Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday 31 May 2014

MBOWE Mnatuhalibia Chama, Chadema Inazidi Kupoteza Mvuto

Mimi nasema tena kuwa mimi nimwanachama hai wa CHADEMA, Nimemsema mh. Mbowe kwakuwa yeye ndiye mwenyekiti wetu na mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, haya yanayoendelea kukishushia heshma chama hayaoni? Dr. Slaa naye kama katibu wa chama hayaoni?.

Ni aibu kubwa sana taasisi kubwa kama hii yenye watu makini kiasi hiki kupambana na mtu mmoja tena mwisho wake tunaishia kupata aibu.

Kwani faida yetu sisi wananchi na wanachama mkimmaliza Zitto Kabwe kisiasa ni ipi?

Hapo awali mmetengeneza migogoro wenyewe kwa kumjengea tuhuma zisizo na ushahidi kama taarifa kutoka makao makuu ya chama kuhusu nyendo za ZZK toka mwaka 2008 kwa kupokea pesa toka CCM, mbona hamjatuletea ushahidi wa uhakika nasi tukajihakikishia?

Matokeo yake kila mmoja ameona utofauti wa CHADEMA ya mwaka 2013 na CHADEMA ya mwaka 2014. 
Kwenye hili swala la leka dutigite, NSSFna TANAPA mmefanya uchunguzi wa kutosha na mkapata uhakika na mlichopeleka bungeni?

Tunataka ushahidi hapa ili na wananchi tujihakikishie sio mnatuletea propaganda za kijinga hapa na kuanza kuaminisha watu.

Nimesoma ufafanuzi wa Zitto mwenyewe, NSSF na TANAPA nimesikitika sana kuona kuwa maelezo haya kama ni ya kweli basi CHADEMA ndio itazidi kupoteza mvuto.

Nashindwa kuwaelewa na hawa washabiki wanaoshinda humu wakishabikia ujinga bila hata kufikiri ilimradi Mbowe kasema.

Watu wanabaki kuchangia changia ujinga wao humu hata katika ujenzi wa chama hawaonekani wakidhani ndio ukomavu wa chama kumbe ndio wanazidi kukibomoa chama.

Mnajifanya wanachama wa CHADEMMA kwa kutetea hata ujinga wa baadhi ya viongozi ndio mnazidi kukimaliza chama, mfano huyu huyu ZZK alipoongelea kidogo habari za Mbowe wengi wenu mlianza kulalamika kwanini aongelee habari za Mbowe. 

Sasa ZZK sio binadamu kama alivyo Mbowe au kiongozi mwingine anayeweza kuumia anapozushiwa na kuchonganishwa kwa wananchi?

Mashabiki nawashauri acheni kupumbazwa.

Akodi ngoma kumfumania mkewe akitoa penzi kwa rafiki yake..mtaa wafungwa


Na Dustan Shekidele, Morogoro
AMA kweli dunia ina mambo na mambo yenyewe ndiyo haya! Katika hali ya kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Ramadhan Ally, mkazi wa Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro amewashangaza wengi kufuatia uamuzi wake wa kukodi ngoma ya asili kwa lengo la kwenda kumfumania mkewe aliyejulikana kwa jina moja la Asha.

Tukio hilo lililofunga mtaa lilijiri asubuhi ya saa 3:14  Jumatatu iliyopita eneo maarufu kwa jina la Sultani baada ya mwanaume huyo kutonywa kuwa, mke wake alikuwa amelala kwa rafiki yake kipenzi, Abdallah Elias.

Baadhi ya wananchi waliobahatika kuwasili katika eneo la tukio walishuhudia mwenye mali akiwashushia kichapo kikali ‘wasaliti’ hao ambapo vurugu zikapamba moto.

Kufuatia hali hiyo, viongozi wa serikali ya mtaa huo waliamua kutoa taarifa kwa Kamanda Mkuu wa Ulinzi wa Jadi Kata ya Mbuyuni, Aidan Mtimbo ambaye alifika eneo la tukio na vijana wake na kuwasomba watuhumiwa hao msobemsobe huku wakisindikizwa na ngoma hiyo hadi Kituo cha Polisi Kata ya Mbuyuni.

Katika hali ya kushangza, nje ya kituo hicho cha polisi baadhi ya wananchi waliokuwa na hasira walishinikiza watuhumiwa watolewe nje wawafanyie kitumbaya huku baadhi yao wakikipopoa mawe kituo hicho kilichokuwa na askari mmoja aliyevaa nguo za kiraia.

Baada ya vurugu hizo, afande huyo alipiga simu kituo kikuu cha polisi kuomba msaada ambapo askari wa pikipiki walifika na kuwakodia teksi watuhumiwa hadi kituoni.

Mwandishi wetu alifanikiwa kuwahoji wahusika wote watatu ambapo mume wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza kama ifuatavyo:
“Huyu mwanamke ni malaya sana, kwanza  nimemtoa kwao Matombo (Morogoro) akiwa na watoto wawili na kila mmoja na baba yake.

“Mimi sikujali hilo, ukipenda bonga penda na ua lake. Miezi mitatu iliyopita aliniambia ana ujauzito wangu, taarifa hizo zilinifurahisha sana. Cha ajabu juzi akaniambia ametoa mimba yangu, nilipomuuliza kwa nini, akasema kwa ujeuri eti hayupo tayari kuzaa na mimi kwa sasa.

“Nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao, jana usiku napokea taarifa kuwa yuko nyumbani kwa rafiki yangu kipenzi, Abdallah Elias.

“Ndiyo asubuhi nikakodi ngoma na kwenda, niliwakuta wamelala kitandani.”
Kwa upande wake Elias alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema: 
“Huyu mwanamke ni mbaya sana, ametuchanganya mimi na rafiki yangu Dullah, yeye kaja kwangu jana Jumapili akaniambia  amefukuzwa na mumewe hivyo anaomba alale kwangu kesho  yaani leo aende kwao Matombo kumbe alisharudishwa kwao toka juzi.”

Naye mwanamke huyo alipohojiwa na paparazi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Huyu mwanaume (Ramadhan) hajanioa, kila siku nikimwambia twende kwa wazazi wangu ananipiga danadana. Ni kweli nimetoa mimba yake, siko tayari kuzaa naye mtoto nje ya ndoa. Huyu Elias, yeye alionesha nia ya kunioa.”

Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya amethibitisha kutokea kwa fumanizi hilo kwenye mtaa wake lakini aliwatupia lawama polisi wa pikipiki kwa kupuuza uongozi wa juu wa kata hiyo ambao kwa kushirikiana na walinzi wa jadi walifanikiwa kuwalinda watuhumiwa wao na kufika salama kwenye kituo cha polisi.

Kifo Cha George Tyson Chamliza Mboni Mwasimba,AY aonesha upendo wa dhati...

Mtangazaji wa kipindi cha Mboni Show, Mboni Masimba akilia kwa uchungu akiwa nje ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakati wakisubiri kusafirisha maiti kuelekea Dar. Marehemu Tyson ndiye alikuwa Mtayarishaji wa kipindi chake na walikuwa wote katika safari hiyo, ingawa walikuwa magari tofauti.
Katika hatua nyingine, msanii wa Hip Hop nchini, Ambwene Yessaya 'AY' (anayehesabu pesa) aliamua kujitole kununua jeneza la kusafirishia mwili w marehemu, jeneza hilo liligharimu kiasi cha shilingi laki sita ambazo AY alizitoa cash!

Wakisaidiana kubeba jeneza hilo kuelekea hospitalini baada ya kulinunua
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kufahamu kila kitakachokuwa kinaendelea kuhusiana na msiba huu

Penzi la Kitale a.ka Mkude simba na Penny lapamba moto.....

Juzi ilisambaa   picha ya KITALE (Kwasasa unaweza kumuita MKUDE SIMBA)  akiwa anapigwa kiss zito na PENNY lenye hisia kali (Daah mtoto P hadi akafumba macho).....Nikawaachia wadau wengi walishangaaa..Sasa leo tena mwanadada Penny Kupitia akaunti yake ya Instagram ametupia hii....

Sina cha ku-comment zaidi ya kukumbuka msemo wa Penzi ni kama kikohozi.....Halifichiki
Endelea kutembelea katemmethsela.blogspot.com uweze kujua undani wa mahusiani wa mastaa hawa wawili hapa Nchini....

Kuna tetesi kuwa Beyonce ana uhusiano wa kimapenzi na bodyguard wake Julius De Boer

Wanandoa mastaa, Beyonce Knowles na Jay Z wamekuwa wakihudhuria sherehe mbalimbali licha ya kuwepo uvumi kuwa ndoa yao ipo matatani lakini tetesi hii inaweza kuwa kubwa zaidi kuwahi kusemwa.

Kuna tetesi kuwa Beyonce amekuwa akimsaliti mumewe na kutembea na bodyguard wake Julius De Boer.

Beyonce anadaiwa kuwa karibu mno na Julius De Boer, mzaliwa wa Uholanzi ambaye amekuwa akimlinda tangu mwaka 2009. Habari zimedai kuwa Jay Z ana wasiwasi pia na uhusiano wao.

“Jay kiukweli anahisi kuwa kunaweza kuwa na kitu cha kimahaba kinaendelea kati ya Bey na Julius,” chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Mstarz News. “He wanted to fire Julius last February, but BeyoncĂ© said, ‘Julius isn’t going anywhere. They’ve spent a lot of time together behind closed doors. He’s even stayed in her hotel room.”

Kumekuwepo na tetesi za wawili hao kupeana talaka japo wamekuwa wakiikwepa. Tukio la Jay Z na Solanga kugombana kwenye lifti hivi karibuni liliongozea nguvu tetesi hizo.
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua ukweli halisi wa skendo hii iliyozushwa hivi karibuni ya Beyonce kutembea na bodyguard wake, Julius De Boer

Tumbaku 'dhahabu' ya Malawi

Malawi na Zambia ndio nchi zinazozalisha kiwango kikubwa cha Tumbaku Afrika
Malawi ni miongoni mwa nchi zinazozalisha tumbaku kwa wingi duniani. Uchumi wa nchi hiyo iliyoko kusini mwa bara la Afrika unategemea kilimo cha zao hilo kwa asilimia 75.
Ikiwa leo ni siku ya kutovuta tumbaku duniani,kila unapopita mitaani kwenye miji mikubwa ya Lilongwe na Blantyre na hata maeneo ya vijijini hakuna tofauti.
Wavutaji wa tumbaku na hasa sigara hawana haja ya kujificha ama kujistiri ili kuwalinda wasiovuta wasidhurike na moshi wa tumbaku.
Malawi haijaathirika kwa lolote kwenye kilimo cha zao hili isipokuwa tu misukosuko ya kawaida
Malawi ni kati ya nchi zenye sheria ya kuzuia watu wasivute sigara hadharani na hata matangazo ya biashara ya sigara hayaruhusiwi, lakini kama ilivyo kwa baadhi ya nchi zingine, sheria hizo hazisimamiwi kabisa. 

'Mhimili wa uchumi wa nchi'
Tumbaku ndiyo dhahabu ya Malawi, wenyewe wanasema bila tumbaku hakuna maisha
Kijana mmoja amezungumza akasema yeye havuti sigara na anafahamu vizuri madhara ya kuvuta sigara, lakini wao kama nchi hawawezi kuacha kulima tumbaku kwani ndiyo msingi wa uchumi wa Malawi, na hawana bidhaa nyingine mbadala ya kufidia kilimo cha tumbaku itakapobidi kuacha kulima zao hilo.
Wamalawi walioko mashambani na hata mijini kwa umoja wao bila kujali wasomi ama mbumbumbu, wana kitetea kilimo cha tumbaku kwa nguvu zote.
Mkulima wa zao hilo Amon Ndewere ambaye anamiliki shamba la ekari 40 anasema kelele za ulimwengu kupiga vita kilimo cha tumbaku kwao hazina tija kabisa wanachoangalia ni jinsi gani wanunuzi na serikali watawaboreshea maisha yao bila kuwanyonya.
'Tumbaku inauzwa kwa mnada
Wauzaji wa Tumbaku mnadani
Wakulima wa tumbaku nchini Malawi hawaruhusiwi kuuza wenyewe tumbaku yao kwa namna yoyote, bali wanapaswa kujiunga pamoja kwenye vikundi vidogo vidogo na kuipeleka kwenye mnada maalum wa tumbaku unaosimamiwa na shirika la Umma Auction Holdings.
Huko wanakutana na wanunuzi ambao ni makampuni makubwa ya kimataifa kama Alliance One, Japan Tobacco, Malawi Leaf na mengine.
Afisa mtendaji Mkuu wa Tume ya udhibiti wa tumbaku nchini Malawi Bruce Muthali, Anasema kazi yao ni kusimamia sera ya zao hilo listawi kwa manufaa ya nchi na watu wake.
'Tumbaku ya kipekee duniani'
Tumbaku ndio dhahabu ya Malawi kama wanavyosema wenyewe
Malawi ni mzalishaji pekee duniani wa tumbaku inayoitwa kwa jina la kitaalam Burley, ambayo huchanganywa na tumbaku zingine ili kupata mchanganyiko bora wa sigara.
Na kwa hakika nchi hii haijaathirika kwa lolote kwenye kilimo cha zao hili isipokuwa tu misukosuko ya kawaida ya kupanda na kushuka kwa bei ya tumbaku kwenye soko la dunia.
Inaelezwa kuwa Malawi kuna wavutaji wengi wa sigara, lakini serikali ilifunga kiwanda chake cha kutengeneza sigara zaidi ya miaka 15 iliyopita,na sasa kuna kiwanda kidogo tu kimoja, sigara zote zinazopatikana nchini humo zinatoka nchi jirani na hasa Zambia na Msumbiji huku Tanzania na Afrika Kusini zikichangia ongezeko kidogo sana.
Nchini Malawi matangazo ya kibiashara ya Sigara hayaruhusiwi
Waswahili wanasema kimfaacho mtu chake! Malawi inategemea zaidi tumbaku kuliko bidhaa nyingine yoyote, swali kwa walimwengu ni jinsi gani itaachana na kilimo hiki.. kwa sababu tu wataalamu wanasema tumbaku ina madhara.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kusoma makala mbalimbali ambazo zinamantiki na kusadifu maisha halisi ya mwanadamu na changamoto mbalimbali katika maisha.

Mnyika aishukia Serikali utoroshaji fedha nje ya nchi

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeilipua Serikali kwa kushindwa kudhibiti utoroshwaji mkubwa wa fedha kwenda nje.

Msemaji wa kambi hiyo, John Mnyika alisema katika kipindi cha miaka 39 kuanzia 1970 hadi 2008, Sh9.6 trilioni zilitoroshwa kiharamu kwenda nje.

“Utoroshaji wa fedha hizi unasadikiwa kutokana na ukwepaji wa kodi, na misamaha mikubwa ya kodi,” alisema Mnyika na kuongeza; “Fedha nyingine zilitokana na usiri mkubwa wa mikataba baina ya wawekezaji na Serikali, upotoshaji wa bei katika biashara na rushwa katika mikataba na wawekezaji” alisema.

Mnyika alisema Serikali ya CCM haiwezi kukwepa kuwajibika kwa sababu utoroshaji wa mapesa yote haya umefanyika wakati na CCM ipo madarakani, ” alisema.

Mnyika alifafanua, utoroshaji huo wa fedha ulifanyika kwa mafungu na kutolea mfano mwaka 1980, Dola 570. 6 milioni zilitoroshwa.

Fedha hizo zilitoroshwa wakati hayati baba wa Taifa mwalimu Jullius Nyerere akiwa madarakani na dola 1,566 milioni zikatoroshwa 1985 wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

“Jambo la kusikitisha zaidi mwaka 2002 zilitoroshwa jumla ya Dola za Marekani 1,1010 milioni katika kipindi ambacho Rais Benjamin Mkapa yuko madarakani,” alisema Mnyika.

Mnyika alisema kambi hiyo imesikitishwa na kitendo cha Bunge kushindwa kuisimamia kikamilifu Serikali hususan Wizara ya Nishati na Madini.

Alisema fedha zote zilizotoroshwa nchini tangu mwaka 1970 mpaka 2008 zinaweza kurejeshwa nchini kwa kuanzia na kuzibaini zilipo.

“Uchunguzi wa kina ufanyike kuzuia fedha hizo katika akaunti za benki zilipotunzwa nje ya nchi na hatimaye kurejesha fedha hizo nchini,” alisema.

Kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU) cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kimetakiwa kukusanya taarifa za kiintelijensia na kuziwasilisha Takukuru ili uchunguzi ufanyike.
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinajiri kutokana na skendo hii iliyoikumba serikali ya utoroshaji wa fedha nje ya nchi.

Mchawi mtanzania jela miaka 3 Kenya

Vifaa walivyopatikana navyo washukiwa walipokamatwa na polisi
Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.
Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.
Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.
Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na Decemba 2012 baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe maradufu
Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwaendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa
Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika nyumba ya kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa mji mkuu Nairobi.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi kumnafiki kwa urahisi na kuwa hawana majuto au toba.

Irene Uwoya adhibitisha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Msami !!!!!

 

Jana May 28 kupitia You heard ya XXL Clouds FM ilikua ni stori kuhusu uhusiano wa Msami wa THT na mwigizaji toka Bongo Movie Irene Uwoya na jana alisikika Msami ambaye alikanusha uhusiano lakini mpenzi wake Rehema aliweka wazi kuwa ni kweli Msami ana uhusiano wa kimapenzi na Irene Uwoya.

Sasa May 29 2014 ishu hii imeendela ambapo katafutwa Irene Uwoya na kuulizwa na Soudy Brown kama ni kweli ana uhusiano wa kimapenzi na Msami na swali la kwanza lilitaka kujua uhusiano wao umekuepo toka lini?

Irene Uwoya: ‘Siku nyingi’
Soudy Brown: Msami kama namuona, unampa huduma zote?
Irene Uwoya: ‘Sanaaa kila kitu’
Soudy Brown: Uhusiano wenu utadumu au ndio kama wa Ndikumana?
Irene Uwoya: ‘Yakudumu kwa sababu nampenda’.
Soudy brown alimpa Irene taarifa kuwa mpenzi wa zamani wa Msami amekasirika kwa sababu Irene kaingilia mapenzi yao jibu kutoka kwa Irene likawa ‘hiyo haijalishi kwa sababu nampenda

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua skendo mbalimbali za mastaa

Google kufuta historia ya watu Ulaya

Google ina wasiwasi kuwa mataifa kandamizi yatafurahia sana amri ya mahakama Ulaya
Kampuni ya Google inatarajiwa kuzindua huduma ambayo, itawawezesha raia wa Ulaya kuomba viambatanishi vya mitandao yenye taarifa kuhusu maisha yao kufutwa
Google ambao hutumiwa kwa ukubwa duniani kutafuta taarifa imesema kamati ya wakurugenzi wakuu na wataalamu wa kujitegemea wataunda mpango wa muda mrefu kushughulikia maombi hayo ya watu kutoka Ulaya.
Hatua hiyo inajiri baada ya mahakama ya haki Ulaya kuamua kwamba viambatanishi vya data za zamani au zisizo muhimu za watu zinapaswa kufutwa iwapo watu wataomba hivyo.
Mkurugenzi mkuu wa Google, Larry Page amesema kampuni hiyo itafuata hukumu hiyo ya Ulaya lakini ameonya huenda ikaathiri ubunifu na ikafurahisha nchi zenye watawala wakandamizaji.

LA Clippers yapata mmiliki mpya

  Shelly Sterling  aliekuwa mke wa zamani wa Donald Sterling ameiuza L.A. Clippers kwa aliekuwa CEO wa Microsoft Steve Ballmer kwa dolla billion 2.

TMZ Sports imeripoti kuwa dili hiyo imesainiwa usiku kabla ya saa sita usiku wa alhamis.NBA lazima wathibitishe uuzwaji wa timu hiyo, lakini watoa habari wa karibu wamesema  kamishna wa NBA Adam Silver alikuwa najua kuhusu kuwepo kwa makubaliano kati ya Shelly na Ballmer na wengine waliokuwa na shauku ya kutaka kuinunua timu hiyo. 


Donald Sterling anasemekana kujaribu kuweka vikwazo lakini anaonekana kutaka kuleta changamoto katika uuzaji huo lakini anaonekana kufeli.

 Donald  alimpa Shelly jukumu lote juu ya timu hiyo, akimruhusu kuiuza timu hiyo, na hata akatuma barua kwa Silver akimtaarifu kuwa Shelly ana haki zote 
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali kutoka katika kila pande za dunua.Jukumu letu sisi ni kukuhabarisha

Matamshi kuhusu ubakaji yakera India


Matamshi ya mwanasiasa mmoja mwanamke nchini India kuhusu ubakaji yamelaaniwa na watu wengi kote nchini humo.
Asha Mirge, ambaye ni mwanachama wa kikundi cha viongozi wanawake serikalini katika jimbo la Maharastra, amesema kuwa wanawake pia wanachangia pakubwa kwa wao wenyewe kubakwa kutokana na mavazi pamoja na wanavyotembea na hata kuzungumza.
Amehoji kwa nini wanawake hutoka nje nyakati za usiku.
Matamshi haya yaliyozua gumzo katika vyombo vya habari kote nchini India, yamesababisha kero kubwa kutoka kwa makundi ya wanaharakati wa maswala ya wanawake na wanasiasa wengine.
Bi Mirge hata hivyo ameomba radhi kwa matamshi yake akisema yametiwa chumvi.
Inda imekuwa ikimbwa na visa vya mara kwa mara vya ubakaji kiasi cha serikali kubuni sharia kali dhidi ya wabakaji.
Ni wiki jana tu ambapo wazee wa kijiji waliamrisha kubakwa kwa mwanamke ambaye alikuwa na uhusianao wa kimapenzi na mwanamume ambaye sio wa kutoka jamii moja naye.

Morogoro yamuaga George Tayson

 
   Baada ya hapo Jana kupata ajali mbaya ya gari.Mtayarishaji na mwongozaji wa vipindi vya filamu na vya runinga George Tayson aliyepata ajali jana eneo la Gairo,mkoani Morogoro.
Na baadae mwili wake kuchukuliwa na kwenda kuhifadhiwa hospitali ya Morogoro.
Leo hii watu mbali mbali mkoani Morogoro walijitokeza kuuaga mwili wa marehemu na sasa ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu wako safarini  kuelea jijini Dar es salaam ambapo taratibu nyingine zitafuata.


Kufuatia msiba huu Monalisa aliandika hicho hapo juu katika akaunti yake ya Instagram
 

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kula kitakachokuwa kinajiri kuhusiana na msiba huu wa Mtayarishaji na muongizaji huyu wa filamu Mashuhuri hapa nchini.

Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3


Kampuni kubwa ya teknolojia Apple imethibitisha kwamba itanunua vipokea sauti na huduma ya kusikiliza muziki kupitia kwenye mtandao wa inteneti kutoka kampuni ya Beats Electronics katika makubaliano ya dola bilioni 3.
Hayo yakiwa ni makubaliano makubwa katika historia ya miaka 38 ya kampuni hiyo.
Hatua hiyo inaonekana kama jitihada ya kuiendeleza sifa ya Apple katika soko la kusikiliza muziki kwenye mtandao.
Pamoja na ununuzi huo, waanzilishi wa Beats Jimmy Lovine na msanii mtajika katika mtindo wa kufoka na Hip Hop Dkt. Dre watajiunga na kampuni hiyo ya kiteknolojia.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook alisema kuwa mkataba huo ungewezesha kampuni hiyo ‘kuendelea kutengeneza bidhaa na huduma za muziki zenye ubunifu duniani.’
Beats ilianzishwa na mzalishaji wa muziki Jimmy Lovine na nyota wa mziki wa kufokafoka, Dr. Dre, na mitambo hiyo imejulikana kuwa bora zaidi hadi siku za hivi majuzi.
Beats ilianzisha huduma ya muziki unaolipiwa mapema mwaka huu.
Apple ina huduma ya iTunes ambayo ndio kubwa zaidi duniani inayohusiana na mziki, na ilianzisha kituo cha radio cha iTunes mwaka uliopita.

Ijapokuwa kampuni hiyo ya Carlifornia ndio walikuwa waanzilishi wa zamani wa mziki wa mfumo wa dijitali, imekuwa ikikumbwa na ushindani mkubwa kutoka kwenye huduma zinazolipiwa kama vile Spotify, Pandora na Rdio.
Hata hivyo, huduma ya mziki ya Beats ina wateja wapatao 110,000 pekee waliojisajili ikilinganishwa na Spotify ilio na watu milioni 10 waliojisajiliwa.
Mkataba huo na kampuni ya Beats imeonyesha kudidimia kwa Apple ambayo hujulikana kwa kutengeneza bidhaa mpya wala sio kununua kampuni ndogo ndogo kama wanavyofanya wapinzani wao Google.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata stori mbalimbali kama hizi zinazojiri sehemu mbalimbali za dunia.Jukumu letu sisi ni kukuhabarisha.

Umeisikia hii kutoka kampuni ya kutengenreeza magari aina ya Ford

ford
Inawezekana ukawa mmiliki wa magari aina ya Ford ambay ni miongoni mwa kampuni kubwa za kutengeza magari nchini Marekani kwa sasa imeagiza magari milioni 1.4 yarejeshwe kutokana na hitilafu
Hitilafu iliyotajwa ni ya usukani ambapo takriban magari milioni 1.1 yaliyoundwa kwa mtindo wa kispoti yaliyokuwa yameuzwa Marekani Kaskazini yametakiwa kurejeshwa.

ford3
Magari mengine 200,000 yenye muundo wa Taurus yaliyoundwa kati ya mwaka wa 2010 na 2014 yanaweza kukutwa ana tatizo la kushika kutu kwa harakakwa matukio hayo yaliyofanywa hivi karibuni huenda yakaifanya kampuni hiyo kuvunja rekodi ya kutaka magari mengi zaidi yarejeshwe katika kipindi cha mwaka mmoja.
Kurejeshwa huko kwa magari hayo kumetokea wakati sakata ya usalama inawakumba wapinzani wakuu wa kampuni ya hiyo ambao ni General Motors (GM).
GM iliwahi kulaumiwa kwa kutotoa ilani za kiusalama kwamba baadhi ya magari yake hata baada ya kubaini kuwa magari hayo yanazima ghafla,dosari hiyo imehusishwa na vifo 13,ingawa wasanifu wa Marekani wanaamini kuwa idadi hiyo itaongezeka.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata stor mbalimbali zinazovutia kutoka pande zote za dunia

Uingereza yakemea hukumu ya kifo Sudan

Miriam Ibrahim na mumewe
Viongozi wa kisiasa nchini Uingereza akiwemo waziri mkuu nchini humo wamekemea hukumu ya kifo iliopewa mwanamke mmoja wa kikristo kwa kukataa kubadili dini yake.
Wameitaja hukumu hiyo kama ya kuudhi.
Mwanamke huyo Mariam Ibrahim anazuiliwa katika jela moja ambapo alijifungua mtoto wa kike juma hili.
Mwanawe wa kiume aliye na miezi 20 pia yuko naye katika jela hiyo.
Amekuhukumiwa kwa kuwacha dini yake baada ya kukataa kubadilika kuwa muislamu.
Bi Ibrahim ambaye ameolewa na mkristo pia amehukumiwa kuchapwa viboko 100 kwa kuzini kwa kuwa ndoa na mtu ambaye si muislamu si halali chini ya sheria za Sudan.

Endelea kuutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kitakchojiri kuhusiana na tukio hilo huko Sudan.

Meli yalipuka Bandarini huko Japan...

 Screen Shot 2014-05-30 at 11.57.11 AM 

Mlipuko mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini Japan katika Pwani ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha mtu mmoja kati ya wanane waliokuwa ndani ya meli hiyo kupotea huku wengine wanne wakijeruhiwa vibaya.
Moto mkubwa ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo yenye uzito wa tani 998 iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea ndani ya maji baada ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na majanga ya moto.
Screen Shot 2014-05-30 at 11.57.46 AM
Watu saba wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne wakiuguza majeraha ya moto kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo kapteni wa meli hiyo amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado unaendelea.
Screen Shot 2014-05-30 at 11.57.52 AM
Afisa usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti kuwa wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli wakati mlipuko unatoke.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kupata taarifa mbalimbali zinazojiri sehemu mbalimbali katika kila pande ya dunia.

Balloteli aidharau Uingereza kombe la dunia Brazil..


 Photo: #BRAZUKA Mario Balotelli amesema timu ya taifa ya England haina uwezo wa kuchukua kombe la dunia, alisema: "Siangalii England kama timu inayoweza kuchukua kombe la dunia. Wana wachezaji wazuri, lakini sioni kama wataweza kushindana na Italy. 
‘Sisemi kwamba Italy watachukua ubingwa, lakini tuna wachezaji uzoefu wa kiakili na wa uwanjani kuwashangaza watu - sidhani kama England wana kitu kama hicho.
‘Tuna wachezaji ambao wameshashinda ubingwa wa Dunia, sidhani kama England wana wachezaji wanaojua angalau nin namna gani inakuwa kucheza zaidi ya robo fainali."
 
Balloteli amesema timu ya taifa ya England haina uwezo wa kuchukua kombe la dunia, alisema: 
 
"Siangalii England kama timu inayoweza kuchukua kombe la dunia. Wana wachezaji wazuri, lakini sioni kama wataweza kushindana na Italy.
‘Sisemi kwamba Italy watachukua ubingwa, lakini tuna wachezaji uzoefu wa kiakili na wa uwanjani kuwashangaza watu - sidhani kama England wana kitu kama hicho.
‘Tuna wachezaji ambao wameshashinda ubingwa wa Dunia, sidhani kama England wana wachezaji wanaojua angalau nin namna gani inakuwa kucheza zaidi ya robo fainali."
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali za michezo....


Walichokiandika Vanessa Mdee,Ay,JokateM,HemedyPHD kuhusiana na kifo cha George Tyson

TYSON
Jana usiku habari zilizoshtua watu wengi ni kuhusu kifo cha director mashuhuri George Tyson. Hivi sasa kuna taarifa ambazo hazijawahi kutolewa na hawa wahusika kuhusu marehemu Tyson.

Zipo tano hadi sasa na zinatoka kwa watu mashuhuri kwenye kiwanda cha burudani.
J1

Jokate Mwegelo amesema kuhusu kazi nzuri aliyokuwa anafanya George Tyson kama director wa The One show ambayo inaruka kupitia TV1

J2
Venessa Mdee hajawai kusema sababu ya kuacha kufanya The One show ambayo alianza hadi ku-shoot. Hivi sasa amesema sababu hiyo akimhusisha George Tyson kama mtu aliyempa moyo kwenye maamuzi yake.

T1
Hemed PHD na yeye anasema kwamba George Tyson ndiye mtu ambaye aligundua kipaji chake cha kuigiza wakati akiwa kwenye Tusker Project Fame.

T3
Kazi kubwa ya George Tyson ilikuwa ni ku-direct vipindi vya TV kama unavyoona hapo chini na juu ambapo AY anamzungumzia baada ya kufanya show ya Boys Boys. Pia Mboni Masimba anamtaja kama director wa show yake.
Y2

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua walichokisema wasanii mbalimbali kuhusiana na kifo cha Director mashuhuri hapa nchini George Tayson.

Harusi ya Kim Kardashian na Kanye West yaweka rekodi ya dunia

kim
Hadi sasa vituo vingi vya burudani wanaitaja kuwa ni harusi ya mwaka kutokana na stori kubwa zilizotengenezwa na harusi ya hawa wawili.
Ukiachana na pesa zilizotumika na watu waliofika kwenye harusi hiyo, picha ya Kanye West na Kim K imekuwa picha  maarufu zaidi kwenye instagram hivi sasa.
Tangu mtandao huo uanzishwe hakuna picha iliyowai kupata likes nyingi kama hiyo hapo juu. Justin Bieber alipost picha akiwa na Selena Gomez na kupata likes milioni 1.8.ser
Lakini hadi hivi sasa picha ya Kimye imefikisha like like milion 2.01 na kuifanya kuwa picha maarufu kuliko zote duniani kwenye mtandao huo tangu uanze kufanya kazi.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com upate habari mbalimbali kutoka katika pande zote za dunia

Maombi ya kumuombea Falcao yaanza kujibiwa Colombia....


 Photo: #BRAZUKA Nchini Colombia maombi ya kumuombea Rademel Falcao yanaonyesha kupata majibu mazuri baada mshambuliaji huyo kuanza mazoezi na wachezaji wenzie wa kikosi cha timu ya taifa ya Colombia. David Beckham alivujika kwenye mechi ya Champions league kati ya Deportivo La Coruna vs Man United - ikiwa imebaki miezi michache kabla ya kombe la dunia, waingereza walikusanyika makanisani kumuombea mchezaji apone kwa ajili ya kombe la dunia. Majibu yalifanya kazi na David Beckham alipona na kuitumikia England iliyoishia robo fainali kwa kufungwa na Brazil.
    Nchini Colombia maombi ya kumuombea Rademel Falcao yanaonyesha kupata majibu mazuri baada mshambuliaji huyo kuanza mazoezi na wachezaji wenzie wa kikosi cha timu ya taifa ya Colombia.
      David Beckham alivujika kwenye mechi ya Champions league kati ya Deportivo La Coruna vs Man United - ikiwa imebaki miezi michache kabla ya kombe la dunia, waingereza walikusanyika makanisani kumuombea mchezaji apone kwa ajili ya kombe la dunia. 
      Majibu yalifanya kazi na David Beckham alipona na kuitumikia England iliyoishia robo fainali kwa kufungwa na Brazil.
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kila taarifa itakayohusiana na michiano ya Kombe la dunia huko Brazil


Apelekwa Mahakamani kwa kesi ya kubaka, alipofika Mahakamani akataka kumbaka mtu tena

Screen Shot 2014-05-31 at 2.22.49 AM 
Hii ni stori nyingine tena ya 2014 ambayo inaingia kwenye list ya zile stori ambazo ukishaisoma au kuipata unaanza kufikiria mara mbilimbili na kujaribu pia kutengeneza picha yako mwenyewe kama upo eneo la tukio.
Watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili kuangalia kama ndugu yao aitwae Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana kwenye kesi inayomkabili ya kubaka mtoto wa miaka tisa.
Imetokea Kenya ambapo jamaa alikua amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumaka Mwanamke aliekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.
Screen Shot 2014-05-31 at 2.41.44 AM

Mshukiwa huyu alikuwa kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April 2014 ambapo wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye eneo la wazi, alimpiga mtama kwanza Mwanamke huyo lakini kwenye purukushani zake hakufanikiwa manake Polisi walimuwahi.
Shughuli za Mahakama zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada ya hapo Mwanamke alietaka kubakwa alisema ‘nilikua nimeketi karibu naye na mara ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni mwizi lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma nikaanguka sakafuni
Baada ya hapo dada wa mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake akisema yuko katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu ya kesi ya ubakaji.
Tukio la Mwanza
Hili linakua tukio jingine mimi kulisikia mwaka 2014 la kituko Mahakamani baada ya mawili ya Mwanza ambapo moja ni Mahabusu kujipaka kinyesi na kujaribu kutoroka akidhani hiyo mbinu itasaidia mtu asimshike, mwingine ni alievua nguo zote kushinikiza atendewe haki kwa kisa cha mauji alichobambikiwa.
Kituko kingine ambacho kilivunja rekodi kabisa ni cha Wafanyakazi wawili wa Mahakama nchini Italia kufanya Hakimu kuahirisha kesi baada ya wawili hao kuonekana wakifanya mapenzi kwenye chumba cha pili pembeni ya chumba kilichokua kinaendeshewa kesi.
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata stori mbalimbali zinazojiri pande zote za dunia

China yakusanya hawa watu Uwanja wa Mpira na kuwahukumu kifo.

 china2 
Watu 55 nchini China wamekumiwa kutumikia adhabu mbalimbali kwa makosa ya ugaidi, uhalifu wa kutumia silaha pamoja na mauaji, hukumu iliyotolewa katika Jimbo la Kaskazini Magharibi la Xinjiang mbele ya umati mkubwa wa watu katika Uwanja wa mpira
Kwa mujibu wa ripoti za shirika la habari la nchi hiyo, Washtakiwa hao ambao walifikishwa mbele ya umati wa takribani watu elfu 7,000 walihukumiwa adhabu mbalimbali huku watatu kati yao wakihukumiwa adhabu ya kifo.

china1
Maafisa wa nchini China wamevishutumu vikundi vya kijeshi vya Uigher ambao ndio sehemu kubwa ya wahalifu hao kwa kusababisha kukua kwa idadi ya mashambulizi katika nchi hiyo.
china3
Picha kutoka katika uwanja huo zimeonyesha magari makubwa ya polisi yakiwa yameegeshwa karibu na kundi kubwa la wahalifu hao kuhakikisha ulinzi wa kutosha huku idadi kubwa ya watu wakishuhudia hukumu hiyo ikitolewa.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata habari mbalimbali kwa wakati muafaka.

Cristiano Ronaldo ajiunga na timu ya taifa,tazama jinsi alivyowasili

 Screen Shot 2014-05-30 at 12.09.53 PM

Ni juzi tu May 29 2014 Cristiano Ronaldo ametajwa kushika namba moja kwenye list ya mastaa kumi wa soka ambao wanavutia kibiashara na kufanya kazi na makampuni makubwa ya kibiashara duniani.
Hii post inahusu kuwasili kwa Ronaldo kwenye hoteli timu yake ya taifa ya Portugal ilikoweka makazi ya muda kujiandaa na kombe la dunia litakaloanza siku chache zijazo nchini Brazil.
Screen Shot 2014-05-30 at 12.46.45 PM 
Kulikua na mashabiki wengi waliokua wakimsubiria wakiwemo kina mama, baba na watoto ambao wengine walijaribu hata kumgusa, wengine kumsemesha na wengine kumpiga picha.
Screen Shot 2014-05-30 at 12.46.37 PM
Screen Shot 2014-05-30 at 12.02.32 PM
Screen Shot 2014-05-30 at 12.46.22 PM
Yaani huyu mtoto hakuamini kamshika Ronaldo…. hahahha hii picha ya huyu mtoto nimeipenda.

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com  kupata habari zote zitakazokuwa zinahusiana na Kombe la dunia.

Beyonce atupia picha akiwa analea mtoto nyumbani kwake

 
 Msanii maarufu wa Marekani BeyoncĂ© ame 'share' picha za familia yake kwenye tovuti yake kuonesha upande wake kama 'mama' kutokana na wengi kuzoea kumuona kama muimbaji akishambulia jukwaa.
Katika picha hizi anaonekana akimbembeleza mwanaye Blue Ivy alale. Picha nyingine mwanaye huyo anaonekana akijaribu kuvaa viatu vya mama yake. Nyingine inaonesha baba wa Blue Ivy (ambaye ni Jay Z kama hujashtukia) akipiga misele kwa pikipiki. Nyingine anaonesha style yake ya rasta na mapozi ya kimtindo.
Bila shaka anatuonesha kuwa licha ya kuwa bize na kufyatua album na 'singo' nyingi, za 'kutisha' bado ana muda wa kulea na kuwa kama 'mama wa kawaida'. Hii unaweza ku- share na masharo.

 
 
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata stori mbalimbali zinazowahusu wasanii mbalimbali.