Facebook

Saturday, 21 February 2015

UTABIRI NA UCHAMBUZI WA MECHI ZA LIGI KUU UINGEREZA NA Mr. Martin kiyumbi

 Displaying IMG-20150221-WA0006.jpg
Ligi Kuu Uingereza leo na kesho itaendelea tena baada ya mapumziko ya juma lililopita.
Inaingia round ya 26 .

Na itakuwa imebakisha round 12 ushindani upo sehemu zote kwa mara ya kwanza timu nne za jijini London zimeingia katika nafasi 8 za juu mpaka hivi sasa.
Nafasi  4 za juu ziko wazi kwa timu 7 hadi hivi sasa kama ifuatavyo:-
Chelsea    59
Man City  52
Man Utd  47
Soton       46
Arsenal    45
Spurs       43
Liverpool 42


Huku katika nafasi za chini kuna msuguano  wa hatari
Sunderland     23
Hull city         23
QPR                22
Burnley           21
Leicester city  17


UTABIRI WA MICHEZO YA LEO LIGI KUU UINGEREZA
kwa misuguano hii ya nafasi za juu na nafasi za chini ningependa nitoe utabiri wangu wa matokeo ya mechi za leo na kesho.
 
-----------------------------------------------------------------------------

Swansea City 1-1 Manchester United
Manchester United wanaenda Liberty Stadium.Ikumbukwe mechi ya kwanza Manchester United alipigwa, mechi ya leo itakuwa ngumu. habari nzuri kwa Swansea City ni kurudi kwa  Sirgusson .Ujio wake na umuhimu wake katika kuunganisha timu.Ndo unaofanya niamn mechi hii itaisha kwa sare.Huku Manchester United,Van Persie yuko fiti kuwavaa Swansea.Van Gaal anajiamini huku mchezaji pekee aliyebaki majeruhi ni Michael Carrick.Siipi sana nafasi Manchester United kushinda mechi ya leo.
 
-----------------------------------------------------------------------------

Sunderland 1-1 West Brom Albion
Wiki iliyopita kwenye FA Sunderland alitolewa na timu ya daraja la pili Bradford City.Ilihali Westbrom Albion iliifunga Westham.
Hii ni mechi ngumu sana.Westbrom wanaenda kwa Sunderland.Naamini wanaenda kuambulia pointi moja.

--------------------------------------------------------------------------------

Southmpaton 1-2 Liverpool
Southmpaton itaingia ikiwa na majeruhi kwenye kikosi chao.Naamini hiyo ndiyo nafasi pekee watakayotumia Liverpool kushinda.Utakuwa mchezo mzuri kila timu zinatafuta nafasi ya kuingia top 4.


-------------------------------------------------------------------------------

Chelsea 3-1 Burnely 
Sioni cha kuizuia Chelsea kushinda mechi hii.Chelsea wanataka kujichimbia zaidi kileleni
----------------------------------------------------------------------------------

Man city 3-0 Newcastle 
Ujio wa Yaya Toure na kurudi kwa Aguero kwenye makali yake naipa nafas Man City kuibuka na ushindi kwenye mechi hii.
---------------------------------------------------------------------------------

Tottenham Hotspurs 2-1 Westham United
Hii ni london derby .Spurs wanaitaka kwa udi na uvumba nafasi ya nne.Westham  wanazidi kupoteza mwelekeo kadri siku zinavyozidi kwenda.Itakuwa derby nzuri ila nampa mwenyeji ushindi.

---------------------------------------------------------------------------------

Everton 2-1 Leicester city
kwa upande wangu Leicester wamekuwa wakicheza vizuri ila hawana bahati.Everton alhamisi hii wametoka kucheza EUROPA LEAGUE .Pamoja na uchovu naipa Everton ushindi.

----------------------------------------------------------------------------------

Crystal palace 0-3 Arsenal
Hii ni london derby.Mechi hii wengi wanasema itakuwa ngumu kwa Arsenal ila mimi sioni ugumu wowote.Arsenal inapigania kuepuka kutokucheza UEFA kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16 .Uwepo wa sanchez,Carzola unaipa nguvu asernal.

--------------------------------------------------------------------------------

Aston villa 2-1 StokeCity
Mchezo wa kwanza wa kocha Sherwoods akiwa kwenye benchi.Matokeo mazuri ya FA wikendi  iliyopita,morali ya timu ya Aston villa kushuka ghafla kwa kiwango cha stoke city inatosha kuipa Villa ushindi leo.

--------------------------------------------------------------------------------

Hull City 1-1 QPR
Ni mchezo mgumu ambao kila timu haitaki kupoteza.QPR imetoka kushinda dhidi ya Sunderland ugenini.Leo hii nahisi wanaenda kuchukua point moja ugenini.

----------------------------------------------------------------------------------

ASANTENI.
Imeandaliwa na ..............
  Martin kiyumbi                                                                                                                        
0758182438   

0 comments:

Post a Comment