Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Wednesday 29 April 2015

Rais Kikwete azindua meli 2 za kivita.

Rais Jakaya Kikwete amezindua meli vita mbili za doria Bahari Kuu ambazo ni TSN Msoga naTSN Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika jana kwenye Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam.

Pacquiao atamba kumchakaza Mayweather

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya dunia kushuhudia mpambano wa
karne wa mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao,Bondia wa
Ufilipino Manny Pacquiao ametamba kumchakaza mpinzani wake
kwenye mpambano utakaofanyika Mei 2 mwaka huu katika ukumbi wa
Mgm Grand Vegas
Akiwa amezungukwa na mamia ya washabiki wake Pacquiao aliwaeleza
"msiwe na wasiwasi mimi ndie ninae pigana na nina uhakika asilimia
mia moja wa kushinda".
"Naamini huu ndio muda wa Mayweather kupoteza mchezo kwa mara
ya kwanza’’
Floyd Mayweather hajawahi poteza mchezo katika mapambano 47
aliyokwisha cheza ,Huku Pacquiao akiwa kapoteza mapambano 5 na
kutoka sare mara 2 katika mapambano 64 aliyocheza.

Barcelona wazidi "kuchanja mbuga" La Liga.

Vinara wa La Liga FC Barcelona Jana Usiku wameishindilia Getafe
Bao 6-0 na kupanda kuwa mbele ya Timu ya Pili Real Madrid kwa
Pointi 5.
Mabao ya Barca yalifungwa na mshambuliaji wao hatari Lionel Messi
aliyefunga mara mbili huku, Luis Suarez nae akitupia kambani mabao
mawili , Neymar na Xavi wakifunga bao moja moja.
Mabao hayo ya washambuliaji wa Barca, Messi, Suarez na Neymar
yamewafikisha zaidi ya mabao 100, kwa Msimu huu.
Hii Leo, Real Madrid walioko nafasi ya pili watakua na kibarua cha
kupetetana na Almeria Uwanjani Santiago Bernabeu.
Vita ya kuwania kiatu cha mfungaji bora kiko kwa Cristiano Ronaldo
mwenye magoli 39 akifuatiwa na Messi mwenye mabao 38.

Borussia Dortmund watinga fainali baada ya kuifunga Bayern Munich.

Borussia Dortmund imetinga Fainali ya Kombe la ujerumani (DFB-
POKAL)baada ya kuwabwaga Mabingwa Watetezi Bayern Munich kwa
Penati 2-0 kufuatia Sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za mchezo
uliopigwa Allianz Arena.
Borussia Dortmund itacheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine
inayochezwa Leo kati ya Timu ya Daraja la 3 Arminia Bielefeld na
Klabu ya VfL Wolfsburg.
Katika Nusu Fainali hii, Bayern walitangulia kufunga Bao la Dakika
ya 29 la Robert Lewandowski na Dortmund kurudisha Dakika ya 75
kwa Bao la mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang.
Katika Dakika za Nyongeza 30, Dortmund walibaki Mtu 10 baada ya
Mchezaji wao Kampl kupewa Kadi Nyekundu lakini mwisho Bao zilibaki
1-1.
Kwenye Mikwaju Mitano ya Penati, Bayern walikosa Penati zao zote 4
zilizopigwa na Xabi Alonso, Philipp Lahm, Mario Gotze na Kipa Manuel
Neuer huku Dortmund wakifunga 2 kupitia Sebastian Kehl na Ilkay
Gundogan.

Jeshi la Nigeria lawaokoa watoto wa kike 293 kutoka katika kambi ya Boko Haram.

Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia mbili na
akina mama tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko
katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale waliotekwa
mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.
Jeshi limesema ya kwamba wanawake na watoto hao wa kike
walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia
zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao
baada ya kuziharibu kambi hizo.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu
wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne
zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua
kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."
Jeshi la Nigeria
Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata
hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi
waliotekwa katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze
kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa
umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu
wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka
jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri
muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote. "

Tuesday 28 April 2015

HIZI NDIZO FAIDA ZA KUNYWA MAJI MWILINI

1: Kupunguza uzito: Kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uzito,
kwani maji hayana mafuta, kalori wala sukari.

2: Afya ya moyo: Unywaji wa maji mengi kunaweza kupunguza hatari
ya kupatwa na ugonjwa wa moyo. Utafiti wa miaka sita uliofanywa
Marekani umeonesha kuwa watu wanaokunywa glasi za maji
zisizopungua 5 kwa siku, hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na
ugonjwa wa moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2
au chini ya hapo.

3: Nishati ya mwili: Mwili unapopungikiwa maji, hukufanya ujisikie
mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha daima utakuwa mwenye
nguvu. Pendelea kunywa maji badala ya vinywaji baridi kama soda,
juisi au bia.

4:Tiba ya kichwa: Dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini ni pamoja
na kuumwa kichwa. Kunywa maji ya kutosha na hutasumbuliwa sana
na kuumwa kichwa mara kwa mara.

5:Ngozi nyororo: Unywaji maji ya kutosha kila siku unaweza safisha
ngozi yako na kuifanya ionekane nyororo.

6: Matatizo ya choo: Maji ni dawa ya kutibu ukosefu wa choo,
kunywa maji ya kutosha kila siku na utajiepusha na tatizo la ukosefu
wa choo mara kwa mara.

7: Usafishaji wa mwili: Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa
uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.

8: Saratarani: Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji,
kwani maji husaidia suala la usagaji wa chakula tumboni na hivyo
wakati wote tumbo lako litakuwa safi. Utajiondoa katika hatari ya
kupata saratani ya tumbo kwa asilimia 45 na asilimia 50 kwa
saratani ya kibofu cha mkojo.

9: Mazoezi: Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, yatakufanya uwe
na nguvu ya kufanya mazoezi yako ya kutosha, hivyo kupata faida
ya mazoezi ipasavyo.

Liverpool watimiza miaka 25 tangu washinde ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza.

Wakati Liverpool leo wakiwa wanatimiza miaka 25 tangu washinde
ubingwa wa EPL. April 28, 1990 ndio ilikuwa siku ya mwisho kutwaa
uchampion wa England. Swali kwa wana Liverpool - wangapi walishuhudia timu hiyo ikitwaa ubingwa huo?

Babake mzazi Kim Kardashian ajitangaza kuwa ni 'Mwanamke'

Bruce Jenner aliyekuwa mwariadha bora duaniani kabla ya kuwa
nyota wa kipindi cha televisheni na familia moja maarufu duniani
''The Kardashians''. sasa amefichua siri ambayo amekuwa akiificha
kwa miaka mingi.
''Kwa nia na madhumuni yote, mimi ni mwanamke.'' Jenner aliambia
Sawyer kutoka ABC katika mahojiano maalum yaliopeperushwa hewani
siku ya Ijumaa.
''Watu wananiona tofauti,wananiona kama mwanaume, lakini moyo na
roho yangu na kila kitu ninachofanya maishani ni sehemu yangu.''
Jenner ambaye ana umri wa miaka 65 amesema. '' Upande huu wa
kike ni sehemu yangu.
hivi ndivyo mimi nilivyo.''
Bruce Jenner
Katika masaa ya mahojiano na Diane Sawyer mjini New York na
California, Jenner alielezea kwa kina mapambano yake ya kuwa na
jinsia mbili tangu utotoni.
''Akili zangu ni za kike sana kuliko za kiume.'' Ameongezea. '' Ni
vigumu sana watu kuelewa, lakini hivyo ndivyo nafsi yangu ilivyo.''
Jenner aliyejawa na hisia na mwenye nywele ndefu shati na suruali
ndefu alisema kuwa amesubiri kwa miaka mingi ili kujitangaza kwa
kuwa hakutaka kuwavunja moyo watu.
Kwa miongo kadhaa wake wa zamani wa Jenner na madada zake
waliweka siri kuhusu jinsia yake na kwamba walikuwa watu waliokuwa
wakijua siri hiyo.
Mtandao wa watu wanaojua siri hiyo hatahivyo ulipanuka hivi majuzi
wakati Jenner alipomwambia mamaake na wanawe 10 .
Jenner ana watoto sita Burt,Cassandra,Brabdon,Brody,Kendall na
Kylie pamoja na watoto wanne wa kambo akiwemo Kourtney,Kim,Khloe
na Rob Kardashian.

Watu zaidi ya 5000 wafariki dunia baada ya tetemeko kubwa la ardhi huko Nepal.

Idadi ya watu ambao wamethibitishwa kuaga dunia wakati
kulipotokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Nepal siku ya Jumamosi
imepanda hadi zaidi ya watu 5000.
Utawala unasema kuwa zaidi ya watu 10,000 walijeruhiwa. Serikali ya
Nepal inasema kuwa imelemewa na kiwango cha janga hilo.
Waziri mkuu Sushil Koirala anasema kuwa utawala unapokea maombi
mengi ya kutaka msaada kutoka maeneo ya mbali ya vijiji vya
Himalaya, lakini jitihada za kuyafikia maeneo hayo zinatatizwa na
uhaba wa vifaa na waokoaji.
Waziri huyo mkuu anasema kuwa kuna mahitaji ya dharura ya
mahema , chakula na maji.Zaidi ya nusu ya nyumba katika kijiji hicho zimeharibiwa.

Madereva wa mabasi ya abiria wapanga kugoma tena.

Siku 17 baada ya madereva wa mabasi mchini kugoma na kutikisa
nchi , Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani ( Taboa)
kimetangaza mgomo mwingine nchi nzima . Mgomo wa Aprili 9 ,
mwaka huu uliodumu kuanzia alfajiri hadi saa 7 :00 mchana
ulitikisa nchi na kuwaathiri abiria wengi waliokuwa wanasafiri
kwenda maeneo mbalimbali ya nchi . Jana Taboa walitangaza
kusitisha utoaji huduma kuanzia kesho ikiwa ni hatua ya kupinga
nauli mpya za mabasi zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini ( Sumatra) . Kufuatia hali hiyo ,
Taboa kimewataka mawakala kutokatisha tiketi kuanzia leo kwa
abiria hadi hapo Sumatra itakapotoa taarifa za kuruhusu nauli
ya zamani ziendelee kutumika . Katibu Mkuu wa Taboa, Enea
Mrutu , alitoa taarifa hiyo jana wakati akitoa majumuisho ya
mkutano mkuu wa dharura uliojumuisha wadau wa usafirishaji.
Mkutano huo ulikuwa na ajenda kuu tatu ambazo ni ajali za
barabarani, nauli mpya zilizotangazwa na Sumatra , madaraja ya
mabasi, mgomo wa madereva na vituo vya kubadilishia madereva
wanaokwenda umbali mrefu . Mrutu akisoma maazimio hayo baada
ya kumalizika kwa majadiliano hayo , alisema sababu iliyotolewa
na Sumatra kushusha nauli kutokana na bei ya mafuta kushuka
siyo kigezo muhimu bali ni shinikizo kutoka kwa wanasiasa . “ Kesho
kutwa ( kesho ) hakuna gari ambalo litatoka kituo cha mabasi
Ubungo kwenda mkoani na kama tutapigwa mabomu tupigwe, ila
msimamo wetu uko pale pale wa kutotoa magari hadi Sumatra
watakapotoa tamko la kutaka nauli za awali ziendelee kutumika, ”
alisema . Kuhusu ajali, alisema kutokana na kukithiri kwa ajali za
mabasi, wanakubaliana na utaratibu uliowekwa na serikali wa
madereva kubadilishana wanaokwenda masafa marefu katika
vituo ambavyo vitatengwa ili kupunguza ajali hizo . KILOMITA 80
KWA SAA Mrutu aliagiza madereva wote watumie mwendo wa
kilomita 80 kwa saa na wazingatie sheria za usalama barabarani
na watakaokiuka sheria hizo wachukuliwe hatua kwa mujibu wa
sheria. Alisema kuanzia Mei mosi , mwaka huu wataanza kutumia
vituo maalum vya kubadilishia madereva kwenye mabasi ya
masafa marefu kwa muda wa miezi mitatu kwa majaribio . Vituo
hivyo ni Singida mjini , kwa mabasi ya Dar es Salaam kwenda
Mwanza , Bukoba , Kahama ; na kituo cha Morogoro kwa mabasi
yanayokwenda mikoa ya nyanda za juu kusini . Uamuzi huo
umechukuliwa kutokana na mapendekezo ya Jeshi la Polisi kikosi
cha usalama barabarani , kubainisha kuwa chanzo cha ajali kwa
mabasi yaendeyo masafa marefu ni uchovu wa madereva . Mrutu
aliwataka wamiliki wa mabasi kuhakikisha madereva wao
wanazingatia taratibu na sheria zilizowekwa na Jeshi la Polisi
pamoja na Sumatra ili utoaji wa huduma uweze kwenda vizuri.
Alisema madereva ambao wameanza tabia ya kuwachafua
wamiliki wa mabasi kwamba wamekuwa wakielekezwa kwenda
mwendo wa kasi ili kuwahi abiria watawachukulia hatua
kwasababu suala hilo siyo la kweli .

“ Mimi ninunue gari la
mamilioni halafu nimlazimishe dereva aende mwendo kasi ni kitu
ambacho hakiniingii akilini inamaana sina uchungu na gari yangu ,”
alisema Mrutu Alisema mwendokasi wa kilomita 80 kwa saa , uwepo
wa vituo vya kubadilisha madereva wa mwendo mrefu na kukoma
kwa urasimu miongoni mwa askari polisi kuwa suluhisho la ajali za
barabarani nchini . Mrutu alisema katika utafiti wao wamebaini
kuwa chanzo kimojawapo kinachosababisha kutokea kwa ajali
nchini ni ubovu wa miundombinu ya barabara . Kwa upande wake ,
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji wa maadili iliyopewa jukumu
la kuchunguza tatizo la ajali nchini , Abdulrazack Kimaro , alisema
ajali za barabarani zinasababishwa na mwendokasi.

Alisema
katika uchunguzi wao wamebaini hakuna hata dereva mmoja
anayezingatia sheria za usalama za barabrani ingawa Sumatra na
askari wa kikosi cha usalama barabarani wanakuwapo bali
kinachofanyika ni kumalizana kwa kupeana ‘ kitu kidogo’ .
Abdulrazack alisema wao kama wamiliki wa mabasi hawako tayari
kuendekeza madereva wanaokwenda kinyume cha sheria, hivyo
kila mmiliki kwa muda wake atoe somo kwa dereva wake juu ya
makubaliano hayo ili kudhibiti ajali.

Alisema madereva
wanatakiwa kusimamiwa kikamilifu kwenye utendaji wao na
kwamba kila mmiliki anapaswa kuwasilisha majina ya dereva wake
na vyeti , leseni kwa Taboa ili kuthibitisha ufanisi wake kwa kazi
anayoifanya. Naye Katibu wa Wamiliki wa Mabasi Mkoani Kigoma
( Kiboa ) , Hussein Kalyango , alisema serikali inatakiwa kuyafanyia
marekebisho baadhi ya mambo yakiwamo kanuni za usafirishaji
zinazomkandamiza mmiliki zaidi huku zikimwacha dereva nje ya
lawama mfano chanzo cha ajali . Kalyango alisema utaratibu wa
sheria za Sumatra zinamlenga mmiliki wa basi kwa utovu wowote
wa basi ambao anaufanya dereva . “ Tunaiomba Sumatra ibadilishe
sheria makosa anayofanya dereva adhibitiwe dereva na hata
kuchukuliwa sheria za zaidi na tunatakiwa kushirikiana Sumatra,
polisi na sisi kumaliza ajali hizi za barabarani ,” alisema .
CHANZO:NIPASHE

Manny Pacquiao atua Las Vagas tayari kwa pambano dhidi ya Mayweather.

Manny Pacquiao atua Las Vegas tayari kwa pambano lake la kihistoria dhidi ya Floyd Mayweather.

Sunday 26 April 2015

TUTIZAME HAYA MACHACHE KUELEKEA PAMBANO LA ARSENAL DHIDI YA CHELSEA NA MCHAMBUZI NICASIUS COUTINHO SUSO

Usimchukie Mourinho na mbinu zake, katika wakati kama huu unahitaji Ulinzi ufanye kazi kuliko ushambuliaji, hii ni akili nyepesi na nzuri ambayo wengi uipuuza.

Coquelin vs Fabregas?  Utamu upo hapa, akishinda huyu mfaransa Mashabiki hawatomkumbuka Fabregas,  akishindwa Wenger atazungumzwa sana Leo, na majuto mengi.

Mesut Ozil.. Yupo katika kiwango ambacho hata mimi ningefurahia kucheza EPL mbele yake. Sidhani kama Mourinho atamhitaji sana Zouma leo, nadhani Ramires anaweza Kuwa option bora kuanza na Matic.

Bellerin vs Hazard..  Nina wasiwasi Wenger akataka kuweka mtu mgumu hapa, kama Chambers, lakini ugomvi wa hawa watu wawili utavutia. Kama Kuna siku ngumu zaidi ambazo Bellerin anaweza kumbana nazo na kuzikumbuka basi ni leo, lakini ni siku ambazo anaweza kuwapa tiketi ya moja kwa moja kwenye mbao Chambers na Debuchy. Kinachoumiza kichwa ni Ile gundi iliyo kwenye viatu vya Hazard, inabidi uwe umeamka vizuri sana kumzuia huyu na wala usiwe mwenye hasira maana maudhi kwake ni kawaida, ndio maana hatumhitaji Chambers wala Debuchy hapo Leo labda Wenger.

Kama Kuna kitu ambacho Arsene Wenger anatakiwa kukiweka kichwani mwa Sanchez na wachezaji wa Arsenal ni Counter Attacks.  Hawazijui kabisa, huyu Sanchez anaupenda sana mpira, wale wengine kukaba Counter Attacks hawajui (mkumbuke Oscar,  Hazard, Willian eneo hili) hapa ndipo panapoweza kumrudisha Wenger nyuma.

Carzola na Oscar ndo wachezaji wakimya zaidi kuelekea kwenye mchezo huu... (wasiozungumzwa wala kuzungumza). Lakini ubora wa Carzola unahitajika sana kuliko wa huyu mwenzie.. Ile kazi ya kupenya alichokipanga Mourinho golini unahitaji akili ya Carzola,  Ozil na Sanchez zifanye kazi kwa Pamoja.

Karata yangu Sasa na wachezaji watakaochanganua mchezo.

Pamoja na yote hayo mchezo utakuwa mguuni kwa Aaron Ramsey. Huyu akicheza vizuri kazi ya Carzola,  Ozil itakuwa rahisi sana,  na atawafanya Azplicueta na Matic kwa Pamoja wafanye kazi kubwa sana, lakini akishindwa ndipo napoona kifo cha Arsenal kitakapokuwa.

WILLIAN / Oscar

Tofauti na mechi ya Manchester United yeyote Kati ya hawa ubora wake Leo utaamua mchezo huu. Kwangu mimi ningemchukua Willian kwa sababu ya Sanchez. Tatizo la Sanchez katika ukabaji ndilo ambalo litaleta shida kule hasa. Ivanovic + Willian. Maana yangu wakati Arsenal wanamtizama Hazard hili ndilo eneo litakalo leta shida sana. Na hii itampa Hazard nafasi ya kufanya athari katika BLIND SPOT (sehemu isiyofikirika).

Kumkaba Drogba Leo ni rahisi sana lakini pia yeye kuwafunga Arsenal inaweza Kuwa rahisi zaidi. Usishangae kumuona Drogba aliye bora hasa Pamoja na umri wake, hata Torres alitembelea hii tabia kwa Manchester United na Vidic, au Wayne Rooney na wale Aston Villa.

Usisahau ni Wenger Vs Mourinho. Hili nalo ni tatizo wakati Mwingine historia ni mbaya sana na watu wanaishi kulingana nayo. Siwezi kusema matokeo lakini nahisi inaweza Kuwa moja ya siku ambazo Wenger anaweza kucheka lakini kama tu akiweza kutibu COUNTER ATTACKS.

Ningekuwa shabiki wa Arsenal ningewaza COUNTER ATTACKS kuliko Ile defense ya Chelsea. Hapa ndo ubovu wa timu yetu unapolala na ubora wa Chelsea ulipojikita.

Ahsanteni.

By Nicasius Coutinho Suso

Mchambuzi bora wa michezo anayekuja kwa kasi (najiita chipukizi..)

Uchambuzi wa mechi kali za leo Ligi Kuu Uingereza.

Everton vs Man United 14:30
   Tukianzia katika mchezo wa mapema kabisa majira ya sa 14:30 vijana wa Martinez ambao wamekumbuka shuka pamesha kucha watakwaana na Man Utd.
     Licha ya matokeo mazuri ya hivi karibuni bado hali si shwari kwa Everton kwani mpaka sasa wapo nafasi ya 12 kwa pointi(41) kulingana na uwezo mkubwa walio uonesha msimu uliopita wengi tulitaraji kuiona miongoni mwa timu zinazo wania nafasi ya nne, ukiachilia mbali majeraha mengi katika kikosi cha kwanza lakini msimu huu timu imekosa muunganiko mzuri hasa safu ya ulinzi na kiungo kitu kilicho pelekea kuwa hapo walipo.

   Mbele ya Utd ambayo imetoka kupoteza dhidi ya Chelsea kazi ya ziada itahitajika kwa vijana wa Goodison Park ukiachilia mbali takwimu nzuri walizo nazo katika mechi 2 kwenye uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Utd ( 1-0 August) 2012  ( 2-0 Aprl 2014) ila bado watahitaji kazi ya ziada kwenye mchezo huu walau wapate pointi kwani pindi wanashinda michezo hiyo walikuwa vyema zaidi ya msimu huu.

    Wamecheza mechi 33 W-10,D-11,L-12, huku waki funga magoli 41 na kuruhusu 43 wana asilimia 27% za kutoruhusu wavu wao kuguswa kwa hizo takwimu inaonesha ni jinsi gani ushindi ni hafifu.
     UTD waliocheza michezo 33, W-19,D-8,L-6, wakiwa na pointi 65 mpaka sasa upande wao wamefunga magoli 59, huku wakiruhusu magoli 31 na wana asilimia 30% za kutokuruhusu nyavu zao kuguswa kikubwa upande wao ni nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulays msimu ujao licha ya kufungwa na Chelsea baada ya mwendelezo mzuri wa matokeo bado wamekuwa na mchezo mzuri.
   Licha ya majeraha wengi waliokuwa nao katika kikosi cha kwanza bado walionesha uwezo mbele ya Chelsea kitu kinacho pelekea kuwa na nafasi mbele ya Everton, watahitaji kuzuia kutokujirudia kwa ile historia ya 1987 ya kufungwa mfululizo na Everton ktk dimba la Goodison Park.
     Uwepo wa Evans anaerejea baada ya kifungo kutokana na sakata lake na Cissé kutakuwa nguvu kwenye safu ya ulinzi ya Van Gaal vilevile kwa RVP.
     Mchezo uliofanyika Old Trafford Everton alifungwa 2-1 lakini pia endapo watafungwa na United watakuwa wamefikia rekodi ya A.Villa ya kufungwa mara nyingi zaidi (32) dhidi ya Manchester.
     Katika michezo ya ugenini Utd si wazuri sana kwani kwenye mechi 9 wameshinda 3 sare 4 na kupoteza mara 2 na ukija pale katka dimba la Goodison Park ukiachilia mbali kupoteza mechi mbili za hivi karibuni bado Manchester wana ubavu kwani kwenye michezo 22 ya Ligi hivi karibuni Utd W-14,D-3,L-5 wakifunga magoli 39, wakiruhusu 23 na mara 8 hawaja ruhusu goli.
     Wenyeji wao Everton mambo yapo hivi wakiwa dimba lao dhidi ya Utd W-5,D-3,L-14 wakifungwa goli 39 huku wakifunga goli 23 hawakuruhusu goli mara 4.
    Ngoja tusubiri kama ni Lukaku ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanne walio ifunga Utd hat-trick wakiwemo kina Kuyt,Bentley na Etoo ama ni kina Mata na Rooney kwenye mchezo wa 170 kati ya timu hizi huku katika michezo 169 kwa ujumla Utd akishinda 76 dhidi ya 53 za Everton.

-----------

    Tukihamia katika Jiji la London miongoni mwa majiji yenye mvuto wa aina yake huku likiwa lina timu nyingi ktk ligi (6)  kutakuwa na bonge la mechi ambalo ni zaidi ya kutafuta pointi ni kati ya

      ARSENAL 18:00 CHELSEA

   Kama mchezo wa awamu ya kwanza ambapo tulishuhudia makocha wa timu hizi wakitaka kunjana sijui nini kitatokea kwenye mchezo ambao Mourinho atahitaji kumfanya Mzee Wenger kama moja ya kipachi cha ngazi kuelekea ktk jukwaa la kuchukua ubingwa wa Epl.
    Ni siku nyingi wana Arsenal hawaja kenua mbele ya Chelsea kwani mara ya mwisho ni 2011 walipo livunja Daraja kwa ushindi wa goli 5-3 Van Persie akipiga tatu huku moja ya tukio la kuvutia likiwa kuteleza kwa John Terry.
    Tangu hapo mambo huwa magumu kwa Arsenal ktk kuzipata pointi tatu kwa Chelsea kosa kubwa ambalo limekuwa likiwagharimu ni kutokuwa makini kwenye safu ya ulinzi.
   Mchezo uliopita Arsenal dhidi ya Chelsea walirudia historia ya mwaka 2003 dhidi ya Utd pale OT ya kutokupiga shuti lililo lenga goli kitu ambacho kilionesha ni jinsi gani safu ya ushambuliaji ilikuwa na kutu.
    Ukiachilia mbali majeruhi kwa pande zote huku hali ya Mertesacker ikiwa haijulikani na upande mwingine wa shilingi kumkosa Costa labda achezeshwe kiulazima bado si sababu ya timu zote kutokupata matokeo.
   Hivi sasa kila upande umekuwa na matokeo mazuri sana Arsenal pointi 66 Chelsea vinara pointi 76 kinacho onekana kuwabeba Arsenal mbele ya Chelsea hivi sasa ni uchezaji mzuri ndani ya uwanja ingawa upande wa Chelsea hawa angalii kucheza vyema zaidi ya kulenga shabaha ya pointi tatu muhimu.
    Hii ni vita kubwa ki mpira ktk mchezo huu wote wakitumia 4-2-3-1 na kwa namna ya uhalisia mbinu za ziada kutoka kwa wachezaji au makocha ndo zitaamua nani mbabe.
     Mourinho anahitaji pointi kuelekea kuchukua ubingwa pia kingine atahitaji kuendeleza ubabe wake kwa mzee Wenger kwani mara 12 amemfunga mechi 7 na kutoa sare 5 hivyo hivyo kwa upande wa Wenger atahitaji kufuta historia hiyo mbaya pia kurejea nafasi ya pili baada ya City kushinda dhidi ya Aston Villa.
    Kwenye michezo 12 ya hivi karibuni Arsenal kashinda mara 2 ambazo Mourinho alikuwa kasha timka zake Darajani huku wakipoteza mara 8 na sare 2.
    Si vita ya Pointi au ya makocha bali kuna vita nyingine tena mbili ya kwanza ni Fabregas ( Fabrepass) huyu ndiye mchezaji anae ongoza kwa kutoa pasi za mwisho za magoli Epl (16) atakuwa anarejea nyumbani ambapo atahitaji uvumilivu mbele ya zomeazomea ya mashabiki wa Arsenal kutokana na kuikacha Arsenal pindi walipo kuwa wanamtaka na kuelekea Darajani kwa kigezo cha kunyanyua makwapa ( kuchukua vikombe).
   Vita vingine ambavyo vitakuwa kwa wachezaji ambao wanawania tuzo ya mchezajo bora wa msimu pia wamekuwa wakisababisha maneno mengi kwa fans wa Arsenal na Chelsea si wengine bali ni Hazard na Sanchez, hawa wote wamekuwa na umuhimu mkubwa kwenye vikosi vyao.
    Hazard ambae mpaka sasa anamagoli 13 na pasi za magoli 8 amekuwa akizungumzwa kama ni miongoni mwa wachezaji bora wa Dunia wanao staili kuchukua Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ukiwaondoa Messi na Cr7, amekuwa aki ibeba timu mara nyingi na kumzuia kwake inakuwa moja ya njia za kuizuia Chelsea kupata matokeo.
     Sanchez yeye mpaka sasa anagoli 14 huku akitoa pasi za magoli 8 amekuwa ni msaada mkubwa kwa Mzee Wenger msimu huu ni msimu wake wa kwanza Epl na kwa kiwango anacho onesha wana Arsenal wataraji makubwa toka kwake kama atazidisha juhudi.
     Mchezo utakuwa ni undava-undava hasa kwa upande wa Chelsea ambao ukiachilia mchezo mzuri wa kufunguka walio anza nao msimu huu asilimia kubwa tangu mwaka uanze wamekuwa wakicheza kwa kujihami hasa wakitumia viungo wao walio wazuri ktk kukaba.
   Usishangae kumuona Zouma hivyo kina Cazorla na Coquelin watahitaji kazi ya ziada kupenya katika nusu ya Chelsea ambao kwenye michezo 6 dhidi yao hawajafunga goli.
    Arsenal kutokuwepo kwa Costa safu ya ulinzi itaweza pumua ingawa uwepo wa Drogba ambae ktk michezo 14 amefunga mara 13 anaweza kuwa tishio kwa kutaka kuendeleza takwimu nzuri dhidi yao achilia mbali umakini hasa utahitajika kwa Hazard.
    

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

Saturday 25 April 2015

IIkaay Gundogan mbioni kutua Manchester United.

Habari za ndani kuptia chombo cha habari cha skysports kimeripot kuwa klabu ya Manchester United inakarbia kupata Saini ya kiungo
matata toka klabu ya Borussia Dortmund,Ilkay Gindogan kwa dau la paund milion 21.5.

Gundogan mkataba wake na Dortmund unaisha msimu huu na atakua mchezaji huru hvyo Borussia wako tayari kumuachia sasa.
Mwez Wa pili kocha Van gaal alisema dirisha kubwa la usajili lazma amsajili kiungo mbunifu na mjuzi wa kupiga pasi murua sifa ambazo
Gundogan anazo, amefunga magoli 15 katika mechi 123 alizochezea
Dortmund ikiwemo penati aliyoifunga kwenye mechi uefa fainali dhidi ya bayern Munich.

Man United yampatia donge nono De Gea kumbakisha.

Kocha wa Manchester United Luis Van Gaal amegeuza karata kwa
David De Gea kwa kusema kuwa klabu imempa pesa nyingi iliabakie Manchester huku mkataba wake ukiatarajiwa kuisha msimu ujao,

United waneweza wakajikuta wanalazimika kumuuza mchezaji bora wa msimu ulio pita
wa Manchester United,uhamisho ambao utawaudhi mashabaiki wengi kwa kuwa mchezaji huyo raia wa spain amekua kipenzi cha mashabiki
kwa sasa.
Alipo ulizwa kuhusu kipa wake,Van Gaal alisema mpira upo kwake na uamuzi upo mikononi mwake
"imechukua muda sasa.inaweza ikatokea,mimi sio bosi,nataka
abakie,mchezaji yeye ndie bosi anaweza akasema ndio au hapana.
"tumemtengea pesa nyingi anatakiwa asaini mkataba mpya"

Thursday 23 April 2015

Volcano ya ajabu yalipuka Chile.

Volcano aina ya Calbuco imelipuka kwa muda mfupi huko nchini Chile ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya zaidi ya miaka 40.

Watu waliokuwa wakiishi maeneo jirani na ulikotokea mlipuko wa Volcano hiyo wamelazimika kuyahama makazi yao.

Picha za televisheni zilionyesha wingu zito na majivu vikipanda hewani umbali kilomita kadhaa angani katika jimbo la Los Lagos kusini mwa Chile.

Mamlaka nchini humo zimetoa tangazo la hali ya hatari kwa wakazi wote ambao wapo umbali wa kilomita la mlipuko wa Volcano hiyo huku safari za ndege kuelekea eneo hilo zikiwa zimeahirishwa.

BantuTz MAGAZETINI:SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO ALHAMIS 22,2015.

DSC01668
BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika kurasa za mbele na nyuma magazeti yote ya leo.

 DSC01667

DSC01669
DSC01670
DSC01671
DSC01672
DSC01673
DSC01674
DSC01675
DSC01676
DSC01677
DSC01678
DSC01679
DSC01680
DSC01682
DSC01683
DSC01684
DSC01685
DSC01686
DSC01687
DSC01688
DSC01689
DSC01690
DSC01691
DSC01692
DSC01693
Endelea kufurahia huduma za BantuTz.com huku ukiusubiria kwa hamu Mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi uitwao Bantuz mwaka huu