Wakuu katika shrika la kupambana na rushwa nchini Nigeria
wanasema maafisa kadhaa kutoka benki kuu ya nchi hiyo
wamepelekwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi wa kiasi kikubwa
cha fedha za thamani ya mamilioni ya dola.
Pia baadhi ya maafisa wa benki za kibiashara wamo kwenye orodha
hiyo ya watuhumiwa baada ya kushukiwa kuhusika kwenye
udanganyifu mkubwa wa pesa.
Shirika hilo la kupambana na ufisadi The Economic and Financial
Crimes Commission lilimeuelezea udanganyifu huo wa fedha kuwa
walijaribu kuingiza katika soko la fedha noti ambazo zilikuwa tayari
zimeondolewa kutoka soko hilo na zilitakiwa kuharibiwa kabisa kwa
kuwa zimezeeka au kwa sababu nyengine yeyote.
Katika ulaghai huo wahusika wanasemekana walitengeneza vipande
vya magazeti kwa kiwango na ukubwa sawa na hizo noti za
kuharibiwa na kudanganya kuwa wanachoma noti hizo zilizopigwa
marufuku na badala yake kuzirudisha kwa matumizi ya kila siku ya
kifedha hivyo kujipatia faida kubwa ya fedha halisi.
Waliokamatwa ni maafisa 6 wa benki kuu ya Nigeria wanaofanya kazi
mjini Ibadan na wafanyikazi 16 kutoka benki za kibinafsi ambao pia
wanatuhumiwa kushiriki kashfa hiyo.
Nigeria
Ufisadi na Udanganyifu huo umeipa hasara Nigeria ya zaidi ya dolla
million 30.
Ingawaje kamata kamata hiyo ilifanyika kabla ya kuapishwa kwa
rais mpya wa Nigeria, Muhammadu Buhari, wengi wanamuona kama
ndiye kichochezi kikubwa kilichosababisha hatua hiyo kutokana na
msimamo wake mkali wa kupambana na rushwa nchini humo.
Kwa miaka mingi vita dhidi ya ufisadi nchini humo vimewalenga zaidi
walarushwa wadogo huku wala rushwa wakubwa wakikwepa mkono wa
kisheria kwa kutumia hizo hizo fedha walizozipata kwa njia za
kifisadi.
0 comments:
Post a Comment