Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Wednesday, 20 January 2016

Ratiba ya Michezo Mbalimbali ya soka Barani Ulaya leo Jumatano

RATIBA YA SOKA LEO JUMATANO 20/01/2016
★English FA Cup 3rd Round Replay
10:45 PM - Leicester City vs Tottenham Hotspur
11:00 PM - Liverpool vs Exeter City

★Spanish Copa del Rey
10:30 PM - Celta Vigo vs Atletico Madrid
11:00 PM - Athletic Bilbao vs Barcelona

★Italian Serie A
10:45 PM - Sassuolo vs Torino

★French Coupe de France
8:30 PM - Chambly Thelle FC vs Lyon
8:30 PM - Concarneau vs Troyes
8:30 PM - Evian Thonon Gaillard vs AS Monaco
8:30 PM - Mantes 78 vs Nantes
8:30 PM - Trelissac FC vs Lille
9:30 PM - Boulogne vs Lorient
11:00 PM - Marseille vs Montpellier

★Italian Coppa Italia
10:45 PM - Lazio vs Juventus

~Abel Alvaro

Taarifa kwa Umma Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa kuhusiana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha Nchini.

Monday, 18 January 2016

Real Madrid,Barcelona zapeta ligi Kuu Hispania kwa ushindi mnono.

Klabu ya soka ya Real Madrid imefanikiwa kuizamisha Sporting Gijon katika mwendelezo wa ligi kuu ya Hispania kufuatia ushindi mnono wa mabao 5-1 ambayo yamefungwa na wachezaji Gareth Bale bao 1 , Chirstiano Ronaldo mabao 2 pamoja na Karem Benzema akifunga mabao 2.

Na klabu ya Barcelona imekwea hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kufuatia ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Althltic Bilbao,mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Lionel Messi , Neymar da Silva Santos , Luis Alberto Suárez , na Ivan Rakitic .

Man United yapata ushindi mwembamba nyumbani kwa Liverpool.

Wayne Rooney alifunga bao lake la kwanza katika uwanja wa Anfield tangu mwaka 2005 na kuiwezesha timu yake kupanda katika msimamo wa ligi ya Uingereza.

Liverpool ilitawala mchezo huo huku mkwaju wa Emre Can ukipanguliwa na kipa David De Gea.Lakini Liverpool walilazimika kulipa makosa yao wakati Wayne Rooney alipofunga mkwaju mzuri akiwa karibu na eneo la hatari baada ya kichwa cha Marouane Fellaini kugonga mwamba wa goli.

Wageni hao ambao sasa wako katika nafasi ya tano walikuwa hawajashambulia hata mkwaju mmoja katika lango la Liverpool hadi mshambuliaji huyo wa Uingereza alipofunga bao hilo la ushindi.Liverpool itasalia katika nafasi ya tisa ikiwa alama sita nyuma ya Manchester United.

Matokeo ya Soka katika Ligi mbalimbali barani Ulaya kwa Michezo ya Jana.

MATOKEO YA SOKA JANA JUMAPILI 17/01/2016:
••Barclays Premier League
Liverpool 0-1 Manchester United
Stoke City 0-0 Arsenal

••Spanish Primera División
Valencia 2-2 Rayo Vallecano
Real Madrid 5-1 Sporting Gijon
Getafe 3-1 Espanyol
Las Palmas 0-3 Atletico Madrid
Barcelona 6-0 Athletic Bilbao

••Italian Serie A
Genoa 4-0 Palermo
AS Roma 1-1 Hellas Verona
Bologna 2-2 Lazio
Carpi 2-1 Sampdoria
Chievo Verona 1-1 Empoli
Udinese 0-4 Juventus
AC Milan 2-0 Fiorentina

••French Ligue 1
Lorient 0-2 AS Monaco
Caen 1-3 Marseille
St Etienne 1-0 Lyon

~Abel Alvaro

Serikali yatoa ratiba mkutano wa Wazalishaji Umeme Wazalendo.

WAZALISHAJI UMEME WAZALENDO 

Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM, Jumatatu, 18-1-2016: WIZARA ya Nishati na Madini imeandaa mkutano wa wazalishaji umeme wazalendo unaotarajiwa kufanyika jijini Dar.

"Wizara itatoa ratiba kwa makampuni ya wazalendo kuja kutoa mapendekezo ya miradi yao tarehe 15-17 February 2016", alisema Prof Muhongo.

Prof Muhongo alisema mkutano huo utahusu miradi yote ya uzalishaji umeme kutoka vyanzo mbalimbali nchini.

Taarifa ya Waziri ilisema vikao na wadau hao vitafanyika katika ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini.

"Iwapo kuna WABIA  kutoka nje ya nchi tungalipenda na hao WABIA wawepo kwenye vikao", alisema Waziri.

Tanzania itazalisha umeme wake kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Gesi Asilia (natural gas), Maji - Maporomoko (Hydro), Makaa ya Mawe (coal) na  Nishati Jadidifu  (Renewable Energies).

Vyanzo vingine ni Jua (solar), Upepo (wind) , Jotoardhi (geothermal) na  Mawimbi (tides&waves).

Alikitaja chanzo kingine ambacho mi maarufu kwa wananchi wengi wa kawaida kuwa ni Bio-Energies ambayo ni biogas (gesi ya kinyesi) na biomass (kuni).

Bantuz.Com

Sunday, 17 January 2016

Serikali yalifungia gazeti la 'Mawio'.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”.Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati alipokutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nnauye amesema kuwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016 Serikali imelifuta Gazeti hilo ikiwa ni uamuzi uliotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).

Alieleza kuwa, hatua ya kulifuta gazeti hilo inazuia pia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.‘’Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu’’, alisema Nnauye.

Aidha, alifafanua kuwa hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari,  2016  kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.

‘’Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na Mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya  mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti,Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo’’ alisisitiza Mhe.

Nnauye.Katika hatua nyingine, Waziri nape alitoa pongezi kwa Vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi. ‘’Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja  na wahariri wa magazeti ya; Mwananchi Tanzania, Mtanzania, The East African, Magazeti ya Daily News na Habari Leo, Uhuru na mengineyo’’, alisema Mhe. Nnauye

WAZANZIBARI MNALIJUA HILI KUHUSU MAALIM SEIF?

Na Bollen Ngetti
Kuna baadhi ya wasomaji wa maandiko yangu wameendelea kunilaani na kudai ninamshambulia Maalim Seif na huenda nina chuki binafsi na mwanasiasa huyo wa Z'bar. Wengine wameenda mbali na kudai ninatumika! Ninachojua ni kwamba unaweza kumzuia ndege asitue juu ya kichwa chako lakini kamwe huwezi kumchagulia pa kujenga kiota chake. Sina chuki na Seif, situmiki maana si hulka yangu. Tatizo ni kuwa mimi ni muumini wa dhana ya ukweli hata kama ni mchungu kama "kloriti" ya Masai nitausema tu. Kuna baadhi ya Watu Z'bar kwa sasa hawataki kabisa kuambiwa ukweli maana unawachoma hadi kwenye mfupa.

Wengine wamenitukana huku wengine wakinitisha nakadhalika. Niwaambie tu kuwa nitaacha kusema tu ninachojua ni uongo lakini ukweli ninausema hadi mwisho wa uhai wangu maana bila kuyasema mambo haya mtaendelea kuishi ndani ya boksi jeusi.

Maalim Seif hana mkosi wa kumfanya asiwe Rais wa Z'bar isipokuwa ukweli mchungu ni kwamba amekosea hesabu katika mbio za kusaka Urais toka 1995, 2000,2005,2010,2015 na sasa 2016 na sasa wakati umeshamtupa mkono. Hawezi tena. Niharakishe kusema kwamba Seif anatafunwa na mzimu wa dhambi ya kumsaliti mwalimu wake mkuu wa siasa Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi na labda hili ndilo limemfuja.

Z'bar kwa asili ya Mila, jadi na ilivyojengeka na kuaminiwa na wengi ni kuwa huwezi kumsaliti, kumdharau ama kumdhihaki mwalimu wako wa skuli, amali, madrasa, au sheikh wako wa ilmu au wa kitwanga maana kufanya hivyo ima utapungukiwa na ibra njema au hutofanikiwa katika mbio za kusaka tija au mafanikio ya maisha yako.

Wengi hatujui ama hatutaki kujua ni kwa namna gani Seif aliweza kupenya hadi leo kuwa MAALIM na kuwa mwanasiasa mashuhuri kama walivyokuwa Profesa Abdulrahman Babu au Ali Muhsin Al-Barwan.

Mzee Jumbe alifanya ujasiri wa aina yake kumteua Seif kijana kutoka Pemba kuwa Waziri wa Elimu katika wakati wa siasa za mbinde kufuatia Mapinduzi ya damu yaliyofanywa na wakulima na wakwezi ambao wengi hawakuwa na elimu lakini pia ni kufuatia kuuawa kwa Rais Amani Karume aliyepigwa risasi na Homoud Mahmoud kijana mwenye asili ya uchotara wa ki-Arabu kama Maalim Seif kutoka Pemba.

Ikumbukwe kuwa ndani ASP (sasa CC.) kulijengeka dhana iliyojenga kiongozi wa ZPPP Mohammed Shamte Hamad mwenye asili ya Pemba kulikataa pendekezo la ASP mwaka 1963 la kumtaka aunde Serikali ya mseto yenye sura ya ki-Afrika lakini hakuliafiki na kuamua kupeleka viti vyake kwa ZNP-HIZBU na kuunda ZPPP/ZNP zikiwa na asili ya Upemba kupambana ASP (weusi wa Unguja).

Ni kweli kuwa Jumbe alihitaji wasomi maana alikuwa ni msomi lakini kumchukua mwanasiasa kutoka Pemba kumfanya mtu wa karibu ulikuwa ni ujasiri maana iliaminika kuwa mtu kutoka Pemba asingeweza kuwa mtetezi wa kweli wa mapinduzi ya mwaka 1964 (rejea maadhimisho ya juzi).

Hata hivyo jumbe hakujali pamona na kwamba hata Unguja kulikuwepo na vijana wasomi lakini Jumbe alitaka kuwaunganisha Wazanzibari na kuondoa dhana ovu ya u-Pemba na u-Unguja ambao sasa Seif anashutumiwa kuufufua kwa Ari mpya. Hata sasa Seif anashutumiwa kuwa machotara wa ki-Arabu ndio wenye sauti ndani ya CUF na ndio maana chama hicho kimeota mizizi Pemba tofauti na CCM iliyopo pande zote hata hakina nguvu kubwa kwa Pemba.

Karatasi za SIRI za Rais Jumbe zilizokuwa na mikakati ya kudai Serikali 3 ziliibwa ofisini kwa Jumbe zikakutwa mezani kwa Nyerere Dodoma, NEC huku Seif akiwa msatari wa mbele kumwambia Nyerere, "Mwl ukitaka muungano uendelee kumwondoe Jumbe kwenye Urais" na hata sasa kina Seif Khatib wanasema wazi, "Seif aliwasaliti Wazanzibari kupata kiti Chao UN nk."

Miongoni mwa wasemaji wakubwa katika mkutano huo wa NEC kutaka Jumbe abanduliwe nyadhifa zake abaki kapuku alikuwa Maalim Seif kwa mategemeo ya kutwaa Urais. Hapo mwanafunI anaamua kumsulubu mwalimu wake hadharani!

Mwalimu wake aliyemfanya agile hapo juu hadi sasa anataka avuliwe nguo hadharani. Hii kwa Wazanzibari ni laana mbaya sana na ishangaze leo huyo huyo aliyekataa serikali 3 leo anasafiria nyota ya Jumbe ya Serikali 3. Tuiteje hali hii kama si unafiki na uzandiki? Seif akawa kama Petro (Biblia) alivyomkana Bwana Yesu aliyekuwa kipenzi na msaidizi wake wa karibu.

Zama za Jumbe imebebeshwa lawama nyingi kuwa Wapemba walinyimwa elimu huku Waziri wa Elimu akiwa ni Mpemba. Mdaini elimu yenu.

Leo wapambe wanaliangalia kundi la machotara kutoka Pemba wakimuunga mkono Seif lakini hawaliangalii abadan lile la Waafrika weusi titii lilipo Unguja likilinga na kujenga hofu iliyowagusa Enzi za Maalim Seif akiwa Waziri wa Elimu na usaliti alioufanya dhidi ya Mzee Jumbe.

CUF bado ina nafasi ya kumpata mgombea Urais anayeweza kuunganisha visiwa vya Pemba na Unguja na ijulikane kuwa Maalim anatafuta Urais kwa ajili ya machotara wa Pemba na si kuunganisha Wazanzibari maana historia ni mwalimu mzuri. Mkataeni Seif kwa usalama, amani na umoja wa visiwa vya Zanzibar. Nawasilisha.

BNgetti 15/01/2016