Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday 6 June 2015

WARAKA KWA WANAVYUO VIKUU TANZANIA KUHUSU KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA KUSHIRIKI  KUPIGA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU OCTOBA 25/2015

Leo tarehe 5/6/2015, baadhi ya wanafunzi  kutoka vyuo vikuu tumeweza kuonana na m/kit wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Jaji Damian Lubuva.Ambayo ilikuwa ni makubaliano tuliyoyafanya juzi tarehe 3/06/2015 kuhusu kuonana nae.

Madhumuni ya kuonana na m/kiti wa NEC ,ni kama ifuatavyo

Moja ni kujua namna gani wanafunzi tunaweza kujiandikisha na kupata fursa ya kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Pili ni namna gani tutaweza kupiga kura ikiwa maeneo tuliyojiandikishia yatakuwa tofauti na ambapo tutakuwa wakati wa uchaguzi.

Mengine zaidi ya hayo tumeyaeleza kwenye WARAKA WETU KWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI(NEC).

Makubaliano yetu na Jaji Damiani Lubuva ni kama ifuatavyo

Moja wanafunzi wote wa vyuo vikuu atahakikisha tunajiandikisha na kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu maeno mbalimbali ambayo tutakuwa wakati wa uchaguzi......Pia swala hili limejieleza wazi katika ibara ya 5(3)(c) kwenye katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977

Pili WARAKA WETU KWA TUME YA UCHAGUZI(NEC), utajibiwa pia kwa maandishi tarehe 10/06/2015, baada ya kikao cha wajumbe wa Tume kukaa na kujadili namna gani wataweza kutuandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu.

Changamoto tulizokutana nazo ni

Viongozi wa shilikisho la vyuo vikuu Tanzania(TAHILISO) waliofika ofisi za tume ya uchaguzi(NEC), Kutaka kujaribu kukwamisha mazungumzo yetu na m/kiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva kwa malengo yao binafsi.

Lakini tunashukuru watendaji wa Tume ya uchaguzi(NEC) kwa pamoja na m/kiti wa NEC waliweza kuheshimu makubaliano yetu ya kufanya nao mazungumzo.

Hata hivyo viongozi hao wa TAHILISO walishindwa kujumuika nasi katika mazungumzo hayo na kutokomea kusikojulikana.

Wito wetu kwa Wanavyuo vikuu Tanzania tunahitaji ushirikiano kwa pamoja ili kuweza kufanikisha na sisi tunapata haki yetu ya msingi ya kikatiba kushiriki kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi wakitaifa tunao wataka na hatuwezi kuchagua viongozi hao kama tutakuwa hatujajiandikisha.

Wanafunzi walioshiri kwenye mazungumzo hayo ni wafuatao

1.)LUSEKELO  AMIMU-Chuo kikuu Ardhi
2.)BARAKA NYEUA-T.I.C.D Arusha
3.)NTILE  JOEL-UDSM
4.)PATRICK JOHN-UDSM
5.)MWIDADI  MSANGI-Ardhi
6.)FRANK JOASH-CPS &CPA
7.)SHIRIMA  JUVENAL-Ardhi
8.)SHITINDI  VENANCE-UDSM

Baada ya Tume ya uchaguzi NEC kutoa majibu kwa maandishi tutawaletea tena mrejesho kwenu.

Kwa mawasiliano zaidi:
0684-615128

Wakuta chura ndani ya kopo wa tomato

Mtu na mkewe waliokuwa wakiandaa chakula cha mchana walipigwa na butwaa walipopata chura kilichokuwa kimekufa ndani ya mkebe wa tomato.
Muhammad na Sanam Hussain waligundua hayo wakati bi Hussain alipokuwa akipika mchuzi katika nyumba yao huko Alum Rock mjini Birmigham.
Bi Hussain ambaye ni mjamzito wa miezi saba amesema kuwa anaugua baada ya kukiona kiumbe hicho ndani ya mkebe wa tomato.
Kampuni ya Euro Foods inayouza bidhaa hiyo imesema kuwa inachunguza ni vipi chura hicho kiliingia ndani ya mkebe huoBi Hussain amesema,''kwa kweli inachukiza ,nimeshtuka sana,nina wasiwasi kuhusu mtoto wangu kwa kuwa mimi ni mjamzito''.
''Nimeongea na mkunga wangu kuhusu niliyoyaona na akaniamibia niende hospitalini nitakaposikia vibaya.'',Mumewe amesema kuwa alishtushwa na makelele yaliopigwa na mkewe.
''Mke wangu alikuwa akiniandalia chakula cha mchana na mwanagun wa miezi 15 Wakati alipofungua mkebe huo alionekana na kuanza kupiga makelele akiniita''.

Henderson afurahia Brendan Rodgers kubaki Liverpool.

Kiungo Jordan Henderson amefurahia maamuzi ya uongozi kumbakisha kocha wa Liverpool Brendan Rodgers
Kapteni huyo amesisitiza watamaliza msimu ujao kwa mafanikio na kuiletea heshima timu hiyo.
Kocha Rodgers alikuwa na wakati mgumu baada ya matokeo yasiyofurahisha mwishoni mwa msimu na kushindwa kuwapa kikombe chochote.
Kwa kikosi cha sasa cha Liverpool kitaweza kushindana na miamba mingine ya soka katika mbio za ubingwa?

Falcao kutua Darajani

Mchezaji Radamel Falcao anayecheza kwa mkopo Old Trafford anataka kubaki kucheza Premier League. Mcolombia huyo ameshindwa kuishawishi Manchester United kumnunua jumla.
Falcao amefunga magoli manne tu Old Trafford, mchezaji huyo anataka kuchezea Chelsea msimu huu.Uwepo wa Eden Hazard, Diego Costa,Oscar, Willian, kutamshawishi Meneja Mourinho kumpa nafasi Falcao Stamford Bridge?

Raheem Sterling kuelekea Man United.

 
Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.
Hatahivyo Liverpool imesema kuwa haiko tayari kufanya biashara na wapinzani wao wakuu kutoka Kaskazini Magharibi.
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Luois Van Gaal anavutiwa na kasi ya mchezaji huyo na uwezo wake wa kuwaponyoka mabeki.
Sterling amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa kushinda mataji.

Angel Di Maria "Nabaki old Trafford

Mchezaji raia wa Argentina Angel di Maria amethibitisha kubaki Manchester United msimu ujao.
Pamoja na tetesi za kujiunga PSG kwa ada ya ya Euro milioni 60.
Di Maria amefunga magoli manne na kutoa pasi za magoli 12 kwa mashindano yote.

Mesut Ozil ajinyakulia tuzo Ujerumani.

Mchezaji nyota wa Arsenal Mesut Ozil ameshinda tuzo ya balozi wa mpira wa Ujerumani 2015.
Mesut Ozil ametangazwa kuwa balozi wa mpira wa Ujerumani mapema wiki hii.Tuzo hii hutolewa kwa watu wanofanya kazi za kuitolea.Ozil, amesema tuzo hii ina mana kubwa kwake.

Rais wa Afrika Kusini ahusishwa kashfa ya rushwa FIFA.

Waziri wa michezo wa Afrika Kusini , Fikile Mbalula, sasa anasema rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki ndie aliyeruhusu ulipwaji wa fedha ,dola milioni 10 kwa FIFA , hela ambayo sasa inakumbwa na madai kwamba ilikuwa rushwa .
Utawala wa Afrika Kusini umekuwa ukisisitiza kwamba ulikuwa ni mchango wa kusaidia kukuza soka katika nchi za Caribbean.
Lakini waendesha mashtaka wa Marekani wanadai ilikuwa hongo, iliyoshawishi kupewa uenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010 .
Bwana Mbeki mwenyewe hajatoa kauli yoyote kuhusiana na swala hilo.
Barua inayosemekana iliandikwa na shirikisho la soka nchini Afrika kusini , inaonekana kuongeza uzito kwenye shutuma kwamba serikali ya nchi hiyo ilitoa malipo hayo kwa siri.

Simba yakaribia kumnasa mshambuliaji hatari kutoka Burundi.


SIMBA SC imekaribia kabisa kukamilisha usajili wa mchezaji mpya wa sita kuelekea msimu ujao, na huyo si mwingine bali mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba SC, Collins Frisch yuko mjini Bujumbura kukamilisha usajili wa mchezaji huyo na habari zisizo rasmi zinasema, amefanikiwa.
Chanzo cha habari kutoka Simba SC kimedai kwamba Mavugo tayari ni mchezaji wa Wekundu wa Msimbazi kwa miaka miwili ijayo.
Kijana huyo aliyezaliwa Oktoba 10, mwaka 1989 kwa sasa anachezea Vital’O ya kwao Burundi, lakini awali alichezea Kiyovu na Polisi za Rwanda na aliyekuwa kocha wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic ndiye aliyempendekeza mkali huyo wa mabao asajiliwe.
Kopunovic amewahi kufanya kazi na Mavugo katika timu ya Polisi ya Rwanda, kabla ya wawili hao kuihama timu hiyo kwa wakati tofauti.
Iwapo Simba SC itamtangaza rasmi Mavugo kuwa mchezaji wao mpya- atakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa ndani ya kipindi cha wiki tatu, baada ya awali Wekundu hao wa Msimbazi kuwasaini kipa Abraham Mohammedwa JKU, mabeki Samih Hajji Nuhu wa Azam FC, Mohammed Fakhi wa JKT, kiungo Peter Mwalyanzi wa Mbeya City na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi kutoka Mtibwa Sugar.

Xavi kuondoka Barca kwa heshima.

Wakati Xavi Harnandez,35, anajiandaa na kustaafu rasmi baada ya kuitumikia Barcelona kwa miaka 17 ya maisha yake, swali je, atafanikiwa kuongeza kombe jingine hapo keshokutwa.

Barcelona inashuka dimbani mjini Berlin, Ujerumani kucheza fainaliya Ligi ya Mabingwa Ulayadhidi ya Juventus ya Italia.Utaona katika picha hiyo hapo juu, Xavi akiwa amezungukwa na makongwe 24 aliyowahi kubeba akiwa na Barcelona kwa miaka 17.

Hapo kuna makombe manane ya La Liga, matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mawili ya UEFA Super Cups, matatu ya Copa del Reys, sita ya Spanish Supercups na mawili ya Kombe la Dunia kwa klabu.
.JE! ATAWEZA KUBEBA UBINGWA WA 25 NDANI YA BARCA KABLA AJASEPA?

TFFyaingilia kati mgogoro wa Simba SC na Singano 'Messi'


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’(pichani)na klabu yake,Simba SC.
Taarifa ya TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne Juin 9, mwaka huu kwa mazungumzo.
“Kila upande umetakiwa uje na vielelezo vyake.Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo, TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania,”imesema taarifa ya TFF.
Messi aliyeibukia timu ya vijana ya Simba SC miaka minne iliyopita, hivi karibuni ameibua shutuma dhidi ya klabu yake hiyo kwamba imeghushi Mkataba wake.
Messi anadai Mkataba wake halali ulikuwa unamalizika mwaka huu, na si huu wa sasa ambao inaelezwa utamalizika mwakani.
Na Messi si mchezaji wa kwanza kuishutumu Simba SC kughushi Mkataba wake, kwani wachezaji wengine za zamani wa klabu hiyo Athumani Iddi ‘Chuji’ naKevin Yondan wamewahi kutoa malalamiko kama hayo wakati wanahamia kwa mahasimu, Yanga SC.

BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika magazeti yote ya leo Jumamosi,Juni 06

DSC03357
MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhimu baada ya maombi ya wadau mbalimbali.
DSC03358
DSC03359
DSC03360
DSC03361
DSC03362
DSC03363
DSC03364
DSC03365
DSC03366
DSC03367
DSC03368
DSC03369
DSC03370
DSC03371
DSC03372
DSC03373
DSC03374
DSC03375
DSC03376
DSC03377
DSC03378
DSC03379
DSC03380
DSC03381
DSC03382
DSC03383
DSC03384
DSC03385
DSC03386

Friday 5 June 2015

Tetesi zote za Usajili barani Ulaya siku ya leo.

Winga wa England Raheem Sterling, 20 hana tatizo na uwezekano wa kuhamia Manchester United kutoka Liverpool, ingawa mchezaji huyo
ana wasiwasi kuhusu jinsi uhamisho huo utakavyopokelewa, kwa kuzingatia uhasama baina ya timu hizo mbili (Guardian),

Liverpool wanasisitiza kuwa hawatofanya biashara yoyote na mahasimu wao wa Manchester (Liverpool Echo),

Radamel Falcao, 29, anataka kukamilisha uhamisho wake kwenda Chelsea kabla ya michuano ya Copa America kuanza Juni 14 (Daily Telegraph),

Dick Advocaat atapewa pauni milioni 50 za kukijenga kikosi cha Sunderland baada ya kukubali kuongeza mkataba wake wa kuwafunza Paka Weusi (daily Mirror),

Beki wa Bayern Munich kutoka Brazil, Dante, 31 amekataa kuhamia Manchester United baada ya kusema ana nafasi ya kushinda makombe mengi zaidi akiwa na klabu yake ya Ujerumani (Daily Star),

Manchester United wapo tayari kumuuza Nani msimu huu na huenda akaelekea Inter Milan na sio Sporting ambapo amecheza kwa mkopo msimu uliopita (Independent),

Sampdoria ya Seria A inajiandaa kumsajili beki wa kati wa Chelsea Kurt Zouma, 20 kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo ya Italia (Metro),

Dani Alves, 32, amekubali mkataba wa awali na Manchester United na atahamia Uingereza tarehe 1 Julai (Daily Star),

kiungo wa Southampton, Victor Wanyama, 23 amesema "itakuwa vizuri" kujiunga na Arsenal (Daily Mail),

Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers imeripotiwa amemfukuza mwalimu wa kikosi cha kwanza Mike Marsh (Sun),

Mshambuliaji wa QPR Charlie Austin anasakwa na Tottenham, Newcastle, Aston Villa na Southampton kwa pauni milioni 10 na ameonesha ishara kuwa yuko tayari kuihama klabu yake iliyoshuka daraja (Daily Express),

Arsenal wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 25 kumsajili kiungo wa Monaco Geoffrey Kongodbia, 22, ikiwa watamkosa Morgan Shneiderlin wa Southampton (Independent),

Liverpool wamepata matumaini makubwa
ya kumsajili kipa wa Sporting Lisbon, Rui Patricio, 23 baada ya klabu hiyo ya Ureno kumsajili Azbe Jug kutoka Slovenia (Daily Express),

Manchester United wanajiandaa kumsajili kipa wa Galatasaray Fernando Mulsera, 28, kuziba nafasi ya David De Gea anayeelekea Real Madrid (Metro),

Wakati huohuo winga wa Manchester United
Ashely Young, 29 anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu mwezi ujao kusalia Old Trafford (Daily Mirror),

Paris St-Germain wamemfanya winga wa Manchester United Angel Di Maria, 27, kuwa
mchezaji kipaumbele wa kumsajili msimu ujao (TalkSport),

Hata hivyo Di Maria amesema atasalia Old Trafford msimu ujao licha ya kutokuwa na msimu mzuri (Sun),

Beki wa Ubelgiji Jan Vertonghen, 28,
anapanga kusaini mkataba mpya msimu ujao Tottenham, licha ya kuhusishwa na kuhamia Napoli (Times).

Habari zilizothibitishwa za uhamisho tutakufahamisha zitakapothibitishwa.

Golden State Warriors yaishangaza Cleveland Cavaliers fainali ya kwanza NBA.

LeBron James alifunga pointi 44 lakini hazikutosha kuzuia Cleveland
Cavaliers kupoteza dhidi ya Golden State Warriors 108-100 katika
mchezo wa mwanzo wa fainali za NBA siku ya Alhamis.
Warriors waliweza kurejesha pointi 14 na kupata ushindi katika muda
wa nyongeza, ingawa James angeweza kushinda katika sekunde za
mwisho za muda wa kawaida, lakini alikosa mtupo wa mbali.

Everton yamnasa Tom Cleverley.

Everton watamsajili Tom Cleverley kwa mkataba wa miaka mitano wakati mkataba wake na Manchester United utakapomalizika Julai 1.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa msimu huu na meneja Roberto Martinez. Cleverley alicheza mechi 38 za Ligi Kuu ya England, mechi 37 akiwa anaichezea Aston Villa kwa mkopo.

Nikki Mbishi ajibizana na Nikki wa Pili katika mtandao wa kijamii.


Jana kwenye ukurasa wa Instagrama wa @Cloudsfmtz waliposti mambo ambayo Nikki wa Pili aliyaandika ili kuwapa husia wasanii wanao kuja kuwa na style yao tofauti katika muziki huu wa Hip Hop pia alielezea ni kwa jinsi gani wasanii wa HipHop wa zamani ambavyo wamekuwa hawafanyi vizuri na mambo mengi alizungumzia kuhusiana na muziki wa Hip Hop Sasa baada ya Cloudsfm kupost Nikki Mbishi akaona na ikabidi amjibu Nikki Wa Pili kwa kumwambia "Kama wewe unafanya na uko happy nacho then fanya ila usipotoshe tena kwa kutumia kivuli cha Hip Hop ili hali tunafahamu wewe ni mfanya biashara That’s not Hip Hop ,That’s something else

Google yamuorodhesha Waziri Mkuu wa India kama muhalifu kimakosa.

Kampuni ya mtandao wa Google imeomba radhi baada ya picha za waziri mkuu wa India Narendra Modi kuonekana katika picha za watu kumi wahalifu.
''Tunaomba radhi kwa kuchanganyikiwa na kutoelewana ambako kumesababishwa na picha hizo'',taarifa iliotoka kwa kampuni hiyo ilisema.
 
Viongozi wengine duniani waliomo katika orodha hiyo ni aliyekuwa rais wa Marekani George Bush na Libya Muammar Gaddafi.
Viongozi wengine wakuu wanaopatikana ni waziri mkuu wa Delhi Arvind Kejriwal,wakili Ram Jethmalani na mtoro Dawood Ibrahim pamoja na mwigizaji wa Bollywood Sanjay Dutt ambaye kwa sasa anahudumia kifungo kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea mjini Mumbai mwaka 1993.
''Haya matokeo yanatushangaza na hayawakilishi maoni ya Google'',kampuni hiyo ilisema katika taarifa yake iliotolewa jumatano usiku.
Picha za Modi zinaonekana unapowatafuta watu 10 wahalifu pamoja na magaidi,wauaji na madikteta.
Kampuni hiyo imesema kuwa matokeo hayo yanatokana na gazeti moja la Uingereza ambalo lilichapisha picha ya Modi kimakosa.
Msamaha huo unajiri baada ya wanasiasa wengi wa India kuonyesha wasiwasi wao katika mitandao ya kijamii.