Mabingwa wa zamani wa kombe
la dunia Italy imeanza vyema kampeni yake ya kuwania kombe la dunia
nchini Brazil baada ya kuichapa Uingereza mabao mawili kwa moja katika
mechi kali.
Bao la ushindi la Italy lilifungwa kwa kichwa
kupitia mshambuliaji matata Mario Baloteli mda mchache tu baada ya
kipindi cha mapumziko.Mechi hiyo ilichezwa chini ya viwango vya juu vya joto katika uwanja wa Manaus uliopo katikati ya msitu wa Amazon.
Katika mechi za awali ,Costa Rica ilitoka nyuma na kuishinda Uruguay mabao matatu kwa moja huku Colombia nayo ikiicharaza Ugiriki mabao matatu bila katika mji wa Belo Horizonte.
Wakati huohuo miamba ya soka barani afrika Ivory Coast imeimarisha matumaini ya bara hili baada ya kutoka nyuma na kuishinda Japan kwa mabao mawili kwa sufuri.
Ivory Coast ilijipatia mabao yake kupitia wachezaji Wilfried Bony na aliyekuwa mchezaji wa Arsena Gervinho huku Japan ikifunga kupitia mshambuliaji wake keisuke Honda.
Hivi sasa
tunahamia katika site yetu mpya inayoitwa www.bantutz.com
ni katika kuboresha huduma zetu za kutoa habari za uhakika na burudani.
0 comments:
Post a Comment