Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Monday 30 June 2014

"Utata" wa penati za Costa Rica na Ugiriki

 Photo: "Utata" wa penati za Costa Rica na Ugiriki
Hivi ndivyo penati zilivyopigwa baada ya mpira kumalizika 1-1
Costa Rica walianza, Celso Borges 1-0
Ugiriki wakasawazisha, Konstantinos Mitroglou 1-1
Bryan Ruiz (Costa Rica) 2-1
Lazaros Christodoulopoulos (Ugiriki) 2-2
Giancarlo Gonzalez (Costa Rica) 3-2
Jose Cholevas (Ugiriki) 3-3
Joel Campbell (Costa Rica) 4-3
Theofanis Gekas (Ugiriki) ALIKOSA PENATI
Michael Umana (Costa Rica) 5-3
Iwapo Michael Umana angekosa, ingebidi Ugiriki wapige penati yao ya tano, kwa kuwa walipata, hakukuwa na haja ya kufanya hivyo kwa sababu walikosa penati moja, hata wangefunga isingebadili matokeo. HAKUNA UTATA- Matokeo yalikuwa 5-3 ya mikwaju ya penati.

Hivi ndivyo penati zilivyopigwa baada ya mpira kumalizika 1-1
Costa Rica walianza, Celso Borges 1-0
Ugiriki wakasawazisha, Konstantinos Mitroglou 1-1
Bryan Ruiz (Costa Rica) 2-1
Lazaros Christodoulopoulos (Ugiriki) 2-2
Giancarlo Gonzalez (Costa Rica) 3-2
Jose Cholevas (Ugiriki) 3-3
Joel Campbell (Costa Rica) 4-3
Theofanis Gekas (Ugiriki) ALIKOSA PENATI
Michael Umana (Costa Rica) 5-3
Iwapo Michael Umana angekosa, ingebidi Ugiriki wapige penati yao ya tano, kwa kuwa walipata, hakukuwa na haja ya kufanya hivyo kwa sababu walikosa penati moja, hata wangefunga isingebadili matokeo. HAKUNA UTATA- Matokeo yalikuwa 5-3 ya mikwaju ya penati.

Orodha Kamili Ya Washindi Wa BET Awards 2014.

BET Awards 2014 ilifanyika jana Los Angeles, Marekani na kuwahusisha wasanii wa kimataifa kutoka katika kona mbalimbali za dunia.
Katika tuzo hizo, Beyonce Knowles, Pharrell Williams na August Alsina waling’aa zaidi. Beyonce alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo tatu ambazo ni Best Female R&B/Pop artist, Best Collaboration na Fandemonium.
Pharrell-na-Beyonce1
Pharrell na BeyonceMshindi wa tuzo ya Grammy, Pharrell Williams aliendeleza ushindi wake kwa mwaka huu baada ya kuibuka mshindi wa tuzo ya Video of the Year na Best Male R&B/Pop artist. Na August Alsina alishinda tuzo ya Best New Artist na Viewers’ Choice Award.
Muigizaji kutoka Kenya Lupia Nyong’o alikuwa moja kati ya washindi wa awali na alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Muigizaji bora wa kike (Best Actress)
Lupita-Nyongo1

Hawa ndio washindi wa BET Awards 2014
Best Female R&B/Pop Artist
Beyoncé

Best Male R&B/Pop Artist
Pharrell Williams

Best Group
Young Money

Best Collaboration
BeyoncĂ© f/ JAY Z – “Drunk In Love”

Best Male Hip-Hop Artist
Drake

Best Female Hip-Hop Artist
Nicki Minaj

Video of the Year
Pharrell Williams – “Happy”

Video Director of the Year
Hype Williams

Best New Artist
August Alsina

Best Gospel Artist
Tamela Mann

Best Actress
Lupita Nyong’o

Best Actor
Chiwetel Ejiofor

YoungStars Award
KeKe Palmer

Best Movie
12 Years a Slave

Subway Sportswoman of the Year
Serena Williams

Subway Sportsman of the Year
Kevin Durant

Centric Award
JhenĂ© Aiko – “The Worst”

Best International Act: Africa
Davido (Nigeria)

Best International Act: UK
Krept & Konan

Coca-Cola Viewers’ Choice Award
August Alsina f/ Trinidad Jame$ – “I Luv This Sh*t”

Fandemonium
Beyoncé


Endelea kutembelea www.bantutz.com kupta habari mbalimbali zinazowahusu watu mashuhuri ulimwenguni na habari mbalimbali kutoka katika kila pembe ya dunia.

Mfalme wa Saudi Arabia awashukia Waislamu wenye misimamo mikali

ISIL ni kundi la kijihadi lenye nguvu ambalo limeshiklilia eneo kubwa nchini Iraq, lengo lao ni kutaka kuanzisha serikali ya Kiislamu nchini humo.
ISIL (Islamic State of Iraq and Levant) ni kundi la kijihadi lenye nguvu ambalo limeshiklilia eneo kubwa nchini Iraq, lengo lao ni kutaka kuanzisha serikali ya Kiislamu nchini humo.
Siku ya Jumapili, Mfalme wa Saudi Arabia, Abdullah aliwakosoa vikali waislamu wenye misimamo mikali, “akiwakemea magaidi waache kuwatisha Waislamu”, kwenye hotuba yake ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhan.
Uislamu ni “dini ya umoja, mshikamano na ya kusidiana”, ila kuna baadhi ya watu “wamerubuniwa na miito ya uongo, inayowafanya kuufanya Uislamu uwe ni ugaidi”, alisema kiongozi huyo wa kifalme.
“Lengo lao ni kuleta utengano miongoni mwa Waislamu”, alisema huku akitolea mfano wa ghasia zinazofanywa na Islamic State of Iraq and the Levant (ISIL).
Kundi la kijihadi lenye nguvu ambalo limekuwa likiongoza kwa ghasia zinazofanywa na Wasunni nchini Iraq tangu June 9, walivyoweza kushika hatamu ya miji ya kaskazini na kushikilia maeneo makubwa.
ISIL hufanya shughuli zao Syria na Iraq na lengo ni kuanzisha serikali ya Kiislamu katikati ya mpaka wa mataifa hayo mawili, ila hali nchini Iraq inazitishia nchi za Jordan na Saudi Arabia.
“Hatutaruhusu magaidi, kuutumia Uislamu kwa malengo yao binafsi, kuwatisha Waislamu au kuzidunisha nchi na watu wake”, alisema Abdullah.
Mfalme huyo wa Saudia pia aliwatakia Waislamu wote “ulinzi, mafanikio na uimara” kwenye kipindi hiki cha Ramadhan ambao kwa nchi nyingi umeanza siku ya Jumapili.
Wakati wa Ramadhan, ambao ni mwezi mtukufu kwa Waislamu kwa sababu ni mwezi ambao kiutamaduni Koran ilishushwa mwezi huo kwa Mtume Muhammad (S.A.W), waumini wanakatazwa kula, kunywa, kuvuta, na kufanya ngono kuanzia mawio mpaka machweo.

Diamond akutana na Nelly kwenye Red Carpet ya BET,afunguka ya moyoni.

n1 
Tukio la BET awards 2014 limefanyika na mambo mbalimbali yalitokea, zaidi ya interview kwenye redcarpet Diamond amekutana na wasanii tofauti. Hivi sasa ameshare picha zake akiwa na msanii Nelly wakionekana kwenye mazungumzo na salamu. Hayo yote yametokea kwenye redcarpet ya BET usiku wa kuamkia leo 30/6.

n2
n3
n4

KOCHA WA ALGERIA ACHUKIZWA NA MASWALI KUHUSU MFUNGO WA RAMADHANI

Photo: KOCHA WA ALGERIA ACHUKIZWA NA MASWALI KUHUSU MFUNGO WA RAMADHANI

Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amekataa kutaja wachezaji wake watakaofunga mwezi wa Ramadhani, kabla ya mchezo wao wa Jumatatu (leo) dhidi ya Ujerumani.
Katika mkutano na waandishi wa habari, alikasirishwa baada ya kuulizwa suala hilo mara kadhaa.
"Hili ni suala binafsi, na kuuliza ni kukosa heshima na maadili" alisema kocha huyo kutoka Bosnia.
"Wachezaji watafanya wanavyotaka, na sitaki mtafaruku huu uendelee." Ameongeza.
Nahodha wa Algeria Madjid Bougherra amesema atafunga Ramadhani, lakini kiungo wa Ujerumani Mesut Ozil na beki wa Ufaransa Bacary Sagna walisema hawatofunga.
Kikosi cha Algeria kimekwenda Brazil na Hakim Chalabi, ambaye ni mtaalam wa utabibu wa michezo na mmoja wa wataalam wa kutegemewa wa FIFA kwa wachezaji wanaofunga Ramadhani.
Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amekataa kutaja wachezaji wake watakaofunga mwezi wa Ramadhani, kabla ya mchezo wao wa Jumatatu (leo) dhidi ya Ujerumani.
Katika mkutano na waandishi wa habari, alikasirishwa baada ya kuulizwa suala hilo mara kadhaa.
"Hili ni suala binafsi, na kuuliza ni kukosa heshima na maadili" alisema kocha huyo kutoka Bosnia.
"Wachezaji watafanya wanavyotaka, na sitaki mtafaruku huu uendelee." Ameongeza.
Nahodha wa Algeria Madjid Bougherra amesema atafunga Ramadhani, lakini kiungo wa Ujerumani Mesut Ozil na beki wa Ufaransa Bacary Sagna walisema hawatofunga.
Kikosi cha Algeria kimekwenda Brazil na Hakim Chalabi, ambaye ni mtaalam wa utabibu wa michezo na mmoja wa wataalam wa kutegemewa wa FIFA kwa wachezaji wanaofunga Ramadhani.

TETESI ZA USAJILI NA KOMBE LA DUNIA


Photo: TETESI ZA SOKA ULAYA
Arsenal huenda wakamkosa kipa wa Real Madrid, Iker Casillas, baada ya mpenzi wake kudai kuwa hatohama kutoka mji mkuu wa Spain, Madrid (Daily Express),lakini Arsenal huenda wakamsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata na wapo tayari kupambana na Tottenham na Inter Milan wanaomtaka pia (Daily Express), Barcelona wamefikia makubaliano yasiyo rasmi na Marcus Reus wa Borussia Dortmund. Reus amekuwa akifuatiliwa pia na Manchester United (Talksport), wakati huohuo Manchester United wapo tayari kupokea pauni milioni 12 kwa kiungo wake Marouanne Fellaini ambaye alisaini mwaka jana kutoka Everton kwa pauni milioni 27 (Daily Star), Chelsea wanajaribu kumsajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona katika mkataba ambao utahakikisha Arsenal haipati nusu ya faida itakayopata Barcelona (Daily Telegraph), Pepe Reina atarejea Liverpool kwa kuwa Napoli inashindwa kufikia madai ya Liverpool ya kubadili mkataba wa mkopo kuwa wa moja kwa moja (Metro), Manchester City watakamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Porto, Fernando ifikapo mwisho wa wiki hii na pia kukamilisha usajili wa Bacary Sagna kutoka Arsenal(Daily Mail), Everton wana tumaini watafanikiwa kupambana na Arsenal katika kumsajili Samuel Eto'o kutoka Chelsea (Daily Express). Share tetesi hizi na wapenzi wa soka. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Adios! 
 Mchezaji Roben ameomba msamaha kwa kitendo cha kujidondosha na kuzawadiwa penati iliyowavusha uholanzi hadi kufika robo fainali. 

Klabu ya Real Madrid wametoa ofa ya E31mil kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling,

 Vilabu vya Liverpool, Arsenal, Man United na Chelsea vipo katika rada ya kumuwania mchezaji Sami khedira kutoka Real Madrid (The Sun), 

Liverpool wametoa ofa ya E 25mil mchezaji Lazar Markovic.

 Liverpool wanatajia kutangaza leo au kesho asubuhi usajiri wa Adam Lallana ambaye alishafuzu vipimo siku ya ijumaa mchana. 

 Madrid wanasema kua wapo tayari kumuachia Di Maria kwa E 50 Mil na si vinginevyo (Daily Star). 

Manchester United wanakaribia kumsajili William Carvaro kutoka Sportings, wapo kwenye maongezi ya kupunguza thamani ya E 36 mil ili waweze kupata huduma ya mchezaji huyo (O Jogo).

 Liverpool wanamhitaji Iker Muniain kutoka Athletic Bilbao ila kikazo ni ada kubwa ya uhamisho wa E 45mil (AS). 

Arsenal wana mpango wa kumsajili kinda la Southampton Morgan Schneiderlin mwenye thamani ya E 20 (Daily Mirror).

 Liverpool wameomba FIFA imruhusu Suarez kufanya mazoezi na klabu wakati huu wa miezi minne aliyosimamishwa (Daily Express).

 Liverpool wamepata upinzani kutoka Tottenham kwenye kupata huduma ya mchezaji Divock Orig (Daily Mirror).

 Barcelona wanasema hawatishwi na mpango wa kumsajili L Suarezi kwa E 100Mil kwani wapo tayari kuitoa hiyo fedha na wanatoa hiyo ofa wiki hii baada ya kukubaliana na Suarezi mwenyewe (Daily Mail). 

Manchester United Wapo tayari kutoa kitita cha E 6Mil kupata saini ya James Rodriguez ambaye wanatarajia kumpata mapema ( Guardian). 


Joel Camplee apata kibali cha kucheza Uingereza,aleta ahueni kwa Arsenal.

JOEL CAMPBELL APATA KIBALI CHA KAZI ENGLAND
Photo: JOEL CAMPBELL APATA KIBALI CHA KAZI ENGLAND 

Joel Campbell amethibitisha kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba amepokea kibali cha kufanya kazi nchini England jana.

Mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Arsenal misimu miwili iliyopita kutoka klabu yake ya nyumabani ya Saprissa, amekua akicheza kwa mkopo nje ya England sababu kubwa ikiwa ni kunyimwa kibali cha kufanya kazi England. 

Campbell alisema: “Nina furaha nimepokea kibali cha kazi nchini England…Bado nasubiri mambo mazuri,” alitweet.

Baada ya kufanya makubwa na kucheza mechi za kutosha timu ya taifa ya nchi yake(Costa Rica) ili kufaulu kupata viza na kubali cha kazi, sasa kijana huyo mwenye miaka 21 anaweza kushiriki katika michezo  ya maandalizi msimu mpya na the Gunners. 

Ingawa anaonekana anaweza kuwemo katika kikosi cha jumla cha Arsenal, lakini ni mapema kusema kama Campbell ataweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza Emirates msimu mpya ujao. 
Kwani kwa sasa inasememkana Wenger yupo mbioni kusajili straika ili kuongeza ushindani kwa Lukas Podolski, Olivier Giroud na Yaya Sanogo. 
Ila kwa sasa ni rahisi kusema kwamba ataweza kucheza klabu za Premier League kwa mkopo hasa Crystal Palace wameshaanza kuonesha kumtaka kwa mkopo kwa ajili ya msimu ujao. 

Maoni Yako
Joel Campbell amethibitisha kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba amepokea kibali cha kufanya kazi nchini England jana.

Mshambuliaji huyo ambaye alisajiliwa na Arsenal misimu miwili iliyopita kutoka klabu yake ya nyumabani ya Saprissa, amekua akicheza kwa mkopo nje ya England sababu kubwa ikiwa ni kunyimwa kibali cha kufanya kazi England.

Campbell alisema: “Nina furaha nimepokea kibali cha kazi nchini England…Bado nasubiri mambo mazuri,” alitweet.

Baada ya kufanya makubwa na kucheza mechi za kutosha timu ya taifa ya nchi yake(Costa Rica) ili kufaulu kupata viza na kubali cha kazi, sasa kijana huyo mwenye miaka 21 anaweza kushiriki katika michezo ya maandalizi msimu mpya na the Gunners.

Ingawa anaonekana anaweza kuwemo katika kikosi cha jumla cha Arsenal, lakini ni mapema kusema kama Campbell ataweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza Emirates msimu mpya ujao.
Kwani kwa sasa inasememkana Wenger yupo mbioni kusajili straika ili kuongeza ushindani kwa Lukas Podolski, Olivier Giroud na Yaya Sanogo.
Ila kwa sasa ni rahisi kusema kwamba ataweza kucheza klabu za Premier League kwa mkopo hasa Crystal Palace wameshaanza kuonesha kumtaka kwa mkopo kwa ajili ya msimu ujao.

Maoni Yako

Beki kisiski wa Ivory Coast mbioni kujiunga Arsenal.

Photo: Marseille wameonyesha kuvutiwa na beki wa kulia wa Toulouse,Serge Aurier lakini raia huyo wa Ivory Coast anasema anataka kujiunga na klabu ya Arsenal huku thamani yake ikifikia kiasi cha Euro milioni 8. 
Mpaka sasa hakuna la msingi lililofanyinywa na Arsene Wenger ingawa beki huyu ambaye hupanda na kushuka ameweka bayana anataka kuchezea Arsenal. 
Binafsi nitajisikia vibaya sana Wenger akidai tuna Jenkinson kama beki mbili na hatumuhitaji Serge Aurier.
 
Marseille wameonyesha kuvutiwa na beki wa kulia wa Toulouse,Serge Aurier lakini raia huyo wa Ivory Coast anasema anataka kujiunga na klabu ya Arsenal huku thamani yake ikifikia kiasi cha Euro milioni 8.
Mpaka sasa hakuna la msingi lililofanyinywa na Arsene Wenger ingawa beki huyu ambaye hupanda na kushuka ameweka bayana anataka kuchezea Arsenal.
Binafsi nitajisikia vibaya sana Wenger akidai tuna Jenkinson kama beki mbili na hatumuhitaji Serge Aurier.

Arsenal wauza hisa za Carlos Vela,na kufuta matumaini ya kumrejesha.


Photo: VELA BYE BYE

Baada ya tetesi zilizodumu kwa muda mrefu kuhusu Carlos Vela kurejea Arsenal, The Gunners wameamua kuuza shea zao zilizobakia zinazohusu usajili klabuni Real Sociedad.
Arsenal wamepokea £8.8m kwa ajili ya kuondoa kipengele cha kumnunua tena Vela kwa bei kiduchu na wanaweza kupewa tena hadi £4m kutegemea na idadi ya michezo atakayoichezea klabu hiyo ya Spain.
Kwa sasa iwapo Arsenal itamuhitaji Vela basi ada haitakua tena £3.5m bali ni ile watakayoitaka Real Sociadad. Na iwapo atauzwa kwa timu nyingine kuna asilimia chache watapewa Arsenal.

Umeliaonaje hilo dili?
Baada ya tetesi zilizodumu kwa muda mrefu kuhusu Carlos Vela kurejea Arsenal, The Gunners wameamua kuuza shea zao zilizobakia zinazohusu usajili klabuni Real Sociedad.
Arsenal wamepokea £8.8m kwa ajili ya kuondoa kipengele cha kumnunua tena Vela kwa bei kiduchu na wanaweza kupewa tena hadi £4m kutegemea na idadi ya michezo atakayoichezea klabu hiyo ya Spain.
Kwa sasa iwapo Arsenal itamuhitaji Vela basi ada haitakua tena £3.5m bali ni ile watakayoitaka Real Sociadad. Na iwapo atauzwa kwa timu nyingine kuna asilimia chache watapewa Arsenal.

Umeliaonaje hilo dili?

Rekodi ya Suarez kung'ata wachezaji wenzake

Photo: SUAREZ NA KUUMA WACHEZAJI WENZAKE 

2010 | Alifungiwa mechi 7 kwa kosa la kumuuma mchezaji wa PSV, Otman Bakkal kipindi hicho akiichezea klabu ya Ajax.

2012 | Aliuma tena safari hii alifungiwa mechi 10 na muathirika wa meno yake alikua ni beki wa Chelsea Branislav Ivanovic. 

2014 | Luis Suarez alionekana kuuma bega la Girogio Chiellini beki wa Italy katika mashindano ya Kombe la Dunia huko Brazil. FIFA bado kuamua adhabu ambayo atapewa.

Pichani; Pozi lake baada ya kumuuma jana Chiellini.

Nini maoni yako juu ya tabia hii, afungiwe mechi ngapi?
2010 | Alifungiwa mechi 7 kwa kosa la kumuuma mchezaji wa PSV, Otman Bakkal kipindi hicho akiichezea klabu ya Ajax.

2012 | Aliuma tena safari hii alifungiwa mechi 10 na muathirika wa meno yake alikua ni beki wa Chelsea Branislav Ivanovic.

2014 | Luis Suarez alionekana kuuma bega la Girogio Chiellini beki wa Italy katika mashindano ya Kombe la Dunia huko Brazil. FIFA bado kuamua adhabu ambayo atapewa.


Nini maoni yako juu ya tabia hii, afungiwe mechi ngapi?

Wenger akana kumsajili Mario Balotelli.

 
 Photo: Wenger, akionekqna kwenye televisheni ya beIN Sport's World Cup show, aliulizwa na Ruud Gullit kama anamnunua straika wa zamani wa Manchester City Mario Balotelli, na jibu lake likawa: 'Hapana. Hapana, Hiyo imetungwa.

'Hatuwezi kuamini vyote kwenye mitandao na magazeti.

'Kuna wakati tetesi hizi hutengenezwa na majenti ama waandishi ili kupata habari, si kweli.'

Milan bado wanahaha kutafuta mnunuzi wa straika huyo mwenye miaka 23 tu.

Balotelli, Arsenal hakuna dili hilo. Habari hii ni nzuri ama mbaya kwako
Wenger, akionekqna kwenye televisheni ya beIN Sport's World Cup show, aliulizwa na Ruud Gullit kama anamnunua straika wa zamani wa Manchester City Mario Balotelli, na jibu lake likawa: 'Hapana. Hapana, Hiyo imetungwa.

'Hatuwezi kuamini vyote kwenye mitandao na magazeti.

'Kuna wakati tetesi hizi hutengenezwa na majenti ama waandishi ili kupata habari, si kweli.'

Milan bado wanahaha kutafuta mnunuzi wa straika huyo mwenye miaka 23 tu.

Balotelli, Arsenal hakuna dili hilo. Habari hii ni nzuri ama mbaya kwako

Arsenal kutema wachezaji 11


 Photo: BREAKING : ARSENAL YAACHA 11
Arsenal wamethibitisha kwamba wachezaji 11 wataihama klabu hiyo pindi mikataba yao itakapomalizika June 30.
Nicklas Bendtner na Ju Young Park kufikia tarehe hiyo watakua ukingoni mwa mikataba yao ilhali Kim Kallstrom na Emiliano Vivian mikataba yao ya mkopo itamalizika na watarudi kwa waajiri wao.
Kama ambavyo imetangazwa awali, Bacary Sagna, Lukasz Fabianski na Zak Ansah wamekamilisha uhamisho wao kwa kuhamia Manchester City, Swansea City na Charlton Athletic kwa kila mmoja.
Huku, wachezaji wa timu za akademi Chuks Aneke, Daniel Boateng, Zach Fagan na Leander Siemann pia wameachwa baada ya kufikia kikomo cha mikataba wao.

Nini maoni yako juu ya taarifa hii?
 
Arsenal wamethibitisha kwamba wachezaji 11 wataihama klabu hiyo pindi mikataba yao itakapomalizika June 30.
Nicklas Bendtner na Ju Young Park kufikia tarehe hiyo watakua ukingoni mwa mikataba yao ilhali Kim Kallstrom na Emiliano Vivian mikataba yao ya mkopo itamalizika na watarudi kwa waajiri wao.
Kama ambavyo imetangazwa awali, Bacary Sagna, Lukasz Fabianski na Zak Ansah wamekamilisha uhamisho wao kwa kuhamia Manchester City, Swansea City na Charlton Athletic kwa kila mmoja.
Huku, wachezaji wa timu za akademi Chuks Aneke, Daniel Boateng, Zach Fagan na Leander Siemann pia wameachwa baada ya kufikia kikomo cha mikataba wao.

Nini maoni yako juu ya taarifa hii?

Mtoto wa miaka 13 aikoa Nigeria Kulipuliwa na bomu kubwa


Siku chache baada ya kutokea shambulizi kubwa la bomu katika soko kubwa ‘Mall’ jijini Abuja, Nigeria mtoto mwenye umri wa miaka 13 amesaidia kuwaokoa raia wa Nigeria kushambuliwa na bomu kubwa baada ya kulishitukia na kutoa taarifa polisi.

 
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Kano, aliyejitambulisha kwa jina la Magaji Majiya, mtoto huyo wa kiume alipata mashaka baada ya kuona gari fulani bovubovu likiwa limetelekezwa huku likiwa na mzigo mkubwa karibu na msikiti mmoja.

 
Na ndipo alipolichungulia na  kuona vitu kama mabomu na akatoa taarifa mapema.

 
“Bomu liliwalenga watu walioenda kuabudu katika msikiti huo na lilikuwa limewekwa kwenye gari aina ya Toyota Tercel.” Alisema Majiya.

 
Polisi walituma kikosi maalum cha kutegua mabomu ambacho kilifanikiwa kulitegua bomu hilo.

 
Mtu mmoja amekamatwa kutokana na tukio hilo.

Manchester United yarusha ndoano kwa Alexis Sanchez

Photo: Manchester United imetupia macho kwa mchezaji wa Barcelona na Chile,Sanchez £40mil

Baadhi ya magazeti nchini Uingereza leo asubuhi na kituo cha SkySport kimezungumzia hili.
 
Manchester United imetupia macho kwa mchezaji wa Barcelona na Chile,Sanchez £40mil

Baadhi ya magazeti nchini Uingereza leo asubuhi na kituo cha SkySport kimezungumzia hili.

Sunday 29 June 2014

Manchester United mbion kunasa saini ya kisiki cha Uholanzi,Arsenal na Man Utd zatiana pembe kwa Vidal

  Photo: Karibu vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa Manchester United na klabu ya Feyernood vimefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kati Stefan de Vrij kwa thamani ya Paund mil 8.. Beki huyo nguzo kwa timu ya taifa ya uholanzi kwa sasa anashiriki fainali za kombe la dunia na uhenda akajiunga kwa miamba hiyo ya Uingereza hasa baada ya Louis Van Gaal kucheza mchezo mchafu kumkwapua baada ya taarifa za awali kudai beki uyo alikua akijiandaa kuelekea kunamo klabu ya Lazio. 

Pia vyombo vya habari nchini Italy na Chile vimeripoti kuwa Manchester United wanajiandaa kumtengenezea Artulo Vidal mshahara wa Paund 230,000 kwa week, huku Arsenal Wenger naye akituma wawakilishi wake kuweza kumpata kiungo uyo mahiri wa club ya Juventus. 

=/ D.P /=
Karibu vyombo vingi vya habari vimeripoti kuwa Manchester United na klabu ya Feyernood vimefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kati Stefan de Vrij kwa thamani ya Paund mil 8.. Beki huyo nguzo kwa timu ya taifa ya uholanzi kwa sasa anashiriki fainali za kombe la dunia na uhenda akajiunga kwa miamba hiyo ya Uingereza hasa baada ya Louis Van Gaal kucheza mchezo mchafu kumkwapua baada ya taarifa za awali kudai beki uyo alikua akijiandaa kuelekea kunamo klabu ya Lazio.

Pia vyombo vya habari nchini Italy na Chile vimeripoti kuwa Manchester United wanajiandaa kumtengenezea Artulo Vidal mshahara wa Paund 230,000 kwa week, huku Arsenal Wenger naye akituma wawakilishi wake kuweza kumpata kiungo uyo mahiri wa club ya Juventus. 

Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata habari na tetesi za usajili barani ulaya kwa wakati na muda muafaka.

Boko Haram waanza kuadhibiwa Kichawi......Nyoka wa Ajabu na Nyuki Wawatoa Msituni


Wanajeshi wa Boko Haram wanaofanya mashambulizi na kuua raia wasio na hatia huko Nigeria wamedaiwa kuanza kukimbia msitu baada ya nyoka wenye sumu kali na nyuki kuwashambulia.

Habari hizi zilielezwa na mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na kuthibitisha kuwa ni mmoja wa member wa kundi la Boko Haram na alieleza kuwa hivi sasa kundi hilo limelazimika kuhama msitu na linaelekea maeneo ya mpaka wa Nigeria na Cameroon baada ya wanajeshi wake wa ngazi za juu kushambuliwa na nyoka na kupoteza maisha.

Kumezuka hisia za kiimani kuwa Boko Haram wanaadhibiwa na mizimu ya watu  waliowauwa kinyama. 

Jeshi la Nigeria limeshafanya juhudi za kuwaondoa msituni lakini imeshindikana  na hadi sasa kundi hilo linawashikilia wasichana zaidi ya 260 na bado linaendelea kushambulia Nigeria kwa mabomu ya kutegwa.

‘Wamatumbi’ wagoma kuondoka Ujerumani

Maombi ya hifadhi ya wakimbuizi hao wa muda mrefu yamekataliwa na serikali ya Ujerumani.
Maombi ya hifadhi ya wakimbizi hao wa muda mrefu yamekataliwa na serikali ya Ujerumani.
Mamia ya maafisa wa polisi wameizunguka shule ya zamani mjini Berlin ambayo imekaliwa na wakimbizi wa muda mrefu ambao hawataki kuondoka.
Wakimbizi hao wa Afrika wanataka haki ya kubaki Ujerumani, pamoja na kukataliwa kwa maombi yao ya hifadhi.
Adam, mkimbizi kutoka Sudan ambaye alitaja jina moja tu, aliwaambia waandishi wa habari kwamba siku ya Ijumaa wakimbizi hao walipanda kwenye dari ya shule hiyo na walikuwa tayari kuruka kama polisi hao wangeingia ndani.
Mgomo huo ulihusisha wakimbizi 40-80 huku wakiwa na wafuasi ndani ya jengo hilo baada ya polisi kuingia humo mapema wiki hii na kuwafurusha wakimbizi 200 ambao walikuwa humo tangu 2012.
Maafisa wa mji wanasema watajadiliana na wakimbizi hao kuhusu mahitaji endapo wataondoka kwenye jengo hilo.
Hao jamaa hawatupendi, basi tu, wamesahau kuwa ndio waliosababisha tukafikia hali hiyo…(1884/85)

Fifa wamuondolea adhabu gwiji wa Ujerumani, Franz Beckenbauer

Photo: Die Nachricht von seinem Tod stimmt mich sehr traurig. Nelson Mandela war ein einzigartiger Mensch und die beeindruckendste Persönlichkeit, die mir jemals begegnet ist. Jeder kennt den Satz von ihm: „Sport hat die Kraft, die Welt zu verändern.“ Er selbst hat sie auch verändert.

It makes me very sad. Nelson Mandela was a unique person and the most impressive personality I have ever met. Everyone knows this sentence of him: "Sport has the power to change the world"

Fifa wameondoa adhabu ya siku 90 za kutojishughulisha na michezo iliyokuwa imewekwa dhidi ya gwiji wa Ujerumani Franz Beckenbauer.
Beckenbauer, mshindi wa Kombe la Dunia akiwa kama kocha na nahodha, siku ya Ijumaa aliambiwa kuwa adhabu hiyo imondolewa haraka iwezekanavyo, alisema meneja Marcus Hoefl.
Franz, 68, alisimamishwa baada ya kushindwa kusaidia uchunguzi wa tuhuma za rushwa kwa wagombea uwenyeji wa Kombe a Dunia 2018 (Urusi) na 2022 (Qatar).
Alikuwa sehemu ya kamati kuu ya Fifa ambao walitoa tuzo hizo.
Beckenbauer alinyanyua Kombe la Dunia kama mchezaji (1974) na kocha (1990).

Uingereza yakumbwa na uhaba wa mbegu za kiume



Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.
Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.
Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.
Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.
Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.
Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.

Wanajeshi wa Iraq wauteka mji wa Tiqrit


Wanajeshi wa Iraq wakielekea mjini Tiqrit
Serikali ya Iraq inasema kuwa vikosi vyake vimeuteka mji wa kazkazini wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa ki-sunni ambao walikuwa wameteka mji huo wiki mbili zilizopita.
Vyombo vya habari vya kitaifa vimesema kuwa wanajeshi wakisaidiwa na mizinga pamoja na ndege za kijeshi waliwafurusha wanamgambo wa kundi la ISIS na kuwaua zaidi ya sitini.

      Waasi hao wamesema kuwa kulikuwa na mapigano makali katika mji huo na kwamba mashambulizi hayo hayakufua dafu.
Iwapo itathibitishwa ,utekaji wa mji wa Tikrit utakuwa hatua kubwa ya jeshi la Iraq tangu ISIS kuyateka maeneo mengi ya Iraq kazkazini mapema mwezi huu.
Serikali sasa inasema kuwa inajiandaa kuelekea mjini Mosul ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.

Alazwa hospitalini baada ya kumkana Mungu

Mubarak Bala
Mwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini NIGERIA.
Mubarak Bala alizuiliwa kinyume na matakwa yake hospitalini baada ya familia yake kumpeleka huko kwa matibabu.
Duru katika hospitali hiyo zimesema kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa kwa matatizo ya kiakili na kwamba hataendelea kuzuilikwa kwa muda mrefu.
Jimbo la Kano lina idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu, na limekuwa chini ya sheria za kiisilamu tangu mwaka 2000.
Kano ni jimbo lenye kufuata sheria za kiisilamu
Shirika hilo la kimataifa limesema kuwa wakati ambapo Bala aliwaambia jamaa wake kuwa hamuamini Mungu, familia yake uilimpekeka kwa daktari kuuliza ikiwa akili yake iko timamu.
Licha ya kufahamishwa kuwa mwanamume huyo hana tatizo lolote la kiakili, familia ya Bala ilitafuta ushauri wa daktari mwingine aliyewafahamisha kuwa hatua yake ya kumkana Mungu, inatokana na matatizo ya kiakili.
Bwana Bala, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu, alilazimishwa kupata ushauri wa daktari wa kiakili , ingawa alitumia simu kuwasiliana na wanaharakati wa haki za kibinadamu.
Hospitali ambako alikuwa ana pokea matibabu ilisema katika taarifa yake kuwa Bwana Bala hana tatizo lolote la kiakili na kuwa yuko sawa.
Alilazwa hospitalini kwa sababu alihitaji kuchunguwa na daktari, ilisema taarifa ya hospitali hiyo

Van Gaal:Tutakunywa maji ya kutosha


Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal anatarajia shirikisho la soka duniani FIFA litawaruhusu wachezaji wake kunywa maji katika mechi yao ya raundi ya pili dhidi ya Mexico itakayochezwa katika uwanja wa Castelao ulioko katika eneo la Fortaleza.
Fortaleza ni eneo linaloshuhudia viwango vya juu vya nyuzi joto.
Kocha huyo wa Manchester United ya Uingereza anasema kuwa utafiti uliofanywa kabla ya mashindano haya yanasema kuwa wachezaji wanapoteza maji lita nne ama zaidi kwa kila mechi wanayocheza katika jimbo hilo la Fortaleza.
Ni dhahiri kuwa mwili wa binadamu yeyote unastahili maji kwa hivyo hawa wachezaji naamini kuwa wanastahili kunywa maji ilikuzuia wasishikwe na kisunzi .
Van Gaal kiwango cha joto ni juu mno
Van Gaal alitishia kuwapa wachezaji wake maji kwa wingi kando kando mwa uwanja iwapo FIFA haitahalalisha kuwepo kwa dakika moja au mbili ambapo mechi zitasimamishwa iliwachezaji wake wapige kopo la maji.
Kiungo wao Leroy Fer, ambaye anauguza jeraha la goti anasema kuwa Uholanzi ilipata kionjo tu cha kucheza katika hali ya kiwango cha juu mno cha joto baada ya kuwasili huko wakitoka Rio de Janeiro.
Fer anasema kuwa japo Uholanzi imezoea kucheza katika maeneo ya Uropa yenye baridi kali,Uholanzi itajikaza kisabuni kwani ni hali ileile itakayoikumba timu pinzani ya Mexico.

Colombia kumenyana na Brazil Robo fainali


Nyota wa Colombia na Monaco James Rodriguez alidhibitisha udedea wake katika kombe la dunia alipofunga mabao mawili na kuisaidia Colombia kuwa timu ya pili kufuzu kwa nane bora .
Rodriguez mwenye umri wa miaka 22 alikuwa nyota katika safu ya ushambulizi ya Colombia ilipokuwa ikichuana dhidi ya Uruguay bila mshambulizi wake mwenye utata Luiz Suarez.
Bila shaka mshambulizi huyo sasa atakumbukwa katika mizani sawa na Neymar wa Brazil na Lionel Messi wa Argetina nyota wa Brazil2014 watakapokuwa wakitajwa haswa kutokana na miondoko yake hapo jana katika uwanja wa Rio.Wengi wanaashiria kukosekana na Suarez kuwa kisababu cha kikosi cha Oscar Tabarez kushindwa kusonga mbele katika kipute hicho kinachoendelea huko Brazil.
Mchezaji huyo wa Monaco alitangaza kuwepo kwake uwanjani kwa mkwaju wa dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza uliomwacha kipa ya Uruguay Fernando Muslera ameduwaa huku maelfu wa mashabiki wa Colombia wakishangilia kwa nusia tikiti ya Robo fainali ya kombe la dunia .
Nyota wa Colombia James Rodriguez anatarajiwa kuibabashia Brazil
Rodriguez hakuachia hapo, aliendelea kuwa mwiba katika safu ya ulinzi ya Vijana wa Oscar tabarez na juhudi zake zikazaa matunda kunako dakika ya 58 Mshambulizi huyo alipofuma bao la pili na ushindi na kuahakiki nafasi hiyo ya nane bora kwa Colombia.
Kufuatia matookeo hayo sasa Colombia watachuana na wenyeji Brazil katika mechi inayotazamiwa na wengi kuwa ngumu ya kuwania nafasi ya nusu fainali.
Mechi hiyo itachezwa siku yaijumaa katika uwanja wa Fortaleza .
Uruguay ilikosa keke zake za kawaida katika mechi hii ilikuwa bayana kuwa japo Suarez hakuwepo uwanjani mashabiki wake walimsifia na kubeba mabango y kumuunga mkono mshambulizi huyo wa Liverpool ya Uingereza .
Washambulizi wake Maximiliano Pereira na Edinson Cavani fndio waliomjaribu kipa wa Colombia David Ospina.

Mlipuko waua watu 10 nchini Nigeria

Takriban watu 10 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika mji wa Bauchi Kaskazini mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa polisi, shambulizi hilo lililoripotiwa Ijumaa jioni lilitokea katika jengo linalojulikana kutumiwa kwa shughuli za ukahaba.
Kiini cha mlipuko hakijulikani ingawa wapiganaji wa Boko Haram wamewahi kushambulia mji wa Bauchi.
Mlipuko huo pia umetokea siku mbili tu baada ya shambulizi mjini Abuja kuwaua watu 22.
Takriban watu 10,000 wanakisiwa kuuawa na kundi la Boko Haram tangu kuanza harakati zao mmwaka 2009.
Wapiganaji hao hulenga maeneo ambayo wanayaona kuwa hayambatani na matakwa ya dini ya kiisilamu kama vile baa, makanisa na shule ambazo hutoa mafunzo ya kimagharibi.
Kundi la Boko Haram, limezua wasiwasi kimataifa hasa tangu lilipowateka nyara zaidi ya wasichana 200 katika eneo la Chibok mwezi Aprili.

Brazil yaponea chupuchupu

Neymar alifinga penalti yake, sababu ya furaha hii
Brazil imeponea kung'olewa kutoka mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini humo.
Hii ni baada ya mechi ya kwanza ya mkondo wa mtoano kati yake na Chile kumalizika kwa mikwaju ya Penalti baada ya timu hizo mbili kwenda sare ya bao moja baada ya kipindi kizima cha mechi.
Na pia baada ya kucheza muda wa ziada.
Wakati wa mikwaju ya Penalti, Brazil ilishinda tatu huku Chile ikishinda mbili.
Wakati wa mechi , Brazil ilifunga bao la kwanza la mechi ndani ya kipindi cha kwanza, lakini Chile ilileta jibu kabla ya kipindi cha kwanza cha mechi kukamilika.
Brazil ilikuwa na kibarua kigumu na shinikizo tele kutoka kwa mashabiki wa Brazil ambao walijaa uwanjani na pia kwa kuwa Brazil ni mwenyeji wa michuano hiyo ,matarajio ya wengi nchini Brazil ni kuwa wanatafanya vyema katika mashindano hayo.

Muimbaji wa Nigeria atoa bikira yake kwa Boko Haram

Mwanamuziki, muigizaji na balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa Adokiye amesema yuko tayari kujitolea bikira yake kwa Boko Haram ili wawaachie wasichana waliowateka nyara.
  Mwanamuziki, muigizaji na balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa Adokiye amesema yuko tayari kutoa bikira yake kwa Boko Haram ili wawaachie wasichana waliowateka nyara.
Mwimbaji wa pop wa nchini Nigeria na balozi wa amani ametuma maoni ya kushtusha kwenye mtandao wa kijamii kwa kudai anatoa bikira yake kwa wanamgambo wa Kiislamu ili wawaachie mamia ya wasichana wa shule waliowateka nyara.
        Adokiye, 23, alitoa mapendekezo hayo kwa wanachama wa Boko Haram ili waweze kuwaachia huru wasichana wa Nigera wapatao 276 ambao waliwachukua mwezi Aprili katika mji wenye Wakristo wa kaskazini-mashariki wa Chibok.
Muimbaji na muigizaji huyo anayetokea jimbo la Imo aliliambia gazeti la Nigeria la Vanguard: ‘Hii ni saa 5 usiku, unajua ninachokifikiria?, wale wasichana wadogo, wako wapi saa hii, nini kitakuwa kinatokea kwao.
Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram Abubakar Shekau ambaye aliongoza utekaji nyara wa wanafunzi wasichana wapatao 276 nchini Nigeria.
Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Boko Haram Abubakar Shekau ambaye aliongoza utekaji nyara wa wanafunzi wasichana wapatao 276 katika jimbo la Chibok, Nigeria.
“Sio haki . bado ni wadogo. Natamani ningejitoa mimi tubadilishane.”
Balozi huyo wa amani wa Umoja wa Mataifa aliongeza: “Kuna wenye umri kati ya miaka 12 na 15. Nimekuwa na nina uzoefu. Hata wanaume 10 mpaka 12 wanaweza kunichukua kila usiku, sijali. Hebu waachieni hao wasichana, warudi kwa wazazi wao”.
Utekaji, ulioongozwa na kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, umeibua kampeni kubwa duniani ya #BringBackOurGirls. Imekuwa ikiungwa mkono na viongozi wakubwa kama David Cameron na Michelle Obama japo watumiaji wa Twitter hawana uhakika na manufaa ya ofa ya Adokiye.



Tumehamia katika site hii mpya na bado tuko katika maboresho,hii ni katika hatua za awali kabisa kuiboresha site yetu na utoaji wa habari na burudani.Vitu vingi vitaonekana katika site hii mpya hivi karibuni.Endelea kutembelea www.bantutz.com
 

Ada vyuo vya ualimu yapanda maradufu

Baadhi ya wahitimu wa chuo cha Ualimu.PICHA|MAKTABA

Serikali imepandisha maradufu ada kwa wanafunzi wanaosomea ualimu kwenye vyuo vya ualimu nchini kuanzia muhula ujao wa masomo.
Ada hizo kwa wale wa ngazi za cheti na stashahada ambazo zimeongezwa kwa karibu mara mbili au zaidi ya zile zilizokuwa zikilipwa awali.
Uamuzi huo ambao huenda ukawaathiri zaidi wanafunzi ambao waliona ualimu kama kimbilio, unaelezwa na baadhi ya wadau wakiwamo walimu, wanafunzi na hata wakufunzi wa baadhi ya vyuo nchini kuwa ni wa ghafla.
Kwa mujibu wa baadhi ya wakufunzi, uamuzi huo umetolewa kupitia waraka wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na unatarajiwa kuanza kutekelezwa muhula wa pili wa masomo utakaoanza Julai 2, mwaka huu.
Kabla ya kupandishwa kwa ada hizo, wanafunzi wanaosomea ualimu kwa ngazi ya cheti walikuwa wakilipa Sh200,000, lakini sasa watalazimika kulipa Sh300,000, ikiwa ni ongezeko la asilimia 50.
Kwa wale wanaochukua stashahada watalazimika kulipa Sh400,000 kwa masomo ya Sanaa na Sh600,000 kwa masomo ya Sayansi kutoka Sh200, 000 za awali.
Mhasibu wa Chuo cha Ualimu cha Mtwara, aliyekataa kutaja jina lake kwa kuwa siyo msemaji wa chuo hicho, alithibitisha kupokea waraka wa Serikali unaowataka kupandisha ada, lakini alisisitiza kuwa Mkuu wa Chuo ndiye angeweza kufafanua zaidi kuhusu ongezeko hilo.
“Taarifa hizo ni za kweli ada imepanda, kama umezipata kutoka wizarani hivyo ndivyo ilivyo kwa hiyo huna sababu ya kupata taarifa zaidi kutoka kwetu,” alisema mhasibu huyo.
Awali, habari zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na uhaba wa fedha na ugumu wa kuviendesha vyuo hivyo.
Habari zinasema kwa muda mrefu sasa, Serikali imekuwa ikidaiwa na wazabuni fedha nyingi, jambo ambalo limeathiri pia uendeshaji wa vyuo vikiwamo vya ualimu.
Baadhi ya wakufunzi wameeleza kuwa fedha za ada sehemu yake itatumika kutatua matatizo ya uhaba wa fedha ambao umekuwa ukiwakabili na hivyo kuathiri utoaji wa huduma zikiwamo za vyakula.
Wizara ya Elimu
Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu alisema viwango vilivyoongezwa siyo vikubwa ikilinganishwa na hali ya ugumu wa maisha ilivyo sasa nchini.
“Unamweka mtu mwaka mzima anakula, analala, anasoma…kweli unaona hiyo ada hiyo ni kubwa? Bado siyo kubwa kiasi cha kushtua watu,” alisema Bunyazu.
Aidha, Bunyazu alisema kuwa wanafunzi watakaopata daraja la kwanza katika masomo ya Sayansi na Hisabati na kuingia katika vyuo vya ualimu vya Serikali watasomeshwa bure na wale watakaopata daraja la pili na la tatu watapewa mkopo.
Wengine wazungumza
Meneja wa Utafiti na Uchambuzi wa Sera wa Shirika la HakiElimu, Godfrey Boniventura akizungumzia suala hilo jana, alisema kuwa siyo kweli kwamba serikali haina fedha za kutosha ndiyo maana inaongeza ada, ila inadhani kuwa idadi ya walimu waliopo inatosha.
“Serikali imeamua kupandisha ada kwa kudhani kuwa walimu waliopo wanatosha, lakini ikumbuke kuwa kuna walimu wengi wazee wanaostaafu kila mwaka, wengine hawaripoti shuleni, hivyo tunahitaji kuwa na benki ya walimu,” alisema Boniventura.

Saturday 28 June 2014

Maximo kuinoa Yanga kwa miaka miwili

Kocha mpya wa klabu ya Yanga Maxio Maximo. Maximo alikuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa Taifa Stars.
Kocha mpya wa klabu ya Yanga Maxio Maximo. Maximo alikuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa Taifa Stars.
Aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya hapa nchini Maxio Maximo kutoka Brazil amepata fursa ya kurudi tena hapa nchini, kuja kuisuka vyema timu ya Yanga ili iweze kucheza katika michuano ya kimataifa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani, wakala aliyemleta Maximo, Ally Mlee alisema kuwa, ilimchukua miaka 3 kumuomba kuja hapa nchini kusuka timu ya yanga, kwa kujali kwake na ukarimu wa watanzania amekuja tena hapa nchini na amesaini mkataba wa miaka miwili.
Kwa upande wake Maximo alisema kuwa, amefurahi kuja kusuka timu ya yanga na anamatumaini itafanya vyema katika michuano mikubwa nje ya nchi lakini hata katika ligi ya hapa nyumbani.
“Watanzania ni wakarimu sana ndio maana nimekubali kuja tena hapa nchini kuinoa Yanga, lakini pia ujio wangu nimekuja na kocha msaidizi ambaye atanisaidia kusimamia na pia nitapendekeza wachezaji wazuri kutoka katika timu kubwa huko Ulaya, ili waje kuchezea Yanga lakini pia ni fursa kwa wachezaji wa yanga kujinoa kupitia wachezaji wakubwa,” alisema Maximo.
Siku ya Jumatatu timu ya Yanga itaanza mazoezi na mwalimu huyo mpya, maandalizi ya kujiandaa na ligi mbalimbali.

Maradona-‘FIFA wanapaswa kumtupa Suarez Guantanamo’

Suarez akishika meno yake kuangalia yapo aua yametoka naada ya kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini wakati Uruguay ilivyomenyana na Italia kweny mashindano ya Kombe la Dunia 2014, Brazil.
Suarez akishika meno yake kuangalia yapo auyametoka baada ya kumng’ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini wakati Uruguay ilipokuwa inamenyana na Italia kwenye mashindano ya Kombe la Dunia 2014, Brazil.
Diego Maradona ameponda adhabu ya Fifa dhidi ya mshambuliaji Luis Suarez aliyemuita mhalifu na kusema shirikisho hilo la soka la kimataifa lilipaswa kumtia pingu na kumfunga kwenye gereza la Guantanamo.
“Nani alimfanya Suarez auwe?,” Maradona aliyasema hayo wakati wa kipindi cha kutoa maoni cha Venezuela Telesur na televisheni ya serikali ya Argentina siku ya Alhamisi usiku.
“Hili ni soka, huu ni mkataba,”alisema gwiji huyo wa Argentina. “Wangeweza hata kumtia pingu na kumpeleka Guantanamo moja kwa moja.”
Guantanamo ni gereza lenye utata la Marekani lililopo nchini Cuba, lilifunguliwa wakati wa utawala wa Bush, linakosolewa zaidi na makundi ya haki za binadamu kwa kuwafunga watu kwa vipindi visivyojulikana bila mashtaka wala kesi.

Coco Beach-Marufuku kufanya biashara na kuegesha magari

Tangazo la kuwazuia watu wanaofanya biashara na kuegesha magari kwenye eneo la Coco Beach.
Tangazo la kuwazuia watu wanaofanya biashara na kuegesha magari kwenye eneo la Coco Beach.
Halmashauri ya manispaa ya Ilala imetoa tangazo linaloagizo kukataza watu kufanya biashara na kuegesha magari katika eneo la Coco Beach.
Tangazo hilo ambalo limewekwa kwa mtindo wa bango katika eneo hilo lilisomeka hivi:
“Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, ILANI: Ni marufuku kufanya biashara na kuegesha magari katika eneo hili, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayevunja amri hii”.
Kamera ya Taarifa News ilikutana na bango hilo, pamoja na baadhi watu katika eneo ambao walikuwa wakijadili kuhusu tangazo hilo.
Taarifa News ilifanya jitihada za kuwatafuta viongozi wa eneo hilo bila mafanikio yoyote.
Kwa waliozoea kwenda Coco Beach na kula, bora mkaja na vyakula vyenu kuanzia sasa.

Uingereza yaomba ruhusa ya jeshi lake

Wanajeshi wa Uingereza
Uingereza imesema kuwa inafanya mazungumzo na kenya ili kutatua mzozo kuhusu mafunzo ya wanajeshi wa Uingereza nchini humo.
Serikali ya Kenya inaaminika kuchelewa kuwaruhusu wanajeshi zaidi wa Uingereza kuingia nchini humo ili kufanya mazoezi.
Maelfu ya wanajeshi wa Uingereza huzuru nchini kenya kila mwaka kwa mafunzo ya wiki sita lakini hilo limesitishwa kwa mda baada ya kenya kuchelewa kutoa ruhusa ya kidiplomasia kwa ndege inayowabeba wanajeshi wanaotarajiwa kufanya mafunzo hayo.
Hatua hiyo inaonekana kama kulipiza kisasi kwa tahadhari ya kusafiri humu nchini iliotolewa na serikali ya Uingereza kwa raia wake ambayo imeathiri pakubwa sekta ya utalii nchini.
Wanajeshi wa Uingereza wamekuwa wakifanya mafunzo nchini kwa zaidi ya miongo minne lakini makubaliano kati ya mataifa hayo mawili kuhusu mafunzi hayo yanakamilika mwezi Aprili.
Masineta kutoka upande wa chama tawala nchini kenya wamemtaka rais Uhuru kenyatta kutotia sahihi mkataba mpya.
Maafisa katika ubalozi wa Uingereza wameiambia BBC kwamba wana matumaini mgogoro huo utatatuliwa kwa haraka.
Wizara ya maswala ya kigeni nchini kenya hatahivyo inasema kuwa swala hilo tayari limetatuliwa.

Barcelona inataka kumsajili Suarez licha ya adhabu kali aliyopewa.


Licha ya kukabiliwa na marufuku ya FIFA ya miezi minne kwa kumng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Barcelona ya Uhispania haijakata tamaa ya kumsajili mshambulizi machachari wa wa Uruguay Luiz Suarez.
Mshambulizi huyo wa kutegemewa wa klabu ya Liverpool ya Uingereza amepigwa marufuku ya miezi minne kumaanisha kuwa hatoshiriki mechi yeyote hadi mwezi Oktoba.
Aidha Suarez hatoweza hata kufanya mazoezi katika kipindi hicho.
Haijulikani kwanini mabingwa hao wa zamani wa kombe la mabingwa barani uropa ambao wanajivunia huduma za Lionel Messi wa Argentina na Neymarwa Brazil bado wanamtaka Suarez.

Liverpool ilimnunua Suarez kwa pauni milioni £25m mwezi Januari 2011 kutoka klabu ya Ajax.
Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.