Facebook

Saturday, 21 February 2015

Millard Ayo apiga hatua kubwa sana,Afungua studio yake ya Radio





Katika maisha mwanadamu yoyote yule anapigana ili kujiletea maendeleo yake yeye mwenyewe na kwa nchi kiujumla.
Maendeleo anayoyapiga kijana wa kipekee sana ambaye amekuwa mfano wa kuigwa katika jamii,Mtangazaji wa Clouds Fm,Millard Ayo ni jambo la kufurahisha sana na kutia moyo.Ni baada ya kufungua studio yake yeye mwenye.Hizi picha ni baadhi ya alizozipost katika ukurasa wake wa facebook #Millard Ayo
 
 Kupitia ukurasa wake wa facebook Millard Ayo alikuwa na haya ya kusema.

"Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu na leo Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu wangu, nilianza kuidizaini hii na baadae watu wangu @francis_ayo na @abdul8819 wa @pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa ‪#‎TZA‬ !! thanks kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na @sebamaganga wamenipa nguvu na nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa."

Ni jambo la kufurahisha sana,vilevile na sisi kama BantuTz.com hatuko nyuma kwani hapo mwezi wa sita tunafungua mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi ambao utaleta mapinduzi ya aina yake.

0 comments:

Post a Comment