Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Showing posts with label Fashion. Show all posts
Showing posts with label Fashion. Show all posts

Tuesday, 6 January 2015

BantuTzMAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO JANUARI 6 2015

.
BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika kurasa za mbele na nyuma magazeti yote ya leo
 .
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.Endelea kufurahia huduma za BantuTz.com huku ukiusubiria kwa hamu Mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi uitwao Bantuz hapo mwakani.

Monday, 15 December 2014

Alichokisema Happiness Watimanywa Baada Ya shindano la Miss World 2014.


Mwakilishi wa Miss World 2014 ametulita pamoja kama nchi kwenye kumpa ushirikiano katika kupiga kura ili ashinde peoples choice awards na kuingia kwenye top ten ya miss world. Ingawa hatukufanikiwa kumweka namba moja Happy ameonekana mtu mwenye kujiamini na kujituma sana. Hizi ni picha zake kwenye show ya Miss World na ujumbe wake baada ya show kuisha.


Kutoka Instagram yake Happy ameandika ” Nampongeza @rolenestrauss (South Africa) kwa kuibuka mshindi Miss World 2014.
Watanzania wenzangu na marafiki kutoka mataifa mengine, tumepiga kura sana, mmeonyesha support kubwa kuliko matarajio ya wengi bahati mbaya kura hazikutosha.
Natumia nafasi hii kuwashukuru wote mmoja mmoja kwa kuniunga mkono kwa kipindi chote ambacho nilikua hapa jijini #London na tokea niliposhinda mashindano ya #MissTanzania. Nisingefika hapa bila support yako. From deep inside my heart. I thank you.

Kuanzia aliyetumia muda na pesa yake kunipigia kura, aliyeandika na kutangaza habari yangu, designers mbalimbali, familia yangu, marafiki wote, wote, wote, I thank you.
Nimejifunza vitu vingi sana kipindi chote hiki na kwakweli watanzania tumeonyesha umoja wa hali ya juu sana. Umoja wetu na udumu katika mambo yote ya kimaendeleo kwa taifa letu.

Mbarikiwe
#Happiness4MissWorld ”

Hongera Happy kwa Ulipotufikisha.

Friday, 7 November 2014

HOT IN TOWN: PICHA JINSI KANGA, BATIKI, WAX NA KITENGE VINAVYONOGESHA MAVAZI

Saturday, 13 September 2014

Asilimia 52 ya wanawake Tanzania hutumia vipodozi vyenye sumu


Zaidi ya asilimia 52 ya wanawake
hutumia vipodozi vyenye sumu
ambavyo huwasababishia matatizo
mbalimbali ikiwamo kansa ya ngozi,
figo pamoja na kuharibika kwa mimba
kwa mama mjamzito. Aidha katika
utafiti uliofanywa na Asasi
isiyokuwa ya kiserikali Envirocare
mwaka jana inaonyesha mikoa ambayo
imeathirika zaidi na matumizi ya
vipondozi hivyo ambayo ni Tanga,
Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma,
Arusha, Mbeya na Kilimanjaro.
Meneja wa Mradi huo, Elfansia
Shayo, alisema Envirocare imeandaa
kampeni kwaajili ya kupinga
matumizi ya vibodozi hivyo
itakayofanyika leo jijini Dar es
Salaam. “Envirocare kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Chakula
na Dawa Tanzania (TFDA) imefanya
utafiti ulionyesha zaidi ya
asilimia 52 ya watumiaji wa
vipodozi hivyo ni wanawake na
baadhi yao wanajua madhara yake,”
alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo,
Loyce Lema, alisema kampeni hiyo
inahusu kutoa elimu kwa jamii
kuhusu matumizi ya vipodozi hivyo
na ambazo viambato hivi husababisha
madhara kwa watumiaji na mazingira.
Alisema pamoja na TFDA kuweka mfumo
thabiti wa udhibiti wa vipodozi
ambao unatumia njia mbalimbali
ikiwamo usajili wa vipodozi, utoaji
wa vibali vya biashara, na ukaguzi
wa maduka bado mfumo huo
unachangamoto kwani vipodozi
vimekuwa vikiingizwa nchini kwa
kutumia njia zisizo rasmi.

CHANZO: NIPASHE

Thursday, 4 September 2014

Mwanamke mwenye kiuno chembamba zaidi Duniani.





Cathie Jung ana miaka 77 na ndiye mwanamke mwenye kiuno chembamba zaidi Duniani. 
 Yumo miongoni mwa watu kwenye kitabu maarufu cha kumbukumbu za Guinness world Hakika hii inashangaza kimtindo

Saturday, 21 June 2014

Lupita azidi kung’ara, alipamba jarida la Vogue

Lupita Nyong'o kwa hapa alipofikia anapaswa kuwa mwalimu wa wasanii na waigizaji wa Afrika hususani Afrika Mashariki. ikiwa wasanii hao watajaliwa akili za kujifunza na ari ya kusaka mafanikio na heshima.
Lupita Nyong’o kwa hapa alipofikia anapaswa kuwa mwalimu wa wasanii na waigizaji wa Afrika hususani Afrika Mashariki, kiwa wasanii hao watajaliwa akili za kujifunza, ari ya kusaka mafanikio na heshima.
Kim Kardashian ndiyo nani? Inaonekana kama 2014 umekuwa mwaka wa Lupita Nyong’o!
Ni miezi kadhaa tu imepita tangu achukue tuzo ya Oscar kama mwigizaji wa kike msaidizi kwa kufanya vizuri kwenye filamu ya 12 Years a Slave, nyota huyo wa Hollywood ametokezea kwenye ukarasa wa mbele wa jarida la Vogue.
Akiwa amevalia gauni, nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, mzaliwa wa Kenya anaonekana kutokuchoka baada ya kutolewa Julai kwenye mitindo ya Biblia.
Akiwa kwenye mahojiano,Nyong’o alizungumzia kuhusu umaarufu na kudai kuwa hajihisi kuchanganyikiwa anapokuwa kwenye umma unaomzunguka.
“Inaonekana kama tasnia ya burudani imevamia katika maisha yangu”, alisema Lupita.
“Watu walioonekana kuwa mbali na mimi ghafla nawaona mbele yangu na kudai kunijua – kabla ya mimi kuwajua”.
“Hata kwenye ndoto zangu za kuwa muigizaji, ndoto yangu haikuwa umaarufu. Ndoto yangu ilikuwa ni kufanya nilichotaka kufanya”.
Wasanii wa kike Tanzania
Dada zetu akina Wema Sepetu, Kidoti, Aunty Ezekiel, Irene Uwoya, mnajitahidi sana lakini haitoshi, Lupita ni mtu wa kumfanya kioo na kumuangalia anachofanya, sio lazima uige kila kitu, msifanye mambo ya kutafutwa na magazeti ya udaku, mjitahidi hata tuwaone kwenye majarida makini ya Kenya tu, itakuwa heshima kwenu, japo kidogo.
Kumbuka hayo hayaletwi na skandali za kipuuzi, bali kazi, nidhamu, ubunifu, kujituma na nyavu kazi, jengeni mahusiano ya kudumu na wasanii wa kimataifa, sio ya kimapenzi bali ya ari ya kutaka kuvuka milima ya mafanikio, mjifunze wazungu husema ‘Think globally, act locally’
Kingine elimu, Lupita Nyong’o kasomea shahada ya uzamivu (master’s degree) ya uigizaji kwenye moja ya Chuo cha heshima Marekani na duniani cha Yale, hajacheza filamu nyingi kuwazidi nyinyi, hazifiki hata tano, tulizeni akili zenu mtathmini nyayo zake, mtajifunza mengi muhimu kutoka kwake kwa manufaa yenu. Ukiacha kujifunza, umeacha kuishi.

Saturday, 14 June 2014

Unamjua mwanaume mwenye uume mkubwa zaidi duniani.? Mfuatilie hapa


Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 41 sasa katika mahojiano yake na The Huffington alisema kwamba huwa anapata shida sana masecurity anapokua kwenye airport anapotaka kusafiri kwani humsumbua sana.
 

Anasema “ilikua imelala tu wakati wa kukaguliwa na huwa inaurefu wan chi 9 ila ikisimama inakua na urefu wa inchi 13.5, Security mmoja aliniuliza kama sijaweka kitu mfukoni nikamwambia hapana na ndipo waliponilazimisha nitoe nilichokificha ndani ya chupi”

Falcon anasema alijitambua anakitu special mungu alomjalia pale alipofikisha miaka 18 baada ya ndude yake kufikia urefu wa inchi 12

Baada ya kstopishwa kwa muda mrefu anasema” Nilijaribu kuwaelewesha na ndipo walipogoma na kunipeleka chumba maalum ambapo niliwavulia na kuwaonesha wote walishika midomo na kuniomba samahani kwa usumbufu

Kiukweli Napata shida wakat mwingine sababu yanakuja makampuni mbalimbali yakiniomba nikacheze porn but the thing is I’m nat intesting, na pia wacheza porn wengi huwa wanadanganya saizi halisi ya maungo yao so endapo ntajiingiza watu hawatanichukulia siriazi

Pia Napata usumbufu kwa wanawake mbalimbali wanaonitaka kimapenzi ila nina mke nampenda na tunaheshimiana. Ebu pata kumcheki jamaa mwenyewe nan dude yake ikiwa imell ndan ya pant

Hivi sasa tunahamia katika site yetu mpya inayoitwa www.bantutz.com ni katika kuboresha huduma zetu za kutoa habari za uhakika na burudani.

Saturday, 24 May 2014

Bunge la Somalia lashambuliwa


Wabunge wawili wameuawa chini ya mwezi mmoja
Milipuko na risasi zimesikika katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu huku majengo ya bunge la Somalia yakishambuliwa, wabunge wakiwa ndani kwa mkutano.
Haijajulikana waliofanya mashambulizi hayo ambayo bado yanaendelea.
Bunge la kwanza rasmi la Somalia lilianza kufanya kazi miaka miwili iliyopita tangu Somalia kutumbukia katika vita mwaka 1992.
Serikali ya Somalia imekuwa ikiendesha vita dhidi ya kundi la kiisilamu la al-Shabab ambalo lilitimuliwa kutoka mjini Mogadishu mwaka 2011.
Bunge hilo, ambalo huendesha vikao vyake mjini Mogadishu limewahi kushambuliwa ikiwemo mwaka 2009 na 2010.
Mwezi jana Mbunge mmoja aliuawa kwa kulipuliwa huku mwingine akipigwa risasi na kuuawa katika mashambulizi mawili tofauti.
Wanajeshi 22,000 walio chini ya muungano wa Afrika wanasaidia vikosi vya Somalia kupambana na Al Shabaab.
Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti mkubwa wa miji kadhaa nchini Somalia, bado linadhibiti maeneo mengi ya vijijini.

Friday, 9 May 2014

Je ! Unamjua mrembo wa Kiafrika anaefananishwa na Rihanna ?

Screen Shot 2014-05-08 at 3.04.24 AM 

Huyu msichana aliwahi kutokea kwenye video ya mmoja kati ya wakali wa Nigeria aitwae Orezi ambae aliimba wimbo unaitwa Rihanna ambapo video ilifanyika Afrika Kusini na unaweza kuitazama chini mwisho kwenye hii post.
Unavyoona…. kafanana na Rihanna kwa asilimia ngapi?

Screen Shot 2014-05-08 at 3.04.10 AM
Screen Shot 2014-05-08 at 3.05.40 AM
Screen Shot 2014-05-08 at 3.06.21 AM
Screen Shot 2014-05-08 at 3.06.45 AM
Screen Shot 2014-05-08 at 3.02.44 AM
Screen Shot 2014-05-08 at 3.02.13 AM
Screen Shot 2014-05-08 at 3.02.02 AM
Screen Shot 2014-05-08 at 3.01.48 AM
Screen Shot 2014-05-08 at 3.01.27 AM