Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Showing posts with label Celebrities. Show all posts
Showing posts with label Celebrities. Show all posts

Tuesday, 26 January 2016

Wema,Idris watarajia kupata mtoto.Waamua kuweka uhusiano wao wazi.

Kulingana na ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Big Brother Idris Sultan,Wema sio tu eti keshapata mchumba ila pia ashapata uja uzito!

Muigizaji huyo maarafu wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu aligonga vichwa vya habari kote kanda ya Afrika Mashariki na Kati walipokosana na mwimbaji huyo nguli Diamond raia wa Tanzania.

Wema alijieleza kuwa amepigwa teke na mwimbaji huyo wa ''Mdogo mdogo'' na ''Number One'' kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa kupata mimba.

Idris, ambaye alikuwa amehusishwa na mlimbwende huyo kwa muda mrefu alikuwa akibubujikwa na penzi katika taarifa hiyo yake kwenye Instagram.

''Mimi nawe sio wa kawaida. Nala, natembea, nalala, nazungumza nikikuwazia wewe tu.''

''Na kama utadhani kuwa umebahatika kuwa nami, pia mimi naona nimebahatika kuwa nawe.''

''At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama.''

“Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike”.

''Au ukiingia jikoni kwangu na unapika na kuniandalia chakula kizuri,” aliandika Idris.

“Nitafanya kila niwezalo ilimradi ufurahi.''Nitakulinda, nikupende, nikutendekeze, tupike nawe, tujiburudishe kwa pamoja na kujivinjari; kwa hakika wewe ndiye uliyekonga moyo wangu''.''Wewe ndiye mke wangu''

Mchumba wake wa zamani mwanamuziki Diamond Platinum amepata mtoto na bi. Zari kutoka Uganda ambaye ni mpinzani mkubwa wa Wema.

Idris na Wema watakumbukwa kwa kuanda matangazo ya kibiashara kama ''mume na mkewe'' Wema kwa upande wake alimsifu Idris kwa ucheshi wake hata mara nyengine akiachilia picha zake kwenye mtandao wake wa Instagram na kumtambua kama ''mpenzi''

Wema alitofautiana na Diamond Platinumz na akakurubiana na mwakilishi mwengine wa Big Brother Luis Munana raia wa Namibia.

Monday, 16 November 2015

Diamond Platnumz na Vanessa Mdee washinda tuzo 4 za AFRIMA 2015 Nigeria

Tuzo za All Afrika Music Awards 2015 (AFRIMA) zimetolewa usiku wa Jumapili November 15 jijini Lagos, Nigeria ambapo Tanzania imetoa washindi wawili.

Diamond Platnumz aliyekuwa akiwania tuzo hizo ameibuka mshindi wa vipengele 3 kikiwemo kipengele muhimu cha Msanii Bora Wa Mwaka (Artist Of The Year) ambayo ilikuwa ikiwaniwa na Alikiba, Davido, Jose Chameleone, Wizkid, Yemi Alade, Sarkodie na Flavour.Vipengele vingine alivyoshinda Diamond ni Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki (Best Male Artist in Eastern Africa) pamoja na Wimbo Bora Afrika (Nasema Nawe)


Vanessa Mdee ameshinda kipengele cha ‘Best African Pop’ kupitia wimbo wake ‘Hawajui’.
msanii mwingine kutoka Tanzania 
aliewania tuzo hiyo 
Ni Linah ambae alikua kwenye kipengere cha msanii bora wa kike wa Afrika Mashariki

Friday, 13 November 2015

Ronaldo anunua 'Private Jet' kwa zaidi ya Bilioni 44.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo anaripotiwa kutumia mkwanja mrefu kununua ndege binafsi, Staa huyo anayeongoza katika list ya rekodi ya watu maarufu wanaongoza kupata likes nyingi katika mtandao wa facebook amenunua ndege binafsi aina ya Gulfstream G200 Business Jet.
CTmoKwwUkAALhqc
Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 anatajwa kununua ndege hiyo kwa thamani ya pound milioni 13.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 44 za kibongo kwa ajili ya kuzunguuka sehemu mbalimbali duniani kuhusiana na mipango yake ya kujitanua kibiashara, ndege ya staa huyo inatajwa kuwa na uwezo wa kubeba watu 8 hadi 10, jiko la umeme, bafu, friji, makabati, simu na internet.
CTmoLGsUwAAD05O
Nyota huyo ambaye anaonekana kujiimarisha zaidi kibiashara tayari amezindua movie ya maisha yake halisi aliyoizindua hivi karibuni Uingereza ila mwaka 2015 alitajwa kuzindua perfume, brand ya viatu vyake.
CTmoLjrU8AA1tuN
Sports-people-and-Private-jets
Cristiano Ronaldo akiwasili uwanja wa ndege wa Centrair International airport uliyopo Nagoya Japan kwa ndege yake binafsi.
GettyImages-79579622-742x505
CR7-742x474

Wednesday, 11 November 2015

Facebook yapata faida kubwa.

Facebook imeandikisha faida kubwa ya dola $891m kati ya mwezi Julai na Septemba.Kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii imeripoti ongezeko la asilimia 11% na na mapato ikilinganishwa na wakati sawa na hii mwaka uliopita.

Mwaka wa 2014 Facebook ilipata dola $806 ikilinganishwa na $891m ilizotia kibindoni mwaka huu kutokana na kukua kwa idadi ya watumizi wa mtandao huo wa kijamii.

Wawekezaji wamekuwa wakitafuta ishara kuwa Facebook imepata faida kutokana na mitandao yake ya Instagram na WhatsApp,ama hata dalili kuwa imeanza kuandikisha faida kutokana na ongezeko la idadi ya video zinazochapishwa kwenye mitandao hiyo.Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa Facebook,Mark Zuckerberg amesema kuwa kampuni hiyo inalenga kukuza mapato yake katika siku za usoni.

Faida hiyo imetokana na kukuwa kwa idadi ya watumizi milioni 60 katika robo ya tatu ya waka huu.Image copyrightReutersImage captionSasa Facebook inazaidi ya watumizi bilioni 1.55 kote dunianiSasa Facebook inazaidi ya watumizi bilioni 1.55.

Kukuwa kwa idadi hiyo kubwa kunamaanisha kuwa mapato yataokanayo na matangazo ya kibiashara pia yanakuwa.Kufikia sasa inakisiwa kuwa watumizi zaidi ya bilioni moja u nusu hutumia dakika 1 kati ya 5 wakidurusu mitandao ya kijamii ya Facebook amd Instagram.Katika mwezi wa Septemba idadi ya watu waliotembelea mtandao wa Facebook imeimarika kwa asilimia 27% na kutimia watu milioni 894.

Mnigeria aibuka bingwa wa dunia.

Raia mmoja wa Nigeria ameushangaza ulimwengu wa mchezo wa kujenga maneno ya Kizungu, Scrabble, kwa kumshinda Mwingereza na kuibuka bingwa wa dunia.Wellington Jighere, 32, aliweka historia kwa kuwa Mwafrika wa kwanza kushinda mashindano hayo.

Jighere alijenga maneno yenye alama nyingi kama; mentored, avouched na fahlores, yaliyomwezesha kumpiku mpinzani wake Lewis Mackay kutoka Uingereza katika fainali hizo zilizoandaliwa mjini Perth nchini AustraliaJighere alimshinda MacKay 4-0.

Licha ya uchovu, aliandika majina magumu kama vile ironists, ungifted, felty, Dacoit, Katti, Yow na Aah.Image captionJighere mwenyewe amesema alihisi kana kwamba ''bara la Afrika lilikuwa linamuunga mkono katika fainali hiyo''Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amempongeza Jighere kwa kuipeperusha bendera ya taifa lake vyema.

''Umeiletea sifa Nigeria,'' alisema Rais BuhariJighere mwenyewe amesema alihisi kana kwamba ''bara lote la Afrika lilikuwa linamuunga mkono katika fainali hiyo''.Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Facebook Jighere amesema anashangaa aliwezaje kuibuka kidedea huku akisema kuwa hajakuwa akipata usingizi vyema katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amempongeza Jighere kwa kuipeperusha bendera ya taifa lake vyemaRaia huyo wa Nigeria alicheza mechi 32 katika kipindi cha siku nne kabla ya kushinda katika fainali hizo.

Aidha yeye pamoja na timu nzima ya Nigeria walifika mjini Perth Australia siku moja kabla ya mashindano hayo baada ya kustahimili safari ya saa 20 angani.Jighere alipigiwa simu na Rais Buhari kufurahia ushindi wake.

Timu ya Nigeria ilifika Perth siku moja kabla ya MashindanoKufuatia ushindi huo Jighere ambaye hana kazi alituzwa dola $10,000 za Marekani.

Rais wa shirikisho la mchezo huo la Nigeria Sulaiman Gora amesema kwa njia ya simu kuwa Jighere ni mtu mnyamavu sana na kuwa ''uwezo wake mkuu ni unyenyekevu''.

CHANZO:-BBC

Thursday, 24 September 2015

Ney Wa Mitego:Wasanii kukashifu viongozi itakuja kutu-Cost.

Zikiwa zimebakia siku 31 kuelekea uchaguzi mkuu, msanii Nay wa Mitego amendika hivii;

"Wasanii tubaki kua wahamasishaji tu!Kuanza kukashfu Viongozi utadhani labda nawewe umekua mwana Siasa au Mgombea itakuja kutu Cost baadae. Hua najiuliza cjui wanalipwa shiling ngapi maana wanasahau wao ni wasanii na wana Mashabiki wenye Imani tofauti, pia kuna Maisha baada ya uchaguzi. Endeleeni kutumika vibaya kwa Njaa ya leo na kwa maslahi ya wachache na kusahau kuna kesho. Pigania unacho amini but si kwa kashfa wala Matusi. Mimi naamini
# Mabadiliko2015 .Tukutane # October25 " ...Ameandika hivyo Nay wa Mitego

Tuesday, 22 September 2015

Lupita Nyong'o alamba dili lingine

Ndani ya uhusika wake katika filamu huyo Lupita atavaa uhusika akitambulika kama Raksha ambayo taarifa zaidi ni kwamba filamu itaingia rasmi sokoni mwezi Aprili mwaka 2016, itahusisha pia mastaa wengine wakubwa kutoka Hollywood akiwepo Idris Alba, Scarlett Johansson , Christopher Walken na Neel Sethi.
Filamu ya kwanza kabisa ya Jungle Book ilitoka mwaka 1967, waratibu wakiona kila sababu ya kufanya tena projekti hiyo kwa kutumia bajeti ya kutosha, na kwenda sawia na mabadiliko makubwa ya ki-teknolojia katika kutayarisha filamu za wahusika wa kutengeneza - yaani Animation.

Msanii Emmanuel Mbasha apiga magoti akilia baaada ya kuachiwa huru katika kesi ya Ubakaji.

Msanii wa muziki wa Injili, Emanuel Mbasha akiwa amepiga magoti akilia hapo jana baada ya kuachiwa huru katika kesi ya ubakaji iliyokuwa inamkabili kwenye mahakama ya wilaya ya ilala.

Monday, 21 September 2015

Kiongozi wa kriket duniani afariki duniam

Rais wa bodi ya Kriket ya India Jagmohan Dalmiya amefariki dunia. Dalmiya mwenye miaka 75 alifikishwa hospitalini siku ya Alhamisi wiki iliyopita kutokana na maumivu ya kifua huku akilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Amehudumu katika nafasi ya Urais wa Kriket nchini humo tokea mwaka 2001 mpaka 2004 kwa kipindi cha mpito wa uongozi wa chama hicho ambapo alirudi tena madaraani mwaka 2013 mpaka Machi 2015.

Alikuwa pia kiongozi katika shirikisho la dunia la mchezo huotokea mwaka 1997 mpaka 2000.

Saturday, 19 September 2015

Bacary Sagna aeleza sababu ya kunyoa rasta zake.

Bacary Sagna alikua anatambulika kirahisi kwa rasta zake ambazo zilikua na rangi. Sasa akiwa kwenye mapumziko ya likizo baada ya msimu uliopita alinyoa rasta zake na picha yake kusambaa sana kwenye mtandao ya kijamii.

Sasa akiwa kwenye kipindi cha maswali na majibu katika Manchester City Tv, moja ya swali lililoulizwa na mashabiki wengi ni kuhusu kwanini amenyoa rasta zake.

Jibu lake ni kwamba yeye binafsi alikua na mpango wa kuzinyoa muda wowote, lakini sababu ya msingi iliyomfanya anyoe zile rasta ni sherehe ya asili aliyoshiriki kwao Senegal ambayo ilikua lazima anyoe nywere zake.

Mshuhudie Msanii Kingwendu Ngwendulile katika harakati zake za Kisiasa.

Ni baada ya msanii huyo kujitosa kugombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama cha CUF.

Friday, 18 September 2015

Joh Makin akataa kujihusisha katika kampeni za Kisiasa.

Joh Makini amesema anawaheshimu mashabiki wake kiasi ambacho amekataa mamilioni ya fedha kushiriki kwenye kampeni za siasa zinazoendelea.

Joh amesema ingawa wakiwa kama wasanii wana uhuru na haki ya kufanya hivyo, lakini wao kama Weusi wameona watawachanganya mashabiki wao.

Baada ya T-Shirt,Lowassa aja kivingine baada ya kutengeneza kinywaji Chake.

Ni katika hali ya kustaajabisha baada ya kutengeneza t-shirt mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha Jina la Lowassa linakuwa katika vichwa vya wapiga kula.Baada ya mabango mbalimbali yenye Picha za Lowassa kusambazwa kila kona.

Hivi sasa amekuja kivingine baada ya kutengeneza kinywaji/Pombe kupitia kampuni ya "John Walker" ambayo itakuwa inauzwa katika sehemu za starehe.

Endelea kutembelea www.bantuz.com kwa habari za kina na uhakika.

Thursday, 17 September 2015

Bondia Manny Pacquiao atia neno baada ya Mayweather kutangaza kustaafu.

Bondia Manny Pacquiao amesema kwamba ameachana na ndoto za pambano la marudiano na Floyd Mayweather kutokana na mpinzani wake huyo kutangaza kustaafu kufuatia kumshinda kwa pointi Andre Berto mwishoni mwa wiki.

Mayweather alimshinda kwa pointi Pacquiao Mei mwaka huu katika pamabano la utajiri mkubwa wa ndondi na baada ya kumshinda Berto katika pambano lake la 49 mfululizo kushinda, ametangaza kustaafu akiwa hajapoteza pambano.

Hata hivyo, mashabiki walikuwa wanataka kuona akirudiana na Pacquiao kwa sababu katika pambano baina yao, Mfilipino huyo alipigana akiwa ana maumivu ya bega na pia hivi karibuni imeripotiwa Mayweather alitumia dawa zilizopigwa marufuku mchezoni. Pac Man anatarajiwa kuwa fiti kurejea ulingoni mwakani baada ya kupona bega.

“Ngumi si kitu nachofikiria kwa sababu naweza kupigana mwakani tu, ili kulipa mapumziko bega langu,”amesema Pacquiao leo ambaye anaendelea na matibabu ya bega lake la kulia aliloumia mazoezini kujiandaa na pambano dhidi ya Mayweather.
Mbabe huyo ambaye pia ni mwanasiasa nchini kwao, amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake katika ujenzi wa nyumba za watu wasio na makazi kusini mwa nyumbani kwao, jimbo la Sarangani.

“Niko sawa. Kuwe na pambano la pili (dhidi ya Mayweather), si tatizo,” amesema. “Nimesikia amestaafu, haijalishi,”. Kwa pambano lijalo, amesema atapigana na bondia yeyote. “Kwa sababu sichagui wapinzani wangu,”.
Pacquiao pia amesema alikuwa anasubiri kuona Mamlaka za ndondi Marekani zitamchukulia hatua gani Mayweather kwa kutumia sindano ya dawa za IV baada ya kupima uzito kabla ya pambano lao mjini Las Vegas.

Bondia Manny Pacquiao kuzichapa na Amir Khan.

Bondia kutoka nchini England, Amir Khan huenda akapambana na Manny Pacquiao, baada ya kushindwa kutimiza ndoto zake za kupanda ulingoni na bingwa wa dunia Floyd Mayweather aliyetangaza kustaafu mwishoni mwa juma lililopita.

Mzungumzo kuhusu mpambano wa Khan dhidi ya Pacquiao yanaendelea kwa sasa kwa kushirikisha viongozi wa pande zote mbili.

Tayari tetesi zimeanza kujitokeza katika mitandao ya kijamii zikieleza kwamba huenda wawili hao wakakutana ulingoni mwezi Novemba mwaka huu huku wengine wakidai pambano hilo litakua la mwisho kwa Pacquiao ambaye tayari ameshaeleza itakapofika mwaka 2016 ataachana na mchezo wa masumbwi.

Khan amekua kimya tangu alipomkandamiza mpinzani wake kutoka nchini Marekani Chris Algieri mwezi may mwaka 2015, na alionyesha dhamira ya kutaka kupanda ulingoni dhidi ya Floyd Mayweather, lakini aliweka masharti ya kutaka kupewa nafasi ya kutimiza ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo Khan, bado ameonyesha dhamira ya kumuhitaji Mayweather, kwa kusema anaamini atabadili msimamo wake wa kustaafu mchezo wa ndondi ili arejee ulingoni na kukamilisha pambano la 50 ambalo amependekeza limkutanishe nae.

Kwa upande wa Manny Pacquiao,
hajarejea tena ulingoni tangu alipopoteza kwa point dhidi ya Floyd Mayweather katika pambano lililounguruma May 02 mwaka huu.
Mayweather alitangaza kuachana na ndondi mara baada ya mpambano wake dhidi ya Andre Berto aliyemshinda kwa point.

Historia inaonyesha kwamba Mayweather anakua bondia aliyetangaza kujiweka pembeni huku akiwa ameshinda michezo 49 pasi na kupoteza hata mmoja.

Bondia afariki baada ya kupigwa kwa "Knock-Out"

Mwana masumbwi mmoja wa Australia amefariki siku nne baada ya kupoteza fahamu alipopigwa 'knock out' katika pigano la kijimbo mjini Sidney.

Davey Browne mwenye umri wa miaka 28 aliangushwa na Carlo Magali wa taifa la Ufilipino mwisho wa raundi ya 12 katika taji la uzani wa Feather siku ya Ijumaa.

Brown ambaye ni baba ya watoto wawili alipelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kabla ya mitambo inayomsadia kuzimwa alipokosa kuimarika kiafya.

Muungano wa wahudumu wa matibabu nchini Australia umetaka mchezo wa ndondi kupigwa marufuku nchini humo kufuatia kifo hicho.

Kifo cha Browne kinajiri wiki sita baada ya mwanamasumbwi wa Queensland Braydon Smith kuzirai na kufariki kufuatia pigano la uzani wa Feather nyumbani kwake huko Toowoomba.

Friday, 5 June 2015

Nikki Mbishi ajibizana na Nikki wa Pili katika mtandao wa kijamii.


Jana kwenye ukurasa wa Instagrama wa @Cloudsfmtz waliposti mambo ambayo Nikki wa Pili aliyaandika ili kuwapa husia wasanii wanao kuja kuwa na style yao tofauti katika muziki huu wa Hip Hop pia alielezea ni kwa jinsi gani wasanii wa HipHop wa zamani ambavyo wamekuwa hawafanyi vizuri na mambo mengi alizungumzia kuhusiana na muziki wa Hip Hop Sasa baada ya Cloudsfm kupost Nikki Mbishi akaona na ikabidi amjibu Nikki Wa Pili kwa kumwambia "Kama wewe unafanya na uko happy nacho then fanya ila usipotoshe tena kwa kutumia kivuli cha Hip Hop ili hali tunafahamu wewe ni mfanya biashara That’s not Hip Hop ,That’s something else

BantuTz MAGAZETINI:Soma kilichoandikwa katika magazeti yote ya leo Ijumaa,Juni 05

MAGAZETINI-Ni uratatibu ambao BantuTz imeuanzisha ili kuwawezesha wadau wote wa Bantu waweze kusomana kupitia kurasa za magazeti mbalimbali nchini kila siku asubuhi ili kuwasogezea karibu zaidi huduma kupata habari nuhimu baada ya maombi ya wadau mbalimbali.
DSC03316
DSC03317
DSC03318 DSC03319
DSC03320
DSC03321
DSC03322
DSC03323
DSC03324
DSC03325
DSC03326
DSC03327
DSC03328
DSC03329
DSC03330
DSC03331
DSC03332
DSC03333
DSC03334
DSC03335
DSC03336
DSC03337
DSC03338
DSC03339
DSC03340
DSC03341
DSC03342
DSC03343
DSC03344
DSC03345
DSC03346
DSC03347
DSC03348
DSC03349
DSC03350
DSC03351
DSC03352
DSC03353
DSC03354
DSC03355