Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Saturday 26 September 2015

PROF KITILA MKUMBO:TADIP(TAASISI ILIYITOA UTAFITI JANA) NI N.G.O YA CHADEMA

Imebainika kuwa Zitto Kabwe alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Development Initiative (TADIP) kabla hajaondoka chadema.

Kwa mujibu wa Prof. Kitila Mkumbo, "...TADIP is chadema's NGO. Zitto was once a Director"

Zitto wa CHADEMA amefanya kazi hiyo ndani ya taasisi hiyo, malengo yake yakiwa ni kutoa mtazamo chanya wa matokeo wakati wa uchaguzi au pia jambo lolote linalohusu chadema.

TADIP pia imekuwa inafadhiriwa na taasisi moja ya ujerumani, ambayo pia imekuwa inaifadhili CHADEMA.

Prof Mkumbo pia aliwahi kuwa mwanachama wa CHADEMA. Taasisi hiyo Jana imetokea matokeo ya maoni ya wananchi kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu. Matokeo yake yaliyotiliwa shaka, yalikuwa tofauti sana na taasisi zingine zote zilizofanya tafiti kama hizo.

Thursday 24 September 2015

MAFAO(PENSHENI) YA BASTIAN SCHWEISTEIGER YANAPO FANYA KAZI SAHIHI MANCHESTER UNITED.

Msemo mmoja kutoka kwenye maandiko matakatifu au wakati mwingine hata mitaani unasema kila mwanaume atakula kwa jasho lake. Ndio,ni kweli kila mbuzi atakula kutokana na urefu wa kamba yake na kila mtu anavuna kile alichokipanda. Mara nyingi tunashuhudia wazee wastaafu wa mashirika fulani ya Serikali au binafsi wakipokea mafao yao ya kazi waliyofanya kipindi cha nyuma.

Bastian Schweisteiger sasa ana miaka 31 ni miaka ambayo ni mara chache sana kumuona mtu wa miaka ya kariba hiyo kutoka ligi moja ngumu na kwenda ligi nyingine ambayo ina ugumu zaidi. Bastian ametoka ligi kuu ya Ujerumani akiwa ameshinda kila kitu ambacho kila mchezaji anapenda kushinda. Miaka 17 aliyokaa Bayern Munich alivuna kila taji na katika timu ya taifa ni mshindi wa kombe la dunia. Maisha yanataka nini zaidi ya hapo tena!!? Hakuna ila kwa Schweisteiger anaona bado nguvu ya kupambana na hamu ya kuendelea kuwa mshindi bado anayo.

Ametoka Ujerumani na kwenda moja kwa moja Uingereza ambako ligi yake ni ngumu na ina ushindani kila wiki. Kwa umri alionao wengi walidhani atashindwa kuendana na kasi ya ligi hiyo lakini babu huyo amekomaa na kuwafunga midomo waliyombeza. Ligi bado haijachanganya sana lakini Bastian ameonekana kuimudu vyema. Uwepo wa Schweisteiger kwenye kikosi cha Manchester United ni taswira tosha kuwa United hawafaidiki na uwepo wake ndani ya uwanja tu bali hata nje ya uwanja.

MWALIMU NA KIONGOZI

Kuna wachezaji wengi vijana wanapenda kuwa kama Schweisteiger na wanajifunza kupitia yeye. Bastian amekuwa mwalimu na kiongozi awapo ndani ya uwanja,kwa uzoefu wake anatoa mchango kwa wachezaji wengine ndani ya timu hasa kwa chipukizi. Amekuwa muhamasishaji na mpambanaji muda wote. Ni mchezaji anayejua mbinu mbalimbali za ushindi kwa timu yake,na pia ni mchezaji ambaye hana makuu ndani au nje ya uwanja. Mchango wake kwenye timu ni zaidi ya kupiga pasi sahihi nyingi au kuhangaika ndani ya uwanja,mchango wa Bastian kwenye timu unatokea pale timu inaposhindwa kujua cha kufanya na yeye hutoa ushauri na kurekebisha makosa machache kabla ya kocha hajafanya hivyo.

Bastian ni darasa tosha kwa wengine. Bastian ni silaha tosha ya kuumizia wengine ndani na nje ya uwanja. Upambanaji wake unatoa fursa ya wachezaji wengine kupambana ni kitu ambacho akiwezekani kumuona mtu mzima anapambana kwaajili ya timu halafu chipukizi ashindwe kufanya hivyo.

Schweisteiger alistahili kwenda timu ambayo haina presha ili afaidi matunda yake aliyovuna akiwa Bayern Munich sababu kwa umri wake ili kuwa vyema angeenda kuvuna mamilioni ya pesa Marekani au mashariki ya mbali. Kiu yake ya kuendelea kupambana na kushinda ndiyo iliyompeleka Manchester United,tumeshuhudia baadhi ya wachezaji wakishindwa kuendana na kasi ya Uingereza mfano Di Maria, Falcao,Kagawa na wengine wengi hao wote kiumri ni chini ya Bastian Schweisteiger lakini walikata tamaa mapema na hawakuwa na kiu ya kupambana ili kupata mafanikio kwenye timu waliyopo.

Mafao ya pensheni anayopata United alitakiwa ayapate Bayern Munich sababu pale ndipo alipofanya kazi kwa miaka mingi lakini mafao hayo yanaleta faida zaidi kwa United ambayo inahitaji muda zaidi ili irudi kwenye fomu kama zamani.

Akamatwa kwa kuhifadhi sehemu za siri

Maafisa wa polisi nchini Afrika Kusini wameomba kupewahabari zaidi baada ya kumkamata raia mmoja wa Denmark kwa madai ya kuhifadhi sehemu za siri za wanawake 21 katika jokovu.

Peter Fredekrisen,ambaye anamiliki maduka mawili ya bunduki mjini Bloemfontein anakabiliwa na mashtaka ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia ,vitisho na unyanyasaji wa majumbani.

Raia huyo wa miaka 58 anadaiwa kuwapatia dawa za kulala waathiriwa kabla ya kuwafanyia upasuaji.
Bwana Fredekrisen hakutakiwa kujibu mashtaka wakati wa kusikizwa kwa kesi yake siku ya jumatatu.

Brigedia Hangwani Mulaudzi kutoka katika kitengo cha upelelezi nchini Afrika Kusini amekwamba mshukiwa huyo atasalia mahakamani hadi atakaporuhusiwa kuomba dhamana. Jumatatu ijayo.

Polisi wanaamini kwamba wateja wake walikuwa wakitoka katika eneo jirani la Lesotho.

Bwana Fredekrisen alikamatwa wiki iliopita kufuatia habari.
Sehemu hizo za siri zilipatikana katika jokovu ,zikiwa na majina ya wanawake waliotolewa na kule wanawake hao walikotoka.
Dawa za kulevya na vifaa vya upasuaji vya madaktari pia vilipatikana katika nyumba yake,polisi wanasema.

AKAMATWA NA VIUNGO VYA BINADAMU SINGIDA

Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mkazi mmoja wa mkoa wa wilaya ya Igunga, Tabora kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu na nyara za serikali vikiwemo vipande viwili vya fuvu la binadamu, ngozi ya chatu, vipande vya ngozi ya simba na chupa tatu za mafuta ya samba.

Ney Wa Mitego:Wasanii kukashifu viongozi itakuja kutu-Cost.

Zikiwa zimebakia siku 31 kuelekea uchaguzi mkuu, msanii Nay wa Mitego amendika hivii;

"Wasanii tubaki kua wahamasishaji tu!Kuanza kukashfu Viongozi utadhani labda nawewe umekua mwana Siasa au Mgombea itakuja kutu Cost baadae. Hua najiuliza cjui wanalipwa shiling ngapi maana wanasahau wao ni wasanii na wana Mashabiki wenye Imani tofauti, pia kuna Maisha baada ya uchaguzi. Endeleeni kutumika vibaya kwa Njaa ya leo na kwa maslahi ya wachache na kusahau kuna kesho. Pigania unacho amini but si kwa kashfa wala Matusi. Mimi naamini
# Mabadiliko2015 .Tukutane # October25 " ...Ameandika hivyo Nay wa Mitego

Barcelona yapokea kichapo La-Liga.

Barcelona walipokezwa kichapo chao kikubwa zaidi La Liga wakiwa chini ya Luis Enrique baada ya kulazwa 4-1 na Celta Vigo Jumatano.
Kushindwa huko kulifikisha kikomo mapema rekodi yao ya kushinda mechi zao zote msimu huu.
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas alifunga mawili baada ya Nolito kuanza ufungaji mabao dhidi ya klabu hiyo yake ya zamani.
Neymar alikomboa moja upande wa Barca zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kuisha, kabla ya nyota wa zamani wa Manchester City na Stoke John Guidetti kufungia wenyeji bao la nne.
Barcelona walikuwa wamepoteza mechi moja pekee kati ya 25 walizocheza majuzi zaidi La Liga.
Ushindi wa Celta uliwaweka kileleni mwa ligi kwa muda, lakini Real Madrid waliwabandua baadaye baada ya kulaza Athletic Bilbao.
Mkufunzi mkuu wa Barca Luis Enrique, alisema: "Kilichoamua mechi hii ni jinsi Celta walivyocheza. Walicheza vyema sana.
“Tulijaribu kuwatatiza lakini walituzidi ujanja. Timu inapokuwa bora kukushinda, huwa huna mengi ya kusema.
"Heri nishindwe na timu inayocheza kama Celta walivyocheza leo, bila kutumia hila, kushinda kwa kucheza vyema soka. Nawapongeza na natumai waendelee kucheza vivyo hivyo.”
Hiyo ilikuwa mara ya tatu kwa Barca kufungwa magoli manne katika mechi tisa walizocheza msimu huu.
Walilazwa 4-0 na Athletic Bilbao katika Super Cup ya Uhispania na pia walicharaza Sevilla 5-4 katika Super Cup ya Uefa.

TFF YAPIGA MARUFUKU ITIKADI ZA KISIASA KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA

Shirikisho la soka nchini Tanzania limepiga marufuku kuvaa jezi ama mavazi yenye itikadi ya vyama vya siasa kwa mashabiki wanaotarajia kuona mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara baina ya Simba na Yanga Jumamosi Septemba 26 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini hii leo Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Baraka Kizuguto amesema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha amani inakuwepo kwenye mchezo huo, ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu hizo zenye upinzani wa jadi Tanzania.

Wakati huo huo viingilio vya mchezo huo vimetangazwa leo ambapo kiingilio cha chini kitakuwa ni shilingi elfu saba (7,000).
Katika mchezo huo kiingilio cha juu kitakuwa ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000) kwa viti vya VIP B & C.

Magari yalioibwa Uingereza yapatikana Uganda

Wapelelezi waliokuwa wakilitafuta gari moja aina la Lexus lililoibwa mjini London nchini Uingereza wamelipata nchini Uganda.
Gari hilo lilikuwa na kifaa kinachoonyesha liliko.
Walipolipata nchini Uganda ,lilikuwa miongoni mwa magari 28 ya kifahari kutoka Uingereza yenye thamani ya zaidi ya pauni milioni moja,kulingana na gazeti la Metro nchini Uingereza.
Inadaiwa kuwa wezi hao walibadilisha mfumo wa kutumia funguo ya kuyawasha magari hayo.

Viongozi wa Upinzani wavalia sare za wanafunzi Kenya

Baadhi ya viongozi wa upinzani nchini Kenya wamevalia mavazi yanayofanana na sare za wanafunzi wakiitaka serikali kulipa walimu nyongeza ya mishahara.

Walimu wamekuwa mgomoni tangu kufunguliwa kwa muhula wa tatu na Serikali ilifunga shule zote za umma Jumatatu.
Mrengo wa Coalition for Reforms and Democracy (Cord) unaoongozwa na Raila Odinga leo umeandaa mkutano wa kisiasa uwanja wa Uhuru Park, Nairobi kuishinikiza serikali iwalipe walimu nyongeza ya asilimia 50 hadi 60 kama ilivyoagizwa na mahakama.

"Kuna pesa za kutosha, lakini zinapotea kwa ufisadi. Uhuru (Rais Kenyatta) anafaa kushauriana na walimu. Asiseme hawezi kulipa na hatalipa," alisema Bw Odinga.
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka alisema "pesa zipo" za kuwalipa walimu.

Mgomo huo wa walimu unatishia kutatiza mitihani ya kitaifa ambayo inatarajiwa kuanza wiki chache zijazo.
Kwa mujibu wa Baraza la Kitaifa la Mitihani Kenya (KNEC) kuna watahiniwa 937,467 wanaojiandaa kufanya mtihani wa darasa la nane KCPE utakaoanza Novemba 10 na kumalizika Novemba 12.
Watahiniwa wanaojiandaa kufanya mtihani wa kidato cha nne KCSE utakaoanza rasmi Oktoba 12 ni 525,802.

Baraza hilo limesema mitihani hiyo haitaahirishwa.

NINACHOAMINI MAESTRO:MATARAJIO NA UHALISIA WA SEPTEMBER 26. SIMNA SC vs YANGA.

Na: Ayoub Hinjo(Ayo's Mata Maestro)  September 26 ni siku ambayo kila shabiki na mpenzi wa mpira hapa nchi ameiweka kwenye kichwa chake. Ni siku ambayo imejaa matarajio kuliko uhalisia wa tukio lenyewe. Ni siku ambayo Tanzania itasimama kwa dakika 90 kushuhudia nyasi za taifa zikiwaka moto. 

Matarajio ya wengi ni makubwa sana kuelekea kwenye mchezo huo. Kila upande unaamini wana timu bora kuliko upande mwingine. Kila upande unaamini kubeba ubingwa bila kumfunga mtani wako hakuna raha ya ubingwa huo. Miaka ya hivi karibuni matarajio yamekuwa yanateka hisia za wengi kuliko uhalisia wenyewe wa mchezo ambao umewekewa matarajio. Matarajio ya wengi ni kuona pambano lenye burudani,ufundi na raha lakini uhalisia unameza matarajio hayo wanayotarajia.  

Uhalisia wake ndio unatunyamazisha na kutukumbusha mpira ni dakika 90 na mpira ni mchezo ambao hauchezwi chumbani. Uhalisia wake ndio unatuonyesha mchezo ni wa kawaida sana ambao hauna ufundi wala burudani iliyotarajiwa.

Uhalisia wake unatuonyesha mchezo ni wakukamiana na butuabutua zisizokuwa na msingi. Maandalizi yanayofanywa kuelekea mchezo huo hayafanani kabisa na uhalisia unaokuja kuonekana uwanjani.  

Matarajio yetu sidhani kama yanaweza kuzidi uhalisia wake. Kama matarajio yatafanikiwa kutimia basi wote tuna haki ya kujaza viti 60000 ambavyo vipo uwanja wa taifa. Picha za mchezo huo tayari zimeshajengwa kwenye vichwa vya watu wengi,lakini picha hizo zitakuja kufutwa kwenye vichwa hivyo kutokana na uhalisia ambao utatokea uwanjani.  

Sitaki kumaliza yote,nahifadhi maneno yangu ili mwishowe nijue ni kipi kitakuwa kimefanikiwa kutimia siku hiyo kati ya matarajio au uhalisia wa Kariakoo derby. Hadi sasa matarajio ni mengi kuliko uhalisia halisi wa mchezo huo. September 26 kila kitu kitajulikana kama ni Matarajio yetu ni sahihi au siyo sahihi.

Man United yaibuka na Ushindi mnono kombe la Ligi.

Manchester United imepata ushindi wa mteremko wa mabao 3-0 pale ilipomenyana na Ipswich Town katika mchezo wa kombe la ligi.
Mabao ya Rooney,Andreas Pereira na Anton Martial yalitosha kuwapa ushindi huo Man U. Katika michezo mingine Arsenal waliichabanga Totenham 2-1, Liverpool wakipata ushindi wa matuta wa 3-2 dhidi ya Carlisle.
Wakati huohuo ligi kuu ya soka ya nchini Hispania,La Liga iliendelea hapo jana ambapo Real madrid waliondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Athletic Bilbao huku Barcelona wakichabangwa mabao 4-1 kutoka kwa Celta Vigo.

Bei za viingilio Simba vs Yanga.

Viingilio vya mchezo wa watani wa jadi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania utakaochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam vimetangazwa leo ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu saba (7,000).

Katika mchezo huo kiingilio cha juu kitakua ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa viti vya VIP A, Elfu Ishirini (20,000) kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha shilingi Elfu Saba (7,000) kikiwa ni kwa viti vyenye rangi ya Blu, Kijani na Orange.

Tiketi za mchezo ho zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vifuatavyo: Karume – Ofisi za TFF, Buguruni – Oilcom, Dar Live – Mbagala, Uwanja wa Taifa, Luther House – Posta, Ferry – Kivukoni, Mnazi Mmoja, Ubungo – Oilcom na Makumbusho – Standi ya mabasi ya daladala.

TFF inawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchin kununua tiketi katika magari yaliyopo kwenye vituo vya kuuzia tiketi ili kuondokana na kuuziwa tiketi zisizo sahihi.

Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi wa kimataifa mwenye beji ya FIFA, Israel Nkongo (Dsm) akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Ferdinand Chacha (Mwanza) mwamuzi wa akiba Soud Lila (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo atakua Charles Mchau kutoka Kilimanjaro.
@Martin Mwambugi

Wednesday 23 September 2015

Papa awasili Marekani apokewa na Obama

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Marekani katika siku ya kwanza ya ziara ya kihistoria nchini humo ambapo amelakiwa na Rais wa nchi hiyo Barack Obama.
Papa Francis aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Andrew Air Force Base kutoka nchini Cuba.
Huku Marekani ikiwa na zaidi ya waumini wa Katoliki wapatao milioni sabini ziara hiyo ya papa inaoneka kuwa tukio kubwa nchini humo.
Kiongozi huyo wa kidini ambaye anaitembelea Marekani kwa mara ya kwanza atafanya ziara na kuongoza ibada katika miji ya Washington, New York na Philadelphia.
Wakati Papa Francis akiondoka nchini Cuba Papa Francis aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye sio muumini wa mlengo wa kushoto kama wengi wanavyodhani.
Papa alisema hatazungumzia suala la vikwazo vya biashara kati ya Cuba na Marekani, licha ya kuchukua nafasi muhimu katika mazungumzo ambayo yamesababisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kurejeshwa mapema mwaka huu.

Tuesday 22 September 2015

Wanasayansi watengeneza figo maabara.

Je una matatizo ya figo ?
Ikiwa jibu lako ni ndiyo kuwa na subira, maanake hivi karibuni figo zilizoundwa kwenye viwanda na maabara vitakuwepo kuwasaidia.
Nafahamu kuwa waganga wengi wamewaahidi tiba lakini hii sio hekaya tu za abuanuasi la.
Ni ukweli mtupu .
Wanasayansi wanakaribia kuunda figo zitakazo pandikizwa kwenye miili ya wagonjwa na watu wenye matatizo ya figo.
Kauli hii imetangazwa baada ya wanasayansi kuandikisha ufanisi mkubwa katika majaribio ya figo hizo kwa wanyama
 
Figo hizo bandia zilifanya kazi vyema katika nguruwe na panya.
Madaktari hao watafiti wanasema kuwa wanyama hao waliopandikizwa figo hizo walitekeleza majukumu yao ya kawaida ya kibayolojia kama vile kupitisha mkojo kama wanyama wowote wale.
Hilo ndilo lililokuwa kikwazo kikubwa katika majaribio ya awali.
Watafiti hao kutoka Japan waliepuka matatizo ya awali yaliyolemaza majaribio kama haya kwa kukuza vimelea ndani ya figo hizo ilikuzuwezesha vifo hizo bandia kuchunga mkojo na kupitisha pasi na kulowa.
Japo majaribio kwa binadamu hayajaidhinishwa,bila shaka matokeo haya mapya yanatoa muamko mpya katika jitihada za kuunda viungo muhimu vya mwili katika maabara ilikusaidia wagonjwa .


Hata hivyo Viungo vya mwili vinavyoundwa kutokana na sehemu za seli shina za mwanadamu vinategemewa kusuluhisha uhaba wa viungo halisi vya kupandikiza kwa wagonjwa.
Daktari Takashi Yokoo na wenzake katika chuo kikuu cha utabibu cha Jikei kilichoko Tokyo walitumia mbinu hiyo kukuza figo hiyo bandia.
Aidha kikosi hicho kilifurahishwa na matokeo ya figo hiyo bandia zaidi ya wiki 8 baadaye walipowapima panya hao na hata wakajaribu mbinu hiyo ya kipekee kwa mnyama mkubwa zaidi yaani nguruwe ambayo matokeo yake pia yalikuwa sawa na yale ya kwanza.
Profesa Chris Mason, ambaye ni mtaalamu wa maswala ya seli shina na muhadhiri katika chuo kikuu cha London, amefurahishwa sana na matokeoa haya.
''Hili ni tukio la kutia moyo sana.''
''Hata hivyo hili halimaanishi kuwa mbinu hii ya kukuza viungo itafaulu kwa binadamu.'
''Aidha kukuzwa kwa figo kunasaidia kubaini jinsi mwili unavyoondoa uchafu mwilini na ukiangalia wagonjwa wanaolazimika
'kutumia mashini ilikusafisha damu ''dialysis''mbinu hii bila shaka inatoa matumaini makubwa mno''. alisema Profesa Mason.
Watafiti wengine tayari wanafikiria kuhusu mbinu ya kukuza figo,moyo na hata mapafu.
Professa Harald Ott na wenzake wameanza kujaribu mbinu mbadala inayokuza seli shina kutoka kwa viungo vya wazee na kukuza viungo changa.

John Terry kurejea kikosini katika kombe la Capital One.

Kapteni wa Chelsea, John Terry alikosa michezo miwili ya mabingwa watetezi wa Premier League kwa kuwekwa benchi na kocha wake Jose Mourinho.
Lakini habari njema kuwa anaweza kuanza kucheza Jumatano katika kombe la Capital One.

Unaonaje maamuzi ya Mourinho kumuweka benchi yana faida ama hasara kwa timu ya Chelsea? Acha maoni yakohapa chini.

Hector Bellerin kusalia Arsenal licha ya kuwindwa na Barcelona,

Mchezaji Hector Bellerin amebainisha kiu yake ya kuendelea kubaki Arsenal kwa muda mrefu.
Beki huyo alijiunga na Gunners akitoka timu ya vijana ya Barcelona La Masia mwaka 2011, na amefuta dhana ya kumfuata mchezaji mwenzake aliyepita Arsenal , Cesc Fabregas aliyerudi Nou Camp kwa muda mchache kabla ya kurudi Premier League na Chelsea.

Simba vs Yanga Sc kupigwa Jumamosi Uwanja wa taifa.

Mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga Sc na Simba kuchezwa Jumamosi,Septemba 26, uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Nani kuibuka mshindi kati ya miamba hii ya soka,Acha maoni yako hapa chini.

Ferguson afunguka kuhusiana na mambo yaliyokuwa nyuma ya pazia katika utawala wake Man United.


1.Fergie anakiri kuwa kabla hata Man City hawajamnyemelea Aguero,Atletico waliiambia Man United itoe £35m kumpata Aguero lakin Fergie aliona nyingi na baadae akaenda Man City kwa £38m coz walikuwa desperate.

2.Fergie anasema kwa mara ya kwanza waliambiwa na scouts kuna wonderkid aitwae Muller huko Ujerumani na ana miaka 10,walitaka kumsajili ila muller aliamua kubaki katika kituo cha kukulia vipaji cha Bayern Munich.

3.David Moyes alikuwa chaguo la 6 la Ferguson katika kuichukua Man United.Chaguo la kwanza lilikuwa ni Pep Guardiola baada ya kukutanaa naye Marekani wakati wa likizo.Mourinho alikuwa chaguo la pili ila alishamuahidi Abramovic kwamba angerejea,Klopp alikuwa chaguo la tatu ila alitaka kusaini mkataba mpya Dortmund.Ancelloti na Van Gaal walikuwa chaguo la nne na la tano lakini walikuwa na timu tayari huku Ancelloti akiwa mrithi wa Mourinho.Na hapo ndipo Fergie na bodi ya Man United wakaamua kumchukua Moyes.

4.Fergie anasema dunia kwa sasa ina "world class players" wawili tu nao ni Messi na Ronaldo.na anasema amewahi fundisha 'world class player' wanne tu nao ni Scholes,Giggs,Ronaldo na Cantona.

Sir Alex Ferguson
"kwa muda wangu wote wa miaka 26 klabuni Old Trafford nimesajili wachezaji wa kiwango cha juu, daraja la kwanza wanne tu ambao ni Eric Cantona, Ryan Giggs, Cristiano Ronaldo na Paul Scholes" 
5.Fergie anasema alipinga upandishwaji mkubwa wa mshahara wa Rooney 2010 ambapo Rooney alisaini miaka 5 na alikuwa akilipwa £180,000 ambapo ni mara mbili ya alichokuwa akilipwa Fergie.Ndipo Fergie akakutana na Joel Glazer na kumwambia haiwezekani na wakakubaliana hakuna mchezaji atakayelipwa zaidi Ya SAF na ndipo SAF alipoongezewa mshahara.
 Sir Alex Ferguson!"Sijakubali mchezaji yeyote klabuni kwangu anizidi mshahara"
 
6.Mnamo mwaka 2010 Fergie alitaka kumsajili Balotelli ila washauri Fergie ndani ya Italia walimshauri Fergie kuwa ni risky sana kumsajili Balotelli kutokana na matendo yake.

7.Fergie anasema Mino Raiola ndo alikuwa chanzo cha Pogba kuondoka man united coz walikuwa hawapatani na alijali pesa kuliko kipaji cha Pogba.

8.Fergie anasema kosa kubwa la Moyes ilikuwa kuwafukuza staff nzima aliyoiacha na anampongeza Van Gaal kwa kumuweka giggs pale kwasababu anaijua vzuri club

9.Fergie anakiri kuwa huwa anaangalia Press conference za Van Gaal kwasababu zinashangamsha na kufurahisha.

10.Fergie Anasema walikuwa karibu kumsajili Varane kabla Zidane hajaingilia kati na kumshauri aende Madrid.

11.Fergie anasema wachezaji wa united walikuwa wakimrushia matani Ronaldo kwasababu alikuwa hawezi kupita mbele ya kioo bila kujiangalia, alikuwa ni mtu wa kujiangalia sana.

12.Katika kipindi chake anasema watu wenye influence sana juu ya wachezaji wengine walikuwa ni Roy Keane,Bryan Robson na Steve Bruce.

Bracelona yammezea mate Coutinho.

Timu ya Barcelona imeongeza kasi kasi ya kutaka kumhamisha Nou Camp mchezaji wa kimataifa wa Kibrazil anayekipiga Liverpool, Philippe Coutinho.

Unadhani kwa mwenendo wa timu yetu ni bora Coutinho aondoke ama abaki apambane? Acha maoni hapa chini.

Ozil:Msituhukumu msimu bado haujaisha.




 "Muda mwingine mambo hayaendi kama mlivyopanga, tumeharibu mechi mbili za karibuni, sasa tunajipanga kutofanya makosa, msituhukumu bado msimu ni mchanga na ni mapema mno kupoteza imani na timu"

Walcott mbioni kujiunga Barcelona.

Mshambuliaji wa Arsenal,Theo Walcott anaweza kujiunga na mabingwa wa La Liga timu na Champions League timu ya Barcelona, Miamba ya soka hiyo ya Hispania inafuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

Lupita Nyong'o alamba dili lingine

Ndani ya uhusika wake katika filamu huyo Lupita atavaa uhusika akitambulika kama Raksha ambayo taarifa zaidi ni kwamba filamu itaingia rasmi sokoni mwezi Aprili mwaka 2016, itahusisha pia mastaa wengine wakubwa kutoka Hollywood akiwepo Idris Alba, Scarlett Johansson , Christopher Walken na Neel Sethi.
Filamu ya kwanza kabisa ya Jungle Book ilitoka mwaka 1967, waratibu wakiona kila sababu ya kufanya tena projekti hiyo kwa kutumia bajeti ya kutosha, na kwenda sawia na mabadiliko makubwa ya ki-teknolojia katika kutayarisha filamu za wahusika wa kutengeneza - yaani Animation.

Anthony Martial amzawadia mtoto wake tuzo ya mchezaji bora wa mechi


Mke wa Anthony Martial wa Manchester United, Samatha, amepost picha hii kwenye Instagram, ya mtoto wao wa kike akiwa na tuzo ya mchezaji bora baada ya baba yake kupachika mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Southampton.

Rais Kikwete akagua kituo cha Michezo cha Kidongo Chekundu kinachojengwa na Klabu ya Sunderland,

 
Rais Jakaya Mrisho kikwete akitambulishwa na Mkurugenzi wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks kwa kocha wa vija na kutoka Uingereza anayetambuliw3a na FIFA ambaye atakuwa mkufunzi Mkuu katika kituo hicho wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wakituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland ya Uingereza na kampuni ya symbion.

Name:  Kikwetee-620x264.jpg
Views: 1153
Size:  51.7 KB

Rais Jakaya Mrisho kikwete akitembezwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya umeme ya Symbion Bw. Paul Hicks wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Michezo kwa vijana cha Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam leo Septemba 16, 2015. Kituo hicho kinajengwa kwa msaada wa Klabu ya Sunderland ya Uingereza na kampuni ya symbion

Name:  unnamed.jpg
Views: 1382
Size:  76.3 KB

Name:  unnamed.jpg
Views: 1373
Size:  66.8 KB

NEC: Kauli ya Bulembo ni ya kawaida kipindi hichi cha Kampeni

 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeyapuuzia malalamiko kutoka muungano wa Vyama vya upinzani(UKAWA) kuhusu kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdallah Bulembo kuwa “CCM haitafanya makosa kukabidhi Ikulu kwa wapinzani”

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amesema kwa sasa kila chama kiko kwenye kampeni kutafuta ushindi, kwa hiyo kuna baahi ya kauli zitatolewa kama mbinu ya kutafuta ushindi.

Mwisho wa wiki Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe aliikosoa kauli ya Bulembo, akasema kauli hiyo inaonyesha CCM hawataki kuachia madaraka kwa amani. Mbowe aliilalamikia NEC kwa ukimya wakati kauli kama hizo za kichochezi zinatolewa

Akijibu kauli a Mbowe Lubuva amesema kama kauli ya Bulembo ingekuwa ni 'hatutakubali matokeo' tume ingeingilia kwa sababu NEC imeshasema kuwa kila chama kikubali matokeo.

Lubuva akaongezea na kusema mpaka sasa tume haina chochote cha kusema kuhusu kauli ya Bulembo kwa sababu wameichukulia kama kauli ya kawaida ya kikampeni.

Utafiti TWAWEZA wambeba Dr.J.P Mgaufuli uchaguzi 2015

Name:  Mkurugenzi wa Twaweza.jpg
Views: 23075
Size:  56.2 KB
Utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti ya TWAWEZA umeonesha kuwa endapo uchaguzi ungefanyika mwezi mmoja uliopita, mgombea urais wa CCM John Magufuli angepata ushindi kwa asilimia 65 wakati mgombea urais wa CHADEMA Edward Lowassa angefuatia kwa kupata asilimia 25.
Matokeo ya utafiti huo yametolewa leo jijini Dar es salaam ambapo yameonesha pia kuwa wagombea wa CCM katika ngazi zote ikiwa ni pamoja na ubunge na udiwani CCM inaongoza.
Katika ngazi ya udiwani CCM imeongoza kwa asilimia 60 ikifuatiwa na CHADEMA asilimia 24 na ngazi ya ubunge CCM imeongoza kwa asilimia 60 ikifuatiwa na CHADEMA yenye asilimia 26, wakatika katika ngazi ya urais bila kujali mgombea, CCM imeongoza kwa asilimia 66 ikifuatiwa na CHADEMA asilimia 22.
“Aidha, walipoulizwa watawachagua wagombea wa chama gani – bila kutajiwa majina ya wagombea – wananchi 6 kati ya 10 walisema kwamba watawachagua wagombea wa CCM kwa Urais, Ubunge (60%) na Udiwani (60%). Takwimu hizi zinatoa picha kwamba CCM inaungwa mkono, kama ilivyokuwa mwaka 2012.” Imesema taarifa iliyotolewa na TWAWEZA.
Akitangaza matokeo hayo mkurugenzi wa TWAWEZA bwana Aidan Eyakuze amesema utafiti huo ulifanyika mwishoni mwa mwezi Agost mwaka huu, na ulifanyika kwa njia ya simu kukusanya maoni ya wananchi katika mikoa yote ya Tanzania.
Eyakuze amesema kuwa wananchi waliulizwa swali kuwa watamchagua nani bila kutajiwa majina na walipoombwa kutaja moja kwa moja jina la mgombea Urais ambaye wangemchagua, asilimia 65 ya wananchi walimtaja mgombea wa CCM, John Magufuli.
Amesema asilimia 25 walimtaja mgombea wa Chadema (na Ukawa), Edward Lowassa. Asilimia 10 iliyosalia iligawanyika kati ya wale waliomtaja mmoja miongoni mwa wagombea urais wengine, waliokataa kujibu na waliokuwa bado hawana mgombea waliyempendelea.
Hata hivyo, takwimu zilikusanywa kabla vyama vingine, kikiwemo ACT-Wazalendo, kuteua wagombea wao wa Urais.
Amesema asilimia 62 ya wananchi wamesema kwamba wanajisikia wapo karibu zaidi na chama cha CCM kuliko vyama vingine.
 
Taarifa hiyo imeongeza pia kuwa “Chadema ni chama cha pili kinachopendwa kushinda vyama vingine vya upinzani. Lakini wananchi wanaosema kwamba watawachagua wagombea wa Chadema kwa Urais, Ubunge na Udiwani wamepungua kidogo. Ikumbukwe kuwa, inawezekana wananchi wanaopenda zaidi mseto wa Ukawa waliunga mkono vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi au NLD”.
Taarifa hiyo imeongeza pia kuwa mbali ya CCM na vyama vinavyounda UKAWA, chama cha ACT-Wazalendo kilitajwa na zaidi ya asilimia moja ya wananchi.
Utafiti huo ambao umetokana na kuwahoji watu 1848 umeonesha kuwa mgombea wa CCM, Dkt John Magufuli anapendwa zaidi na wanawake kuliko wanaume tofauti na Edward Lowassa, lakini pia wengi waliosema watamchagua Edward Lowassa ni wanaume na wengi wao ni walioelimika (wenye elimu kuanzia sekondari.
Waliomtaja Magufuli, wengi wao walisema wanamtaka Magufuli kwa sababu ni mchapakazi na waliomtaja Lowassa wengi wao wamesema ni kwa sababu wanaamini Lowassa ataleta mabadiliko.
Sehemu ya taarifa ya TWAWEZA inasema:-
"Hata hivyo, katika makundi yote haya, John Magufuli wa CCM anaonekana kuongoza. Kwa mfano, asilimia 33 ya wananchi wenye umri wa 18 – 29 na asilimia 30 ya wenye umri wa 30 – 39 wanamuunga mkono Lowassa, tofauti na asilimia 15 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 50. Pamoja na hayo, asilimia 57 ya watu wenye umri wa 18 – 29 na asilimia 76 ya watu wenye umri wa 30 – 39 wanamuunga mkono Magufuli. Upande wa makazi, asilimia 28 ya wakazi wa mijini walimuunga mkono Edward Lowassa tofauti na asilimia 24 ya wakazi wa vijijini. Asilimia 66 ya wakazi wa vijijini na asilimia 61 ya wakazi wa mijini wanamuunga mkono John Magufuli.
Asilimia 26 ya wanaomuunga mkono John Magufuli walidai kwamba ni kwasababu yeye ni mchapakazi, na asilimia 12 ya wanaomuunga mkono Edward Lowassa walisisitiza kwamba anaweza kuleta mabadiliko yanayohitajika nchini. Izingatiwe kwamba kauli hizi zinafanana karibu neno kwa neno na kauli mbiu za kampeni za wagombea hawa wawili.
Hata hivyo, wananchi hawana taarifa sahihi juu ya nafasi rasmi ya Ukawa kama mseto. Asilimia 49 ya wananchi wanafikiri kwamba Ukawa ni chama cha siasa kilichosajiliwa, kinyume na hali halisi. Asilimia 57 wanafikiri kwamba neno ‘Ukawa’ litakuwepo kwenye karatasi zao za kupigia kura. Hii pia, sio kweli. Bila kampeni na juhudi za kuwaelimisha wapiga kura ili wawe na taarifa sahihi kuhusu jambo hili, hali hii inaweza kuleta wasiwasi siku ya uchaguzi."

Makanisa matatu ya kilokole yachomwa moto Bukoba.

Makanisa matatu ya dhehebu la Kipentekoste yaliyopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, yameteketezwa kwa moto usiku wa kuamkia leo na watu wasiofahamika.
Tukio hilo limehusisha makanisa ya Pentecostal Assemblies of God (PAG) lililopo Buyekera Kata ya Bakoba, Living Water International na Evangelical Assemblies of God (EAGT) yote yakiwa eneo la Kashura.
Akizungumzia tukio hilo Mchungaji wa Kanisa la EAGT, Athanas, amesema saa 10 alfajiri alipigiwa simu na jirani yake na kuelezwa kanisa linaungua moto na kumfanya kukimbia kwenda eneo la tukio.
Mchungaji Athanas amesema baada ya kufika eneo la tukio alikuta moto mkubwa ambao usingeweza kuzimwa kwa kumwagia maji, hali iliyosababisha vitu vyote vilivyokuwa ndani ya kanisa hilo kuteketea ikiwa pamoja na viti 60, meza, mabenchi, vifaa vya ujenzi na madhabahu.
Amesema hawajafahamu watu waliohusika na tukio hilo, lakini alidai waliponusa baadhi ya vitu walisikia harufu ya mafuta ya taa hali iliyopelekea wahisi wachomaji walitumia mafuta ya taa kuteketeza kanisa hilo.
Mchungaji huyo alisema hilo ni tukio la tatu la makanisa ya EAGT kuchomwa moto, wakati mara ya kwanza ilikuwa Septemba 2013 na kufuatia lile la Aprili mwaka jana.
Naye Mchungaji Alistides Kabonaki wa kanisa la Pentekoste P.A.G, alisema saa 11.50 asubuhi jana, aliitwa na msichana wake wa kazi na kumweleza kuna moto unawaka kanisani.
Kabonaki alisema kanisa lote limeteketea pamoja na mali zilizokuwamo ndani huku waliohusika na tukio hilo akiwa hawafahamu walikuwa na lengo gani.
Amesema alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa pamoja na polisi, hivyo kwa sasa anasubiri hatua za kiuchunguzi za jeshi hilo ili kubaini waliohusika na sababu za kufanya hivyo.
Mchungaji huyo alisema kabla ya uchomaji wa kanisa hilo, watu hao wasiofahamika walivamia kanisa lao na kuiba baadhi ya mali zilizokuwamo ikiwamo viti na vitambaa vya madhabahu.
Akizungumzia tukio hilo, Regina Bakera, ambaye ni jirani na kanisa la PAG, alisema kama muumini amesikitishwa na matukio hayo na hawafahamu waliosababisha hilo.
Bakera alisema matukio hayo yanadhihirisha kuna kikundi kilichoandaliwa kwa ajili ya kuchoma makanisa na kuiomba serikali kuyashughulikia kufanya upelelezi wa kina.
Kufuatia uchomaji wa makanisa hayo, umoja wa wachungaji katika mkoa wa Kagera, umepanga kufanya maandamano ya kulaani kitendo hicho mkoa mzima maana serikali ilishindwa kutatua matatizo yanayowakabili ikiwamo la makanisa yao kuchomwa moto.
Mwenyekiti wa Makanisa hayo mkoa wa Kagera, Crodward Edward, alisema kwa sasa wanachukua hatua ya kujilinda kwa sababu serikali ilishindwa kufanya hivyo pamoja na vikao ambavyo wamekaa viongozi wa serikali na viongozi wa makanisa hayo.
Akizungumzia matukio hayo amesema siku za nyuma yalichomwa makanisa saba katika mkoa wa Kagera huku moja likihusisha pia mauaji ya muumini mmoja na waliokamatwa wakiachiwa huru bila kuelezwa kinachoendelea na sasa yamechomwa matatu kwa siku moja.
Naye Mchungaji Aneth Sebastian ambaye ni Katibu wa wachungaji katika manispaa ya Bukoba alisema sasa wanashindwa kuiamini serikali na polisi kwa sababu watakuwa wanawafahamu wanaohusika na vitendo hivyo bali wanawakingia kifua.
Tathmini ya hasara iliyotokana na uchomaji wa makanisa hayo ambayo mawili yameteketea kabisa bado inaendelea, ili kujua hasara iliyotokana na uchomaji moto huo.
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, alisema kwa sasa yuko safarini na atatoa ufafanuzi kuhusiana na tukio hilo baadae

Msanii Emmanuel Mbasha apiga magoti akilia baaada ya kuachiwa huru katika kesi ya Ubakaji.

Msanii wa muziki wa Injili, Emanuel Mbasha akiwa amepiga magoti akilia hapo jana baada ya kuachiwa huru katika kesi ya ubakaji iliyokuwa inamkabili kwenye mahakama ya wilaya ya ilala.

VIDEO:Dr.J.P.Magufuli apiga 'Push-Up' kabla ya kuwahutubia Wananchi wa Misenyi-Kagera.


Katika hali ambayo si ya kutarajia Mgombea wa Urais kwa kitu ya Chama Cha Mapinduzi Dr.John Pombe Magufuli alipiga "PUSH UP" kabla ya kuwahutubia wananchi wa wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera asubuhi ya leo.

Angalia video ikimuonyesha Dr.John Pombe Magufuli akipiga "Push-Up"
Bofya hapa-->; DR.MAGUFULI AKIPIGA PUSH-UP

Panya wasababisha kifo 'Jela ya Mandela'

Watu karibu 4,000 wameondolewa kutoka jela ya Pollsmoor nchini Afrika Kusini baada ya panya wengi kuvamia gereza hilo na kusababisha kifo cha mfungwa mmoja.

Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela aliwahi kufungwa katika gereza hilo.
"Tumekuwa tukipuliza dawa, lakini kwa sasa, tumelazimika kuwahamisha wafungwa, na itatuchukua siku kadha,” msemaji wa jela hiyo Manelisi Wolela amesema.

Panya hao wameeneza maradhi yajulikanayo kama leptospirosis, yanayosambazwa kupitia mkojo wa wanyama hao waharibifu.
Muungano wa kutetea haki za maafisa wa polisi na maafisa wa magereza umesema gereza hilo lilikuwa limejaa kupindukia na hali ni ya “kinyama”.

Bw Mandela alihamishwa kutoka jela ya Robben Island na kupelekwa Pollsmoor mwaka 1982
Maafisa wa afya wanasema hakuna mtu afaaye kurejeshwa kwenye gereza hilo hadi panya wote waangamizwe.

" Game of Thrones" yajinyakulia tuzo kubwa Marekani.

Tamasha kubwa la kila mwaka Emmys Awards, la kutoa tuzo kwa vipindi vya televisheni limefanyika mjini Los Angeles Marekani.
Kipindi cha Game of Thrones, kimenyakua matuzo mengi zaidi ikiwemo makala bora zaidi.
Viola Davis naye ametajwa kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kupata ushindi wa muigizaji bora zaidi katika kipindi cha "How To Get Away With Murder".
Jon Hamm ambaye ameteuliwa mara saba kwa tuzo la muigizaji bora zaidi hatimaye amechukua tuzo hilo kwa uigizaji wake katika kpindi Mad Men.

Ahukumiwa kifungo kwa maoni ya Uchochezi Facebook.

Mahakama ya Singapore imemuhukumu muuguzi mmoja kutoka nchini Ufilipino kifungo cha miezi minne kwa kuchapisha maoni ya uchochezi kuhusu taifa hilo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Ello Ed Mundsel Bello ambaye amekuwa akifanya kazi nchini Singapore aliandika kwamba raia wa taifa hilo hawako huru.
Alishtakiwa kwa kuwa muhaini na kuwadanganya maafisa wa polisi.
Akitoa hukumu hiyo jaji huyo alisema kuwa mahakama hiyo haikuweza kupuuza tishio la maoni hayo kwa jamii ilio tulivu.
Singapore ni taifa lenye raia wa mataifa na rangi mbali mbali na mamlaka hujali sana maoni ambayo yanaweza kuchochea wasiwasi wa kibaguzi.

Mtandao wa Skype wakumbwa na tatizo.

Tatizo la kimitambo limesababisha watu wengi kukosa kutumia huduma ya mtandao wa Skype.Ripoti kuhusu Skype kukumbwa na hitilafu zilianza mwendo wa saa tano za Afrika mashariki nchini Uingereza.
Katika taarifa yake,mmiliki wa Skype Microsoft amesema kuwa waligundua tatizo katika mitambo ya huduma hiyo ambayo inaonyesha iwapo kuna mtu anatumia huduma hiyo au la.
Tatizo hilo liliwazuia wanaotumia mtandao huo na hivyobasi kutoweza kupiga simu licha ya kwamba wapo mtandaoni.
Vilevile,Microsoft imesema kuwa majina ya wanaotumia huduma hiyo ambao wameathiriwa yanaonyesha kwamba hawako katika mtandao na hivyobasi kutoweza kuwapigia simu.
Wateja wengi wa Skype kutoka nchini Uingereza,Australia na Japan wameripoti tatizo hilo.
Maafisa wa mtandao huo wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa wanafanya kila njia kutatua tatizo hilo.

Costa na Gabriel washtakiwa na FA.

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ameshtakiwa kwa madai ya kutaka kuzua ghasia ambayo hayakuonekana na maafisa wa mechi hiyo lakini ambayo yalinaswa katika ukanda wa video.
Mshambuliaji huyo alihusishwa katika kisa na beki wa Arsenal Laurent Koscielny katika dakika ya 43 ya mechi.
Mchezaji huyo ana hadi saa kumi na mbili hapo alhamisi jioni kujibu mashtaka hayo.
Naye Beki wa Arsenal Gabriel ameshtakiwa kwa utovu wa nidhamu kwa tabia yake wakati alipopewa kadi nyekundu huku Santi Carzola akionywa kuhusu tabia yake mbaya.
Wakati huohuo vilabu vyote viwili vimeshtakiwa kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake chini ya sheria za FA.
Vilabu vyote viwili pamoja na Gabriel vina hadi saa kumi na mbili jioni siku ya alamisi kujibu mashtaka hayo.

kampuni ya magari ya Volkswagen yaomba msamaha kwa Uchafuzi wa Mazingira.

Mkurugenzi mkuu wa  baada ya wasanifu nchini Marekani kusema baadhi ya magari yake yamekuwa yakichafua mazingira.
''Naomba msamaha mimi mwenyewe kwamba tumevunja heshima kwa wateja wetu na umma kwa jumla'',alisema Winterkorn.
Ameanzisha uchunguzi dhidi ya kifaa kilichowekwa katika magari hayo ili kupunguza hewa chafu wakati wa ukaguzi ikilinganishwa na wakati gari hizo zinapoendeshwa.
Hisa za kampuni hiyo zilishuka kwa asilimia 18 zilipoanza biashara.
Kampuni hiyo ya magari nchini Ujerumani ilishinikizwa kurudisha magari yake nusu milioni siku ya ijumaa.
Idara ya mazingira ilipata kifaa hicho katika magari ya Audi A3,VW jetta,Beetle,Golf na yale ya aina ya Passat.
Mbali na kuyarudisha magari hayo kwa ukarabati kampuni hiyo pia itakabiliwa na faini za mabilioni ya madola.
Huenda wakuu wa kampuni hiyo pia wakashtakiwa na mashtaka ya uhalifu.
Shirika hilo la mazingira linasema kila gari ambalo halikuzingatia sheria ya hewa safi itapigwa faini ya dola 37,500.
Huku magari 482,000 yakiwa yameuzwa tangu mwaka 2008 huenda faini hizo zikafika dola bilioni 18.

Bomu laua watu 6 katika makao ya Rais Somalia.

Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka karibu na lango kuu la jumba la rais katika mji mkuu wa Mogadishu.
Takriban watu sita wamefariki,ikiwemo walinzi wa rais.Raia mmoja wa Uturuki pia aliuawa.
Wengine 10 waliripotiwa kujeruhiwa.
Mkutano kuhusu hali ya baadaye ya uchaguzi nchini humo umekuwa ukiendelea katika jumba hilo,lakini ulikuwa umeisha wakati wa mlipuko huo.
Wajumbe wengi waliripotiwa kuondoka katika eneo la jumba hilo.
Hoteli moja karibu na jumba hilo iliharibiwa.

Mgombea Urais ajitoa katika kinyanganyiro baada ya kufanya vibaya katika midahalo

Scott Walker, ambaye ni miongoni wagombea waliokuwa wakiwania kuteuliwa kugombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amejiondoa kutoka kwa kinyanganyiro hicho.
Bwana Walker ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Winscosin amesema amejitoa kutoka kampeini hizo ili kutoa nafasi kwa uteuzi wa mgombea muafaka atakayekabiliana na Donulkd Trump.
Mgombea huyo, ambaye alikuwa akiungwa mkono kwa wingi na wafuasi wa mrengo wa kulia, lakini hata hivyo katika kura ya maoni kiwango chake kilishuka baada ya kufanya vibaya katika midahalo. Scott Walker, mmojawapo wa wagombea watarajiwa wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican amejiondoa kutoka kwa kinyanganyiro hicho.
Bwana Walker ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Winscosin amesema amejitoa kutoka kampeini hizo ili kutoa nafasi kwa uteuzi wa mgombea muafaka atakayekabiliana na Donulkd Trump.
Mgombea huyo, ambaye alikuwa akiungwa mkono kwa wingi na wafuasi wa mrengo wa kulia, lakini hata hivyo katika kura ya maoni kiwango chake kilishuka baada ya kufanya vibaya katika midahalo.

Monday 21 September 2015

Mabasi ya mwendokasi 138 yawasili Dar es Salaam.

Mabasi 138 yatayotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam yamewasili katika bandari ya Dar es Salaam huku mkuu wa mkoa huo Said Meck Sadick akisema nauli watakayotozwa watu watakaotumia usafiri huo itakuwa katika kiwango ambacho watumiaji wake wanamudu kuilipa.

Mh.Lowassa alitikisa tena Jiji la Dar es Salaam.

Mgombea urais wa Chadema kupitia UKAWA Mh.Lowasa atikisa jijini Dar es Salaam.
Mgombea urais wa UKAWA Edward lowassa Katika mikutano mikubwa ya hadhara aliyoifanya kwa nyakati tofauti na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa jijini Dar es Salaam amesema serikali yake ya awamu ya tano itajikita katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania wanyonge ambao wameshindwa kunufaika na rasmili za nchi kwa miaka 50 iliyopita.

Lowassa ameomba Watanzania wametakiwa kutokukubali kuhadaika na ahadi zinazotolewa na baadhi wa wagombea katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu kwani wengi wao hawana dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo hapa nchini.