Waungwana kila uchwao kwenye jiji hili na viunga vyake sambamba na maeneo mengi ya nchi, kuna neno wa ‘kimataifa’ hulisikia likiimbwa.
Waimbaji wakuu wa neno hilo ni mashabiki wa Yanga wakiongozwa na mpiga zumari wao aliyeacha kazi yake na kujigeuza muimbaji.
Kinyume chake hilo neno klabu ya Simba huitwa wa ‘mchangani’ au wa ‘matopeni’. Wengi wananilaumu kuwa kwa nini huwa sijibu neno lolote la ajabu kwa Yanga. Jibu langu ni jepesi tu, lazima tujitofautishe msemaji wa klabu na mropokaji wa klabu.
Mimi hupenda kuzungumzia issues sio porojo au lugha za uchochoroni. Haiwezekani nikawa kiongozi kisha nikaongea lugha za mashabiki ‘maandazi’.
Kwa hiyo mtaniwia radhi wapenzi wa mpira kwa kutokuwa muimbaji wa ngonjera za uchochoroni. Mara zote nitabaki msemaji wa klabu kubwa nchini na ntaongea facts kwa kadri zilivyo.
Wadau zisomeni sifa za kimataifa kwa klabu ya Simba nje ya nchi halafu zifananisheni na timu nyingine nchini.
Walau kama zitafikia nusu tunawaruhusu watafute tusi jipya. Ombi langu kwenu isambazeni taarifa hii katak kila mtandao wa kijamii kisha waseme wao wanaojiita wa kimataifa.
Simba ndiyo timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa, ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie
Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyewe na hili lilinuliwa mwaka1968.
Simba ndiyo timu ya kwanza kumiliki jengo lake lenyewe na hili lilizinduliwa 1971.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa bingwa wa ligi kuu nchini1966.
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwakilisha nchi na hii ilikuwa 1967.
Simba klabu ya kwanza nchini kwenda Ulaya na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland
Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa mabingwa wa Afrika Mashariki na kati na hii ilikuwa 1974.
Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa Afrika Mashariki na Kati, ndiyo timu iliyochukua ubingwa mara nyingi kuliko klabu yeyote Afrika Mashariki na Kati (Champs off all time.)
Simba ndiyo timu pekee nchini iliyowahi kufika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika na hii ilikuwa1974.
Simba ndiyo timu pekee nchini na Afrika Mashariki kufika fainali ya kombe la Caf na hii ilikuwa1993.
Simba ndio timu inayoshikilia rekodi Afrika kama si duniani kwa kufungwa na Mufurila Wonderers ya Zambia magoli 4-0 na kwenda kuibamiza 5-0 kwao, mbele ya rais wao Kenneth Kaunda. Hii haijafanywa na klabu yeyote Afrika na nina mashaka duniani, hii ilikuwa 1979.
Simba ilicheza katik hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika 2003 kwa mafanikio makubwa kulinganisha na timu yoyote nchini.
Simba ndiyo timu pekee kuivua ubingwa klabu bingwa Afrika nadi Zamalek hii ilikuwa pia 2003.
Simba ndiyo klabu pekee nchini kuzifunga timu zote za mataifa ya kiarabu kuanzia
Waliowatoa mwaka jana Etoile du Sahel (Tunisia)
Widad Casablanca (Morocco)
El Setif (Algeria)
El Harach (Algeria)
halaf tumezifunga timu zote kubwa za Misri Zamelek,Al Ahly, Arab Contractors, Ismailia, Mehala, Al kubra na timu nyingine mnajua huwa inafanywaje ikigusa kule.
Pia imeshaitoa El Merekh ya Sudan 1994 katak klabu bingwa ya Afrika. Simba pia imeshazifunga miamba ya Afrika Magharibi kuanzia Asec, Asante Kotoko, Hafia ya Guinea hata mabingwa wa kihistoria wa Zambia Nkana Red Devils.
Tukirudi juu Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa suti na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland.
Simba ndiyo klabu pekee nchini kujenga jengo lake yenyewe kwa nguvu za wanachama na mashabiki, wenzetu ni mkopo na msaada toka kwa mzee Karume100%, Simba ilipewa kiasi flan na mzee karume baada ya jengo kukamilika na hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 70.
Angalia idadi ya wachezaji wa Simba walioenda Ulaya kucheza soka la kulipwa.
Nico Njohole
Deo Njohole
Kassim Matitu
George Kulagwa
Huku ikiwa na makumi ya nyota wake kadhaa waliowahI kutapakaa sehemu mbalimbali duniani.
Nikutajie wachache.
Khalid Abeid
Haidar Abeid
Martin Kikwa
Athman Mambosasa
Zamoyoni Mogella
Hamis Gaga
Lilla Shomari
Iddi Pazi
Kiwelu Mussa
George Masatu
Hussein masha na wengine wengi.bila kumsahau nguli wa sasa mbwana samata.mutoto ya msimbazi.
Na hapa kumbukumbu zikae vizuri wazee wangu mimi, Sunday na Kassim Manara wakati wanaenda kucheza Ulaya hawakuwa wachezaji wa Yanga, walikuwa wakicheza Pan African.
Nimalizie kwa kuwaambia FIFA ilizitaja timu bora za karne kwa kila nchi kwa Tanzania Simba ilitajwa ndio timu bora ya karne na wenye mpira wao FIFA. Nenda kwenye rekodi za Caf ndio utajua nani wa kimataifa baina ya cc na wao.
Porojo za mjini ntakuwa nimezimaliza sasa na anayebisha abishe kwa data. Wakoloni wetu walitufundisha hivi…No reaserch no data no right to speak.Tafsiri isiyo rasmi, hujafanya utafiti na huna takwimu funga bakuli lako.
Asanteni na nendeni mkawaambie.
Haji S Manara
Msemaji wa klabu bora ya muda wote Tanzania (best club of all time)
Ukiona errors zipotezee jadili issues na nnaruhusu challenges kama zipo
Porojo peleka kuleeeeeee..
Nini maoni yako