Friday, 20 February 2015
KOMBE LA DUNIA 1994 NA KUMBUKUMBU YA ANDRES ESCOBAR
Katika uumbaji Mwenyezi Mungu alimpatia kila mwanadamu "UTASHI" yaani uwezo wa kutambua na kujitambua yeye mwenyewe, vilevile ni uwezo wa kutambua jema na baya,kuchambua na kupambanua vitu mbalimbali katika mazingira yanayomzunguka.
Ukiachana na Utashi Mwenyezi Mungu alimuumbia mwanadamu ubongo wa mbele wenye uwezo wa kumsaidia mwanadamu huyo katika kumbukumbu.
Leo hii nimeuhangaisha kidogo ubongo wangu kukumbuka tukio la mwaka 1994
Michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1994 kamwe sitoweza kuisahau katika maisha yangu ya kufuatilia soka.
Michuano hii siwezi kuisahau kwa sababu kubwa moja sikuwahi kuishuhudia "LIVE" kwa sababu kipind hcho nilikuwa mdogo ila kipindi nakuwa nilikuta ile mikanda mikubwa ya video za michuano hiyo "VHS" ambapo baba alikuwa anatumia kuangalia na sisi ndo tulikuwa tunaangalia.
Naweza nikasema kupitia mikanda mikubwa ya "VHS" ya michuano ya mwaka 1994 ndiyo nilianza kupenda mpira na timu yangu ya kwanza kuipenda ni timu ya taifa ya BRAZIL
Michuano hiyo bingwa alikuwa BRAZIL aliyemfunga ITALY kwa mikwaju ya penalti mechi ya fainali.
Hii ilikuwa fainali ya marudio ya mwaka 1982 ambapo Brazil alimfunga pia ITALY katika fanali.Michuano ya mwaka 1994 tulishuhudia ROMARIO akiwa mchezaji bora wa michuano.Pia ndiyo ulikuwa mwisho wa Utawala wa mfalme DIEGO MARADONA.Sweeden walikuwa katika kiwango bora zaidi kutokea na katika michuano hii walishika nafasi ya tatu.
Kwa mara ya kwanza bara la AFRIkA walipewa nafasi ya timu tatu.Timu zilizowakilisha zilikuwa NIGERIA ambao walikuwa mabingwa wa AFRIKA mwaka huo, CAMEROON na MOROCCO.
NIGERIA ilikuwa inapewa nafasi ya kufika mbali kutokana na ubora wa timu yake.Ila walitolewa na ITALY.kwa goli 2-1 mechi ambayo Nigeria waliongoza kwa kipindi kirefu lakini ROBERTO BAGGIO alikuja kuwaua kwa kupiga misumari miwili.
Katika mashindano haya kuna timu ilikuwa inapewa sana nafasi.Nayo ni COLUMBIA.Ilikuwa inacheza mchezo wa kuvutia sana.Lakini ilitoka kipindi cha makundi, ikishika mkia kwenye kundi lao.Mechi ya mwsho ya kundi ilikutana na USA.
USA walishinda goli 1.Goli la kujifunga la beki kisiki ANDRES ESCOBAR.
Wacheza kamari wengi wazee wa kubeti waliweka mizigo yao kwa Colombia kupita hatua ya makundi kwani timu zote zilikuwa na nafasi ya kupita kwa kundi hilo.
ANDRES ESCOBAR alichana mikeka ya watu wa gambling baada ya mechi hiyo akiwa baa moja ANDRES.ESCOBAR alipigwa risasi na watu waliosadikika ni wacheza kamari.ANDRES ESCOBAR alikufa wiki chache kabla ya ndoa yake na mchumba ake wa USA.
RIP ANDRES ESCOBAR.
Imeandaliwa na ............
Martin kiyumbi.
0 comments:
Post a Comment