Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Tuesday 6 October 2015

Dk J.P Magufuli: Ningemuombea kura Dk Slaa kama angegombea ubunge

Magufuli akihutubia Wananchi katika moja ya milutano ya kampeni ya chama hicho. Picha na Maktaba
Karatu/Zanzibar. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli jana aliwahutubia mamia ya wakazi wa Karatu na kummwagia sifa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa ni kiongozi mwadilifu na kuongeza kuwa kama angekuwa anagombea katika jimbo hilo, angemwombea kura kwani ni mtu safi bila kujali chama chake.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mbowe mjini Karatu, Dk Magufuli alisema Dk Slaa ni kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa mwadilifu akitetea masilahi ya umma.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu wa Karatu, Dk Magufuli aliwataka kumuunga mkono Dk Slaa kwa uamuzi ambao amechukua.
Dk Slaa, alitangaza hivi karibuni kuachana na siasa za vyama na kujitoa Chadema baada ya kutoridhishwa na kujiunga kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika chama hicho.

Lowassa:Sina tena rafiki CCM

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa
Monduli. Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa amesema hana rafiki yeyote CCM kwani yeye tayari alishapakia basi la Chadema.
Lowassa amesema ingawa aliwahi kumshauri mgombea ubunge wa jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM, Namelock Sokoine agombee lakini mambo yalivyobadilika alimshauri ajitoe hata hivyo alikataa na hivyo yeye sasa anamuunga mkono mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo hilo, Julius Kalanga.
Akizungumza na wananchi wa Lokusale katika mkutano wa kampeni Lowassa alisema, "Suala la ubunge wa Monduli ni kweli nilimshawishi Namelock agombee ubunge lakini mambo yalipobadilika nilimshauri ajitoe, sasa kama CCM hainitaki kwa nini abaki, sina rafiki CCM,"alisema Lowassa na kuongeza: "Kama mtu amebaki CCM mimi nifanye nini? Alihoji Lowassa na wananchi wakijibu "Unamwachaaaaaaaa."
Huku wananchi wakishangilia Lowassa alisema amempendekeza Kalanga hivyo Namelock akubali kwa kuwa mbunge anayefaa Monduli ni Kalanga.
Aliwaambia wananchi hao wamnadi Kalanga kama Mbunge wao na wakiulizwa na mtu yeyote wamjibu kuwa Lowassa ndiye amewatuma.
"Moran mfanye kazi hiyo na pia mlinde kura. Nawapa ushauri wa bure kwamba mbunge anayefaa ni Kalanga kwa ushauri wangu mumchague na mtu asiwasumbue."
Lowassa aliwaambia wananchi hao kuwa akiingia madarakani suala la barabara litashughulikiwa kwani ndicho kitu pekee kinachowapa tabu wananchi wa Lokusale.

Majaji 7 wasimamishwa kazi kwa Ufusadi Ghana.

Majaji saba wa mahakama ya juu nchi Ghana kati ya 12 wamesimamishwa kazi kwa mda kufuatia madai ya kuhusika katika ufisadi.
Mwezi uliopita majaji wengine 22 wa ngazi za chini walisimamishwa kazi baada ya filamu moja kuwaonyesha wakichukua hongo kutoka kwa wateja ili wapate kupendelewa katika kesi.
Filamu hiyo ilizua hisia kali wakati ilipoonyeshwa mara ya kwanza mjini Accra.
Majaji wengine kadha wamekataa madai hayo na kwenda mahakamani kupinga kusimamishwa kwao kazi.
Saba hao walikuwa na kesi ya utovu wa nidhamu kufuatia makala yaliyoandaliwa na mwandishi Anas Aremeyaw.
Mwandishi huyo anamiliki ukanda wa video wa takribam saa 500 kuhusu ushahidi unaowaonyesha majaji hao wakitaka kupewa hongo.
Majaji wengine 22 wa mahakama ya chini pia wamesimamishwa kazi huku wengine wakikana madai hayo.
Makala hayo ya bwana Anas yamelishtua taifa la Ghana na yameonyeshwa katika majumba ya kuonyeshea filamu katika mji mkuu wa Accra.
Saba hao ni majaji wenye nyadhfa za juu zaidi kusimamishwa kazi nchini humo.
Jaji mkuu Goergina Theodora Wood ameanzisha kesi dhidi yao kulingana na baraza la majaji nchini humo.
Uchunguzi pia utafanywa ili kubaini iwapo wana hatia au la.

Kampuni ya Mercedes yatengeneza Malori yanayojiendesha.

Amini usiamini huku watu wengi Afrika Mashariki wakilazimika kulipa mabilioni ya shilingi ilikujifunza kuendesha magari,teknolojia sasa imepiga hatua moja zaidi.
Mwanzo ilikuwa ni magari madogo sasa kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari Daimler Mercedes-Benz imezindua lori linalojiendesha lenyewe!
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo yenye asili yake nchini Ujerumani,Wolfgang Bernhard alibofya kidude na mara lori likachukua usukani na kuenda lenyewe pasi na kusababisha ajali ya aina yeyote.
Lori hilo linatumia teknolojia ya kamera kwa pamoja na 'radar' kukwepa magari mengine barabarani.
Aidha mtambo huo unatuma na kupokea taarifa na mawasiliano iwapo lori hilo linasogea karibu zaidi kitu chochote iwe ni gari,mti ama hata mtu barabarani.
Hata hivyo kampuni hiyo ilisisitiza kuwa sharti dereva awe hapo wakati wote kifaa hicho cha "highway pilot" kinapotumika kama tahadhari kusitokee ajali.
Lorry hilo aina ya Actross lilijaribiwa katika barabara inayotumika na uma ya Baden-Wurttemberg Ujerumani.
Kwa mujibu wa bwana Bernhard lori hilo lilimudu kujiendesha na hata kutimia kasi ya Kilomita 80 kwa saa.
Mkurugenzi huyo alikuwa na Waziri Winfried Kretschmann walikuwemo ndani ya lori hilo wakati wa jaribio hilo la kihistoria.
Bernhard alissistiza kuwa wakati dereva anapohisi amechoka gari hilo linaweza kuchukua usukani naye ajipumzishe kidogo japo kwa kutengeneza kikombe cha chai huku kamera na mfumo huo wa radar zikidhibiti usukani.
Mfumo huo unatumia miale kubaini kona na maelezo kwenye mabango barabarani.
''Kwa hakika hata uwe mstadi kivipi , mfumo huu wa "highway pilot" unaendesha vyema zaidi kuliko mwanadamu na hata iwe kwa kiwango kipi haiwezi kuchoka sawa na vile madereva wa malori huwa wanawachoka na kupoteza umakinifu barabarani.'' alisema mkurugenzi wa kampuni hiyo Wolfgang Bernhard.

Facebook kuanzisha Satellite yao.

Kampuni ya Facebook imetangaza kuwa itaanzisha mtandao wa satelite ili kutoa huduma za internet kwenye maeneo yaliyo mashambani barani Afrika.
Kwa ushirikiano na kampuni ya Eutelsat, iliyo Ufaransa, Facebook wanatumainia kuwa mtambo wa kwanza wa satelite utakuwa tayari kuzinduliwa mwaka ujao.

Baadhi ya mataifa, kama India yanapinga hatua hiyo ya Facebook, ambayo wanadai inahujumu kampuni ndogo zinazotoa huduma za simu katika mataifa yanayoendelea.

Watu zaidi ya 60 wauawa kwa Bomu Iraq

Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka na kuwauwa zaidi ya watu sitini nchini Iraq,katika jimbo la Mashariki la Diyala.bomu hilo lililenga mtaa wa kibishara ambapo zaidi ya watu arobaini walifariki huku pia zaidi ya hamsini kujeruhiwa.
Shambulio jingine lilitokea katika mji wa kusini mwa Basra,ambao kwa mara nyingi haukuwahi kukumbwa na milipuko nchini humo.Maofisa mjini humo wanasema bomu hilo lilitegwa katika mtaa wa al Zubair liliwauwa watu kumi.
Kundi la kiislam la IS limethibitisha kuhusika katika mashambulizi hayo.Katika mji wa Baghdad polisi wamesema kuwa bomu lililotegwa ndani ya gari liliwauwa watu kumi na tatu katika kitongoji cha Husseiniya.

Monday 5 October 2015

MAONI NA POLE MITANDAONI-KIFO CHA MCH. MTIKILA!

-Mwigulu Nchemba.
Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha mwanasiasa nguli Mch. Christopher Mtikila. Tumepata pigo kama taifa, tuungane kumuombea apumzike kwa amani.

-Malisa Godlisten.
Buriani Mch. Mtikila. Hatima ya maisha yetu ipo mikononi mwa Mungu pekee. Tusiwadhihaki wagonjwa bali tuwaombee maana hakuna ajuaye kesho yake. However, tunakuombea upumzike kwa amani.

-Manawa M. Bukwimba.
Waliosema Lowasa ni mgonjwa sijui maiti inayotembea, wameanza kuwa maiti wao. Mwingine kafariki leo kwa ajali na wanayemwita maiti anaendelea na maisha yake ya kawaida. Ugonjwa na uzima ni kudra toka kwa Allah. MUNGU NI MWEMA SANA.

-Bob Chacha Wangwe.
Ni dhahiri kuwa Tanzania imepoteza mtu muhimu sana. Pamoja na mapungufu ya kibinadamu, Mchango wa Rev Chritopher Mtikila katika kujenga Demokrasia nchini ni wa MFANO. Nimeumizwa sana na kifo chake. R.I.P!

-Mimi Mwanakijiji.
Harakati za mabadiliko na ukuaji wa demokrasia Tanzania zimepata pigo kubwa leo hii. Habari za kifo cha mpigania haki za raia na binadamu Mchungaji Chritopher Mtikila nimezipokea kwa masikitiko makubwa na mshitiko usio na kifani.

-Joyce Kiria.
May yo soul Rest in eternal peace Mchungaji Mtikila, Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Atukuzwe mola wetu na utukufu wake.

-Halima James Mdee.
R I P Rev. Mtikila. Pole kwa familia, pole kwa wanachama na wapenzi wako. Bwana Ametoa, Bwana ametwaa.

-Philipo Mwakibinga.
Kwasababu ya rangi zao za Bendera! Kwasababu ya mihemko yao ya uchaguzi, watakupuuza na kukupeza. Mimi nitakukumbuka Daima kwa uzalendo wako juu ya Taifa letu na hasa asili yetu na hasa asili yetu watanganyika. R. I. P Mtikila.

-Shy-Rose Bhanji.
Mungu akulaze pema Mchungaji Mtikila.... Hakika duniani tunapita tu.

-John Mnyika.
Pole sana kwa familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na kuondokewa  Mwenyekiti wa DP Mch. Mtikila. Mungu amjalie kuionja mbingu yake.

************************************

Sunday 4 October 2015

NA AYOS MATA MAESTRO:-KUELEKEA DIMBA LA EMIRATES (ARSENAL VS MANCHESTER UNITED)

Na: Ayoub Hinjo
Arsenal dhidi ya Manchester United ni mechi yenye hisia kali na msisimko usiolezeka. Ni mechi ya kihistoria sababu hizi ni timu mbili kubwa na zina mashabiki wengi duniani kote. Ni wapinzani kweli kweli iwe ndani au nje ya uwanja,mafanikio yao ni kielelezo tosha kuonyesha hawa ni wapinzani wakubwa. Mambo yafuatayo yanaweza kuleta taswira ya mchezo huu mkali.

ARSENAL

1: SAFU YA ULINZI

Safu ya ulinzi ya Arsenal ina watu makini wa kazi ambao wamekosa mseto mzuri ndani ya safu hiyo. Kukosekana kwa Konsielny ni pigo kubwa kwa timu hiyo sababu ni beki tegemezi ambaye anajituma na kujitolea kwa ajili ya timu,pindi inapokuwa na hali ngumu. Konsielny na Paulista wanatengeneza mseto mzuri ambao utajenga ukuta mgumu wa kati wa timu hiyo. Kukosena kwa Konsielny kunatoa nafasi kwa beki mzoefu na mkongwe Per Metersacker ambaye kwa mechi za karibuni alikuwa anakaa benchi kutokana na majeraha madogo madogo. Urejeo wa Metersacker kunaleta imani kubwa kwenye ulinzi sababu ni beki mwenye uwezo wa kusukuma timu kwenda mbele kwa pasi zenye macho na zenye madhara,lakini shida inaweza kuja kwao kama safu ya ushambuliaji ya wapinzani itatoa presha kubwa na kuwaweka kwenye pilikapilka muda wote sababu wote sio wazuri sana kwenye kufanya marking za haraka kwenye nafasi muhimu. 

Ugumu na ubishi alionao Paulista ni kielelezo tosha kuwa atafanya kazi kubwa kwenye safu hiyo na kazi ya Metersacker itakuwa kufukia mashimo ambayo Paulista atakuwa akiyatengeneza na kuziba kabisa mianya ambayo mipira itakuwa ikipitishwa.

2: SAFU YA KIUNGO

Mara nyingi kwenye timu ya Arsenal safu ya kiungo huwa na ubora mkubwa kuliko wapinzani. Conquelin na Cazorla wamejenga mseto mzuri ambayo umeleta hatamu nzuri kwenye timu na uelewano wao wa kuzuia na kupandisha timu umekuwa mchango mkubwa kwenye timu hiyo kupata matokeo chanya mara nyingi.

Bila kusahau mchango wa Aaron Ramsey ambaye amekuwa shujaa wa timu miaka ya karibuni. Ramsey ni kiungo ambaye anaweza kubadilika muda wowote kutokana na mfumo au kasi ya timu yake au wapinzani. Uwezo wake mkubwa wa kufunga umetokana na kasi yake ya kusogea eneo la mwisho la kisanduku cha adui.

3: SAFU YA MASHAMBULIZI

Alexis Sanchez na Theo Walcott wanatoa mchango mkubwa kwenye safu hiyo wakisaidiana na Giroud na Ozil. Muunganiko wao umekuwa na madhara kwenye safu ya ulinzi kutokana na kasi na uwezo binafsi wa kuweza kutengeneza mashambulizi ambayo wamekuwa wakiyatengeneza. Sanchez hakufunga mechi 6 wala kutoa pasi ya goli kwenye mechi zilizopita,lakini mechi ya 7 amefunga magoli matatu ambayo leo yanaweza kumletea morali ya kupambana na kuwa na hamu ya kuendelea kufunga pia Walcott amekuwa mwiba kwa mabeki hasa baada ya kutumika kama mshambuliaji wa kati kwa sasa.

Tatizo ambalo linatengenezwa na safu ya ushambuliaji ya Arsenal ni kushindwa kutumia nafasi ambazo wanakuwa wanazitengeneza. Nafasi zinatengenezwa nyingi lakini umakini wao umekuwa mdogo kwenye kuzitumia vyema nafasi hizo.

MANCHESTER UNITED

1: SAFU YA ULINZI

Mseto ambao umetengenezwa na Smalling na Blind umekuwa imara kadri siku zinavyokwenda. Uwezo wa kuzuia hasa Smalling amepevuka kiakili na anafanya kazi vyema kila siku inayoitwa leo. Blind mara nyingi amekuwa akitumika kama beki wa pembeni au kiungo mkabaji,lakini uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi umemweka sambamba na Smalling kati kati ambao wametengeneza mseto mzuri. Uwezo wa Blind ni kupiga pasi na kuhold wapinzani washindwe kusogelea lango la timu.

Safu ya ulinzi ya pembeni ni bora lakini shida ni pale Valencia anapotumika kama beki wa pembeni,uwezo finyu wa kuzuia umekuwa unakaribisha mashambulizi mara kwa mara kwenye sanduku la timu yake na kuwa weka kwenye mashaka makubwa wenzake.

2: SAFU YA KIUNGO

Machaguo mengi ya wachezaji yanaleta ushindani kwenye timu. Schweisteiger, Carrick,Herrera na Schneiderlin kila mmoja ana sifa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza. Uwezo wa kuzuia,kushambulia na kutengeneza nafasi za mashambulizi hufanywa na safu hiyo ambayo imekuwa na madhara sana kwa wapinzani.

3: SAFU YA MASHAMBULIZI

Martial,Martial,Martial ni kinda mwenye kipaji ambaye amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu. Uwezo wa kufunga magoli na kutengeneza nafasi za magoli ni uwezo mzuri na ameonyesha mwanga wa kuwa tegemezi wa timu miaka kadhaa ijayo. Rooney bado hayupo kwenye kiwango bora lakini rekodi ambayo amekuwa nayo dhidi ya Arsenal inaweza kumtia hamasa ya kuonesha uwezo wake wa siku zote anapokutana nao. Rooney ndiye mchezaji wa Manchester United ambaye amefunga magoli mengi dhidi ya Arsenal kwenye ligi,magoli 9 na amefunga magoli 12 kwenye michuano yote aliyocheza dhidi yao. Rekodi aliyonayo inaweza kumuweka kwenye kilele chake. Mata ni mchezaji muhimu kwenye timu,pasi za magoli na uwezo wa kufunga vimemuweka kwenye chati ya ubora sasa ni ufunguo wa Manchester United kwenye mashambulizi. Memphis bado ana mengi ya kujifunza lakini kocha anamjengea imani ya kumwamini kwenye kila mchezo na kumpa nafasi aoneshe alichonacho ni upcoming nzuri na aangaliwe kwa jicho la tatu kwenye mchezo huo.

Bado tatizo ambalo United wanalo ndilo linalowasumbua Arsenal pia. Nafasi ambazo zinatengenezwa na timu ni nyingi lakini zimekuwa hazitumiki vyema.

HITIMISHO:

Arsene Wenger na Louis van Gaal ni makocha wazoefu na wenye mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kuleta alama muhimu kwenye timu.

Arsenal imekuwa timu ngumu hasa msimu uliopita imekuwa inajiamini inapocheza na timu kubwa na kupata matokeo wanayotaka. Miaka kadhaa iliyopita ili kuwa timu ambayo inafungwa magoli mengi kila walipocheza na timu kubwa.

Timu inatakayo tumia nafasi vizuri ina asilimia kubwa ya kushinda.

Imeandaliwa na..........
(Ayo's Mata Maestro) E-mail: hinjo38@gmail.com

Mwanasiasa mkongwe, Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia kwa ajali ya gari asubuhi ya leo.

Mwanasiasa mkongwe, Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha DP na Mtumishi wa Mungu, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki kwenye ajali ya gari asubuhi ya leo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na kwamba walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.

Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU CHRISTOPHER MTIKILA. AMEN.

Saturday 3 October 2015

UCHAMBUZI YAKINIFU DERBY KUBWA SITA WIKEND HII,EPL,BUNDESLIGA,LIGUE 1,LA-LIGA NA EREDIVISIE

Kwa mara nyingine tena tunakutana katika anga hili la soka lenye kila radha na kachumbari yenye mchanganyiko wa kipekee. Najua gumzo kubwa katika medali ya soka la kibongo ni sakata la Nyosso ambapo naona kuna wachambuzi wanajitaftia ushujaa wa kijinga kupitia hili swala ila pia kumbuka jambo jingine ambalo limeteka hisia za wadau wa soka ni rekodi ya C.Ronaldo kufikisha magoli 500 katika historia ya kucheza kwake soka huku akifanikiwa kuwa mfungaji wa muda wote wa Real Madrid.

Pasipo kuchelewa ngoja siku ya leo tujikite Barani Ulaya sehemu ambayo ni kiburudisho tosha cha mchezo wa soka.
Skia juma hili kuna mechi nyingi sana ambazo zimeteka kila kona yenye wanamichezo kule Ufaransa kuna mchezo wa Psg dhidi ya Marseille kule Uholanzi kuna utamu wa Psv dhidi ya Ajax nikichungulia pale Ujerumani kuna ngoma ya kusisimua kati ya Bayern Munich dhidi ya Dortmund.

Wakati nikigeuka kushoto pale Hispania ni Real Madrid dhidi Athletico Madrid nikitupa jicho la upande wa Kulia pale Visiwa vya Malkia Uingereza kuna kimbembe cha Arsenal watakao pambana na Manchester United huku pale katika Jiji la Liverpool ni kimuhemuhe cha ndugu wawili Liverpool na Everton.
::::: PSG VS MARSEILLE

Le Classique
Nikianza kuangaza mchezo wa Psg na Marseille ni mchezo mkubwa kwa ukubwa wa majina ya timu hizi lakini nikiangaza uhalisia wa sasa hivi Marseille hana cha kupata mbele ya kikosi cha Blanc.

Kwa mara ya kwanza timu hizi zilikutana tarehe 12/12/1971 mara ya mwisho ni msimu uliomalizika wa 2014/2015 na kushuhudia Psg wakiibuka na ushindi wa goli 3-2 na kwenye historia ya vilabu hivi pindi vikikutana ushindi mkubwa zaidi ni ule wa 8/1/1978 kwa Paris Saint German kuibuka na ushindi wa goli 5-1.

Siku zinavyo zidi kwenda ndivyo ambavyo tunashuhudia kiwango kibovu cha Marseille msimu huu tofauti na wapinzani wao Psg timu ambayo imekamilika kila Idara huku Marseille wakiteswa na ubutu wa safu ya ushambuliaji lakini pia safu ya ulinzi haipo vyema hivyo wanakazi ya kufanya walau wapate pointi moja mbele ya Psg ambayo ipo katika hali ya ushindi na uimara wa sehemu zote tatu safu ya Ulinzi,Kiungo na Safu ya Ushambuliaji.
Ukiangaza katika msimamo Psg ni vinara wakiwa na pointi 20 wakati Marseille iliyo chini ya kocha raia wa Hispania Jose Miguel aliechukua nafasi ya Muargentina Marcelo Bielsa anawakati mgumu kwani wana pointi 8 wakiwa nafasi ya 15

Kuwashinda Psg panahitaji kazi ya ziada kwa maana hiyo bado kwa kiwango cha Marseille hivi sasa Psg wananafsi kubwa ya kushinda mchezo huu ambao hutawaliwa na ubabe mwingi na kwa mchezaji kupewa kadi nyekundu si jambo la kushtusha. :::::::: AJAX VS PSV
Nikiangaza kule kwa jamaa zangu Uholanzi tutashuhudia wafalme wawili wa soka Nchini humo Psv dhidi ya Ajax timu ambazo zimekuwa na utawala wa kupokezana katika Ligi yao. Kumbuka Ajax wametwaa ubingwa wa Eredivisie mara 25 huku utawala wao wa mwisho ni msimu wa 2013-2014 lakini wapinzani wao Psv wakitwaa ndoo mara 19 ambapo kwa sasa ni mabingwa watetezi. Ukiangaza takwimu za vilabu hivi pindi zikikutana kumekuwa na ushindani mzuri kwani hata katika upande wa takwimu hawaja achana sana wamekutana mara 129 mara ya kwanza ikiwa ni 12/4/1931 Ajax akiibuka na ushindi wa goli 4-2 na kwa ujumla Ajax kashinda mara 56 huku Psv akishinda michezo 51. Kwa muangazo wa ushindani wa sasa ni vigumu kubashiri ushindi mkubwa kwa timu moja wapo kama ule wa tarehe 22/11/1964 Ajax alipo shinda 5-0. Kocha wa sasa wa Ajax beki wao wa zamani Franciscus de Boer msimu huu timu yake imekuwa na matokeo mazuri wakiwa hawaja poteza mchezo hata mmoja wakitoa sare moja na kuwa kileleni kwa pointi 19 wakati mpinzani wake kiungo wa zamani wa Psv kocha wa sasa Phillip Cocu bado hawajawa na msimu mzuri wakiwa na pointi 14. Ajax wako vyema katika safu ya ulinzi huku jicho lao likiwa ni mshambuliaji El Ghazi huku Psv walio wazuri kushambulia kupitia pembeni wakimtegemea De Jong. Kwa tasmini ya uhalisia Ajax ana nafasi kubwa kushinda mbele ya Psv kutokana ma uimara wao hasahasa safu ya Ulinzi. ::::::::: BAYERN MUNICH VS DORTMUND
Der Klaassiker
Sasa Tuangaze kule Ujerumani ambapo kuna ngoma tamu na yenye radha ya kipekee Bayern Munich na Dortmund. Unajua soka la Ujerumani lina radha ya kipekee sana kutokana na ushindani wa vilabu vyao licha ya ligi kuonekana ya mtawala mmoja ambae ni Bayern Munich. Unajua katika mchezo huu hakuna haja ya kuangalia historia kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote msimu huu. Tunaona kikosi cha Guardiola bado kimezidi kupata ushindi wa asilimia 100 huku kikosi kikichagizwa na kiungo Douglas Costa ambae amekuwa na kiwango bora kabisa katika msimu wake wa kwanza ndani ya Bavarian. Ubora wa Bayern msimu huu umetufanya tuzidi kuona ubora wa mshambuliaji raia wa Poland Robert Lewandowski ambae ndani ya michezo mitatu ya karibuni kafunga magoli 10. Dortmund ujio wa kocha mpya Thomas Tuchel msimu huu umefanya tuione Dortmund mpya ambayo mpaka sasa katika michezo 14 michuano mbalimbali hawaja poteza wameshinda michezo 11 na kutoa sare 3 huku timu ikionekana kuwa nzuri zaidi katika safu ya ushambuliaji ambayo Muafrika Pierre Aubameyang akiwa katika kiwango bora kabisa kwani mpaka sasa katika ligi anagoli 9 nyuma ya Lewandowski mwenye magoli 10. Sasa ukija katika uhalisia utagundua Bayern ni timu ambayo imesukwa na kuimalika sehemu zote tofauti na Dortmund ambayo bado safu ya ulinzi inaruhusu magoli kizembe licha ya uhodari wa safu ya ushambuliaji. Ni mchezo ambao utakuwa na presha kubwa kwa uhalisia wa ushindani katika ligi Bayern ni vinara wakiwa na point 21 huku Dortmund wakiwa na point 17 kwa maana hiyo Dortmund wanahitaji punguza gepu la pointi na ili wawe na ndoto za ubingwa basi walau washinde mchezo huu.

Kwa uimara wa vikosi vyote wala usitaraji kuiona historia ya 27/11/1971 pale ambapo Bayern alishinda goli 11-1 Dortmund na safari hii kuna kimbembe kizito kwani timu hizi zimekutana mara 108 huku Bavarian wakishinda mara 49 kwa maana hiyo wanautafuta ushindi wa 50 wakati Die Borussen wameshinda michezo 29 wakitafuta ushindi wa 30 au pengine tukashuhudia sare ya 31.

Kwa kutumia kaunta na kupita pembeni kwa maana ya krosi itakuwa chagizo la ushindi kwa Dortmund lakini wanatakiwa kuwa makini sana upande wa Costa ambao ni hatari zaidi.

Tusubiri tuone kama Bayern wataandika historia ya Bundesliga kwa kushinda michezo 8.
:::: ATHLETIC MADRID VS REAL MADRID

El-Derbi Madrileno Hilo ndo jina linalo tamkwa zaidi nchini Hispania hususani viunga vya Jiji la kifalme Madrid. Wajanja wa mitaa hiyo wanafananisha vita vya watoto wa Uswazi dhidi ya watoto wa kishua. Unajua radha ya Charanga sharti uicheze ingawa lazima uwe mwepesi wababe hawa wamekutana mara 210 huku Real Madrid wakiibuka na ushindi mara 107 sare 50 na Atletico Madrid wakishinda michezo 53. Katika La-Liga Real Madrid wameshinda mara 85 wapinzani wao wakishinda mara 38 sare 33 katika michezo 156. Msimu uliopita tulishuhudia dhahma kwa Real kupigwa michezo yote ya ligi nyumbani na ugenini kwa kufungwa 2-1 na 4-0. Rojiblancos ambao ni Atletico Madrid imekuwa ni timu inayo cheza kitimu zaidi licha ya kutokuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kama Real Madrid. Simeone kaijenga timu yake kwa misingi ya kupambana kwapamoja pasipo kutegemea kiwango cha mchezaji mmoja, msimu huu bado hawajawa vyema sana lakini ngoma ya watani hiko huwa sio sababu kuu. Los blancos walio chini ya Benitez tumeona wakiwa na kiwango kizuri huku kocha huyo akifanya mabadiliko ya hapa na pale hasahasa safu ya ushambuliaji kwa kumchezesha Bale namba 10 kitu ambacho kimeonekana kuwa na manufaa zaidi kwa Benzema akiwa kama ndie mshambuliaji namba 9 na kwa sasa anamagoli 5 akiwa kinara sawa na Ronaldo. Unajua Benitez ni miongoni mwa makocha waliopita ligi nyingi kwa maana ni mtu anae jua kubadilika kimbinu dhidi ya timu ambayo anakutana nayo na ukiangaza mchezo huu dhidi ya watani wao ambapo mara nyingi wanacheza soka la undava halito mpa tabu sana.

Kocha huyu Rafael tangu atue Santiago Bernabeu amekuwa anabadili wachezaji mara kwa mara na kati ya wachezaji 23 wa klabu hiyo tayari wachezaji 22 wamepata walau nafasi ya kucheza kulingana na uhitaji wa mchezo na kubadilika huko mara kwa mara imekuwa inatoa ugumu kwa mpinzani anaekutana nae. Kuna sare naiona kwenye mchezo huu ambao utawala wa mpira utakuwa kwa Real huku Simeone akishambulia kwa kustukiza kwa kumtumia Mfaransa Griezman na huenda akamuanzisha Torres ambae amekuwa anafanya vyema mbele ya Real. Upande wa Real nadhani chagizo ni ndelemo za Ronaldo kwa historia aliyo iandika Bernabeu kwa maana atahitaji kuendeleza moto wake wa kufunga . Kumbuka Real wanapoint 14 nafasi ya 3 na A.Madrid wana point 12 nafasi tano katika msimamo wa ligi.


:::::: EVERTON VS LIVERPOOL

The Merseyside derby
Haya safari inamalizikia Uingereza katika Ligi kuu inayojulikana kama EPL sehemu ambayo imetanda giza nene kutokana na kushuka kwa viwango vya wachezaji wengi katika timu kubwa na kupelekea kufanya vibaya kwenye michuano ya Vilabu Barani Ulaya. Tukitupia jicho pale Jiji la Liverpool kutakuwa na sebene lililopoa kwa maana timu ya Liverpool na Everton hivi sasa wanaonekana kuwa na viwango vinavyo shabihana. Kiukweli hakuna wavumilivu kama mashabiki wa Liverpool lakini hakuna mzembe kama kocha wao Rogers kwa maana bado hajui cha kufanya mbele ya mashabiki wa Liverpool. Kiukweli amekuwa haeleweki katika maswala ya kutumia mifumo kulingana na wachezaji waliopo pia timu imekuwa haina muunganiko mzuri inapata matokeo kwa kubahatisha huku safu ya Ulinzi ikiwa kichocheo cha matokeo mabovu. Dhidi ya Everton Sturridge karejea na tunajua umuhimu wake na mchezo huu ndo atakuwa mwanga kwa Rogers . Everton wao hawatabiliki ingawa msimu huu walau wako vyema wakichagizwa na safu ya ushambuliaji inayo ongozwa na Kone pamoja na Lukaku.

Mchezo lazima utakuwa wa kasi na timu zote zikishambuliana hapa na pale lakini matokeo yataamuliwa na safu za ulinzi kwa maana ya makosa ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa katika beki za timu hizi.

Nakumbuka mara ya kwanza kabisa timu hizi zilipokutana ilikuwa ni 13/10/1894 hapo hata Tanganyika haitambuliki kwa jina hilo na mchezo huo Everton wakaibuka na ushindi wa goli 3-0 kisago kikubwa ni mwaka 1935 Liverpool akishinda goli 6-0 ila msimu uliomalizika mchezo wa mwisho tukashuhudia sare ya 0-0.

Kumbuka wamesha kutana mara 224 kwa maana hiyo mchezo wa jumapili utakuwa wa 225 Liverpool wameshinda michezo 88 Everton akishinda michezo 66 na sare 70.

Ni hayo ila kwa kiwango cha hivi sasa kuna kila dalili za Liverpool kuendelez kupotea kama hakuta fanyika mabadiliko maana tumekumbuka enzi zile za kina Ian Rush,Dixie Dean ngoja tusubiri ujuzi wa Milner na Barry wakipigania timu zao Everton nafasi ya 5 pointi 12 huku Liverpool nafasi ya 9 point 11.

::::
ARSENAL VS MANCHESTER UNITED



Hapa bhana pana maneno mengi sana lakini pia kuna majigambo ya kila namna kwa mashabiki wa vilabu hivi ingawa upande mmoja huonekana kulemewa na kejeli za hapa na pale nawazungumzia mashabiki wa Manchester United majigambo yao kwa mashabiki wa Arsenal.

Kumbuka kwa wewe mshabiki wa kati ya vilabu hivi kwa mara ya kwanza kabisa timu hizi zilikutana 13/10/1894 kipindi hicho Manchester walijulikana kama Newton Heath na Arsenal wakitambulika kama Woolwich Arsenal na kwenye mchezo huo walitoka sare ya kufungana 3-3.

Sasa timu hizi zimekutana mara 221 safari hii itakuwa mara 222 na mara hizo 221 Manchester United wameibuka na ushindi mara 93 Arsenal wakishinda mara 79 na tukashuhudia sare 49 kwa maana hiyo Arsenal anatafuta ushindi wa 80, Manchester United wanatafuta ushindi wa wa 94 au pengine tukashuhudia sare ya 50.

Mchezo wa mwisho walipo kutana tulishuhudia sare ya 1-1 lakini kumbuka kipigo kikubwa zaidi pindi timu hizi zilipo kutana Arsenal alipokea kichapo cha goli 8-2 ilikuwa ni tarehe 28/8/2011 mchezo ambao umekuwa ukiwatesa sana mashabiki wa Arsenal mpaka leo.

Ni mchezaji mmoja tu aliebaki ambae anauwezo wa kuboresha zaidi rekodi yake ya kufumania nyavu pindi timu hizi zikikutana si mwingine bali ni Rooney ambae mpaka sasa anagoli 9 akiwa kinara.

Arsenal wapo nafasi ya 4 wakiwa na pointi 13 wakati Manchester United wapo kileleni kwa mara ya kwanza baada miaka 2 wakiwa na pointi 16.

Sasa kuelekea katika mchezo huu ambao umekuwa na matokeo ya upande mmoja kwa maana hata kama Manchester United hawafanyi vyema basi pindi wakikutana na Arsenal kumekuwa na mteremko.

Safari hii hali ya mambo ipo kinyume kwa maana katika misimu miwili Manchester United haikuwa vyema ukilinganisha na Arsenal lakini bado walikuwa na uhakika wa kupata matokeo mbele ya arsenal tunaona msimu huu kikosi cha Van Gaal licha ya kwamba bado kinatafuta ubora kama ule wa enzi ya Ferguson lakini wamekuwa na matokeo mazuri kuliko wapinzani wao kikosi cha Wenger ambacho bado hatuoni mabadiliko yoyote.


Tunaiona Arsenal ambayo nafasi ya kiungo mkabaji ni tatizo na kumekuwa hakuna mawasiliano mazuri kati ya safu ya beki za kati na kiungo kwa maana hiyo pasipo marekebisho kwa kuangalia kiwango kizuri cha Martial na Mata tutazungumza mengine.

Van Gaal kuelekea mchezo huu huku akiwa na kumbukumbu nzuri ya kutokufungwa na Arsenal katika mara mbili walizo kutana katika ligi nadhani marekebisho kwa upande wake ni katika beki kujisahau hapa na pale lakini kwa asilimia kadhaa anauwezo wa kupata matokeo mbele ya Arsenal.

Miaka 19 ya Mzee Wenger licha ya mafanikio makubwa aliyo ipatia Arsenal lakini ''CV'' yake inashuka kwa kasi sana na kama atacheza kama ambavyo tumeishuhudia Arsenal ikicheza mpira mwingi pasipo kujilinda katika Uefa basi itakuwa dhahma kwa upande wake mbele ya Mashetani wekundu.

Mpira sio historia kwa maana ya kuipa Manchester United ushindi lakini Arsenal wataamua matokeo yaweje kama watacheza kwa wimbi la Manchester hatuwawezagi basi itakula kwao mazima.

Ni hayo tu ngoja tusubiri michezo hii ya kusisimua Jumapili hii.


KWA MAONI NA USHAURI: