Wanawake katika kijiji kimoja cha kazkazini mwa Uganda wamefanya
maandamano wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya
utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kwa takriban miaka
10.
Wakati wa maandamano hayo ,mawaziri wa serikali na watafiti
walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko
Amuru.
Maandamano
Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu
wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakaazi wakidai
kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.
Katika kabila la Acholi ,mwanamke
anapovua nguo na kusalia uchi ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa
laana kwa mpinzani wake.
0 comments:
Post a Comment