Wanafunzi wa kitivo cha elimu katika chuo kikuu cha
Dodoma wameipindua serikali ya wanafunzi wa kitivo
hicho kwa madai ya kutowajibika kwa viongozi pamoja na
madai ya ubadhirifu wa fedha.
Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM).
Mapinduzi hayo yamefanyika leo asubuhi ambapo
wanafunzi hao wamempindua aliyekuwa Rais wa kitivo
hicho, John Nzilanyingi na kumuweka aliyekuwa waziri wa
afya na mikopo, Simon Mpandalume kuwa Rais wa mpito
wa serikali hiyo hadi hapo uchaguzi mkuu utakapofanyika
Juni mosi mwaka huu.
Rais aliyepinduliwa anadaiwa kutumia madaraka yake
vibaya kwa kuwakandamiza wanafunzi wenzake kwa
kushirikiana na uongozi wa chuo.
Aidha anatuhumiwa kwa ufujaji wa fedha za wanafunzi
ambapo anadaiwa kutumia sh milion 7 za michango ya
wanafunzi kununulia gari yake ya kutembelea.
Mpaka sasa Rais huyo hajulikani alipo kwani baada ya
kupinduliwa alitoweka eneo la chuo.
Mmmmh
ReplyDelete