Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday 27 September 2014

RATIBA YA MECHI LIGI KUU YA UINGEREZA .

BantuTz SPORTS

RATIBA YA MECHI LIGI KUU YA UINGEREZA LEO HII

14:45
Liverpool vs Everton

17:00 Chelsea vs Aston Villa

17:00
Crystal Palace vs Leicester City

17:00
Hull City vs Manchester City

17:00
Manchester United vs West Ham United

17:00
Southampton vs Queens Park Rangers

17:00
Sunderland vs Swansea City

19:30
Arsenal vs Tottenham Hotspur

JUMAPILI
18:00 
West Bromwich Albion vs Burnley

JUMATATU
22:00 Stoke City vs Newcastle United

Powered by::www.bantutz.com::

Bantu Social Network inakuja hivi Karibuni.

~Katemi Methsela.

Friday 26 September 2014

Mchinjaji wa kundi la Islamic State abainika.

Mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey
amesema kitengo chake kimemtambua
mtu ambaye huficha sura yake ambaye ni
muuaji,ambaye pia huoneshwa wakati
akiwachinja mateka watatu kwenye video
inayo nadi wanamgambo wa dola ya kiislam
IS.

Pamoja na hayo Bwana Comey amegoma
kuutaja uraia wa mtu huyo ama hata kutaja
jina lake,ingawa imeshajulikana lafudhi ya mtu
huyo kuwa ni mwenye asili ya mji wa London,
na Comey amesema kwamba utambuzi wa mtu
huyo umefanikishwa kwa msaada mkubwa wa
marafiki wa kimataifa.

Muuaji huyo wa waandishi James Foley na
Steven Sotloff pamoja na mfanyakazi wa
kujitolea David Haines walipigwa picha ya
video na kuwekwa kwenye mitandao na
wanamgambo hao wa dola ya kiislam na
kusaidia kufanya maamuzi juu ya mipango ya
wapiganaji wa jihad.

Chanzo:BBC

Inakisiwa kuwa zaidi ya raia 3000 kutoka Ulaya ni wafuasi wa Islamic State

Idadi ya raiya kutoka Uropa wanaojiunga
na kundi la wapiganaji wa Kiislamu nchini
Syria na Iraqi imeongezeka hadi zaidi ya
3,000 kulingana na mkuu wa kitengo cha
kupambana na ugaidi bara la ulaya.
Gilles de Kerchove ameonya kuwa
mashambulizi ya hewa yanayofanywa na nchi
za Magharibi yataongezea hatari ya
mashambulizi ya kulipiza kisasi katika bara la
Ulaya.
Vikosi vikiongozwa na Marekani vimetekeleza
mashambulizi ya hewa mia mbili dhidi ya
wanamgambo wa Islamic state wa Iraqi tangu
Agosti na Jumatatu iliyopita wakaanza kulenga
wale walioko Syria.
Bunge la Uingereza litapiga kura kwa
mashambulizi ya hewa dhidi ya Iraqi siku ya
Ijumaa.
Kundi la IS wameteka sehemu kubwa za Syria
na Iraqi katika miezi ya hivi karibuni.
CIA inakisia kuwa kundi la IS linaweza kuwa na
wapiganaji mpaka 31,000 huko Iraq na Syria,
mara tatu zaidi ya wale waliohofiwa.

Mashambulizi haya yaliotekelezwa siku ya
Alhamisi na ndege za Marekani, Saudi na UAE
zilikuwa zinalenga mitambo 12 ya kusafisha
mafuta nchini Syria .
Msemaji wa Pentagon Rear Admiral John Kirby
alisema kuwa kusudi la mashambulizi haya ya
hewa halikuwa kuwaua wanamgambo hao lakini
ilikuwa kuharibu maeneo ambayo yalikuwa
yakiletea kundi hilo fedha kupitia soko nyeusi.
Baadaye, siku ya Ijumaa, wabunge wa
Uiungereza wataulizwa kuunga mkono
mashabulizi dhidi ya wanamgambo wa IS Iraqi
lakini sio Syria.

Chanzo:BBC

Thursday 25 September 2014

Lifahamu Eneo la "kafara" Bermuda Triange


Bermuda triangle ni eneo katika uso wa Dunia ambalo linahusishwa na masuala mbalimbali ya nguvu za maajabu, ni eneo ambalo maelfu ya watu wamepoteza maisha, ndege na meli nyingi sana zimezama katika eneo hilo pasipo kujulikana zinaelekea wapi.

Wanasayansi wengi wamepoteza pesa zao pasipo kutoa majibu kuhusu maajabu ya eneo hilo na kila aliyeenda hajafanikiwa kutoka na inasemekana Zaidi ya ndege na meli 1000 zimepotea kwa mud wa miaka 500. Bermuda Triangle inapatikana pwani ya kusini mashariki ya marekani na iko katika bahari ya Atlantic.

Kona zake huunda pembe tatu ambazo ni Miami huko marekani, San Juan Nchini Puerto Rico na Buermuda katika kisiwa kaskazini mwa kisiwa cha Atlantic. Ajali/mgongano kati ya kimondo na dunia Inasemekana kuwa Bermuda triangle ilitokea baada ya Dunia kugongana na kimondo huko angani miaka 11,000 iliyopita.

Mgongano huo ulitokea katika eneo la bahari la Dunia na kusababisha bahari kuzama kwa futi 10,000 chini ya usawa wa bahari. Kimondo hicho kiliacha mionzi ambayo ambayo husababisha ndege kupoteza uelekeo inapofika katika eneo hilo na kuzamsha meli, ndege pamoja na binadamu.

Viumbe vigeni viishivyo sayari nyingine (aliens). Inasemekana kuwa viumbe viishivyo angani, huwa vinakaa aktika eneo hilo la Bermuda triangle na hilo ni kama Mecca yao. Viumbe hao wana teknolojia ambayo hukinzana na teknolojia yetu ya Duniani, kwahiyo basi ndege, meli pamoja na binadamu wanapopita pale huvutwa na kani ya uvutano ambayo ni kubwa sana toka kwa wale viumbe waishio katika ilo eneo hilo la Bermuda.

Kituo cha majaribio ya silaha. Inasemekana serikali huwa zinajaribia silaha ambazo zinakuwa zimetengenezwa na uangalizi wa silaha hizo, pia inasemekana kwamba serikali ikishirikiana na viumbe watokao sayari (Aliens) zingine huhusika katika majaribio hayo.

Na hiyo teknolojia ni kubwa kiasi cha kukinzana na teknolojia ya duniani na hatimaye kusababisha madhara kwa meli na ndege pia.

Mji uliopotea Inasemekana katika eneo hilo kulikuwa na mji wa kale chini ya maji katika bahari ya Atlantic, ulioitwa Atlantis, mji huo ulikuwa umejengeka kwa barafu ambazo zilikuwa kama kioo ambazo pia zilikuwa ni chanzo cha nishati.

Na huo mji ulisahaulika milele kwahiyo basi Bermuda iko kwenye huo mji uliozikwa kitambo ambapo kuna kani kubwa ambayo huharibu meli na ndege.

Kituo cha Maharamia Inasemekana Bermuda ni eneo kwa ajili ya maharamia kufanya kazi zao, maharamia hao ni wale wanaojulikana kwa bendera nyeusi zenye picha ya fuvu.

Lakini dhana hii imeshindwa kuelezea ni kwanini ndege na meli huwa zunapotea katika eneo hilo kwani wachunguzi wa mambo wamehusisha na utekaji nyara wa meli baharini ambao hufanywa na maharamia hao.

Volkano. Inasemekana Volkano pamoja na gesi ya methane katika eneo la Bermuda hupunguza mgandamizo wa maji katika eneo hilo na kufanya meli kupoteza uwezo wa kuelea na hatimaye kuzama.

Eneo hilo mlimekuwa likitoa gesi hiyo ya Methane tangu miaka 15,000 iliyopita. Ukungu wenye hali ya ki-electronic na sumaku. Ukungu wenye nguvu ya kuzalisha umeme ambapo husababisha dira hupoteza uelekeo na kuwachanganya marubani pamoja na manahodha.Na hatimaye ndege pamoja na Meli hizo hupotelea katika ilo eneo la Bermuda.

Mawimbi na hali ya hewa kubadilika kwa kasi. Eneo la bahari ya Atlantic hasa upande wa Caribbean hukumbwa na kimbunga kikali pamoja na mawingu mazito, Bermuda ni eneo ambalo limepakana sana na Caribbean na hukabiliwa na upepo na wingu zito ambavyo husababisha mushkeli kwa ndege, meli pamoja na binadamu.

Je freemason wanaweza kuwa wanatumia eneo la bermuda kama eneo la kafara kwao au la.?? Changia kwa kutoa maoni/comment kupitia Facebook au Google account.

Chanzo

-Emmie Gerrie

-Maregesi

-Katemi P.M.

Magaidi wa Algeria wamchinja mtalii kutoka Ufaransa kuiunga mkono ISIS

Kundi la kigaidi la Jund al-Khilifa limemuua kwa
kumchinja mtalii wa Ufaransa ikiwa ni sehemu
ya ahadi yao kwa nchi hiyo ikiwa haitasitisha
mashambulizi dhidi ya kundi la ISIS nchini
Iraq.

Jumapili iliyopita, kundi hilo liliweka YouTube
video inayoonesha wapiganaji walijifunga
kitambaa usoni wakimfanyia tukio hilo mtalii
aliyetajwa kwa jina la Herve Gourdel mwenye
umri wa miaka 55, waliyemteka alipokuwa
nchini humo.

Ufaransa imeungana na Marekani katika
kampeni ya kushambulia kundi la ISIS lililoteka
sehemu kubwa nchini Iraq na Syria.

Mwanzilishi wa kampuni ya 'Apple' aliwazuia watoto wake kutumia iPad, iPhone na iPod, fahamu sababu

Bidhaa za kampuni ya Apple zina mashabiki na
wateja wengi duniani, hii inathibitishwa na
foleni kubwa ya watu waliojitokeza kwenye
vituo mbalimbali duniani kununua toleo jipya
la iPhone6.

Tumesikia watu wakiachana ama familia
zikitengana kwa sababu tu baba ameshindwa
kununua bidhaa za kielekroniki za kampuni ya
Apple.

Mwaka jana familia moja nchini China
iliwauza watoto wao ili kupata pesa ya kununua
iPhone5.
Kwa kuzingatia hayo, huenda ukadhani watoto
wa mwanzilishi wa kampuni ya Apple na
mgunduzi wa bidhaa hizo, Steve Jobs wanafaidi
zaidi bidhaa hizo.
Na huenda ukadhani hata kuta za nyumba yao
zingeweza kuwa za mfumo wa simu za kisasa za
kupangusa ‘Screen Touch’ na mawasiliano ya
hali ya juu ndani ya nyumba hiyo kwa mfumo
huo.

Lakini ukweli ni kwamba, marehemu Steve Jobs
hakuwaruhusu hata kidogo watoto wake
kutumia iPhones, iPods wala iPads nyumbani
kwake.
Katika article iliyoandikwa na New York Times
wiki hii, mwandishi wa habari Nick Bilton
ameeleza jinsi ambavyo alishangaa majibu ya
Steve Jobs alipomuuliza jinsi ambavyo watoto
wake wanapenda bidhaa za kampuni hiyo.

“Hawajawahi kutumia kabisa. Tunadhibiti kiasi
ambacho watoto wetu wanatumia teknolojia
nyumbani.” Alijibu Steve Jobs.
Nae mwandishi maalum wa Steve Jobs, Walter
Isaacson ambaye alikuwa akitumia muda
mwingi nyumbani kwa boss wake huyo
alithibitisha kuwa maoengezi ya uso kwa uso
yalitawala katika nyumba hiyo.
“Kila jioni Steve alikuwa akipata chakula cha
usiku na familia yake kwenye meza kubwa
jikoni, wakijadili vitabu na historia na vitu
vingine vingi. Hakuna mtu aliyekuwa na iPad au
computer. Watoto hawakuonekana kuwa
addicted hata kidogo na vifaa hivyo.” Alieleza
Isaacson.

Inaelezwa kuwa hata Steve Jobs hakuwa na
tabia ya kutumia vifaa hivyo kwa muda mrefu.
Hata hivyo, Steve Jobs aliyefariki mwaka 2011
sio mtu maarufu pekee aliyeamini katika
kuweka sheria kali kwa watoto wake kutumia
vifaa hivyo, Chris Anderson, mhariri wa zamani
wa Wired pia alieleza kuwa yeye na mkewe
wamewazuia watoto wao kiasi kwamba watoto
hao huwalalamikia sana wakilinganisha na
uhuru wanaouona katika familia za marafiki zao.
Utafiti uliofanywa katika eneo la Chuo Kikuu
cha California, Los Angeles na kuchapishwa hivi
karibuni unaonesha kuwa siku chache baada ya
kuzuia watoto kutumia vifaa vya kieletroniki
vya simu, ufaulu wa watoto katika masomo
ulipanda ghafla.

Utafiti unaonesha kuwa kwa wastani watoto
nchini Marekani hutumia zaidi ya saa saba na
nusu kwa siku katika matumizi ya simu za
kupangusa na vifaa vingine vya kielekroniki
kama iPads, iPod n.k.

Uamuzi ni wako, kumnunulia mwanao vifaa vya
hivyo au kumuweka mbali na mapinduzi hayo
ya kiteknolojia.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata taarifa na stori mbalimbali.

Wednesday 24 September 2014

Mmiliki wa Kampuni ya ALIBABA ndiye anaeongoza kwa utajiri nchini China.

Mwanzilishi wa mtandao wa Alibaba ndiye
tajiri mkubwa zaidi nchini Uchina kulingana
na rekodi za kampuni yake.
Hili imethibitishwa na ripoti rasmi ya kifedha
ya Hurun.
Bw.Ma ameongoza orodha ya watu tajiri zaidi
nchini Uchina kwa mali ya takriban dola bilioni
25 akifuatwa na mwenyekiti wa Wanda Group
Wang Jianlin.
Matajiri watano katika ya kumi walio katika
orodha hiyo, wanamiliki kampuni za
mitandaoni huku wakiwabwaga wale
wanaomiliki mali isiyohamishika ambao kwa
muda mrefu wamekuwa wakiongoza orodha
hiyo.
Orodha hiyo inahusisha pia kiongozi wa
Tencent Pony Ma.
Mabwenyenye wengine walio katika orodha
hiyo ni mwanzilishi mwenza wa mtandao wa
intanet marufu sana nchini China Baidu, Robin
Li na pia mwanzilishi wa soko la mtandao la
JD.com, Richard Liu Qiangdong.
Bw Liu ambaye kampuni yake ilihusika katika
ubadilishanaji wa hisa huko New York hapo
Agosti mwaka huu, aliorodheshwa katika nafasi
ya kumi.

Kulingana na mtafiti mkuu ambaye pia ndiye
mwenyekiti wa Hurun Report, Rupert
Hoogewerf amesema orodha hiyo imeonyesha
kwamba ari ya kufanya biashara kati ya
wananchi wa Uchina bado haijafa.
"Jack Ma ambaye ameorodheshwa wa kwanza,
ni wa kumi na moja kuwahi kushikilia nafasi
hiyo katika muda wa miaka 16. Hii inaonyesha
mabadiliko makubwa katika uchumi wa Uchina
na kutukumbusha uwezo ulio na masoko
mapya yanayojitokeza kwa sasa.”
Orodha ya matajiri inayotolewa na Hurun
Report ndiyo inayoaminika sana kwa kuwa
hukadiria vizuri utajiri nchini Uchina.

Tuesday 23 September 2014

Kiumbe cha ajabu kutoka baharini chaonekana Pemba.

Taarifa zilizotufikia BantuTz hivi punde kutoka huko Pemba ni kwamba;

Wananchi wa Kengeja Likoni,Kisiwani Pemba wameshuhudia kiumbe kikubwa na cha ajabu kilichotoka Baharini na kuja hadi nchi kavu kikiwa kinaelea baada ya kufariki.

Watu wengi wa Kengeja ambao wanajishughulisha na uvuvi wanasema kwamba kiumbe hicho ni Nyangumi huku wengine wanasadiki kusema kwamba ni Chongowe na baadhi wanasema hawajui ni aina gani ya Kiumbe.

Vijana wa tawi la Likoni zaidi ya 200 wamejitokeza katika fukwe za bahari hiyo kukishangaa kiumbe hicho cha ajabu chenye urefu wa Mita 40,Upana wa Mita 25 na amekwenda juu zaidi ya Mita 15.

Hakika ni kiumbe cha ajabu;Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinajiri huko Kengeja Likoni,Kisiwani Pemba kuhusiana na kiumbe hicho cha ajabu.

Credited by-Oscar Kiria.

Marekani imeanza mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la ISIS huko Syria.

Marekani imepanua
operesheni yake dhidi ya
kundi la Dola la Kiislamu
nchini Syria, ikisaidiwa na
mataifa matano ya Kiarabu -
Bahrain, Qatar, Saudi Arabia,
Jordan na Umoja wa Falme
za Kiarabu.

Shirika la uangalizi wa haki
za binaadamu nchini Syria
lenye makao yake mjini
London limesema
mashambulizi hayo yalilenga
mkoa wa kaskazini wa Raqq
na pia mji mkuu wake.
Ukanda wa video
uliyowekwa mtandaoni leo,
unaonesha mabomu
yakidondoka katika eneo la
wazi, miripuko
inayosemekana kutokana na
mashambulizi ya washirika.

Msimulizi katika ukanda huo
anasikika akisema
unaonyesha mashambulizi
kwenye kijiji cha Kfar Derian,
huku akitamka Allah Akbar,
yaani Mungu mkubwa.
Wanaharakati wamesema
mashambulizi hayo yalilenga
maeneo ndani na nje ya mji
wa Raqqa nchini Syria, na
kuongeza kuwa
yalisababisha maafa
miongoni mwa wapiganaji
wa Dola la Kiislamu. Mji wa
Raqqa ndiyo uliyotangazwa
na kundi hilo la wapiganaji
kuwa mji mkuu wao nchini
Syria.

Mwanaharakati
mwigine alieko mkoa wa
kaskazini wa Idlib,
alithibitisha kuwa
makombora kadhaa
yaliushambulia mji wa Kfar
Derian katika saa za asubuhi
leo Jumanne. Mashambulizi
yore yaliwalenga wapiganaji
wa IS pamoja na wale kundi
lenye mafungamano na
mtandao wa Al-Qaeda la Al-
Nusra Front.

Syria yasema iliarifiwa
Ndege za Marekani pia
zilifanya mashambulizi 30
katika mkoa wa Deir al-Zour
mashariki mwa Syria,
unaopakana na Iraq. Serikali
ya Syria ilisema iliafiriwa
mapema juu ya
mashambulizi ya Marekani.
Shirika la habari la Syria,
likiinuku wizara ya mambo
ya nje ya nchi hiyo, limesmea
kuwa upande wa Marekani
ulimuarifu balozi wa
kudumu wa Syria katika
Umoja wa Mataifa mjini New
York kwamba kungefanyika
mashambulizi dhidi ya Dola
ya Kiislamu mkoani Al-
Raqqa.

Uamuzi wa kufanya
mashambulizi ulichukuliwa
mapema siku ya Jumatatu na
kamandi kuu ya Marekani
kwa idhini ya rais Baracl
Obama. Mashambulizi hayo
ndiyo yalikuwa ya kwanza
dhidi ya Dola ya Kiislamu
nchini Syria. Marekani
ilishafanya mashambulizi
dhidi ya kundi hilo nchini
Iraq, lakini ilisema
ingelifuata ndani ya Syria
ikibidi.

Maafisa wa Marekani
walisema mashambulizi hayo
yalianza saa tisa Alfajiri, na
yalifanywa na Marekani,
Bahrain, Qatar, Saudi Arabia,
Jordan na Umoja wa Falme
za Kiarabu. Mkuu wa
upinzani unaoungw amkono
na mataifa ya magharibi
Hadi Bahra, alikaribisha
kuanza kwa mashambulizi
nchini Syria. Viongozi wa
kijeshi wamesema theluthi
mbili ya wapiaganaji
wanaokadiriwa kufikia
31,000 wako nchini Syria,
lakini baadhi ya maafisa
wameelezea wasiwasi kuwa
mashambulizi hayo
yanaweza kumsaidia rais
Assad ,kwa sababu hao
wanapigana kwa sehemu
kumn'goa yeye.

Ufaransa yasema
itamkomboa raia wake
Wakati huo huo, Ufaransa
imesema kuchukuliwa
mateka kwa raia wake nchini
Afghanistan hakutaizuwia
nchi hiyo kushiriki
operesheni za muungano wa
mataifa zinazoongozwa na
Marekani dhidi ya Dola ya
Kiislamu, waziri wa mambo
ya kigeni wa Ufaransa,
Laurent Fabius amewambia
waandishi wa habari.
"Nia ya Ufaransa inaendelea
kuwa ile ile: Tuna mpango
wa kufanya kadiri
tuwezavyo kuwaokoa
mateka, na hasa mateka
huyo lakini kundi moja la
kigaidi haliwezi kushawishi
msimamo wa Ufaransa,"
alisema waziri Fabius.

Raia huyo wa Ufaransa
alitekwa mashariki mwa
Algeria siku ya Jumapili, na
watekaji wake walitoa
mkanda wa video wakitishia
kumuuwa ikiwa Ufaransa
haitasitisha uingiliaji wake
kijeshi nchini Iraq inakounga
mkono operesheni ya
Marekani dhidi ya IS

Chanzo:DW

Monday 22 September 2014

Baraza laamuru mwili wa marehemu ufukuliwe Arusha.

Baraza la ardhi na nyumba mkoani
Arusha limeamuru mwili wa marehemu
Paulina Lucas aliyezikwa katika
eneo la mgogoro wa shamba katika
kijiji cha Elkiushin ufukuliwe mara
moja na kisha ukazikwe kwenye
makaburi ya umma .

Amri hiyo ilitolewa mwishoni mwa
wiki iliyopita na mwenyekiti wa
baraza hilo mkoani hapa ,Cyriacus
Kamugisha kufuatia shauri nambari
222 la mwaka 2006 lililofunguliwa
na Francis Levava aliyekuwa
akiwakislishwa na wakili,Ezra
Mwaluko.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo mbele ya
pande zote ,Kamugisha alisema kuwa
mnamo juni 11 mwaka 2006 mara baada
ya shauri hilo kufikishwa mbele ya
baraza hilo ilimariwa ya kwamba
kisifanyike kitu chochote katika
eneo hilo hadi shauri hilo la
msingi litakaposikilizwa lakini
upande wa wajibu maombi ulikiuka
agizo hilo.

Kamugisha,alisema kuwa upande wa
mlalamikiwa ambaye ni ,Kerusoi
Loilole aliyewakilishwa na wakili
Daud Haraka ulikiuka amri ya msingi
ya baraza hilo kwa kuzika mwili wa
marehemu sanjari na kujenga nyumba
na choo katika eneo hilo ihali eneo
lina mgogoro.
“Kitendo alichokifanya mjibu maombi
kuhifadhi mwili wa marehemu
hakikuwa sahihi kwani eneo lilikuwa
na mgogoro,kitendo hiki ni kudharau
amri halali ya mahakama”alisema
Kamugisha.

Hatahivyo,akisoma hukumu hiyo
mwenyekiti huyo alitamka kwamba
jengo la choo na nyumba
vilivyojenga katika eneo hilo
vibomolewe mara moja na kuagiza
zoezi hilo linapaswa kusimamiwa na
mkuu wa polisi wilayani Arusha(OCD)
pamoja na maafisa watendaji wa
kijiji na kata katika eneo la
mgogoro.

Alisema amri hiyo inapaswa
kutekelezwa mara moja kuanzia
tarehe ya hukumu na kimsingi maombi
ya mleta maombi yanakubaliwa kwa
gharama na baraza hilo kufukua
mwili wa marehemu huyo.
Akiongea mara baada ya hukumu hiyo
upande wa mlalamikiwa,Loilole
alisema kuwa hakumu hiyo haikutenda
haki na huenda ikazua maafa kwa
kuwa walianza kuzika miili
mbalimbali katika eneo hilo tangu
miaka ya nyuma hata kabla ya
marehemu Lucas.

Kwa upande wa walalamikaji kupitia
kwa wakili wake,Mwaluko alisema
kuwa wameridhishwa na hukumu hiyo
kwani imetenda haki kwani eneo hilo
ni mali halali ya mteja wake.

Producer Man Walter afunga ndoa,huyu ndiye mkewe.

Producer kutoka Combination Sound anaefanya
vizuri nchini, Man Walter amepiga hatua kubwa
katika maisha yake baada ya kufunga ndoa na
mrembo ambaye alidaiwa kumuimbia wimbo
wa ‘Wife Material’.

Wimbo ''Happy'' wa Pharrel Williams wasababisha matatizo makubwa Iran.

Kikundi cha mashabiki wa muziki
nchini Iran walioiga wimbo maarufu
wa mwanamuziki maarufu wa Marekani
Pharrell Williams, 'Happy'
wamejipata matatni baada ya
kukamatwa na polisi.
Kanda ya video waliyoirekodi
wakiiga wimbo huo, inaonyesha
vijana watatu na wanawake kadhaa
ambao hawakuwa wamejitanda
mitandoa, wakicheza densi kwenye
barabara za nchi hiyo na kwenye paa
za nyumba mjini Tehran.

Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia,
alisema kuwa kanda ya video
inayoonyesha vijana hao wakicheza,
imekiuka maadili ya jamii.
Kituo cha televisheni ya serikali
kilionyesha vijana hao wakikiri
makosa siku ya Jumanne.
Inaarifiwa maelfu ya wananchi wa
Iran wamekamatwa katika miaka 35
iliyopita wakisherehekea na
kujiburudisha kwa mambo ambayo
serikali inaona kama ya kukiuka
maadili.
Hata hivyo vijana hao wanaosema ni
waigizaji wanadai kuwa walihadaiwa
kushiriki katika kanda hiyo na watu
waliokuwa wanatafuta waigizaji
wakisema ulikuwa kama mtuhani kwao.

Wamekiuka maadili'
Kulingana na taarifa ambazo bado
hazijathibitishwa, watu 13
walikamatwa kuhusiana na kanda
hiyo, ingawa idadi kamili ya
waliokamatwa haijatangazwa rasmi.
Pharrel aliyeteuliwa kwa tuzo la
Oscar kwa wimbo wake huo mwaka huu
ambao umekuwa maaruufu sana
duniani, alielezea kukasirishwa na
hatua ya vijana hao kukamatwa.

"Yani siamini kama watoto hawa
walikamatwa kwa kujaribu kueneza
furaha,'' alisema Pharrell katika
ukurasa wake wa Facebook.

Chini ya sheria za kiisilamu,
sharti mwanamke ajitande kutoka
kichwani hadi katika viganja vya
mguu.
Polisi ambao jukumu lao ni
kuhakikisha kuwa sheria ya mavazi
inafuatwa, hushika doria mara kwa
mara katika barabara za mji mkuu
Tehran.

Kanda hiyo ya "Happy we are from
Tehran" ilionekana kwenye mtandao
wa Youtube tarehe 19 Mei na kufikia
sasa imetazamwa mara 40,000.
Baadhi wametuma ujumbe wa kukejeli
serikali ya Iran wakisema kuwa Iran
ni nchi ambako ni hatia kwa mtu
kuwa na furaha.

Wimbo halisi wa Pharrell 'Happy'
umepelekea maelfu ya watu kote
duniani kuiga video ya wimbo huo na
kutengeza video zao wenyewe. Kutoka
Kenya, Marekani , Uingereza yaani
nchi nyingi duniani tu, watu
wameiga video hiyo kwa kutengeza
yao wenyewe.

Hukumu iliyotolewa
Watu sita nchini Iran waliokamatwa
baada ya kuonekana kwenye kanda ya
video iliyokuwa inaiga wimbo wa
'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri
Pharrel Williams, wamehukumiwa
kifungo cha hadi mwaka mmoja jela
kila mmoja pamoja na adhabu ya
kuchapwa mijeledi 91.

Wakili wa sita hao amesema kuwa
hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi
sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu
jela ikiwa watarejelea kosa hilo.
Kanda hiyo inaonyesha wanaume
watatu na wanawake watatu ambao
hawajafunika vichwa vyao wakicheza
densi kwenye barabara na katika paa
za nyumba mjini Tehran.

Kanda hiyo iliyowekwa kwenye
mtandao wa kijamii wa You Tube,
imetazamwa na zaidi ya watu milioni
moja. Wengi wa waliohusika
kuitengeza kanda hiyo, walifungwa
kwa miezi sita , huku mmoja wao
akifungwa kwa mwaka mmoja,
alinukuliwa akisema wakili wao
Farshid Rofugaran.
Mmoja wa watu waliokamatwa kwa
kucheza densi
Kanda hiyo kwa jina, "Happy we are
from Tehran" ilifikishwa kwa
maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei
baada ya kutazamwa na watu 150,000
kwenye You Tube.

Waliohusika pia walikamatwa na
kushitakiwa kwa kosa la kukiuka
sheria za kiisilamu ambazo
zinawazuia wanaume kucheza densi na
wanawake na pia wanawake kutoka nje
bila hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye
televisheni wakijitetea kwamba wao
ni waigizaji walihadaiwa kushiriki
katika kanda hiyo Kukamatwa kwa
vijana hao kulizia ghadhabu kutoka
anga za kimataifa huku watetezi wa
haki za binadamu
wakianzisha kampeni kwenye mitandao
ya kijamii kutaka waachiliwe.
Mwanamuziki Paharrel Williams
mwenyewe, ambaye wimbo wake huo,
uliteuliwa kwa tuzo la Oscar,pia
alieleza kukerwa na kukamatwa kwa
watu hao.

Chanzo: BBC

Mourinho amponda Lampard.


Mouringo akimuongelea Lampard baada ya kufunga
bao lililopelekea matokeo dhidi ya City kua
1-1.

'Alipoamua kujiunga na wapinzani wetu
tunaochuana nao kuwania ubingwa, hadithi
za mapenzi zikaisha. Amefanya kazi yake
(kufunga) kama mwana taaluma.
Chelsea hatukumpa mkataba na yeye
akajiunga na klabu ya USA, kwa kuwa ligi hiyo kwa
sasa ipo mapumziko. Lampard akaamua
kurudi EPL kwa mkopo:

Mourinho anadai
angeenda timu yoyote lakini si Arsenal, Man
United, Man City ama Liverpool kwani hao
ndio anaogombea nao Ubingwa.

Na kwa kuwa kafanya hivyo basi mambo ya kusema ana
mapenzi na Chelsea hakuna.

Sunday 21 September 2014

Clash of the Titans...Chelsea Vs Manchester City

Usithubutu kunywa uji wa mgonjwa...Wala mtoto hatotumwa dukani majira ya saa 12:00 Jion kwa masaa ya Afrika Mashariki mtanange kati ya Vijana wa Darajani,The Blues almaarufu kama Chelsea watakapopambana na The Citizen,Manchester City katika dimba la Etihad katika Jiji la Manchester.

Kwa teknolojia ya sasa ni mambo machache
sana unaweza kuyafahamu bila kutumia
Computer ila kuna mengine yanaeleweka
kabisa kuwa hivi sasa mechi kubwa na yenye
upinzani kisoka ni mechi kati ya Manchester City na
Chelsea.

Kwanza hizi ndizo timu zinazopewa
kipaumbele cha kuchukua ubingwa wa Ligi
kuu ya Uingereza.

Timu hizi zimekamilika kila idara
kuanzia benchi la ufundi, mchezaji mmoja
mmoja na timu kwa ujumla.

Haihitaji Computer kugundua mchezo wa leo
utaamuliwa katikati ya uwanja, hebu fikiria
pale kuna Ramires,Oscar,Willian, Matic na
Fabregas na huku kwingine kuna Yaya Toure ,
Fernadinho, Silva, Samir Nasri kwa kifupi
timu zote zimekamilika katikati ya uwanja.
Uimara wa safu za ushambuliaji wa timu zote mbili pia kunaongeza utamu wa mechi hii Chelsea msimu huu wametibu tatizo lililowatatiza sana msimu uliopita,sehemu ya ushambuliaji,haipingiki Diego Costa amekuwa mwiba kwa beki hivi sasa bali vilevile Manchester City nao si wa kubezwa Sergio "Kun" Aguero,Dzeko na Stephan Jovetic muda wowote ule wanalichungulia goli.

Ukiangalia mechi mbili za mwisho walizokutana ambazo
Chelsea ilishinda zote walikuwa wakitumia
viungo watatu wenye asili ya ukabaji ili
kuwazima Man City wasicheze mpira hapo
David Luiz, Ramires na Matic walifanya kazi ya
kuzia "movement" za kina Nasri, Toure na Silva.
Chelsea ya sasa haina Luiz bali ina Fabregas ni
jukumu la Man City kuwazima kina Fabregas
na Oscar ili waweze kumfanya Diego Costa asipate
mipira , kama Man City
watafanikiwa kwenye hili basi watashinda
mechi ya leo ila wakishindwa basi chelsea
itaendeleza gharika ya ushindi kwa 100%

Imeandaliwa na...
                             Katemi Methsela.

Moto wateketeza nyumba 21, Tufani yaezua 11, 240 wakosa makazi Sengerema

Wakazi 240 wanaoishi kisiwa cha Nyamango
kijiji cha Lushamba kata ya Buliaheke
Wilayani Sengerema hawana makazi ya kuishi
kutokana na kuzuka kwa moto usiku wa
septemba 19 na mvua iliyombana na tufani
mapema asubuhi ya jana(leo).

Mkuu wa Wilaya Sengerema Elianas Balangyo
alisema kuwa kamati ya maafa ilikuwa
haijafika katika eneo la tukio na ilikuwa
ikisubiri kutulia kwa mawimbi ziwani ili
kuanza safari ya kufika kisiwani hapo
kutathimini kiasi cha maafa kichotokea ili
kutoa msaada unaohitajika.

“Mpaka sasa hatujafika eneo la tukio
kutokana na kuwa eneo lililokumbwa na
matatizo hayo haliko nchi kavu hivyo
tunasubiri ziwa litulie ili kamati iende
kufanya tahimini na kupata kiasi cha msaada
kinachotakiwa kupelekwa na aina ya msaada
unaotakiwa pia” alisema DC. Balangyo.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyamango
George Lwezaula alisema kuwa haijulikani
chanzo cha kuzuka kwa moto na kuwa
ulitokea saa 6.05 usiku katika nyumba moja
ya mkazi wa katika kitongoji hicho. Inadaiwa
kuwa moto huo ulitokana na familia hiyo
kusahau kuzima jiko baada ya kumaliza
kuandaa chakula na kuingia kulala na
kuchukuliwa na upepo na kushika nyumba
yake kisha nyumba nyingine.
“Nyumba 21 zimeungua na kuteketea kabisa,
ukizingatia kuwa vyumba hizi za wavuvi
zinajengwa karibu karibu lakini hakuna mtu
aliyedhurika licha ya mali zote kuungua
ndani” alisema Lwezaula Mwenyekiti wa
kitongoji cha Nyamango.

Hata hivyo alieleza kuwa asubuhi
mvua iliyoambatana na upepo mkali ilizuka
na kuezua nyumba 11 likiwemo kanisa la
Roman Katoliki na kufanya jumla ya nyumba
zilizoezuliwa na kuteketea kufikia 32. “Mvua
hii imeanza saa 1 asubuhi lakini ilikuwa na
upepo mkali ambao umebeba paa za nyumba
na kuacha wananchi wakiwa hawana pa
kujistili” alisema Lwezaula.
Mtendaji wa kata ya Buriaheke Mabula Enock
alisema taarifa hiyo aliipata kwa njia ya simu
na alikuwa Wilayani Sengerema kutafuta
usaidizi wa kamati ya maafa ya Wilaya kuona
ni jinsi gani wanatoa msaada kwa wakazi hao.

“Nilipata taarifa hiyo jana na kuutaarifu
uongozi wa Wilaya, hapa nipo nafuatilia
kuona kuwa wanaingia saa ngapi kisiwani ili
kutathimini” alisema Enock.

Saturday 20 September 2014

Yanga yaanza kwa Kipigo,Azam yaangua Kicheko Ligi Kuu Tanzania Bara.

Dar es Salaam Young Africans imeianza ligi
kuu kwa kichapo baada ya kufungwa 2-0 na
Mtibwa Sugar katika mchezo uliofanyika
uwanja wa Jamhuri. Magoli ya Mtibwa
yalifungwa na Musa Hassan Mgosi katika
dakika ya 16 baada ya kupokea pasi nzuri ya
Ame Ali huku bao la pili likifungwa dakika ya
82 naye mpikaji wa goli la kwanza Ame Ali.

Matokeo ya michezo mingine ni kama
ifuatavyo:
Azam FC 3-1 Polisi Morogoro
Mtibwa Sugar 2-0 Yanga
Mbeya City 0-0 JKT Ruvu
Ruvu Shootings 0-2 Prisons
Stand United 0-4 Ndanda FC
Mgambo JKT 1-0 Kagera Sugar

Hoteli iliyojengwa katikati ya Maji huko SpitBank Fort-Uingereza miaka 134 iliyopita.

HOTELI ya Spitbank Fort ikionekana kwa juu ikiwa imejengwa mwaka 
1879 katikati ya kina maji ya habari nchini Uingereza  ikiwa na umri wa miaka 134.

Hapa ikionekana katikati ya kina cha maji ya bahari. 
Sehemu ya mbela ya hoteli hiyo. 


Ndani 
Sehemu ya kupunga upepo 
mandhali ya ndani. 
hii nayo ni sehemu nyingine ya kupunga upepo 
jiko 



hapa ni chumbani 


Mandhali wakati wa jiono muonekano wake.

Viwanja vya ndege vilivyo "busy" zaidi duniani.

ATL 3Wakati nchi kama Tanzania inapambana kujenga viwanja vya ndege ili ndege kubwa kama za Fastjet ziweze kutua sehemu kama Musoma, Kigoma na Arusha baada ya kuweza kufanya safari zake kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Dar na Mwanza, ifuatayo ni list ya viwanja vya ndege duniani ambayo hutoka kila mwaka.
Kiwanja kilichoshika namba moja kwa kuwa busy kuliko vyote duniani ni kiwanja cha Atlanta Georgia Marekani wanakotoka mastaa kama rapper T.I ambacho kwa mwaka 2013 pekee kimehudumia abiria milioni 94.4, namba mbili inashikwa na Beijing Capital International Airport ambacho kilihudumia abiria milioni 83.7
Beijing
Beijing
London Heathrow
London Heathrow
Kiwanja namba 3 ni cha London Heathrow Airport kilichobakia kwenye nafasi hiihii ya mwaka jana ambapo kimehudumia abiria milioni 72.4 huku kiwanja cha Tokyo Japan (Haneda) kikishika namba 4, cha tano ni Chicago O’Hare International Airport nchini Marekani na cha sita ni Los Angeles International Airport hukohuko Marekani.
Screen Shot 2014-09-18 at 11.42.01 AM
Kiwanja cha ndege Tokyo (Haneda)
Tokyo
Tokyo
Kiwanja cha ndege Chicago Marekani
Kiwanja cha ndege Chicago Marekani
Kiwanja cha ndege Dubai kimeshika namba 7 kutoka namba 10 mwaka uliopita ambapo kimehudumia abiria milioni 66.4 ambapo kiwanja cha ndege cha Paris kimeshuka nafasi moja kutoka ya 7 mwaka uliopita na kushika ya nane mwaka huu, ya tisa imeshikwa na kiwanja cha ndege cha Dallas/Fort na namba 10 imeshikwa na kiwanja cha Jakarta Indonesia.
Los Angeles
Los Angeles
Hii ripoti imefanywa kwa kuhusisha viwanja vya ndege karibu 2000 ndani ya nchi 160 duniani ambapo kwenye mistari ya ziada, kiwanja cha ndege cha Hong Kong kimebaki kushika namba moja kwa kusafirisha sana mizigo duniani ambapo mwaka jana kilisafirisha karibu tani milioni 4.2