
SWANSEA vs MANCHESTER UNITED 18:00
Kule Liberty stadium Swansea watawakaribisha Man United mara ya mwisho Man United kushinda katika uwanja huo ilikuwa msimu uliopita kwa ushindi wa goli 4-1 lakin msimu huu katika mchezo wa kwanza Man U walifungwa 2-1 pale Old Trafford.

Garry Monk bado timu yake haina matokeo mazuri sana hasa upande wa ushambuliaji umeonekana butu tangu Bonny atimkie Etihad lakini leo walau atapata faraja baada ya kiungo wake kutoka Iceland aliekuwa moja ya wauaji pale Old Trafford Sigurdsson akirejea dimbani lakini Kyle Bartley hatokuwepo.

Ngoja tusubiri leo kama ni kina Ki-Sung-Yieng, Shelvey au ni Rooney,Di maria.
Katika michezo mitano iliyopita Swansea, W-1,D-1,L-3 huku Man, W-4,D-1.
-----------------------------------------------------------------------------------
CHELSEA vs BURNLEY 18:00 JIONI
Baada ya kutoka sare na Psg ktk mchezo wa 16 bora ya Uefa vinala wa Epl Chelsea watakipiga na Burnley timu inayoshika nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi.
Kwa upande wa Chelsea hakuna majeruhi katika kikosi cha kwanza na upangaji hauto badilika sana.

Katika michezo mitano iliyopita ya timu zote mambo yapo hivi.
Chels- W-3,D-2 huku Burnley. L-4,D-1.
---------------------------------------------------------------------------------
CRYSTAL PALACE vs ARSENAL 18:00 JIONI
Katika 'London derby' leo hii Vijana wa Allan Pardew watawakaribisha vijana wa mzee Wenger pale Selhurst park katika mchezo wa ligi kuu
Kuelekea mchezo huo C. Palace watamkosa Chamakh lakini pia Sanogo hatocheza kwani yupo kwa mkopo akitokea Arsenal huku kwa upande wa mzee Wenger bado atakosa huduma ya Ramsey,Arteta na Debuchy walio majeruhi huku Wilshere na Chamberlain wakirejeaa.

C. Palace-W-2,D-1,L-2 na upande wa Arsenal ni W-4, L-1 hayo ni yale yatakayo jiri pale London.
----------------------------------------------------------------------------------
MAN CITY vs N'CASTLE 20:00 USIKU
Pale Etihad stadium majira ya saa mbili na nusu baada ya kutoka kuwafunga Stoke goli 4-1 Pellegrin leo atatafuta point 3 muhimu mbele ya N'castle inayo nolewa na John Carver ilikuendelea kuwapa presha Chelsea.


Leo N'castle watamkosa Tylor ,Cheik Titote na Dumet huku Rolando Aarons ikiwa haijulikani kama atakuwa fiti leo, mara ya mwisho N'castle kushinda pale Etihad ilikuwa chini ya Pardew katika mchezo wa Capital One kwa ushindi wa goli 2.
Kumbuka katika michezo 6 dhidi ya N'castle Yahaya Toure amefunga magoli 5 ngoja tusubiri kama leo ni City au N'castle pale Etihad
NB:: Man City imefunga magoli 31 katika kipindi cha pili ndani ya dakika 90 ikiwa ni kiwango cha juu ktk ligi kuu.
---------------------------------------------------------------------------------
Imeandaliwa na................
CHOIKANGA
Choikangta.ckt@gmail.com
WhatsApp -0765 691418
0 comments:
Post a Comment