Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Sunday 31 August 2014

Hatimaye Shinji kagawa arejea Dortmund.

Kiungo mshambuliaji Shinji Kagawa aliyenunuliwa na Manchester United kutoka Borrusia Dortmund miaka miwili iliyopita,hatimaye leo hii amerejea kunako klabu yake hiyo ya zamani.

Shinji kagawa amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo baada ya kushindwa kuwika katika misimu yake miwili aliyokuwa Manchester United.

ARSENAL YAJITOA KUMUWANIA REMY

Klabu ya Arsenal imejitoa ghafla katika mbio za
kuifukuzia saini ya mshambuliaji wa QPR
Mfaransa Loic Remy masaa machache baada ya
kudaiwa kuwa imerudi kumuwania tena siku ya
jana.
Sasa milango iko wazi kwa nyota huyo kutua
Chelsea baada ya klabu hiyo kufikia kifungu cha
bei iliyowekwa na klabu yake hiyo inayokipiga
katika dimba la Loftus Road.

Daley Blind atua Manchester United

Hizi ni baadha picha za mchezaji mpya wa Manchester United aliyesajiliwa kutoka Ajax Amsterdam kwa ada ya uhamisho wa Paundi milioni 14.

Anatarajiwa kumaliza taratibu za kujiunga na klabu hiyo ndani ya masaa 12 yajayo.

Lady Jay Dee afunguka baada ya kuzushiwa kutoka na "Serengeti Boy"

Baada ya kuzushiwa kutoka kimapenzi na kijana mdogo "serengeti boys" na gazeti moja kubwa nchini linaloongoza kwa udaku,Lady Jay Dee kupitia ukurasa wake wa Facebook akanusha taarifa hizo.

Akiwa katika hali ya kusononesha sana na kuhuzunishwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini vinavyofanya kila njia ya kumchafua na kuharibu taswira yake katika jamii.

Jay Dee almaarufu kama "KOMANDO" aliiandika hiki kupitia ukurasa wake wa facebook....

"Zamani ilikuwa haipo sehemu ya kujitetea,
gazeti likishaandika ndio limeandika.
Lakini sasa ulimwengu umebadilika, sio muda
wa watu wote kulishwa chakula kisichofaa.
Kwanza hicho kichwa cha habari kimenivunjia
heshma sana
Nafikiri lengo ni kuilazimisha jamii
inayomuelewa JayDee tofauti imuone kuwa ni
mtu asiefaa, sawa.
Dogo anaswa na mkoko? Huo mkoko
mmemnasa nao wapi wakati hizo picha ni
mimi nilizi post mwezi February
Instagram?????
Picha ambazo zilipigwa Nyumbani lounge
tena kutumia simu ya Gardner.
Jide, dogodogo gumzo mjini ��������
Gumzo ni kitu kinachoongelewa sana na
kilichoenea kila kona ,,,,,sasa hii habari ni
gumzo wapi ambapo haisikiki, ......
Mngeandika tumeamua kumuanzishia Jide
gumzo hili, ndio ningewaelewa.
Vitu vya kuzua.
Ni watu wengi tu wakija band wakipata nafasi
wanaomba kupiga picha na mimi na wengine
pia wanaomba kupiga picha na gari sababu
wanaipenda.
Kama mtu yoyote anavyoweza kupiga picha
na sanamu la kitu chochote anachokipenda.
Hivi je! Wimbo wa JayDee mgumba, JayDee
tasa umechuja? Umeisha chati?? Nashangaa
na najiuliza tu
Inawezekana wimbo huo umechuja ndio
maana mnatafuta wimbo mwingine utakao
hit zaidi ya ule
Ndio kinachopelekea kuandika story za
namna hii ����������������
Sio nyinyi mliokuja kuomba radhi kwa yote
mliowahi kuniandika na kudai kuwa
mmejirekebisha, miezi kadhaa tu iliopita?
Sio boss wenu aliemfuata Gardner na
kumwambia tumalize tofauti zetu?
Kama hizo tofauti zilikuwepo ������
Inawezekana nyie ndio mna tofauti na mimi,
sijawahi kuwa na tofauti na mtu hata
nisiemfahamu. ..
Nashukuru Mungu nilikataa msamaha wenu
ni kama nilihisi hamkumaanisha
Au sababu sijawahi kukubali show mlizotaka
kufanya na mimi?
Je! Hiki ni kisasi? Sielewi
Mungu alienisimamia ataendelea
Hii sio vita ya kwanza wala ya mwisho
Dunia ni mapambano.
Kama nia ni kufanya niishi maisha ya uoga,
kudhoofika na msongo wa mawazo
mmefeli ,,,,, wengine mkijidai ni wacha
Mungu huku mkiumiza nafsi za watoto wa
binadamu wenzenu.
No wonder mnaishi bila amani mbali na
utajiri mlionao kwa kuogopa visasi.
Sikuzaliwa kukata tamaa
Pia wapo wanaopenda kuandikwa kwenye
hayo magazeti yenu
Wafanyieni favor ya kuwapa hiyo nafasi mi
sifanyi muziki wa magazeti ya udaku
Mkiachana na mimi nitashukuru sana
Hata ndoa yangu ikivunjika haimaanishi
mnitafutie story za kunichafua
Ndoa ya Madiba ilivunjika sembuse yangu
nina utofauti ipi na binadamu wengine?
Nyie ndoa zenu ziko perfect si ndio?
Hewala watakatifu nyie, mnaoficha yenu na
kutangaza ya wenzenu.
Mwisho nawaomba watu mnaonielewa
kutoamini tu habari yoyote ambayo haijatoka
kwangu wala kwa muwakilishi wangu ambae
ni "Webiro Wakazi Wasira".
Kama kuna chochote cha watu kujua
nitakiongea mimi kwa mdomo wangu sio
kuwekewa maneno mdomoni.
Kila siku ooooh tulimpigia simu hapatikani,
namba yangu yenyewe kwanza hata
mnaijua???
Mngekuwa mnaijua msingekuwa mnahangaika
mnawapigia watu wangu wa karibu
kunitafuta , na hao watu hawawezi kunisaliti
ndio sababu mpaka miaka 70 mtaishia
kusema tulimpigia simu JayDee hapatikani.
Nyie muongee chochote mnachojiskia
Ila sie hatuna haki kujitetea ??
Hili nalo litapita kama mengine
Na inshallah nitakuwa hapa hapa
nimesimama nawaangalia
Picha moja wapo ni hiyo ambapo mtoto wa
vitoto alikuja siku hiyo hiyo na akapiga picha
na Gardner, mbele ya gari hiyo hiyo
mnayodanganya watu kuwa mmemkuta nayo
na mahala ni hapo hapo Nyumbani
Lounge, ,,,,, na picha nyingine ni hizo
nilizowahi kuzi post mimi mwenyewe mwezi
february leo zinanihukumu
endeleeni kudanganya jamii
Na hizo ni chat alizoniandikia huyo mtoto wa
vitoto ambae ndio ilikuwa mara yangu ya
kwanza kumuona na sijawahi kumuona tena. .
Zaidi ya kuongea nae twitter ,,, sisemi kama
mimi malaika lakini
Ukweli huwa hauchanganywi na uongo
Kwa hili mmenidhalilisha sana
Kama nia yenu jamii inione mwanamke
nisiefaa na ninaependa dogodogo
Basi Mungu atawaonyesha ukuu wake.8+**7"

Itakuwa ni jambo jema sana kwa "blogs" au chombo chochote cha habari kutokuandika taarifa yoyote kwa nia ya kumuharibia au kumchafua msanii au mtu falani katika jamii kwa msalahi ya mtu au watu fulani.

Sisi kama BantuTz tunaahidi hatutoandika habari yoyote isiyo na ukweli halisi.Ni wajibu wetu kukuletea habari iliyo haririwa vizuri pasipo mmpendelea au kumkandamiza mtu yeyote yule.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata habari za muhimu,za uhakika na zenye mantiki.

Imeandaliwa na........Katemi Methsela.

Tetesi za Usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya na BantuTz SPORTS.

Arsenal huenda wanakaribia kumsajili Alessio
Cerci, 27, kutoka Torino baada ya mchezaji
huyo kuachwa katika kikosi kitakachocheza
na Inter Milan Jumapili (Daily Star),

Arsenal
wanakaribia kumsajili kiungo wa
Southampton Morgan Schneiderlin, 24, baada
ya kukubali kutoa pauni milioni 24
(CaughtOffSide),

Manchester United huenda
ikashuhudia wachezaji 11, ama wakiondoka,
au kuingia Old Trafford kabla ya dirisha la
usajili kufungwa Jumatatu (Daily Star),

Real
Madrid wapo tayari kuwajaribu tena
Manchester City kumtaka Alvaro Negredo, 29
(Mirror),

Louis van Gaal alimshawishi Robin
van Persie kuahirisha upasuaji wa goti kabla
ya Kombe la Dunia, lakini sasa huenda
akamkosa mshambuliaji huyo wakati fulani
msimu huu (Daily Mirror),

Juventus
wanaamini kukamilisha uhamisho wa
Radamel Falcao. Real sasa wanamtaka Javier
Hernandez (Gazetta dello Sport),

Arsenal
wameacha kumfuatilia Loic Remy wa QPR
ambaye anajiandaa kujiunga na Chelsea
(BBC).

Imesalia siku moja tu kabla ya dirisha
la usajili kufungwa. Tetesi nyingine na
uhamisho wa dakika za mwisho, tuwe sote
kesho tukijaaliwa.Endelea kutembelea www.bantutz.com

HAYA NDO MAPYA YALIYOBUKA OLD TRAFORD KUHUSU ROJO


Mlinzi Marcos Rojo aliyesajiliwa Manchester
United kutoka Sporting Lisbon ya Ureno
anakabiliwa na shauri la jinai kwao Argentina,
na
ndilo linamzuia kuanza kuchezea timu yake
mpya. Hadi Jumapili hii asubuhi alikuwa
hajapatiwa visa ya kumwezesha kufanya kazi
nchini, kutokana na madai kwamba ana kesi ya
jinai ya kupigana na jirani nchini Argentina
tangu
2010 ambayo bado ipo kwenye majalada ya
polisi. Rojo (24) alikamilisha usajili kwa dau la
pauni milioni 16 wiki mbili zilizopita, lakini
upelelezi wa vitendo vyake vya jinai
unasababisha zuio la yeye kupewa visa, walau
kwa muda huu, japokuwa Kocha Mkuu wa Man
U, Louis van Gaal anasema ana uhakika
mchezaji huyo atakuwa tayari kwa mechi dhidi
ya Queen Park Rangers (QPR) Septemba 14.
Imeelezwa, hata hivyo, kwamba Chama cha
Soka
(FA) cha England kimeshamalizana na suala la
mtu huyo wa tatu na kimetoa hati ya
kumwezesha kucheza, lakini kinachosubiriwa
sasa ni visa, kwani aliyoingia nayo ni ya utalii.
Hivi sasa Rojo yupo Madrid, Hispania kwa ajili
ya kusubiri kuhojiwa na watumishi wa Ubalozi
wa Uingereza ambao watatathmini kwa kina
ugomvi aliosababisha wakati huo, na wakiona
inafaa watampatia visa ya kufanya kazi nchini
Uingereza. Fernando Burlando ambaye ni
mwanasheria wa Rojo, amedai kwamba
mchezaji
huyo aliyekuwa kwenye Timu ya Taifa ya
Argentina ameshaonekana na polisi kuwa na
kesi, hivyo anasubiriwa kupelekwa mahakamani,
lakini akasema watalimaliza suala hilo. Amedai
hata akitiwa hatiani, anaweza kuwekwa chini ya
uangalizi na kupewa adhabu ya kufanya kazi za
jamii, ambazo si lazima azifanyie nchini
Argentina, hivyo ataweza tu kuingia Uingereza.
Kabla ya mechi ya Jumamosi hii ya Man United
dhidi ya Burnley iliyoisha kwa suluhu, Van Gaal
alisema; “ni suala la muda tu. Mimi ni kocha
wa
klabu kubwa zaidi duniani lakini siwezi kubadili
sheria.” Baada ya mechi hiyo, akasema;
“naamini kwamba tutakapocheza na QPR
atakuwa ameshaipata (visa).”

Tambwe afungua akaunti ya magoli.

Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu
uliopita, Khamisi Tambwe ameanza kuonyesha
makali baada ya kupiga bao mbili katika
mechi ya jana usiku Simba ilipoiadhibu
KMKM ya Zanzibar kwa mabao 5-0.

Tambwe raia wa Burundi alipiga bao mbili na
kuiwezesha Simba kuongoza kwa mabao 4-0
hadi mapumziko kwenye Uwanja wa Amaan,Zanzibar.

Wengine waliofunga mabao ni wakongwe
Amri Kiemba na Shaaban Kisiga ambaye
alipiga bao zuri sana baada ya kupokea pasi
ya Tambwe.

Kipindi cha pili, Elius Maguri naye alipiga bao
la tano huku wanachama wa kundi la Friends of
Simba (Fos) wakishuhudia uwanjani hapo.
Simba ilionyesha soka safi na la kuvutia
katika kipindi cha kwanza lakini ikaendelea
kuwapa kazi KMKM katika kipindi cha pili
huku ikitumia vijana zaidi.

Saturday 30 August 2014

Gerrard akabidhiwa jukumu la "kumfunda" Balloteli.

Gerrard amepewa jukumu la kumuongoza
kimaadili Mario Balotelli kiwanjani na suala
la ndani ya klabu litakua juu ya Brendan
Rodgers huku Balotelli mwenyewe akiambiwa
ajiangalie nje ya klabu kimatendo na
kimaadili, kutokufanya jambo lolote
litakalomchafua ama kuchafua klabu.

Manchester United yamsajili Daley Blind

Manchester United wamekubaliana na Ajax
kumsajili mchezaji Daley Blind kwa thamani
ya pauni milion14.2, kwa mkataba wa miaka
4 na uwezekano wa kumuongezea mwaka wa
5 kama mambo yakienda sawa,pia
Manchester United imekubaliana na Ajax
kuwa endapo Man United itataka kumuuza
Daley Blind basi baadhi ya pesa yake ya
usajili watapewa Ajax.
Daley Blind anatarajiwa kucheza kama kiungo
mkabaji katika timu ya Manchester
United,kutokana na mapungufu ya kiungo
yanayo iandama klabu ya Man Utd,lakini pia
Daley Blind anauwezo wa kumudu kucheza
kama beki wa kushoto.

Diamond atajwa kuwania tuzo za kimataifa.


Muimbaji wa Tanzania, Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz ametajwa kuwania tuzo za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (International Reggae and World Music
Awards (IRAWMA).
Diamond ametajwa kuwania kipengele cha Best African Song/Entertainer na wimbo wake ‘Mdogo Mdogo’.
Kwenye kipengele hicho, Diamond anachuana na Aye – Davido (Nigeria). “Bundelele, –Awilo Longomba (Congo) “Tam Tam” – Willy Paul Msafi (Kenya), ”Sitya Loss” – Eddy Kenzo
(Uganda), na “Mama Africa” – Bracket (Nigeria).


Kufahamu namna ya kumpigia kura Diamond bofya hapa:MPIGIE KURA DIAMOND

Alichokiandika katika ukurasa wake wa facebook
"Nashkuru sana Shabiki zangu pendwa.. Naamini support yenu ndio imefanya nyimbo hii ya Mdogo Mdogo kuchaguliwa kuwania kuwa Nyimbo bora Ya Africa katika tunzo za IRAWMA nchini America...na namini huu ni mwanzo tu! NOW LET THE VOTING GAME BEGIN!!!! hii ndio
Link ya kupiga kura wadau..
http://irawma.com/irawma_vote2014"

"El Nino" ajiunga AC Milan.

Fernando Torres ameondoka Stamford Bridge
na kuhamia San Siro.
Straika huyo atakua AC Milan kuziba pengo la
Mario Balotelli baada ya mu-Italiano huyo
kujiunga na Liverpool kwa ada ya £16m.
Torres na Chelsea wamwfikia makubaliano
hayo ya kukatisha mkataba wao wa miaka 5
na nusu, baada ya straika huyo kuitumikia
The Blues bila mafanikio kwa miaka mitatu na
nusu.
Amesaini mkataba wa miaka miwili na AC
Milan kama mchezaji huru huku ikiaminika
Chelsea imemlipa kiasi cha pesa ili
kuhitimisha mkataba wake uliokua ukimlipa
£150,000-kwa-wiki kwa kua alisalia na miaka
miwili mkataba huo kumalizika.
Torres ameifungia Chelsea bao 45 tu katika
michezo 172 tokea kusajiliwa kwa ada ya
£50milioni akitokea Liverpool.

Friday 29 August 2014

Di Maria afanya mazoezi na wachezaji wenzake kwa mara ya kwanza Manchester United

Mchezaji mpya aliyesajiliwa kwa pesa iliyovunja rekodi katika soko la usajili Ligi Kuu ya Uingereza.Angel Di Maria,kwa mara ya kwanza ameanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake huko Carrington AON Training Complex

Baada ya kusajiliwa kutoka Real Madrid,kwa kitita cha Paundi milion 59.7

Angel Di Maria ambaye amekuwa tumaini jipya kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kupoteza uelekeo katika mechi mbili za awali,amekabithiwa jezi namba 7 ambayo huvaliwa na magwiji katika klabu hiyo.

Kwa mara ya kwanza amejumuika na wenzake huku akionekana mwenye furaha na shauku ya kufanya makubwa katika klabu yake Mpya.

Ratiba ya Ligi kuu Uingereza Mwisho wa Juma hili.

RATIBA | England - Premier League

Kesho Jumamosi

14:45 Burnley vs Manchester United

17:00 Manchester City vs Stoke City

17:00 Newcastle United vs Crystal Palace

17:00 Queens Park Rangers vs Sunderland

17:00 Swansea City vs West Bromwich Albion

17:00 West Ham United vs Southampton

19:30 Everton vs Chelsea

Jumapili
15:30 Aston Villa vs Hull City

15:30 Tottenham Hotspur vs Liverpool

18:00 Leicester City vs Arsenal

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata matokeo na uchambuzi wa michezo itakayopigwa hapo kesho.

Tetesi za Usajili katika magazeti mbalimbali Barani Ulaya na BantuTz SPORTS

Real Madrid wamekamilisha uhamisho wa
pauni milioni 20 wa Radamel Falcao, 28,
kutoka Monaco (Calciomercato),

Arsenal
wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa
beki Sorkatis Papastathopoulos, 26, kutoka
Borussia Dortmund, lakini wamesema
hawatalipa pauni milioni 20 (Daily Mirror),

Meneja wa Aston Villa Paul Lambert ametoa dau
la pauni milioni 8 kumtaka kiungo wa
Manchester United Tom Cleverly, 25, (Daily
Telegraph),

Lakini Lambert huenda wakapata
upinzani mkali kutoka Valencia, ambao nao
pia wamepanda dau kwa Cleverly (Sky
Sports),

Danny Welbeck, 23, anajiandaa
kuondoka Old Trafford, na akitajwa kwenda
Tottenham kwa mkopo (Daily Star),

Chelsea
wanakaribia kutoa ruhusa kwa Fernando
Torres, 30, kwenda Inter Milan (Times),

Manchester United wameongeza bidii
kumfuatilia kiungo Martin Odegaard, 15,
anayechezea Stromsgodset kutoka Norway
(Daily Telegraph),

Valencia na Juventus
wametoa dau la kutaka kumsajili Javier
Hernandez, 26, kutoka Manchester United
kwa kiasi cha pauni milioni 15 (Guardian),

Mshambuliaji Demba Ba, 29, alikaribia
kujiunga na Arsenal kabla ya kusaini kwenda
Besitkas ya Uturuki kutoka Chelsea kwa pauni
milioni 8 (Independent),

kiungo anayesakwa
na Manchester United Arturo Vidal, 27,
amekaririwa akisema hataki kuondoka
Juventus (Daily Express),

kiungo wa zamani
wa Arsenal Alex Song, 26, ana matumaini ya
kurejea katika Premier League na Liverpool
baada ya Barcelona kuonekana kutomtaka
(Daily Mirror),

kiungo wa PSG Adrien Rabiot
ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao
anasakwa na Roma na Arsenal (Le Parisien).

Zimesalia siku tatu kabla ya dirisha la usajili
kufungwa.

Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze taarifa mbalimbali za Usajili barani Ulaya.

Damu yazidi kumwagika katika eneo la Mlima Mbalizi huko Mbeya.

Watu kumi wamefariki papo hapo na wengine saba kujeruhiwa  vibaya baada ya Gari toyota Hiace waliyokua wakisafiria kugongana uso kwa uso na Fuso katika eneo la Mbalizi jijini Mbeya.

Eneo hili limekua kitovu cha ajali mbali mbali kwa mda wa Miongo kadhaa sasa kwani katika Mwezi huu pekee zimeshatokea ajari tatu.

Majina ya waliopoteza maisha hayajajulikana bado kutokana na baadhi ya maiti kujrruhiwa vibaya na dereva wa fuso kutimkia kusiko julikana!!

Endelea kutembelea www.bantutz.com tutakuwa tunakujuza kila kitakachokuwa kinaendelea.

Imeandaliwa na....
                               Peter Bulimbe.

MGANGA KUFIKISHWA KIZIMBANI KISA KUPATA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU NA KUMUINGILIA KIMWILI MTEJA WAKE.


Mganga wa kienyeji Michael Yahya(34) anashitakiwa na  Mwanahamisi Omary kwa kosa la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu na kumuingilia kimwili mwana mama hyo.

>Mwanahamis 26, ambaye ni mke wa mtu  alikua akisumbuliwa na tumbo la uzaz na ivo akaamua kwenda kwa mganga hyo aliyekua akitoa matibabu nyumbani kwake na baadae kuyaamishia katika nyumba ya wageni iliyoko maeneo ya kigogo luhanga

>Akizungumza kuputia kwa wakili wake  Felista  Mosha Mshitaki hyo ameieleza mahakama ya wilaya ya ilala kua Mganga hyo alikua akipaka dawa kwenye uume wake na kumuingilia kimwili bila kujua kwani alimwambia kua anamajini ambayo yanataka mtoto na baadae akampigia  simu mme wake Bw.Edrick Elinezer na kumweleza kua mkewe anamajin yanayotaka mtoto ivo alete gari yake aina ya toyota Lav 4, yenye namba za usajili T 139 BSG.

>Lakin hta ivo baada ya kuendelea kupokea  matibabu hayo kwa  mda mrefu Mwanahamisi hakupata mafanikio kwa mda wa miez sita na ivo kutambua kua alidanganywa na kuliwa changa la macho kwani Gari hyo ilikua na thaman ya Tsh.  12mil.

Baada ya kufikishwa mahakaman mtuhumiwa alipewa dhamana lakin akatoroka ivo Hakim ameamuru wadhamini wake kumtafta na endapo atakosekana watalazimika kulipa faini ya Sh. Mil 6, kila mmoja.

Kesi hyo itatajwa tena tar.18 Septemba!!

Spika wa Bunge ahusishwa na kashfa ya kuwauza watoto


Spika Hama Amadou alitoroka baada ya kuhusishwa na kashfa ya kuwauza watoto
Spika wa bunge la Niger ametoroka nchini humo baada ya kamati ya bunge hilo kuafikia kukamatwa kwake kuhusiana na kashfa ya kuwauza watoto.
Hama Amadou, ambaye tayari ameelezea azma yake ya kugombea urais mwaka 2016, anasema kuwa madai hayo dhidi yake yamechochewa kisiasa.
Mke wa pili wa spika huyo na watu wengine 16 walikamatwa mwezi Juni baada ya kutuhumiwa kuwauza watoto wachanga Kusini Mashariki mwa Nigeria.
Watoto hao huuzwa kwa maelfu ya dola kila mtoto.

kesi hiyo imetoa fursa tosha kwa chama tawala kumuondoa Bwana Amadou kutoka katika chama hicho tangu kukosana na muungano tawala.
Kashfa hii pia imewashtua wengi katika nchi hiyo yenye idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu hasa kwa kuwa ni kosa kuonyesha kuwa watoto walioasiliwa na wako binafsi.

Imeripotiwa kuwa baadhi ya wanawake walidai walikuwa wajawazito na kwenda Nigeria kabla ya kurejea na watoto wao.
Kamati kuu ya bunge la taifa ambalo linamjumuisha naibu spika na wakuu wengine wa kamati nyinginezo, walikutana Jumatao, na kukubaliana kuwa polisi wanaweza kumkamata na kumhoji bwana Amadou kuhusiana na tuhuma hizo.

Wanasiasa sita wa upinzani walikataa kuhudhuria vikao hivyo ingawa idadi ya wabunge waliofika ilitosha kutoa uamuzi.
Kikao kamili cha bunge kitahitajika kufanyika ili kuondoa uwezekano wa bwana Amadou kushitakiwa.
Inadaiwa watoto 30 wameuzwa katika kashfa hii ambayo imehusisha kutengeza stakabadhi bandia na kubadili vyeti vya kuzaliwa vya watoto waliouzwa.

HEKIMA ZA KIIMBILA "MANCHESTER WANAPOJIFUNIKA KITAMBAA CHEUSI WAKATI WA JUA KALI"





Photo: Louis van Gaal hails Di Maria as a team player and believes he will succeed at United: “He can accelerate the game for us but he can also play in the interest of the team. That is what I like in Di Maria, not only his class.” 

More from the boss: http://bit.ly/1vqewT5    Naona sasa Manchester united wameamua kwenda Muhimbili na kupasuliwa kichwa wakati wao wanaumwa goti.

      Inasikitisha sana yani kwa jinsi walivyoshangilia ujio wa Angel di Maria ni kama vile hawana wachezaji wakubwa au pengine wachezaji wakubwa zaidi ya huyo,wapo wengi sana. 

 Photo: Robin van Persie returned to action for the Reds last weekend and we can’t wait to see what he can do this season. Watch his highlights and best goals from the last two years at United here: http://bit.ly/18yPo2B
Kagawa,Rooney,Juan Mata na Robin Van Persie wote hawa wana uwezo mkubwa na hata majina makubwa,tatizo hawa Red Devils wanaumwa kichwa lakini wameamua kwenda Muhimbili kupasuliwa goti sasa tusubiri tuone matokeo yake utasikia mara Edwood kapigiwa makofi mara anazomewa. 
Photo: Walking out last night as captain of Manchester United was an unbelievably proud moment for me and my family. It’s a huge honour for me to captain this great club and I will take great pride in doing so. I would like to thank all the fans for their support, I am looking forward to the exciting times ahead and leading their club to more success.
Manchester United wamefunika macho yao na vitambaa vyeusi yani wao hata mchana wanaona giza tatizo la timu yao hawalioni wanakimbilia kusajili majina makubwa.
 Photo: Welcome to Manchester United Marcos Rojo looking forward to playing with you.
Sawa bwana kwani mara nyingine uzuri wa mapambo huficha ubaya wa bibi harusi japo siyo siku zote. 
 
Hapo naanza kumkumbuka Sir Alex Ferguson kama daktari basi alikuwa daktari bingwa sana au mashuhuri kwani aligundua tatizo na kulifanyia kazi kwani alimchukua Robin Van Persie kutoka kwa jirani yake mmoja akiona kabisa kuwa alikosa ubingwa kisa hakuwa na mshambuliaji makini na wa uhakika. 
Photo: How many LIKES For Chicharito???
Mi naamini Chicharito hajawai kushuka wala kupanda kiwango lakini Chelsea walikuwa wakimwona akitokea bench basi suruli zao zilijaa maji, jasho na wengine hata mikojo, kwanini? 
 Sir Alex Ferguson
Hilo swali majibu yake anayao Ferguson akiwa ameketi nyumbani kwake au kwenye mashindano ya farasi hana habari kabisa ila majibu anayo. 

We unamkumbula Welbeck dhidi ya Real Madrid au mi sikuona naamini isingekuwa kadi Nyekundu ya shujaa wa siku hiyo na muoga wa leo Luis Nani basi Manchester United wangempiga yule jamaa.

Rafael Da Silva- The Brazilian Beast        Tazama hii Rafael, Evra, Vidic na Ferdinand sawa hata kama watu wanazeeka au wanafulia ila usingepita kirahisi kwenda kufunga goli wakati nje Ferguson kakaa pale kwenye bench fundi peke yake fundi mwenyewe.
 Photo: Louis van Gaal blames "big errors” in the build-up to MK Dons' goals but encourages fans to stick by the Reds: “Of course it’s very disappointing; I hope they maintain their confidence in the club and in our philosophy because that philosophy takes time.”
 Mi naamini Luis Van Gaal baba yake na Robben, Sneijder, Van Persie na Huntelaar ni kocha mzuri ila naomba tu mniruhusu nimnyanganye kitambaa cheusi walichovaa mashabiki wake ili yeye asione giza na nimkataze kwenda Muhimbili asije akapasuliwa kichwa wakati yeye ni mgonjwa wa goti.
    
       Imeandaliwa na..........

                                             Kelvin Kiimbila Ngote Jr.
                                        {BantuTz CABINET MEMBER}
                                               {+255719580495} 
                                              
Ni muendelezo wa BantuTz kuinua vipaji mbalimbali vilovyojificha,kama unauwezo wa kuandaaa makala makini na zenye mantiki usisite kuwasiliana +255716418657

Mji wenye "wanawake Warembo" Brazil watafuta wanaume.


Mji mmoja nchini Brazil ambao una wanawake watupu, wengi wakiwa vijana na "warembo mno" umetoa wito wa kutaka vijana wa kiume - ambao bado ni makapera (yaani single).
Kwa mujibu wa tovuti ya Metro, mji huo uitwao Noiva do Cordeiro, una watu 600,ambao wote ni wanawake. Watoto wa kiume wanaozaliwa katika mji huo hutakiwa kuondoka wakitimiza umri wa miaka 18, na waume kadhaa wenye wake zao huko,hutakiwa kwenda mjini humo siku za wikendi tu.
Wanawake vijana katika mji huo sasa wamechoshwa na kutokuwepo na wanaume na wametoa wito kwa wanaume makapera kujitokeza.


"Hapa, wanaume pekee tunaokutana nao,ama wameoa, au ni ndugu zetu, kila anaye kuja hapa ni binamu. Sijapata kubusu mwanaume kwa muda mrefu," amesema Nelma Fernandes, 23, akizungumza na gazeti la Mirror.

"Sote tunaiota siku ambayo tutakutana na mwanaume na kupendana naye na kufunga ndoa. Lakini tunapenda kuishi hapa, na
hatutaki kuuhama mji wetu kwenda kutafuta waume."
Mji huo wa 'ajabu' ulianzishwa na Maria Senhorinha de Lima, aliyekimbia ndoa ya kulazimishwa na pia kubandikwa jina la
mzinzi.


Wanawake wengine waliotengwa na jamii waliungana naye na mji wa Noiva do Cordeiro ukazaliwa.Lakini kabla makapera hamjakata tiketi kwenda huko, kuna tahadhari:"Utafuata tunalosema na kuishi kwa sheria zetu," anasema Nelma. "Kuna vitu vingi ambavyo wanawake hufanya vizuri zaidi kuliko wanaume. Mji wetu ni mzuri, una utaratibu mzuri, na una amani zaidi kuliko kama ungekuwa unaongozwa na wanaume.
"Na pia mara zote kuna muda wa umbea, na vilevile kujaribu nguo na kutengeneza nywele na kucha."
Haya, makapera, kazi kwenu.

Mawaziri wa Afya nchi za Afrika Magharibi wakutana kujadili Ebola


Mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika Magharibi wamekubaliana kuondoa upigaji marufuku wa safari za ndege na ufungaji wa mipaka kwa nchi ziliathirika kutokana na ugonjwa wa Ebola. Mawaziri hao ambao wamekutana mjini Accra, Ghana kupitia upya mikakati iliyokuwa ikitumika kupambana na virusi vya ebola pia wametoa ombi maalum kwa mashirika ya ndege kurejesha safari zao katika nchi zilizoathirika.

Mawaziri wa afya wamesisitiza mkakati wa pamoja kuwa bado ni mpango bora kabisa katika kupambana na ugonjwa wa ebola. Mawaziri hao wamezitaka nchi kutofunga mipaka yao kwa nchi zilizoathirika lakini wabakie kuwa waangalifu.
Wamekubaliana kupeleka timu ya wataalam katika nchi hizo pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu ambapo Ghana imekubali kuwa kituo cha kuratibu shughuli za misaada ya kibinadamu kwa nchi zilizoathirika katika eneo la Afrika Magharibi.
Wafanyakazi wa afya wakimhudumia mgonjwa wa Ebola
Pia wamekubaliana kuongeza raslimali watu ikiwa ni pamoja kutakiwa haraka kwa wafanyakazi wa afya, vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo, na vituo vya kuwahifadhi wagonjwa.
Shirika la Afya la Afrika Magharibi lina wiki moja ya kuandaa hatua za kuchukua na kuandaa bajeti ili kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani na wadau wengine.

Mawaziri wote wa afya isipokuwa wale wa kutoka nchi zilizoathirika kutokana na ugonjwa wa ebola za Guinea, Sierra Leone, Liberia na Nigeria walihudhuria mkutano huo.

Waliobaki hawakuweza kuhudhuria kutokana na matatizo ya ndani na matatizo ya usafiri wa ndege ambao umesitishwa katika nchi zilizoathirika.
Mawaziri wa faya wametoa ombi maalum kwa mashirika ya ndege kurejesha safari za ndege na kuendelea kuruka kwenda katika nchi zilizoathirika.
Hata hivyo wamesisitiza upimaji wa joto la mwili na kuhakikisha usafi wa mikono katika vituo vya kuingia na kutoka

Okwi arejea Msimbazi aahidi makubwa Ligi kuu bara


Njia zile zile walizotumia mahasimu wao Dar es salaam Young Africans kumpata mshambuliaji mganda Emmanuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani,wekundu wa Msimbazi Simba SC imeitumia kumrejesha kundini Mganda huyo hii leo Mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi akitambulishwa na mwenyekiti wa kama ya usajili ya klabu ya Simba Zakaria Ha
Pope.


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya
kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji “Baada ya kulipitia suala lake na Yanga
kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia,tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili
acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe


Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na mganda mwenzake, Joseph Owino,Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni “Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea,tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.


Kwa upande wake Okwi ambaye ameahidi makubwa msimu huu mara baada ya kurejea hii leo alianza kuichezea Simba kwa mara ya kwanza akiwa kinda wa miaka 17 akitokea Sports club Villa ya
Uganda mnamo mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya
Tunisia Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake
kwa miezi mitatu na hivyo Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea,aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya
kwao 


Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya
Jangwani Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu
uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu mwezi Machi, ikiwa ni miezi minne tangu asajiliwe.


Lakini majaliwa ya mshambuliaji huyo mwenye kasi ya kutisha na uwezo wa kufumania nyavu kuichezea Simba kwa sasa yako mikononi mwa TFF na FIFA