chache tu baada ya tukio lingine la kifo cha binti mdogo
wa umri wa miaka 16 ambaye alifariki dunia kwa mtindo huu huu akiwa
anachaji simu yake akiwa bafuni ambapo alipigwa na shoti ya umeme wakati
akiwa anaoga.
Mwezi Agosti mwaka jana mamlaka nchini
China ziliripoti tukio kama hili baada ya kijana mdogo wa umri kati ya
miaka 11 na 17 alipopigwa shoti ya umeme wakati simu yake aina ya iPhone
ilipokuwa imechomekwa kwenye chaja isiyo rasmi.
Kijana huyo Wu Weiyan
alikutwa na dada yake akiwa amefariki dunia baada ya dada huyo kusikia
harufu ya kitu kikungua na alipokwenda kutazama alikuta ndugu yake akiwa
amefariki dunia .
Kampuni ya Apple hapo awali imewahi
kuonya juu ya hatari za matumizi ya chaja zisizo rasmi ambazo
hazijatolewa na wauzaji rasmi wa bidhaa za Apple.
0 comments:
Post a Comment