
Klabu
ya Barcelona ya nchini Hispania leo imebadili jina la uwanja
wake wa mazoezi na kuupa jina la kocha wa zamani wa
klabu hiyo Tito Vilanova
aliyefariki Aprili mwaka jana kwa ugonjwa wa kansa ya koo.
Uwanja huo uliokuwa unafahamika kwa jina la
Joan Gamper umepewa jina hilo ikiwa ni sehemu ya kumuenzi kocha huyo aliyeifundisha timu hiyo msimu wa 2012/2013.
Zoezi
hilo la
uzinduzi limefanyika leo asubuhi likuhudhiliwa na wachezaji na viongozi mbalimbali wa timu hiyo.

Pia leo asubuhi kikosi cha kwanza cha Barcelona kimeutumia uwanja huo kufanya
mazoezi wakati
wakijiandaa na mchezo wa La
Liga hapo kesho dhidi ya
Malaga kwenye dimba la
Camp Nou.
0 comments:
Post a Comment